Ugonjwa Wa Kichocho Ni Nini?

 

 

Kichocho ni ugonjwa unaotokana na maji ambao huwapata zaidi wavuvi, wakulima, watoto wanaocheza kwenye maji uasiyo salama, na watu ambao wanatumia maji yasiyo salama kila siku. Kitaalamu ugonjwa huu huitwa schistosomiasis au bilharzia. Baina ya magonjwa yanayotokana na vimelea, ugonjwa huu unachukua nafasi ya pili duniani kwa kuleta maafa baada ya malaria.

Kichocho ni ugonjwa unaopatikana kwenye nchi za tropiki na huathiri watu takribani milioni 240 katika dunia. Ugonjwa huenezwa na minyoo waitwao schistomes. Minyoo hawa huishi ndani ya maji, kwenye mito na maziwa. Kuna aina (species) kuu tatu za schistosome ambao husababisisha kichocho kwa binadamu:

. Schistosoma haematobium
. Schistosoma mansoni
. Schistosoma japonicum

Aina nyingine za schistosome huleta magonjwa kwa wanyama. Kwa mfano, Schistosome bovis hushambulia ng’ombe.

 

Dalili Za Kichocho Ni Zipi?

 

. Dalili za kichocho husababishwa na kinga za mwili kupambana na mayai ya schistosome

. Mayai huweza kukaa kwenye eneo lo lote la mwili na kusababisha uvimbe. Hali hii huweza kusababisha kutokea kwa chembe ndogo (granulomas) na kusababisha tishu kuwa za nyuzinyuzi (fibrosis.) Hali hii huwezakusababisha dalili mbalimbali kulingana na eneo lililoathiriwa.

. Kichocho huweza kuwa ni ugonjwa mkali wa ghafla (acute) au ukawa ni ugonjwa sugu (chronic.)

. Ikiwa ni acute schostosomiasis, dalili zinazotokea husababishwa na kinga za mwili kupambana na kimelea na kwa kawaida huwa ni wa muda mfupi.

. Dalili za acute schistosomiasis huweza kutokea wiki chache baada ya kimelea kujipenyeza kwenye ngozi ya mgonjwa. Dalili hizi hutokea mayai ya kwanza ya kimelea yanaponasa ndani ya ini na bandama.

. Dalili za awali na kama mafua, yanayoendana na joto kali la mwili na kuumwa misuli, lakini wakti mwingine hutokea ukurutu, kikohozi na maumivu ya tumbo.

. Wakati mwingine dalili za acute schostosomiasis ni ndogo na hazijionyeshi.

. Kwenye maeneo ya dunia ambako huduma za afya ni duni na watu wana kinga za mwili zilizo dhaifu ugonjwa huwa huweza kuwa sugu. Maana yake ni kwamba ugonjwa unakaa kwa muda mrefu ndani ya mwili.

. Kichocho sugu hutokea miezi au miaka toka maabukizo ya awali na husababisha matatizo ya kiafya ya muda mrefu. Uharibifu wa viungo unaotokana na kichocho sugu hautibiki.

. Dalili za kichocho sugu hutokana na uvimbe na makovu ya tishu na viungo kutokana na kinga za mwili kupambana na mayai ya vimelea wa kichocho.

. Maumivu wakati wa kutoa haja ndogo -mayai ya kimelea wa kichocho yanayoziba mkondo wa mkojo husababisha uvimbe na kuleta dalili zinazofanana na maambukizo ya kwenye njia ya mkojo na kibofu. Mara chache hali hii imeendelea na kuwa kansa ya kibofu. Kwa wanawake, maabukizo sugu ya mkondo wa mkojo yanahusishwa na uharibifu wa shingo ya kizazi, mirija ya uzazi na uke.

. Damu katika mkojo – hii hutokana na kuvimba kupita kiasi kwa kibofu cha mkojo kutokana na mayai yaliyomo ndani ya mishipa ya damu ya kuta za kibofu.

. Kuharisha kukiwa na damu -nayai ya kumelea wa kichochohuweza kukaa ndani ya mishipa ya damu ya utumbo na kusababisha uvimbe, na, hatimaye, kuharisha.

. Maumivu ya kifua -hii hutoana na lava wa kimelea wa kichocho kutembea katika tishu za mapafu na baadaye mayai kunasa katika mishipa ya damu ya kwenye mapafu. Hii husababisha uvimbe, kutokea kwa granuloma na makovu.

