Ugonjwa Wa Osteporosis Ni Nini

 

 

kupungua kimo

 

Osteoporosis ni hali inayojitambulisha kwa kupungua kwa ujazo wa mifupa, kupungua kwa nguvu za mifupa na kuifanya kuwa rahisi kuvunjika. Osteoporosis huufanya mfupa kuwa na vijitundu vingi isivyo kawaida unaoweza kushindilika (kupungua ukubwa kwa kugandandamizwa) kama sponji.

Mfupa wa kawaida hujengwa kwa protini, collagen na calcium ambayo huupa mfupa ugumu. Osteporosis husababisha mifupa kuwa dhaifu na inayovunjika kirahaisi – kiasi kwamba kuanguka kidogo au kujikunja au hata kukohoa kutasababisha mvunjiko. Mvunjiko unaweza kuwa na mwundo wa ufa (kama mvunjiko wa nyonga) au mshindiliko (kama kujishindilia kwa pingili za uti wa ngongo.) Uti wa mgongo, nyonga, mbavu, na vifundo vya mikono ni sehemu ambazo huathiriwa zaidi na osteoporosis ingawa mfupa wa sehemu nyingine yo yote ya mwili unaweza kuathirika.

Osteoporosis huathiri watu wa jinsia zote na jamii zote. Lakini watu weupe na watu wa Asia – hasa wanawake waliokoma hedhi – wanakuwa kwenye hatari kubwa zaidi. Matumizi ya dawa, mlo mzuri na mazoezi ya kuweka uzito sawa vinaweza kusaidia kupunguza uharibifu wa mifupa au kuiimarisha mifupa iliyokwisha athiriwa.

 

Dalili Za Osteoporosis

 

Kuna dalili zinazoonekana kwenye hatua za mwanzo za uharibifu wa mifupa. Lakini mara baada ya kuwa mifupa imeharibika, unaweza kuona dalili, baadhi zikiwemo:

. Maumivu ya mgongo, yanayosababishwa na nyufa au pingili zilizojishindilia
. Kupungua urefu baada ya muda
. Kuwa na umbile la kupinda
. Kuvunjika mifupa kirahisi kuliko kawaida.

 

Chanzo Cha Osteoporosis

 

Mifupa yako kila wakati inajikarabati – mfupa mpya hujengwa na wa zamani kuyeyushwa. Unapokuwa mdogo, mifupa mipya hujengwa kwa kasi kubwa zaidi kuliko mifupa iliyozeeka inavyoyeyushwa, kwa hiyo ujazo wa mifupa yako huongezeka. Watu wengi hufikia kilele cha uzito wa mifupa wanapofikia miaka 20. Watu wanapozeeka, mifupa iliyozeeka huvunjwa kwa kasi kubwa zaidi kuliko ile inayojengwa.

 

osteoporosis ujazo wa mifupa

 

Kuwa utapata osteoporosis au la, itategemea kiasi cha mifupa uliyojijengea wakati wa ujana wako. Kama ulifika kilele na kiwango kikubwa, una hifadhi kubwa kwenye “benki” yako na unakuwa umejipunguzia uwezekano wa kupata osteoporosis uzeeni.

 

Vihatarishi Vya Osteoporosis

 

Kuna vitu kadhaa ambavyo huongeza uwezekano wa kupata osteoporosis – vikiwa ni pamoja na umri, jamii unakotoka, mtindo wa maisha, na tiba unazotumia. Vihatarishi vilivyo nje ya uwezo wako ni:

. Jinsia. Wanawake wapo kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata osteoporosis kuliko wanaume.

. Umri. Kadiri unavyokuwa mzee, ndivyo unavyokabiliwa na osteoporosis kirahisi zaidi.

. Jamii. Una hatari kubwa zaidi ya kupata osteoporosis kama ni mtu mweupe au kutoka Asia.

. Historia ya familia. Kuwa na mzazi mwenye osteoporosis kunakuweka kwenye hatari kubwa zaidi, na hasa kama baba au mama alikwishapata ufa kwenye nyonga.

. Ukubwa wa umbile la mwili. Wanaume na wanawake wenye maumbile madogo ya mwili wapo kwenye hatari kubwa zaidi kwa sababu wana ujazo mdogo wa mifupa ya kutumika watakapokuwa wanazeeka.

