Ugonjwa Wa Glaucoma Ni Nini?

 

ugonjwa wa glaucoma

 

Ulishawahi kusikia mtu anaumwa macho na akaambiwa na madaktari kuwa tatizo ni pressure ya macho?

Kuna magonjwa mengi ya macho ambayo yanaweza kusababisha kutoona vizuri na wakati mwingine yakaleta upofu wa kudumu. Katika ukurasa wetu wa leo, tutauzungumzia ugonjwa uitwao glaucoma, ambao unawasumbua watu wengi sasa hivi, na hasa wale wenye umri mkubwa. Tutaona chanzo cha ugonjwa huu, mambo ambayo unaweza kuyafanya unapokuwa unakabiliwa na tatizo hili na tiba utakayopewa pale utakapobainika kuwa na ugonjwa huu.

Glaucoma ni hali inayoharibu neva ya jicho (optic nerve). Hali huendelea kuwa mbaya kila siku zikiongezeka. Hali hii inahusishwa na kuongezeka kwa msukumo (pressure) ndani ya jicho. Ugonjwa wa glaucoma hufuata koo. Ugonjwa huu huja baadaye sana katika maisha.

Kuongezeka kwa pressure hiyo ndani ya jicho, kunakoitwa intraocular pressure, kunaweza kuharibu optic nerve, ambayo hupeleka picha kwenye ubongo. Kama glaucoma ikizidi, uharibifu wa kudumu wa kuona hutokea au pengine kusababisha upofu katika miaka michache.

Watu wengi wenye glaucoma hawaoni dalili za awali au kupata maumivu. Yafaa kumwona daktari wa macho mara kwa mara ili kuyalinda macho yako. Watu wengi wenye glaucoma waliofuata mpango wao wa tiba na kumwona daktari mara kwa mara wameweza kutunza hali yao ya kuona vizuri.

Macho yako yakiharibika, huwezi kuyarudisha kwenye hali yake. Kwa kupunguza pressure ya macho, unaweza kulinda afya ya macho yako.

 

Chanzo Cha Glaucoma

 

Majimaji yaliyomo ndani ya jicho, yaitwayo aquemous humor, kwa kawaida hutiririka nje ya jicho kupitia mfereji wenye matundu kama ya wavu. Mfereji huu ukizibwa, maji hujazana ndani ya jicho. Wakati mwingine wataalamu hawana maelezo kwa nini mfereji huu huziba. Lakini, tatizo laweza kuwa la kiurithi.

 

 

 

sababu za glaucoma

 

 

Madhara mengine machache yanayoweza kuwa visababishi vya glaucoma ni kuumizwa jicho na kitu butu au cha kemikali, maambukizo makali ya ndani ya jicho na kuziba kwa mishipa ya damu ndani ya jicho. Aghalabu, upasuaji wa jicho kuondoa tatizo jingine huweza kusababisha glaucoma. Kwa kawaida, ugonjwa huu hushambulia macho yote mawili, ingawa moja laweza kuwa na hali mbaya zaidi.

 

Hali Zinazochangia Ugonjwa Wa Glaucoma

 

Ugonjwa huu huwapata zaidi watu wenye umri wa zaidi ya miaka 40, lakini vijana, watoto na vichanga huweza pia kuathirika. Wamerekani weusi wapo kwenye hatari kubwa zaidi ya kuupata ugonjwa huu wakiwa wadogo, na hupoteza uwezo wa kuona kwa wingi zaidi.

Unaweza kuupata ugonjwa huu:

. Kama ni mmarekani mweusi, irish, Russian, japanese, Hispanic, Inuit, au kama ni Scandinavian

. Kama umri wako ni zaidi ya 40

. Kama una ndugu wenye glaucoma

. Kama una matatizo ya kuona

. Kama una kisukari

. Kama unatumia dawa kama prednisone

. Kama uliwahi kuumia macho

. Kama una cornea nyembamba kuliko kawaida

. Kama una high blood pressure, ugonjwa wa moyo, kisukari, upungufu wa damu kutokana na sickle cell

. Kama una pressure ya jicho
. Kama ni farsighted au nearsighted.

 

Aina Za Glaucoma

 

Kuna aina kuu mbili:

Open-angle glaucoma. Hii ndiyo aina inayoonekana zaidi. Madaktari mara nyingine huiita wide-angle glaucoma. Mfumo wa kutoa maji nje ya jicho uitwao trabecular meshwork huonekana kuwa nzuri, lakini majimaji hayatiririki inavyotakiwa.

