Vidonda Vya Tumbo Ni Ugonjwa Gani?

 

Vidonda vya tumbo (Peptic Ulcers) ni ugonjwa unaompata mtu ambapo kunatokea vijitundu au michubuko katika kuta za ndani za viungo vya mfumo wa uyeyushaji chakula. Michubuko hiyo huweza kutokea katika eneo la mfuko wa tumbo, katika duodenum au katika eneo la koo. Inakadiriwa kuwa asilimia 5 hadi 10 ya watu hupatwa na ugonjwa huu angalau mara moja katika maisha yao. Vidonda vya tumbo ni ugonjwa ambao unaweza kumrudia mtu baada ya kupona endapo chanzo chake hakikudhibitiwa. Kama ugonjwa huu utamrudia mgonjwa , mtu huyu atakuwa amejiweka kwenye hatari kubwa ya kupata madhara makubwa zaidi kama kutokwa na damu au kutokea tundu kubwa katika kuta za mfuko wa tumbo.

 Chanzo Cha Vidonda Vya Tumbo

Bacteria: Chanzo kikubwa cha ugonjwa wa vidonda vya tumbo ni bacteria waitwao Helicobacter pylori (H. pylori). Bacteria hawa huenezwa kwa kula chakula na kunywa maji. Katika mwili wa binadamu bacteria hawa wapo katika mate na katika ute unaotanda juu ya kuta za duodenum na mfuko wa tumbo.

wadudu wa vidonda vya tumbo

Vidonda vya tumbo mara nyingi husababishwa na maambukizi ya Helicobacter pylori (H.pylori) ambaye ni bakteria au kwa kutumia anti-inflammatory drugs (NSAIDs), kama ibuprofen na aspirin.

Vitu hivi huharibu ulinzi wa tumbo dhidi ya tindikali inayotengenezwa ili kumeng’enya chakula., hivyo kuruhusu utando laini wa juu ya tumbo kuharibiwa na kujenga vidonda.

H.Pylori

Ni kitu cha kawaida kuwa na bakteria huyu aitwaye H.pylori, na kwa kawaida haleti madhara kwa walio wengi. Lakini kuna wakati anaweza kusababisha vidonda ndani ya tumbo au kwenye eneo la duodenum. Haijaeleweka wazi ni kwa nini baadhi ya watu wanaathirika kuliko wengine.

H. pylori hushambulia utando laini unaolinda tumbo. Bakteria huyu hutengeneza kumeng’enya kiitwacho urease. Kimeng’enya hiki hufanya tindikali za ndani ya tumbo kupungua nguvu yake (neutralizes them). Hii huudhoofisha utando wa juu ya tumbo.

Seli za tumbo sasa zinawekwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kuharibiwa na tindikali ya tumboni na pepsin, vyote vikiwa ni vimeng’enya vyenye nguvu. Hali hii huweza kuleta vidonda ndani ya tumbo au kwenye eneo la duodenum.

Bakteria wa H. pylori anaweza kunata kwenye seli za tumbo. Tumbo lako halina uwezo mkubwa wa kujilinda. Eneo hili hugeuka jekundu na huvimba.

H. pylori pia anaweza kusababisha tumbo kutengeneza tindikali nyingi zaidi. Wataalamu hawajajua kwa nini hili hutokea.

Anti-inflammatory Medicines (NSAIDs)

NSAIDs ni madawa yanayotumika sama kwa ajili ya maumivu, homa na uvimbe.

Dawa hizo ni pamoja na:

. ibuprofen
, aspirin
. naproxen
. diclofenac

Watu wengi wanaweza kuzitumia dawa hizi bila madhara. Lakini kuna uwezekano wa kupata nadhara, kama vidonda vya tumbo, hasa zinapotumika kwa muda mrefu au kwa dozi kubwa.

Paracetamol inaweza kutumika kama dawa mbadala kwa ajili ya maumivu.

Matumizi ya madawa haaya huweza husababisha vidonda vya tumbo.  Dawa hizi hupunguza uwezo wa tumbo wa kutengeneza utando wa ute wa kulikinga tumbo ( gastric mucosa) hivyo kulifanya liweze kuliwa kirahisi zaidi na tindikali. Dawa hizi pia hupunguza mtiririko wa damu kuelekea kwenye eneo la tumbo hivyo kupunguza uwezo wa tumbo wa kukarabati seli zilizoharibika.

 Urithi: Ugonjwa huu wa vidonda vya tumbo umeonyesha kuwa ni wa kurithishwa kwani wagonjwa wengi walibainika kuwa na ndugu wengi ambao wanaugua pia ugonjwa huu.

