Umuhimu Wa Selenium Katika Mwili

 

 

Selenium ni madini yanayotakiwa kwa kiwango kidogo (trace mineral) na mwili na husaidia mwili katika shughuli nyingi. Inasaidia kuboresha ufahamu, kinga za mwili, na uzazi.

Kulingana na Office of Dietary Supplements (ODS), selenium inachukua nafasi kubwa katika kuendeleza shughuli za kimetaboliki za tezi ya thyroid, ujenzi wa DNA na kulinda mwili dhidi ya free radicals na maambukizo.

Kwa kawaida mwili hutunza selenium ndani ya tishu za mwili, na hasa ndani ya misuli ya mifupa, baada ya kuipata kutoka kwenye chakula chenye selenium kidogo. Chakula hiki ni pamoaja na Brazil nuts, chakula cha bahari, na nyama.

Kiasi cha selenium katika chakula kinategemeana na udongo na maji kilipooteshwa. Watu pia hujiongezea madini haya kwenye chakula walacho au kama supplements.

Faida Za Selenium

Seleniun inaweza kuhusika kwenye sghughuli kadhaa za afya ya mwili, ingawa bado wanasayansi wanaendelea na utafiti zaidi.

Magonjwa Ya Moyo

Kulingana na ODS selenoproteins zinaweza kuwa na faida kwa afya ya moyo kwa kuzuia madhara ya oksijeni kwenye lipids,au mafuta ya mwili. Hii inaweza kusaidia kupunguza uvimbe (inflammation) na kujijenga kwa platelets.

Kushuka Kw Ufahamu

Tabia ya selenium ya antioxidant inawaweza kupunguza kudhoofika kwa ufahamu kunakotokana na umri na madhara mengine yabnayotokana na hali mabaya za kiafya ka ma ugonjwa wa Alzheimer’s.

Matatizo Ya Tezi Ya Thyroid

Selenium inachukua nafasi kubwa katika kutunza utendaji wa kiafya wa tezi ya thyroid.

Utafiti wa International Journal of Endocrinology na Nature Review Endocrinology unashauri kuwa kupata kiwango kizuri cha selenium kunaweza kuusaidia mwili kuzuia matatizo ya taezi ya thyroid. Hii inaonekana kuwa ni kweli zaidi hasa kwa wanawake.

Saratani

Kuhusika kwa selenium katika ukarabati wa DNA maana yake inaweza kusaidia katika kuzuia saratani, lakini itategemea aina ya selenium na aina ya saratani ambayo mtu anayo, kulingana na uatafiti wa 2016.

Faida Nyingine

Tafiti nyingine zinaonyesha kuwa selenium inaweza kusaida kuzuia HIV kuendelea kuwa AIDS na kupunguza uwezekano wa mimba kutoka (miscarriage).

Wanasayansi wnashauri pia kuwa viwango vya selenium wakti wa ujauzito vinahusika katika kutokea kwa pumu ya utotoni.

Chakula Chenye Selenium

Selenium inapatikana kwa wingi ndani ya nafaka nzima na mazao ya yanayotokana na samaki na mayai. Kiwango cha selenium katika nafaka au chakula kinachotokana na nafaka kinategemea udongo ambako nafaka zilioteshwa.

Chakula kifuatacho ni chanzo kizuri cha selenium:

. Brazil nuts: Aunsi moja inatoa microgramu 544, au asilimia 989 ya kiwango kinachoshauriwa kwa siku
. Tuna: Aunsi tatu, za kuokwa, zina microgramu 92, au asilimia 167 ya kiwango kinachoshauriwa kwa siku
. Baked halibut: Aunsi tatu, za kuokwa, zina microgramu 47, au asilimia 85 ya kiwango kinachoshauriwa kwa siku
. Cooked brown rice: kKikombe kiomja kina microgramu 19
. Yai: Yai moja kubwa lina mcg 15
. White bread: slesi moja ina mcg 10.

Kiwango Kinachoshauriwa

Kiwango cha selenium kinachoshauriwa kwa siku ni mcg 55 kwa watu wazima walio wengi. Wakati wa ujauzito mtu anatakiwa apate mcg 60, na wakati wa kunyonyesha, wanatakiwa kupata mcg 70 kwa siku.

Upungufu wa selenium huonekana mara chache sana, na huchukua muda mrefu kutokea. Unaweza kutokea tu kwenye maeneo yeenye udongo wenye upungufu mkubwa wa selenium, kama katika baadhi ya majimbo katika nchi ya China.

Matatizo Ya Afya Yanayoweza Kutokea

Kiwango cha juu cha selenium katika mwili ni mc 400 kwa watu wazima. Ni m=nadra sana mtu kupata kiasi kikubwa zaidi ya hicho, na hasa kutokana na kula chakula chenye selenium.

Lakini, viwango vya kupitiliza kutoka kwenye supplements vinaweza kuleta madhara. Madhara hayo ni pamoja na:

. harufu inayofanana na ya kitunguu ukipumua na ladha ya chuma mdomoni
. kucha ngumu za kuvunjika kirahisi
. meno kuoza
. matatizo ya mfumo wa mmeng’enyo wa chakula, kama kichefuchefu
. matatizo ya neva
. uchovu na hasira
. madonda na mikwaruzo
. kupunyuka nywele

Katika hali mbaya zaidi, selenium nyingi mno inaweza kusababisha kufeli kwa figo, kufeli kwa moyo, na kifo.

Supplements Za Selenium

Watu wanaweza kupata selenium kupitia multivitamins na supplements nyingine. madini haya hupatikana katika miundo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na selenomethionine na sodium selenate.

Mada yetu nyingine itachambua umuhimu wa iodine katika mwili. Usisite kuuliza maswali kuhusu mada yetu ya leo.

 

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu ndani ya saa za kazi kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

 

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.