Umuhimu Wa Maji Katika Mwili

faida ya kunywa maji

Mwili wa binadamu unaweza kwenda wiki kadhaa bila chakula, lakini siku chache tu bila maji. Mwili huundwa kwa asilimia 50-75 na maji. Maji ndiyo msingi wa damu, maji-tumbo, mkojo na jasho, na yanapatikana katika misuli isiyo na mafuta, mafuta na mifupa.

Kwa vile mwili hauna uwezo wa kutunza maji, unahitaji kupata maji kila siku, kufidia maji yanayotolewa na mapafu, ngozi, mkojo na kinyesi. Kiasi kinachotakiwa kinategemea ukubwa wa mwili, shughulu za mwili za ujenzi na uvunjaji wa seli, hali ya hewa, chakula tulacho na shughuli tunazozifanya.

Maji katika Miili Yetu

Baadhi ya dondoo kuhusu maji katika mwili:

. Maji ya ndani ya mwili ni mengi zaidi katika miili ya wanaume kuliko wanawake kwa sababu miili ya wanawake ina mafuta zaidi na hupungua na umri katika jinsia zote.
. Watu wazima walio wengi hupoteza lita 2.5 hadi 3 za maji kila siku. Upotevu wa maji huongezeka wakati wa joto na ukifanya mazoezi ya muda mrefu.
. Watu wenye umri mkubwa hupoteza lita 2 za maji kwa siku
. Mtu anayesafiri angani anaweza kupoteza maji hadi lita 1.5 kwa saa tatu za kuwa angani.
. Maji yaliyopotea yanatakiwa kurudishiwa.
. Wakati asilimia ya wastani ya maji katika mwili ni 60, asilimia hii inaweza kucheza kuanzia 45-75 kulingana na mwili. Kwa mfano, watoto wadogo wana asilimia kubwa zaidi ya maji katika miili yao.
. Tishu za mafuta zina maji kidogo zaidi ya misuli.

Majedwali yafuatayo yanaonyesha asilimia za wastani na viwango vya maji katika mwili, kulingana na jinsia na umri.

 

Maji Hupatikana Wapi Katika Mwili?

Maji hupatikana sehemu zote za mwili. Seli zina asili,ia 60 ya maji yote ya mwili, na karibu theluthi moja ya maji yaliyosalia, huzunguka seli.

Baadhi ya viungo vina maji zaidi ya vingine. Ubongo na figo ndivyo vyenye asilimia kubwa zaidi ya maji, mifupa na meno ndivyo vyenye asilimia ndogo zaidi.

Jedwali lifuatalo linaonyesha viwango vya maji katika tishu za mwili:

 

Namna Ya Kukokotoa Asilimia Ya Maji Katika Mwili

Kuna njia nyingi za kisayansi za kukokotoa vijenzi vya mwili, ikiwa ni pamoja na asilimia ya maji.

Watu wanaweza kutumia vikokotoo vya mtandaoni kutafuta asilimia ya maji katika mwili.

Wanaweza vile vile wakatumia Watson Formula kutafuta idadi ya maji katika mwili katika lita.

Watson Formula Kwa Wanaume

2.447 x (0.09156 x umri) + (0.1074 x urefu katika sentimeta) + (0.3362 x uzito katika kilo)=uzito wa jumla (TBW) katika lita.

Watson Formula Kwa Wanawake

-2.097 + (0.1069 x urefu katika sentimeta) + (0.2466 x uzito katika kilo)=uzito wa mwili wa jumla (TBW) katika lita.

Ili kupata asilimia ya maji katika mwili, watu huchukulia kuwa lita moja ni sawa na kilo moja kwa hiyo basi gawanya TBW kwa uzito wa mwili. Hii huweza kukupa picha kama mwili wa mtu huyo upo katika kiwango kizuri cha asilimia ya maji.

Umuhimu Wa maji Katika Mwili

Maji yanahitajika katika shughuli nyingi za mwili, zikiwa ni pamoja na:

. Kutunza afya na ukamilifu wa kila seli katika mwili
. Kutunza umajimaji wa damu ili damu itiririke katika mishipa ya damu
. Kusaidia kuondoa mabaki ya utendaji kazi wa mwili, vimininika vinavyopitisha umeme vya ziada (mfano sodium na potassium), na urea ambayo ni zao la maji linalotokea wakati wa uvunjaji wa protini
. Kurekebisha joto la mwili kupitia jasho
. Kutunza utando laini (kama wa mapafu na midomo)
. Kulainisha maungio ya mifupa
. Kupunguza kutokea kwa maambukizi ya UTI, kama cystitis, kwa kuondoa bakteria ndani ya kibofu cha mkojo
. Kusaidia mmeng’enyo wa chakula na kuzuia kufunga choo
. Kudumisha unyevunyevu wa ngozi na kulinda muundo na mwonekano wake
. Kusafirisha oksijeni na virutubishi kwenda kwenye seli
. Kuzuia mishituko ndani ya macho, uti wa mgongo na ngozi inayokizunguka kichanga wakati wa ujauzito.