 Pombe Na Tumbaku: Watu wanaokunywa pombe na wale ambao wanatumia tumbaku wanakuwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kuupata ugonjwa huu wa vidonda vya tumbo.

 Msongo Wa Mawazo: Haijabainishwa moja kawa moja kwamba msongo wa mawazo unaweza kusababisha vidonda vya tumbo, bali mtu mwenye vidonda vya tumbo atakuwa na hali mbaya zaidi pale atakapokuwa na msongo wa mawazo.

Dalili Za Vidonda Vya Tumbo

Maumivu Ya Tumbo: Dalili ya kwanza kabisa ya ugonjwa huu ni maumivu ya tumbo ambayo yanaongezeka pale tindikali inapogusa eneo lililoathirika. Maumivu haya yanaweza kutokea sehemu yoyote kuanzia eneo la kitovuni hadi kwenye mifupa ya mabega na yanaweza kuchukua muda mfupi au kuendelea kwa saa chache. Maumivu husikika zaidi wakati tumbo ni tupu, yaani kama hujala, na huwa makali zaidi nyakati za usiku. Maumivu hupungua kwa muda mfupi baada ya kula chakula. Mgonjwa anaweza kupata nafuu kwa siku au wiki chache halafu maumivu humrudia tena.

vidonda vya tumbo

Madhara Ya Vidonda Vya Tumbo

 Matatizo Wakati Wa Kumeza: Mtu mwenye vidonda vya tumbo hupata matatizo pale anapojaribu kumeza chakula au hujisika vibaya mara baada ya kupata chakula.

 Kutapika: Dalili nyingine ya tatizo la vidonda vya tumbo ni kujisikia kutapika au kutapika baada ya kupata chakula.

 Kukonda: Mtu mwenye vidonda vya tumbo hukosa hamu ya kula chakula na hukonda.

Dalili za ugonjwa huu  huweza kuwa mbaya zaidi kama vile kutapika damu, kutoa haja kubwa yenye rangi nyeusi au iliyochanganyikana na damu nyeusi na kusikia kichefuchefu.

Vipimo Na Uchunguzi Wa Vidonda Vya Tumbo

Kuna vipimo vya aina mbili vya kuchunguza vidonda vya tumbo. Vipimo hivi huitwa upper endoscopy na upper gastrointestinal (GI) series.

Upper endoscopy

Katika kipimo hiki dakatri ataingiza kibomba kirefu chenye kamera kupitia umio hadi kwenye tumbo na utumbo mdogo ili kuona eneo lenye vidonda. Njia hii inatumika pia kuchukua sampuli ya tishu kwa ajili ya uchunguzi.

Si kila wakati njia hii hutumika. Njia hii hutumika kwa watu wenye uwezekano mkubwa wa kupata vidonda vya tumbo. Hii ni pamoja na watu wenye umri wa kuanzia miaka 45, au watu wanaosikia yafuatayo:

. upungufu wa damu
. kukonda
. kutoka damu kwenye tumbo
. shida kumeza

Upper GI

Kama hupati shida ya kumeza, daktari anaweza kushauri kipimo cha GI. Katika kipimo hiki, dakatri atashauri unywe namna ya uji mzito uitwao barium (barium swallow). Kisha fundisanifu atachukua X-ray ya tumbo lako, umio, na utumbo mdogo. Uji huu utamsaida daktari kutazama na kutibu vidonda vyako vya tumbo.

Kwa sababu H. Pylori ni moja ya vyanzo vya vidonda vya tumbo, daktari pia atachukua vipimo ili kuona bakteria hawa katika tumbo lako.

Madhara Yatokanayo Na Vidonda Vya Tumbo

Vidonda vya tumbo abavyo havikutibiwa vinaweza kuwa vibaya zaidi baada ya muda. Vinaweza kusababisha hali mbaya zaidi za kiafya kama:

. Matundu: Tundu linaweza kutokea kwenye ukuta wa tumbo au utumbo mdogo na kusababisha maambukizo. Dalili ya kutoboka kwa kidonda ni, maumivu makali ya ghafla.

. Kuvuja damu ndani: Vidonda vay tumbo vinavyovuja damu huweza kusababisha upotevu mkubwa wa damu na hivyo kuhitaji kulazwa. Dalili za kuvuja kwa damu ni pamoja na kizunguzungu, na choo kikubwa chenye rangi nyeusi.

. Makovu: Hizi ni tishu nene zinazotokea baada ya kuumia. Tishu hizi hufanya chakula kupita kwa shida kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. Dalili za makovu ni kutapika na kupungua uzito.

