Umuhimu Wa Madini Katika Mwili Wa Binadamu

 

 

 

Watu wengi huchanganya kati ya madini na vitamini, hivi ni vitu viwili tofauti. Tofauti kubwa ni kwamba vitamini ni vitu vyenye elementi ya kaboni (organic substances) wakati madini hayana kaboni (inorganic substances.)

Madini ni muhimu kwa afya ya mwili. Mwili hutumia madini katika kufanya kazi nyingi, pamoja na kuwezesha mifupa, misuli, moyo na ubongo kufanya kazi vizuri. Madini pia ni muhimu katika utengenezaji wa vimeng’enya na homoni.

Chuma na shaba nyekundu ndani ya vyombo vya kupikia ni madini yale yale tunayoyapata katika chakula. Hii ndiyo sababu kupikia vyombo vya chuma hutusaidia kupata madini ya chuma katika chakula. Tutumiapo vyombo hivi, chuma kidogo huyeyuka na kuchanganyika na chakula. Mwili hufyonza na kuyatumia madini haya katika chuma kile cha kwenye chakula. Madini ni sehemu inayodumu zaidi katika mwili. Madini hayaungui, na unaweza kuyaona kwenye majivu ya kitu kilichoungua.

Kuna aina mbili za madini: macorominerals na trace minerals. Trace minerals ni madini yanayopatikana kwa kiasi kidogo sana. Mwili unahitaji kiasi kikubwa cha macrominerals. Macrominerals ni pamoja na:

. calcium

. phosphorus

. magnesium

. sodium

.potassium

. chloride

. sulfur.

Macrominerls husaidia mwili kufanya shughuli zifuatazo:

. kuweka vizuri viwango vya maji
. kutunza afya ya ngozi, nywele na kucha
. kuboresha afya ya mifupa

Mwili unahitaji kiasi kidogo sana cha trace minerals. Trace minerals ni pamoja na:

. iron (chuma)

. manganese

. copper

. iodine

. zinc

. cobalt

. fluoride

. selenium.

Trace minearls zinasaidia katika:

. kuimarisha mifupa
. kuzuia kuoza kwa meno
. kusaidia kuganda kwa damu
. kusaidia kusafirisha oksijeni
. kusaidia kinga za mwili
. kusaidia kutunza pressure

Watu wengi hufikia mahitaji yao ya madini kwa kula chakula mchanganyiko. Lakini, kuna wakati daktari atakushauri kupata madini ya ziada. Watu wenye matatizo ya kiafya ya aina fulani au wanaotumia aina fulani ya dawa wanaweza kutakiwa kutumia kiasi kidogo cha madini ya aina fulani. Kwa mfano, watu wenye matatizo sugu ya figo wanatakiwa kupunguza chakula chenye madini ya potassium.

Kazi Za Madini Katika Mwili

Mwili una madini ya aina nyingi. Madini ni elementi za kikemikali ambazo hazishiriki kwenye shughuli za kikemikali, kama chuma katika sufuria au calcium ndani ya jiwe. Lakini katika mwili, calcium hutumika kujenga mifupa na meno, chuma hutumika katika kutengeneza hemoglobin ndani ya seli nyekundu za damu. Mwili hutumia chuma hiki kusafirisha oksijeni hadi kwenye seli. Madini mengine huusaidia mwili katika shughuli nyingine:

. Madini huwa ni sehemu ya tishu, kama mifupa na meno
. Madini husaidia kutunza uwiano wa asidi na besi (acid-base balance), kuweka pH ya mwili kuwa neutral
. Madini husaidia kudhibiti mlolongo wa matukio ya mwili, kama mifumo ya vimeng’enya
. Madini husaidia kutawanya misukumo ya neva na kukaza kwa misuli
. Madini husaidia utolewaji wa nishati kutoka kwenye chakula.

Electrolytes

Sodium, potassium na chloride ni madini ambayo huitwa “elektroliti.” Katika mwili hufanya kazi ya kuweka vizuri kiwango cha maji na kutoa msukumo unaofaa kati ya seli na maji yanayozizunguka. Sodium na chloride ndizo elektroliti kuu katika majimaji yanayozizunguka seli za mwili. Potassium ndiyo elektroliti kuu ndani ya seli za mwili. Chumvi ndicho chakula chenye chloride na sodium. Watu wengi hutumia sodium kupita kiwango. Wataalamu wanaamini kuwa matumizi makubwa ya chumvi huchangia tatizo la pressure.

Madini Na Sumu Za Mwili

Madini huweza kujazana ndani ya mwili, na huweza kuwa sumu na kuleta madhara. Hivyo, yafaa kufuata ushauri wa daktari kabla ya kutumia madini ya ziada.

Katika kurasa tofauti tutatoa maelezo ya kila moja ya madini yafuatayo:

. Calcium

. Iron

. Zinc

. Selenium

. Phosphorus

. Potassium

. Copper

. Magnesium

. Manganese

. Cobalt

. Iodine

. Nickel

. Fluorine

. Molybdenum

. Vanadium

. Tin

. Silicon

. Strontium

. Boron

Katika mada yetu nyingine tutazungumzia umuhimu wa vitamini katika mwili. Usisite kutoa maoni yako wala kuuliza maswali kuhusu mada hii.

Pata ushauri zaidi kwa kututumia ujumbe kupitia ukurasa huu hapa chini kwa kujaza fomu, au kututumia barua pepe kupitia promota927@gmail.com au tupigie simu ndani ya muda wa kazi kwa namba zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.