Maji Ndani Ya Chakula Chetu

Chakula cha aina nyingi, hata kile ambacho kwa macho kinaonekana kikavu, kina maji. Mwili unaweza kupata asilimia 20 ya mahitaji yake ya maji kutokana na chakula kigumu pekee.

Tendo la kumeng’enya chakula nalo hutengeneza kiasi kidogo cha maji kama matokeo ya ziada. ambayo yanaweza kutumika na mwili. Maji ya aina hii yanaweza kuwa asilimia 10 ya mahitaji ya jumla ya mwili.

Asilimia 70 inayobakia ya mahitaji ya mwili lazima itokane na vimininika.

Kiasi Cha Majimaji Ndani Ya Chakula Kinachopendekezwa

The Australian Dietary Guidelines wanapendekeza kuwa tunywe maji mengi lakini ni kiasi gani kinatosha?Jedwali hapa chini linaonyesha viwango vya maji kwa siku vinavyotakiwa kunywewa:

Viwango hivi toshelezi vinajumuisha majimaji ya aina zote, ingawa inashauriwa kuwa kiasi kikubwa kiwe ni maji yasiyochanganywa na kitu.

Kuna baadhi ya watu watahitaji maji pungufu ya kiasi hiki, kama:

. Wale wanaokula chakula chenye majimaji mengi (kama matunda na mboga za majani).
. Wanaoishi kwenye mazingira ya baridi
. Ambao kazi zao ni za kukaa muda mwingi.

Watu wengine wanaweza kuhitaji maji zaidi ya viwangO vilivyotajwa na watatakiwa kuongeza maji zaidi kama:

 

. Wanakula chakula chenye uwingi wa protini
. Wanakula chakula chenye uwingi wa nyuzinyuzi
. Wanatapika au wanaharisha
. Kazi zao ni za kutoa jasho
. Waliopo kwenye mazingira ya joto kali.

 

 

Namna Ya Kupata Maji Ya Kutosha Kutoka Kwenye Chakula

Kama wazo la kutakiwa kunywa vikombe vingi vya maji kwa siku ambayo hayajachanganywa linakupa shida, usijali -maji ni pamoja na yale ambayo hayajachanganywa na mengineyo (kama maziwa, kahawa, chai, supu, juisi na hata vinywaji baridi kama soda).

Maji ambayo hayakuchanganywa ndiyo bora zaidi kwa sababu hayana nishati (kilojoules) na ndiyo bora kuupa mwili maji. Maji ya bomba mara nyingi hayana vitu vingine na hupatikana kirahisi kila uendako.

Asilimia 90 ya maziwa ni maji na ni chanzo cha maji muhimu, na hasa kwa watoto.Kumbuka kutumia full-fat milk kwa watoto wa chini ya miaka 2 na aina za low-fat na reduced fat kwa makundi ya watu wengine.

Chai inaweza kuwa chanzo kizuri cha maji. Chai inaweza kukidhi mahitaji yako ya maji kwa siku na ni chanzo cha antioxidants na polyphenols, ambavyo vimeonekana kusaidia kukinga dhidi ya magonjwa ya moyo na saratani.

Kama unapendelea kupata baadhi ya mahitaji ya maji kutoka kwenye matunda, jenga tabia ya kula vipande vizima vya matunda yaliyotoka shambani badala ya kuntywa juisi ili upate pia faida ya nyuzinyuzi (fibres) na virurubishi wakati ukikwepa sukari ya ziada ndani ya juisi.

Dondoo Za Kunywa Maji Zaidi

. Kamulia au weka kipande cha limau au ndimu, au strawberries ndani ya maji safi kuongeza ladha
. Weka chupa au glasi ya maji karibu na wewe juu ya dawati au ndani ya mkoba
. Kunywa maji kila baada ya mlo au asusa
. Ongeza vipande vya barafu vya matunda ndani ya glasi yako ya maji.

Punguza Matumizi Ya Maji Ya Soda

Maji yaliyosindikwa kibiashara yana chumvi, ambayo inasababisha utunzwaji na kuleta uvimbe, na hata kuongeza pressure kwa wahanga wa tatizo hilo. Punguza matumizi ya maji ya soda au chagua maji yenye kiwango kidogo cha madini ya sodium (pungufu ya mg 30 kwa mililita 100).