Madhara yote hapo juu ni mabaya na yanaweza kuhitaji upasuaji. Tafuta ushauri wa haraka endapo utaona dalili zifuatazo:

. maumivu makali ya ghafla ya tumbo
. Kuzimia, jasho kali, au kuchanganyikiwa
. Damu ukitapika au ndani ya choo kikubwa
. Tumbo lenye maumivu makali hata kwa kugusa tu
. maumivu makali ya tumbo yanayozidi ukitembea na kupungua ukijilaza

 Tiba Ya Vidonda Vya Tumbo

Tiba ya vidonda vya tumbo hutolewa kulingana na chanzo kilichosababisha ugonjwa huo kama ni bacteria au matumizi ya dawa. Lengo kubwa ni kupunguza makali ya tindikali katika tumbo ili vidonda vipone au kuua bacteria wanaosababisha ugonjwa huu.

 1. Dawa za Kuua bacteria (antibiotics) wa H. pyroli

Kama daktari atagundua kuwepo wa bacteria wa  aina ya H. pyroli katika mfumo wako wa uyeyushaji chakula, atakuandikia mchanganyiko wa dawa za kuua bacteria hao ambazo utazitumia kwa kipindi cha angalau wiki mbili pamoja na dawa nyingine za kupunguza tindikali katika tumbo.

 2. Dawa za kuzuia utengenezaji wa tindikali na kusaidia uponyaji

Dawa hizi ambazo huitwa Proton Pump Inhibitors (PPIs) hupunguza tindikali katika tumbo kwa kuzuia ufanyaji kazi wa seli zinazohusika katika kutengeneza tindikali. Dawa hizi ni kama omeprazole (Prilosec), lansoprazole (Prevacid), rabeprazole (Aciphex), esomeprazole (Nexium) na pantoprazole (Protonix).

3. Dawa za kupunguza utengenezaji wa tindikali

Dawa hizi huitwa acid blockers au histamine (H-2) blockers. Hizi ni dawa zinazofanya kazi kwa kupunguza kiwango cha tindikali itakayoingizwa kwenye mfumo wa uyeyushaji chakula hivyo kupunguza maumivu na kusaidia uponyaji. Mfano wa dawa hizi ni ranitidine (Zantac), famotidine (Pepcid), cimetidine (Tagamet) na nizatidine (Axid).

 4. Matumizi ya antacids kupunguza makali ya tindikali

Dawa hizi hupunguza makali ya tindikali ambayo tayari ipo ndani ya tumbo na kumpa mgonjwa nafuu ya mara moja. Dawa hizi si za kuponya ugonjwa huu bali kukupa nafuu ya muda mfupi tu.

 5. Dawa za kulinda kuta za mfuko wa tumbo na utumbo mwembamba

Wakati mwingine daktari anaweza kukupa dawa za kulinda kuta za tumbo lako na utumbo mwembamba. Dawa hizi huitwa cytoprotective agents, nazo ni kama sucralfate (Carafate), misoprostol (Cytotec) na bismuth subsalicylate (Pepto-Bismol).

Namna Ya Kuzuia Vidonda Vya Tumbo

Baadhi ya tabia na uchaguzi wa staili za maisha vinaweza kusaidia kuzuia vidonda vya tumbo. Hivi ni pamoja na:

. Kunywa pombe kwa kiwango kinachostahili
. Kutochanganya pombe na dawa
. Kuosha mikono kila wakati kuzuia maambukizo
. Kutumia dawa kwa uangalifu; dawa kama ibuprofen, aspirin, na naproxen (Aleve)

Kuacha kuvuta sigara na kula chakula chenye uwingi wa matunda, mboga, na nafaka nzima kutasaidia kuzuia kupatwa na vidonda vya tumbo.

vidonda vya tumbo

Mada yetu ya leo imeeleza maana ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo na vyanzo vya ugonjwa huo. Tukazungumzia dalili za kuweza kutambua kama unaumwa vidonda vya tumbo. Na mwisho tukaoorodhesha dawa za vidonda vya tumbo. Matumaini yetu ni kwamba umejifunza na kuuelewa ugonjwa huu vizuri. Katika mada yetu ijayo tutazungumzia ugonjwa wa stroke na kuona unasababishwa na nini. Usikose kuwa nasi.

Tunaomba usisite kutoa maoni yako kuhusu uandishi wa mada hii au kutoa maswali uliyo nayo. Ni furaha yetu kuona kwamba tumekujibu vizuri pale ulipokuwa na swali.

 

tiba ya vidonda vya tumbo

 

Kama una tatizo la ugonjwa huu na bado hujapata tiba kamili,  tupigie simu ndani ya saa za kazi kwa namba  zifuatazo:

Simu 0655 858027 na 0756 181651 au jaza fomu utakayoiona chini kwenye ukurasa huu.

 

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.