GREEN WORLD TANZANIA – Unatafuta Biashara Ya Mtaji Mdogo?

 

green world tanzania

Wanachama wa Green World baada ya mkutano mjini Nairobi

Kama umekuwa ukihangaika kutafuta biashara ya kuianza kwa mtaji mdogo, leo nitakudokeza kuhusu aina moja ya biashara ambayo mimi binafsi nimeifanya kuanzia mwaka 2015 na hadi sasa bado naendelea nayo. Nimeendelea kuifanya kwa miaka yote hii kwa sababu moja kubwa kwamba nimekuwa nikipata mafanikio makubwa zaidi kila siku. Ni biashara ambayo niliianza kwa mtaji mdogo sana , mtaji ambao kila mmoja wetu anao na imekua hadi kuwa biashara kubwa sana. Karibu sana ndugu  yangu  usome kuhusu  biashara hiyo na ukiipenda, usisite kuwasiliana nami.

Green World Tanzania ni moja ya matawi ya kampuni ya kimataifa ya Green World yenye makao yake makuu kwenye mji wa Michigan huko Marekani. Kampuni ya Green world ilianzishwa mwaka 1994 na toka wakati huo imekuwa ikikua kwa kufungua matawi mapya na kujenga viwanda vipya sehemu mbalimbali duniani.  Kiongozi wa kampuni ya Green World , Dr Deming Li, ni msomi aliyehitimu PhD kwenye chuo kikuu cha Cornell cha Marekani kwenye fani ya microbiology. Dhamira yake kubwa ilikuwa ni kutumia teknolojia ya kisasa kuboresha tiba ya asili ya China (Traditional Chinese Medicine) ili kizazi cha sasa kiweze kunufaika.

Kampuni ina vituo vya utafiti kwenye vyuo vikuu tofauti saba nchini Marekani, kila kimoja kikijikita kwenye eneo tofauti linalohusu afya ya binadamu. Kampuni pia ina kliniki kubwa huko Marekani kwa ajili ya kufanya majaribio kabla ya kuanza uzalishaji. Kwa sababu hii, bidhaa nyingi za Green World zimepasishwa na shirika la udhibiti wa chakula na madawa la Marekani (FDA). Kampuni ina bidhaa zaidi ya 120 na ina matawi kwenye nchi zaidi ya 90 duniani.

Faida Za Kujiunga Na Green World

Kuna faida kuu mbili za kuwa mwanachama wa Green World Tanzania:

Kwanza, ni fursa ya kuweza kuanza kufanya biashara na kupata mafanikio makubwa ukianzia na mtaji mdogo sana wa pesa au wakati mwingine kwa mtaji ambao ni juhudi zako tu. Green World ni kampuni inayofanya bishara kwa mtindo wa mtandao (MLM), mtindo ambao unaruhusu kupata kipato kinachotokana na juhudi zako binafsi na ukipenda, kutokana na juhudi za watu utakaowashirikisha na kuwafundisha. Kampuni hutoa mafunzo ya awali ya jinsi ya kuweza kuianza biashara yako bure. Kujua zaidi kuhusu aina hii ya uanachama rejea ukurasa wa Green World – Fursa Bora Ya Biashara Ya Mtaji Mdogo.

Pili, unaweza kuitumia fursa hii ili kununua bidhaa za kuboresha afya yako na ya jamii yako kwa bei ya jumla, bila kuwajibika kujihusisha kwenye biashara. Wewe sasa utaitwa mwanachama mlaji. Kinachovutia katika aina hii ya pili ya uanachama, ni bonasi endelevu utakayokuwa unaipata baadaye baada ya kuwa umenunua bidhaa za kiwango fulani. Na kama umependa aina hii ya uanachama, rejea ukurasa wa jinsi ya kuwa mwanachama mlaji wa Green World kwa maelezo ya kina na maelekezo ya jinsi ya kujiunga.

