Ugonjwa Wa Rheumatoid Arthritis

 

rheumatoid arthiritis mgonjwa

Rhematoid arthritis (RA) ni ugonjwa wa kinga za mwili (autoimmune disease) ambapo kinga za mwili – ambazo kazi yake ni kuulinda mwili kwa kushambulia vitu vinavyouvamia mwili kutoka nje kama bakteria na virusi – kwa bahati mbaya hushambulia maungio ya mifupa. Hii huleta madhara ambayo husababisha tishu ambazo zinatanda kwenye maungio ya mifupa kwa ndani (synovium) kuongezeka unene, na kusababisha kuvimba na maumivu kwenye maungio ya mifupa. Synovium hutengeneza ukano (ute) ambao hulainisha maungio ya mifupa na kuisaidia kufanya miondoko kiulaini.

rheumatoid arthiritis kwenye vidole

Hatua zipaswazo zisipochukuliwa kuidhibiti hali hiyo, gegedu huweza kuharibiwa pamoja na mifupa yenyewe. Hatimaye, gegedu huisha kabisa, na nafasi kati ya mifupa huwa ndogo. Maungio ya mifupa inaweza kuwa legelege, isiyo imara, kuleta maumivu na kusababisha kushindwa kucheza. Umbo la maungio hayo ya mifupa huweza kuharibika. Umbo la maungio ya mifupa haliwezi kukarabatiwa.

Kwa baadhi ya watu, ugonjwa huu huweza kuharibu idadi kubwa ya mifumo ya mwili, ikiwa ni pamoja na; ngozi, macho, mapafu, moyo na mishipa ya damu.

Chanzo Cha Rheumatoid Arthritis

Rhematoid arthritis hutokea pale kinga za mwili zinapoishambulia synovium – utando wa ngozi laini unaozunguka maungio ya mifupa.

Mashambulio hayo husababisha synovium kuwa nene, ambayo baadaye huharibu gegedu na mfupa ndani ya maungio hayo.

rheumatoid arthiritis chanzo

Tendoni na ligamenti zinazoyashikilia maungio, hudhoofu na kuvutika. Taratibu maungio huanza kupoteza umbo lake na ukaaji wake.

Chanzo cha mlolongo wa matukio hayo bado hakijaeleweka vizuri, ingawa madaktari wanajua kuwa kinga za mwili zina nafasi kubwa katika kuleta uvimbe na uharibifu wa maungio haya ya mifupa. Hakuna ajuae kiusahihi kwa nini kinga zinafikia kufanya ndivyo sivyo, lakini utafiti wa kisayansi unaonyesha kuwa jeni, homoni na mazingira vinahusika.

Vitu Vinavyoongeza Uwezekano Wa Kupata Rhematoid Arthritis

Baadhi ya vitu vimeonyesha kuongeza uwezekano wa kupata RA, navyo ni:

. Jinsia. Wanawake wameonyesha kupata RA zaidi ya wanaume

. Umri. RA inaweza kutokea kwenye umri wo wote, lakini zaidi kwa watu wa umri wa kati ya miaka 40 na 60

. Urithi. Kama una ndugu mwenye RA, basi uwezekano wa wewe pia kupata ni mkubwa

. Uvutaji wa sigara. Uvutaji wa sigara huongeza yamkini ya kupata RA

. Mazingira. Baadhi ya mazingira kama ya asbestos au silica yanaweza kuongeza uwezekano wa kupata RA

. Unene. Watu wanene wanaonyesha kupata zaidi RA, na hasa wanawake.

Madhara Ya Rheumatoid Arthritis

Rheumatoid arthritis inaongeza hatari ya kupata:

. Osteoporosis
. Rheumatoid nodules
. Kukauka macho na midomo.
. Maambukizi.
. Abnormal body composition.
. Matatizo ya moyo.
. Magonjwa ya mapafu.
. Lymphoma.

Dalili Za Rheumatoid Arthritis

Dalili za rheumatoid arthritis ni pamoja na:

rheumatoid arthiritis magoti

. Maumivu, joto na kuvimba kwenye maungio ya mifupa

. Kukakamaa kwa maungio hasa asubuhi au baada ya kujipumzisha

. Uchovu, homa na kukonda

. Wekundu

. Kuchechemea

. Kubadilika kwa umbo la eneo la maungio ya mifupa

. Kupungua kwa kukunjuka kwa maungio

. Kupungua damu

Rheumatoid arthritis katika hatua za mwanzo huathiri maungio madogo – hasa maungio ya vidole na mikono na vidole vya miguu na miguu.

Ugonjwa unapoongezeka, huenea kwenye viwiko, magoti, vifundo vya miguu, vifundo vya mikono, nyonga na mabega. Mara nyingi, dalili hutokea kwenye viungo vya pande zote kwa wakati mmoja.

rheumatoid arthiritis miguu

Asilimia 40 ya wagonjwa wa RA huona dalili nyingine ambazo hazihusu maungio ya mifupa. Rheumatoid arthritis inaweza kuathiri:

. Ngozi
. Macho
. Mapafu
. Moyo
. Figo
. Tezi za mate
. Tishu za neva
. Uboho
. Mishipa ya damu

Dalili za RA huweza kuja na kupotea. Vipindi vya ugonjwa mzito hupishana na vipindi vya kujikia vizuri. Hatimaye, RA huweza kusababisha viungo kupoteza maumbo ya asili na kuhama sehemu ya asili.

Ugonjwa huu wa rheumatoid arthritis huwaanza zaidi watu walio kwenye umri wa kati ya miaka 30 na 60. Kwa wanaume, ugonjwa huu huwaanza kwenye umri mkubwa zaidi. Ukiwa na mtu wa ukoo wako mwenye rheumatoid arhritis, waweza pia kuupata, lakini watu wengi wanaougua ugonjwa huu hawana historia ya ugonjwa huu kwenye koo zao.

Vipimo Vya Rheumatoid Arthritis

Hakuna kipimo kimoja cha kubainisha kwamba una RA au la. Daktari wako atakuchunguza, atakuuliza kuhusu dalili unazoziona, na pengine kuchukua vipimo vya  X-Ray na damu.

Rheumatoid arthritis inagundulika kwa kuchunguza vitu vingi, vikiwemo:

  • Eneo la joint na uwiano wake na viungo vingine, na hasa joints za mikono
  • Kukakamaa kwa joints asubuhi
  • Vijiuvimbe chini ya ngozi (rheumatoid nodules)
  • Matokeo ya vipimo vya X-Ray na damu

Tiba Ya Rheumatoid Arthritis

Malengo ya kutibu ugonjwa wa rheumatoid arthritis ni :

. Kuondoa maumivu
. Kuondoa dalili
. Kuzuia uharibifu wa maungio ya mifupa na viungo vingine
. Kuboresha utendaji kazi wa viungo
. Kuondoa madhara ya kudumu

Kufikia malengo haya, dakatari atatoa tiba kulingana na hali ya mgonjwa.

Mazoezi. Mazoezi yana faida sana kwa mgonjwa wa RA na huchukuliwa kama kipengele cha kwanza katika tiba yake. Mpango wa mazoezi uhusishe mazoezi laini ya aerobics, mazoezi ya kukomaza misuli na mazoezi ya mnyumbuliko.

Virutubishi. Utafiti umeonyesha kuwa matumizi ya tumeric na omega-3 oil yanasaidia kuondoa maumivu ya RA na kukakamaa misuli asubuhi.

deep sea fish oil

Katika mada nyingine tutazungumzia ugonjwa gout. Usisite kutoa maoni yako kuhusu mada yetu ya leo au kuuliza maswali uliyo nayo

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.