 

Viwango Vya Homoni

Osteoporosis inawapata watu wenye uzidifu au upungufu wa homoni fulani katika miili yao. Mifano ni kama:

. Homoni za kijinsia. Upungufu wa homoni za kijinsia hudhooofisha mifupa. Kupungua kwa estrogen kwa wanawake wakifika kukoma hedhi ni sababu moja kubwa ya kupata osteoporosis. Wanaume hupungukiwa na testosterone kadiri wanavyozeeka. Tiba za tezi dume na kansa ya matiti hupunguza homoni hizo na kusababaisha osteoporosis.

.Matatizo ya thyroid. Kuzidi kwa homoni ya thyroid hupunguza mifupa.

Tezi zingine. Osteoporosis imehusishwa na utendaji kazi wa kuzidi wa homoni za parathyroid na adrenal.

 

Vihatarishi Kutokana Na Mlo

Osteoporosis huwatokea zaidi watu:

. Wanaopata calcium kwa kiwango kidogo. Kukosa calcium katika maisha ya mtu husababisha osteoporosis. Upungufu wa calcium hufanya mifupa kuwa myepesi.

. Tabia mbaya za ulaji. Kujinyima kula na kuwa na mwili mdogo hudhoofisha mifupa.

Upasuaji wa tumbo. Upasuaji wa kupunguza ukubwa wa tumbo la chakula au kuondoa sehemu ya utumbo hupunguza eneo la kufyonzea virutubishi, ikiwa ni pamoja na calcium.

 

 

Vihatarishi Vya Tiba

Osteoporosis huwapata zaidi watu wenye matatizo ya kiafya, kama ya:

. Ugonjwa wa Celiac
. Magonjwa ya mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
. Magonjwa ya figo na maini
. Kansa
. Lupus
. Multiple myeloma
. Rheumatoid arthritis

 

Mtindo Wa Maisha

Baadhi ya tabia huongeza uwezekano wa kupata osteoporosis. Nazo ni kama:

. Kutojishughulisha.
. Matumizi ya pombe.
. Matumizi ya tumbaku.

 

Namna Ya Kuzuia Osteoporosis

 

Chakula kizuri na mazoezi ya mwili ni vitu muhimu kaatika kuiweka mifupa yako kwenye afya bora.

Protini

Protini ni moja ya vitu vya kujenga mifupa.

Uzito Wa Mwili

Kuwa na uzito mdogo huongeza uwezekano wa kupata osteoporosis. Uzito mkubwa kupita kiasi unajulikana kuongeza uwezekano wa kupata nyufa kwenye mikono na vifundo vya mikono.

Calcium

Wanaume na wanawake wa kati ya miaka 18 na 50, wanahitaji miligramu 1,000 kila siku. Kiwango hiki huongezeka hadi miligramu 1,200 kwa siku wanawake wafikapo umri wa 50 na wanaume wafikapo 70.

Kama inakuwa vigumu kwako kupata calcium katika chakula, tumia virutubishi vya calcium. Hata hivyo, viwango vikubwa vya calcium vimehusishwa na kidney stones.

Vitamini D

Vitamini D huboresha ufyonzwaji wa calcium na mwili na afya ya mifupa. Binadamu unaweza kupata vitamini D kwa kiwango cha kutosha kutoka mwanga wa jua. Wanasayansi bado hawajajua kiwango sahihi cha vitamini D kwa siku. Kiwango kizuri cha kuanzia kwa mtu mzima ni miligramu 600 hadi 800 kutoka kwenye chakula au virutubishi. Watu wasio na vyanzo vya vitamini D ya kutosha au wanaoishi kwenye maeneo yasiyo na mwanga wa jua, wanahitaji kupata virutubishi. Bidhaa nyingi za multivitamini zina miligramu 600 hadi 800 za vitamini D.

Mazoezi

Mazoezi yanaweza kukusaidia kukomaza mifupa yako na kuzuia kupungua kwa uzito wa mifupa.

 

 

 

Katika kurasa nyingine zinazohusiana na matatizo ya mifupa na maungio ya mifupa, tutazungumzia magonjwa ya rheumatoid arthritis na gout.

Tafadhali jisikie huru kutoa maoni yako kuhusu mada yetu ya leo. Kama una maswali, usisite kuuliza.

 

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

 

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.