Ofisi Za Green World Tanzania

Kampuni hii ina ofisi moja tu kwa sasa hivi iliyoko katika jiji la Dar Es Salaam ndani ya jengo la Machinga Complex, eneo la Karume .

ofisi za green world machinga complex

Bidhaa Za Green World Tanzania

Kampuni ya Green World Tanzania inajishughulika na usambazaji wa bidhaa  zilizotengenezwa kutokana na vitu vya asili, ikiwemo mimea, madini na vitu vingine kama samaki, asali, n.k. Virutubishi hivi vimegawanyika katika makundi makuu yafuatayo:

1.  Matatizo Ya Mifupa Na Viungio Vya Mifupa
2.  Matatizo Ya Maambukizi Ya wadudu
3.  Matatizo Ya Kuwa Na Uzito Mkubwa (Unene).
4.  Matatizo Ya Ubongo
5.  Magonjwa Ya Watoto
6.  Magonjwa Na Afya Ya Akina Mama
7.  Matatizo Na Afya Ya Mwanamme
8.  Afya Ya Macho
9.  Matatizo Ya Uyeyushaji Chakula Tumboni
10. Matatizo Ya Ngozi
11. Ukosefu Wa Kinga Ya Mwili
12. Matatizo Ya Moyo
13. Kansa.

Kuona vifurushi vya bidhaa za kampuni ya Green World, soma ukuraa wa vifurushi vya Green World.

Mafanikio Ya Watanzania Katika Kampuni Ya Green World

Kampuni hii imekuwa ikiwanufaisha sana watanzania walioigundua na kujiunga nayo. Kwa mfano, tarehe 18 Augusti 2012 katika hoteli ya Holiday Inn, watanzania walitunukiwa zawadi mbalimbali likiwepo gari, tiketi za kusafiria kwenda China na kutalii kwa gharama ya kampuni na zawadi nyingine nyingi kama kamera, oveni za microwave na TV. Katika hafla hiyo, jumla ya wanachama 60 walipata zawadi.

Mafanikio makubwa zaidi kwa watanzania yalipatikana tarehe 28 Februari 2015 ambapo jumla ya watanzania 200 walipata zawadi mbalimbali. Katika hao 4 walipata magari yaliyokuwa na  thamani ya milioni 15 kila moja, 14 walipata tiketi za kwenda kutalii China na wengine zawadi mbalimbali. Sherehe hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Blue Pearl Hotel (Ubungo Plaza).

Angalia kipande cha mkanda wa video hapa chini kinachoonyesha sherehe hiyo na wanachama waliofanikiwa kupata zawadi hizo za magari.

Zawadi za magari

Green World Barani Afrika

Katika hafla ya kuadhimisha miaka 10 toka Green World ilipoingia Afrika iliyofanyika Novemba 2017 ndani ya ukumbi wa Ellis Park Arena huko Johannesburg, Afrika ya Kusini, Raisi wa kampuni hii barani Afrika, ndugu David Zhang, alieleza kuwa hadi mwaka huo kampuni ilikuwa tayari ina wanachama zaidi ya milioni 1.6 na kuifanya kuwa ni kampuni inayoongoza katika tasnia ya Network Marketing barani Afrika ikiwa na bidhaa tofauti zaidi ya 80.  Katika kipindi hicho cha miaka 10, wanachama walipata zawadi mbalimbali kama zifuatazo:

.  2349 – magari madogo ya biashara, kila moja likiwa na thamani ya Tshs milioni 20

.  95 – magari ya kifahari kila moja likiwa na thamani ya Tshs milioni 70

.  24 villas – nyumba kila moja ikiwa na thamani ya Tshs milioni 300

Hapa chini ni picha ya wanachama wa Green World waliokwisha pata mafanikio makubwa.

Umependa kujiunga na kampuni  ya Green World ili uanze biashara yako ya kukupa uhuru? Soma ukurasa wa Green World – Fursa Bora Ya Biashara Ya Mtaji Mdogo.

Kama unataka kujiunga na kampuni hii au kama una maswali yo yote, usisite kuniandikia kupitia promota927@gmail.com. Pia unaweza kuwasiliana nami kwa simu moja kwa moja kupitia 0655  858027 au 0756  181651 (Usitume ujumbe [SMS] tafadhali).

Laurian Mwajombe, Machinga Complex, Dar Es Salaam.