 

 

aina za glaucoma

 

Narrow angle glaucoma hutokea pale iris inaposogea mbele, utolewaji wa maji kuzibwa kwa sababu ya kuziba kwa drainage angle. Kwa sababu hiyo, kunaweza kukatokea msukumo ambao utaharibu upelekwaji wa taarifa zinazoonwa na macho kwenye ubongo.

Dalili za awali za narrow angle glaucoma ni maumivu makali ya macho, maumivu ya kichwa au kipandauso, mwanga kuzunguka maumbo, kutanuka kwa pupil, matatizo ya kuona na damu kwenye macho. Dalili hizi hudumu kwa saa chache au hadi pale msukumo ndani ya macho utakapopungua.

 

Angle-closure glaucoma. Hii huonekana zaidi Asia. Unaweza ukasikia ikiitwa acute au chronic angle-closure au narrow-angle glaucoma. Macho yako hayatoi maji inavyotakiwa kwa sababu nafasi ya kutolea maji kati ya iris na cornea ni nyembamba. Hali hii inaweza kusababisha kutokea mgandamizo mkubwa wa ghafla ndani ya jicho. Hii huhusishwa na farsightedness na mtoto wa jicho (cataract)- ukungu juu ya lensi ndani ya jicho.

Aina nyingine ambazo hujionyesha mara chache sana ni:

Secondary glaucoma. Hii ni hali ambapo sababu nyingine, kama mtot0 wa jicho (cataracts) au kisukari, inaongeza pressure ndani ya jicho.

Normal-tension glaucoma. Hii ni pale unapoona vidoa vyeusi unapotazama au endapo optic nerve imeharibika hata kama pressure ndani ya jicho ipo katika kiwango sahihi.

Pigmentary glaucoma. Hapa vipande vidogo vya rangi kutoka eneo la iris, eneo la jicho lenye rangi, huingia ndani ya majimaji ya jicho na kuiziba mifereji ya kutolea maji nje.

 

Dalili Za Glaucoma

 

Watu wengi wenye open-angle glaucoma hawaoni dalili zo zote. Kama dalili zitatokea, ni baadaye wakati tatizo limeshakua. Hii ndiyo sababu ugonjwa huu huitwa “sneak thief of vision.” Dalili kuu ni kushindwa kuviona vitu vya pembezoni.

Dalili za acute-angle glaucoma huja haraka zaidi na zinajitambulisha. Uharibifu huweza kutokea haraka. Ukiyaona yafuatayo mwone daktari:

. Kuona mwanga wa mviringo kuzunguza vyanzo vya mwanga
. Kushindwa kuona
. Macho kuwa mekundu
. Kuchafuka tumbo au kutapika
. Maumivu ya macho

 

Tiba Ya Glaucoma

Daktari anaweza kuchagua kukupa dawa ya matone ya macho, kukufanyia laser surgery, au microsurgery kupunguza pressure ndani ya jicho lako.

Dawa Za Kunywa. Dawa hizi huweza kuboresha mtiririko au kupunguza utengenezwaji wa majimaji.

Laser Surgery. Yafuatayo yaweza fanyika.

. Trabeculoplasty. Hii hufungua njia za majimaji.

. Iridotomy. Hapa kijitundu kidogo hutengenezwa kwenye iris kuacha maji yatoke nje kirahisi zaidi.
. Cyclophotocoagulation. Hii huponya maeneo ya tabaka la kati la macho yako ili kupunguza uzalishwaji wa majimaji.

Microsurgery. Kwa utaratibu wa trabeculectomy, daktari anaweza kutengeneza mfereji mpya wa kutolea maji na kupunguza pressure. Aina hii ya upasuaji unaweza kutakiwa kufanyika zaidi ya mara moja. Daktari anaweza kuweka kijimrija ili kusaidia utolewaji wa majimaji. Ni upasuaji unaoweza kuleta upofu wa muda au wa kudumu, kutokwa damu au maambukizi.

Katika mada nyingine, tutaona jinsi kisukari kanavyoweza kuleta upofu wa macho.

 

Pata ushauri zaidi kwa kututumia ujumbe kupitia ukurasa huu hapa chini kwa kujaza fomu, au kututumia barua pepe kupitia promota927@gmail.com au tupigie simu kwa namba zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

 

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.