Ugonjwa Wa Tonsils Ni Nini?

 

mafindofindo

 

Tonsils ni vibonge viwili vya tishu vilivyo nyuma ya koo. Tonsils ni sehemu ya mfumo wa kinga za mwili na hufanya kazi ya uchuchaji, zinanasa vijidudu na viini vya maradhi ambao wangeweza kupita kwenye njia ya hewa na kuleta maradhi. Pia hufanya kazi ya kutengeneza kingamwili (antibodies) za kupambana na maambukizo. Wakati mwingine, tonsils huzidiwa na virusi na bakteria hali ambayo inaweza kusababisha zivimbe. Hali hii huleta ugonjwa wa uitwao mafindofindo au tonsilitis.

Ugonjwa huu ni wa kawaida, na hasa kwa watoto. Ugonjwa si mbaya sana. Watu wengi huweza kupona katika siku chache hata kama hawakutumia dawa. Dalili nyingi za ugonjwa huu hupotea zenyewe katika siku 7 hadi 10.

Sababu Za Ugonjwa Wa Mafindofindo -Tonsilitis

Tonsils ni kinga ya mwanzo kabisa ya mfumo wa kinga za mwili dhidi ya bakteria na virusi waingiao mdomoni. Hii ndiyo sababu tonsils huwa kwenye hatari kubwa ya maambukizo na kuvimba. Lakini, kinga za mwili zitolewazo na tonsils hupungua nguvu mtu akifikia balehe -sababu inayofanya watu wazima kuupata ugonjwa wa mafindofindo mara chache sana.

 

ugonjwa wa mafindofindo

 

Kimsingi mafindofindo husababishwa na virusi. Mara chache bakteria nao wanaweza kuhusika. Mafindofindo yaliyobabishwa na bakteria au virusi huweza kuambukiza kutoka mtu mmoja kwenda mwingine. Lakini, tonsils iliyosababishwa na ugonjwa mwingine, kama sinusitis au hay fever, si rahisi sana kuambukiza.

Mafindofindo Yatokanayo Na Virusi

Maambukizo ya virusi ndiyo sababu kubwa ya ugonjwa wa mafindofindo. Aina za virusi wanaohusika kuleta maambukizo kwenye tonsils ni:

. adenovirus, ambao wanaaminika kuleta mafua na kukauka kwa koo
. rhinovirus, ambayo ndiyo sababu kubwa ya mafua
. influenza au flu virus
. respiratory syncytial virus, ambayo huleta magonjwa ya mfumo wa upumuaji
. aina ndogo mbili za coronavirus, moja ndiyo iletayo SARS

Mara chachea sana, wafuatao wanaweza kuleta viral tonsilitis:

. Epstein-Barr virus (EBV)
. Herpes simplex virus (HSV)
. cytomegalovirus (CMV)

Mafindofindo Kutokana na Bakteria

Bakteria ambaye mara nyingi hushambulia tonsils ni Streptococcus pyogenes. Lakini, mara chache bakteria wengine wanaweza kuhusika, ambao ni:

. Staphylococcus aureus
. Mycoplasma pneumonia
. Chlamydia pneumonia
. Bordetella pertussis
. Fusobacterium
. Neisseria gonorrhoeae

Dalili Za Ugonjwa Wa Mafindofindo (Tonsilitis)

Dalili zinazotokea mara nyingi za mafindofindo ni:

. kukauka koo na maumivu wakati wa kumeza
. tonsils nyekundu zilizovimba na alama za usaha
. homa
. shida kumeza
. maumivu masikioni na shingoni
. kuchoka
. shida kupata usingizi
. kukohoa
. kusikia baridi
. kuvimba kwa tezi.

Dalili za mara chache ni kama:

. unyong’onyevu
. maumivu ya tumbo na kutapika
. kichefuchefu
. utando kwenye ulimi
. mabadiliko ya sauti
. harufu mbaya kinywani
. shida kufunua mdomo.

Watu wenye tonsilitis wanaweza wakawa na tonsil stones, ambayo madaktari huita tonsilloliths au tonsillar calculi ambayo hutokana na kujijenga kwa vitu vya calcium kwenye nyufa za tonsils. Mawe haya ni madogo lakini aghalabu huweza kuwa makubwa kiasi. Mawe yanaweza kuleta shida katika kuyaondoa lakini huwa hayana madhara.

Tiba Ya Mafindofindo

Kama bakteria wanasababisha mafindofindo, daktari atakuandikia antibiotics. Antibiotics hazifanyi kazi dhidi ya virusi. Penicillin ndiyo antibiotic inayotumika zaidi. Mtu akiwa kwenye dozi ya antibiotic anatakiwa aimalize hata kama dalili zinaonekana kwisha. Kusimamisha dozi katikati kunaweza kuruhusu maambukizo kusambaa.

Kuziondoa Tonsils

Hapo zamani, madaktari walikuwa wanashauri upasuaji wa kuziondoa tonsils. Lakini siku hizi, daktari hatashauri tonsillectomy labda hali ikiwa sugu au ya kujirudirudia.

Pamoja na kwamba tonsils hazina kazi sana mwilini ukifikia balehe, bado zina kazi fulani. Kwa hiyo daktari hataziondoa, labda kwa sababu maalumu.

Daktari anaweza kushauri upasuaji endapo kuna yafuatayo:

. sleep apnea, ambayo ni matatizo ya kupumua usiku
. kuna matatizo ya kupumua au kumeza
. kuna usaha ambao hautibiki kirahisi
. tonsillar cellulitis, ambayo sehemu iliyoathiriwa inapanuka kuelekea maeneo mengine na kujenga usaha nyuma ya tonsils.

Katika ukurasa mwingine tutaujadili ugonjwa wa kukoroma usiku. Tafadhali usisite kutoa maoni yako au kuuliza maswali kuhusu somo letu la leo. Ni furaha kwetu kukujibu.

 

Pata ushauri zaidi kwa kututumia ujumbe kupitia ukurasa huu hapa chini, kwa kujaza fomu, au kututumia barua pepe kupitia promota927@gmail.com au tupigie simu ndani ya  saa za kazi kwa namba zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

 

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.