. Kufeli kwa ini -kinga za mwili zikipambana na mayai ya kimelea yaliyomo ndani ya mishipa ya damu ya ini granuloma na makovu hutokea. Hali hii huweza kusababisha ini kushindwa kufanya vizuri kazi yake na kusababisha sumu kujaa ndani ya mwili.

. Viungo kugoma (kama kiharusi) na kupooza -hii inaweza kusababishwa na mayai ya kimelea kukwama ndani ya uti wa mgongo au ubongo, na kusababisha uvimbe.

. Watoto wnaoshambuliwa mara kwa mra na vimelea wa kichocho huweza kupugukiwa damu, kupata utapiamlo na matatizo ya kujifunza.

. Kichocho huwapata zaidi watu wa umri wa kati ya miaka 15-20.

. Kadiri umri unavyozidi kuwa mkubwa, ingawa uwezekano wa maambukizi unabaki pale pale, idadi ya vimelea ndani ya mwili hupungua.

 

Mzunguko Wa Maisha Wa Kimelea Wa Kichocho – Life Cycle of Schistosomas

 

 

. Mayai ya kimelea hudondoshwa ndani ya maji kupitia mkojo au kinyesi cha mtu mwenye maambukizo.

. Mayai hujiangua na lava wanaoogelea, waitwao miracidia, huenea ndani ya maji.

. Lava hawa hujificha ndani ya konokono wa kwenye maji, kama ndani ya konokono aitwaye Biomphalaria.

 

 

 

 

. Ndani ya konokono huyu, miracidia hujibadili mara kadhaa na kuwa lava waliopevuka, waitwao cercariae. Huwa hurudi majini na kuogelea wakimtafuta mwenyeji ambaye ni binadamu.

. Cercariae wakikutana na binadamu hijipenyeza kwenye ngozi. Wakati wakijipenyeza, hupoteza mikia na kugeuka schistosomulae.

. Scistosomulae hawa huingia kwenye mkondo wa damu na kupitia mapafu hadi kwenye maini ambako hukua na kuwa minyoo waliokua.

. Mnyoo mkubwa huambatana na mnyoo wa jinsia tofauti na kutembea wakikinzana na mtiririko wa damu hadi kwenye mishipa ya damu ya maeneo ya tumbo, eneo la haja kubwa au kibofu cha mkojo.

. Wakifika kwenye mishipa ya damu damu ya karibu na tumbo, eneo la haja kubwa au kibofu cha mkojo huanza kutaga mayai. Karibu nusu ya mayai haya yatatolewa nje ya mwili na mkojo na kinyesi lakini yatabaki ndani ya damu na kuelekea kwenye maini na kusababisha uvimbe.

. Schistosoma mansoni na Schistosoma japonicum kwa kawaida huelekea kwenye eneo la tumbo au haja kubwa na kutoa mayai kwenye kinyesi.

. Schistosoma haematobium huelekea kwenye kibofu cha mkojo na kutoa mayai kwenye mkojo.

 

Tiba Ya Kichocho

 

. Karibu watu wote wanapata tiba ya kichocho hupata nafuu.

. Dawa ya kwanza kwa tiba ya kichocho ni praziquantel.

. Dawa ya praziquantel huleta matokeo yasiyotarajiwa (side effects) kidogo sana.

. Hutolewa kama vidonge kama dozi moja au dozi mbili kwa siku moja.

. Praziquantel huwaua moinyoo wakubwa kupoozesha misuli yao. Mabaki yao huvunjwavunjwa na mwili.

. Vimelea uweza kuuawa muda wo wote baada ya kuwa wakubwa (wiki sita baada ya maambukizo), pamoja na wagonjwa wenye maambukizo sugu.

. Kama tiba itafanywa mapema mno, wakati minyoo hawajawa wakubwa, praziquantel haisadii katika kuondoa maambukizo.

. Dawa za zamani zinatumika kutibu kichocho. Dawa hizo ni kama metrifonate, ambayo hufanya kazi vizuri dhidi ya S. haematobium, na oxamniquine, ambayo ni nzuri dhidi ya S. mansoni.

 

katika mada yetu nyingine tutauzungumzia ugonjwa wa malaria. Usisite kutoa maoni yako au kuuliza maswali kuhusu mada hii.

 

 

Pata ushauri zaidi kwa kututumia ujumbe kupitia ukurasa huu hapa chini kwa kujaza fomu, au kututumia barua pepe kupitia promota927@gmail.com au tupigie simu kwa namba zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

 

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

K