Kuziba Pumzi Usingizini (Obstructive Sleep Apnea)

 

 

 

 

Tatizo la kuziba pumzi usingizini (obstructive sleep apnea) ni tatizo la usingizi linaloweza kuwa kubwa kiafya. Ni tatizo linasababisha mtu apate vipindi vinavyojirudia vya kusimama na kurudia upumuaji akiwa usingizini.

Kuna aina nyingi za sleep apnea, lakini inayoonekana zaidi ni obstructive sleep apnea. Aina hii ya sleep apnea inatokea wakati misuli ya koo inakuwa na vipindi vya kujilegeza na kuziba njia za hewa ukiwa unasinzia. Ishara kuu ya obstructive sleep apnea ni kukoroma.

Tiba kwa tatizo la obstructive sleep apnea zinapatikana. Tiba moja inahusu matumizi ya kifaa kinachotoa msukumo ili kuzifanya njia za hewa kuwa wazi wakati umelala. Namna nyingine ni kutumia kifaa cha mdomo cha kusukuma mbele taya la chini wakati umelala. Wakati mwingine, upasuaji huwa ndiyo njia sahihi.

 

Dalili Za Kuziba Pumzi Usingizini

 

Dalili za kuwa unapata tatizo la kuziba pumzi usingizini ni pamoja na:

. Kuwa na usingizi mchana usio wa kawaida
. Kukoroma kwa sauti
. Kubainika kwa vipindi vya kutopumua ukiwa usingizini
. Kuamka ghafla kukiambatana na kutweta au kukabwa pumzi
. Kuamka ukiwa na mdomo au koo lililokauka
. Maumivu ya kichwa asubuhi
. Kushindwa kutuliza akili mchana
. Mabadiliko ya hisia, kama mfadhaiko au hasira
. Pressure ya juu
. Kutoa jasho usiku
. Kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa

 

Sababu Za Kuziba Pumzi Usingizini

 

Obstructive sleep apnea hutokea wakati misuli ya nyuma ya koo inajilegeza kupita kiasi na kuzuia upumuaji wa kawaida. Misuli hii hubeba maungo pamoja na yale ya nyuma ya sehemu ya juu ya mdomo (soft palate), kimeo (kiungo cha pembetatu kinachoning’inia kutoka kwenye soft palate – uvula), tonsils na ulimi.

 

chanzo cha kuziba pumzi usiku

 

Misuli hii ikijilegeza, njia ya hewa huwa nyembamba au hufungwa wakati ukivuta hewa ndani na upumuaji unaweza kuwa si wa kutosha kwa kipindi cha sekunde 10 au zaidi. Hali hii inaweza kupunguza kiwango cha oksijeni ndani ya damu na kusababisha kuongezeka kwa carbon dioxide.

Ubongo unalihisi tatizo hili la upumuaji na kwa muda unakuamsha kutoka usingizini ili uweze kuifungua njia ya hewa. Uamshwaji huu huchukua muda mfupi hivi kwamba pengine unaweza kutoukumbuka.

Unaweza kuaamka ukiwa umebanwa pumzi hali ambayo inajirekebisha yenyewe haraka sana, kwa kuvuta pumzi nzito mara moja au mbili. Unaweza kutoa sauti ya kukoroma, sauti ya kukabwa au kutweta.

Mpangilio huu unaweza kujirudiarudia mara 5 hadi 30 au zaidi kila saa, usiku mzima. Kuvurugwa huku kunaweza kusababisha ukakosa mzito unaotakiwa , wa amani na uwezekano wa kujisikia kulala mchana wakati wa kazi ukatokea .

Watu wenye tatizo la sleep apnea wanaweza wasijue kuwa usingizi wao ulivurugwa. Kwa kawaida, watu wenye tatizo hili hufikiri kuwa walilala vizuri usiku mzima.

 

Vihatarishi Vya Kuziba Pumzi Usingizini

 

Mtu ye yote anaweza kupatwa na tatizo la kuziba pumzi akiwa usingizini. Lakini kuna vitu vinavyochochea hali hii kutokea, vikiwa ni pamoja na:

. Unene wa kupindukia. Watu wengi ingawa si wote wenye tatizo la kuziba pumzi usingizini ni wanene. Kujazana kwa mafuta kwenye eneo la juu la njia ya hewa kunaweza kuziba pumzi. Matatizo mengine ya kiafya kama hypothyroidism na polycystic ovary syndrome vinaweza kusababisha obstructive sleep apnea.

. Njia ya hewa kuwa nyembamba. Unaweza ukarithi njia nyembamba za hewa. Au tonsils au adenoids zinaweza kuvimba, hali itakayofunga njia ya hewa.

. High blood pressure. Obstructive sleep apnea huwapata sana watu wenye hypertension.

. Kuziba sugu kwa pua. Tatizo la kuziba pumzi huwapata mara mbili zaidi watu wenye pua zinazoziba usiku, bila kujali chanzo. Hii inaweza kuwa ni kwa sababu ya njia nyembamba ya hewa.

. Kuvuta sigara. Watu wanaovuta sigara wanakuwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata tatizo la kuziba pumzi usiku.

. Kisukari. Tatizo la kuziba pumzi huonekana zaidi kwa watu wenye kisukari.

. Jinsia. Wanaume na wanawake waliokoma hedhi wana tatizo hili mara mbili zaidi.

. Historia ya familia. Tatizo la kuziba pumzi usiku linaweza kuwa ni la kurithi.

. Pumu. Utafiti umeonyesha uhusiano wa asthma na obstructive sleep apnea.

 

Tiba Ya Kuziba Pumzi Usingizini

 

Kubadili mtindo wa maisha

Kama hali ya tatizo si kubwa sana, daktari anaweza kushauri mabadiliko ya kitabia yafuatayo:

. Kupunguza unene wa mwili kama ni mnene sana
. Kufanya mazoezi ya mwili mara kwa mara
. Kunywa pombe kwa kiasi, kama ni mnywaji, na kutokunywa saa kadhaa kabla ya kulala
. Kuacha uvutaji wa sigara
. Kutumia dawa za kuzibua pua na za mzio (allergy)
. Kutolala kwa mgongo
. Kuacha matumizi ya baadhi ya dawa kama za usingizi.

 

 

tiba ya kuziba pumzi usiku

 

 

Kama hatua hizi hazileti mabadiliko au kama tatizo lako ni kubwa, daktari atakushauri tiba za namna nyingine. Kuna vifaa vya kufungua njia ya hewa. Wakati mwingine, upasuaji unaweza kufanyika.

 

Katika mada yet nyingine tutaliona tatizo la kukoroma usiku. Usisite kutoa maoni yako kuhusu mada yetu ya leo au kuuliza maswali uliyo nayo.

 

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

 

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.