Utangulizi

Karibu kwenye tovuti yetu.

Kwanza tutoe shukrani zetu za dhati kwa uamuzi wako wa kuitembelea tovuti yetu, kwetu ni faraja kubwa sana kuwa nawe siku hii ya leo.laurian mwajombe

Hii ni tovuti  tuliyoiandaa kwa lengo moja kuu la kumwezesha mwananchi wa kawaida ambaye hawezi kuelewa maelezo yanayotolewa na tovuti nyingine zinazotoa maelezo kuhusu matatizo mbalimbali ya kiafya na dawa mbalimbali za kuondoa matatizo hayo  kwa lugha za kigeni. Lengo letu ni kumwezesha mwananchi wa kawaida kupata maelezo ya matatizo hayo na dawa hizo kwa lugha nyepesi ya kiswahili ili aweze kuelewa na kutoa maamuzi yaliyo sahihi.  Tunaamini watu wengi hushindwa kunufaika na tovuti mbalimbali kwa sababu ya kushindwa kuzielewa lugha zilitotumika katika tovuti hizo.

Kuna tovuti nyingi zinazolenga kumsaidia mteja kupata mahitaji yake ya kuboresha maisha, kwa bahati mbaya nyingi hutumia lugha za kigeni hivyo kumfanya mtu anayetumia kiswahili pekee kushindwa kunufaika na maelezo hayo. Kwa kugundua pengo hilo, tumeamua kuanzisha tovuti hii.

Malengo Ya Tovuti

Kukusanya maelezo kwa kutumia wataalamu wetu wenye uzoefu wa biashara za kwenye mitandao ya dawa mbalimbali ambazo zimethibitika kusaidia watu wengi duniani na kuziorodhesha katika tovuti hii.

Kumsadia mwanachi ambaye atavutiwa na dawa aliyoisoma kuinunua nje ili aweze kuipata na kuitumia.

Kutoa fursa kwa watu wote wenye uzoefu katika fani hii na watumiaji wa dawa zilizoorodheshwa ndani ya tovuti hii kutoa michango yao ya mawazo kuhusu ubora wa dawa mbalimbali kwa kupitia blog yetu au sehemu ya comments chini ya kila ukurasa. Imani yetu ni kupata mawazo zaidi kuhusu ubora wa dawa tulizoziorodhesha humu na dawa nyingine ambazo hazijaorodheshwa hapa ambazo watu wengine wameshazitumia.

Mpangilio Wa Tovuti

Tovuti hii imepangwa kwa kutumia aina ya matatizo ambayo mtu anaweza kuwa nayo na anatafutia suluhisho. Kwa mfano, dawa zote zinazosaidia kupunguza uzito au unene ( weight loss products ) zitaorodheshwa pamoja na zile za kupunguza mwonekano wa kiumri ( anti-aging products ) zitaorodheshwa kwenye kundi moja hali kadhalika dawa za matatizo ya mifupa ( bone  and joint products ), dawa za  afya ya  mwanamke na dawa za afya ya viungo vya  uzazi vya mwanamme. Tumetenga sehemu nyingine kwa ajili ya matatizo ya afya mseto ambapo hapa tumejuimisha matatizo mengi yakiwemo matatizo yanayohusiana na ugonjwa wa kisukarividonda vya tumbo (peptic ulcers)kiharusi (stroke)msongo wa mawazo (stress)mfadhaiko (depression)PumuUTIKansaHigh Blood Pressure (Hypertension)UKIMWIherniatezi dumemkanda wa jeshi Chunusi, n.k.

 

ushuhuda wa green world

                                                             Video Ya Ushuhuda Wa Christina Kupata Mtoto

Bonyeza juu ya picha hiyo hapo juu kuangalia video ya ushuhuda wa Christina kupata mtoto baada ya kutumia bidhaa za kampuni ya Green World Tanzania.

 

ushuhuda wa green world

 

Video ya Ushuhuda Wa Mama Wa Afrika Ya Kusini Kuhusu Kupona Arthrits Kwa Bidhaa Za Green World

Imani yetu ni kuwa ndugu msomaji wetu utaridhika na kile ambacho tumekiandaa. Hata hivyo tunaamini kuwa hatujafikia ubora wa kikomo katika utayarishaji hivyo tunaomba maoni yako ili tuweze kuboresha tovuti hii. Maoni yako pekee ndiyo msaada mkuu katika kuiboresha tovuti hii.

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.

Karibu tuwe sote