Fluoride Katika Maji

Faida ya ziada ya kunywa maji ya bomba, ni kwamba fluoride huongezwa. Maji yaliyosindikwa, kwa kawaida, hayana viwango vizuri vya fluoride. Kuongeza fluoride huyafanya maji hayo kuzuia kuharibika kwa meno na hivyo kutunza afya ya meno ya kila mmoja wetu.

Kwepa Vinywaji Vyenye Sukati Au Kuongezwa Utamu

The Australian Dietary Guidelines inashauri wananchi kupunguza unywaji wa vinywaji vyenye sukari. Hivi ni pamoja na:

. Vinywaji baridi vilivyoongezwa utamu kwa sukari
. Vinywaji vya matunda
. Vitamin-style waters
. Maji yenye madini yaliyowekwa ladha
. Vinywaji vya energy na sports

Kunywa vinywaji vyenye sukari kunaongeza nishati juu ya chakula, lakini si virutubishi vingine. Kuna ushahidi wa kutosha wa kuhusisha unywaji wa vinywaji vyenye sukari na uzito wa mwili wa ziada baina ya watoto na watu wazima, vile vile kupungua kwa uimara wa mifupa na kuoza kwa meno.

Upungufu Wa Maji Katika Mwili (Dehydration)

Upungufu wa maji mwilini (dehydration) hutokea wakati maji ya ndani ya mwili ni kidogo. Hali hii huweza kurekebishwa kwa kunywa vitu vyenye maji mengi.

Dalili Za Upungufu Wa Maji Katika Mwili

Dalili za kuwa na upungufu wa maji katika mwili ni pamoja na:

. Kiu
. Maumivu ya kichwa
. Uchovu
. Mabadiliko ya mara kwa mara ya hisia na uzito wa vitendo
. Ukavu wa njia za pua
. Ukavu au kuchanika kwa midomo
. Mkojo kuwa na rangi nyeusi
. Kukosa nguvu
. Kuchanganyikiwa.

Kama upungufu wa maji hautafanyiwa kazi, mwishowe mkojo husimama kutoka, figo hufeli na mwili hauweza kutoa sumu nje ya mwili. Hali ikiwa mbaya sana, upungufu wa maji husababisha umauti.

Sababu Za Upungufu Wa Maji Mwilini

Kuna sababu nyingi za upungufu wa maji katika mwili, zikiwa ni pamoja na:

. Kutokunywa maji ya kutosha
. Kutoa jasho zaidi wakati wa hali ya joto, kupungua unyevu hewani, mazoezi au homa
. Utolewaji ishara hafifu kwa sababu ya umri -wakati mwingine watu wa umri mkubwa hawasikii kiu pamoja na kwamba mwili umepungukiwa maji
. Kuongezeka kwa utolewaji wa mkojo kutokana na upungufu wa homoni, kisukari, ugonjwa wa figo au madawa
. Kuharisha au kutapika
, Kupona baada ya kuungua.

Nani Yupo Kwenye Hatari Ya Kuwa Na Upungufu Wa Maji?

Vichanga na watoto wadogo wanaweza kuwa na upungufu wa maji kirahisi sana na hasa wakiwa wagonjwa, wanatapika, na homa na kuharisha.

Upungufu wa maji unaweza kuwa tishio la maisha kwa vichanga na watoto wadogo. Ukihisi kuna upungufu wa maji, mpeleke mwanao kwenye hospitali ya karibu mara moja.

Baadhi ya dalili za upungufu wa maji kwa vichanga na watoto wadogo ni:

. ngozi baridi
. kulegea
. mdomo mkavu
. bluu kwenye ngozi
. utosi kubonyea

Watu Wa Umri Mkubwa

Watu wa umri mkubwa huwa kwenye hatari ya upungufu wa maji kwa sababu ya:

. Mabadiliko ya utendaji wa figo
. Mabadiliko ya homoni
. Kutosikia kiu (mifumo ya mwili ya kutufanya tusikie kiu haifanyi kazi vizuri umri ukiwa mkubwa)
. Madawa (kama diuretics na laxatives)
. Magonjwa sugu
. heat stress

Kutokunywa maji ya kutosha kunaweza kusababisha kidney stones na kwa wanawake UTI. Kunaweza kusababisha kushuka kwa utendaji wa akili na mwili, na utendaji wa tezi za mate, na kusababisha upungufu wa maji mwilini.

Lakini, unajua kuwa kuna uwezekano wa kunywa maji mengi na kutokewa na hali iitwayo hyponatraemia?

Sumu Ya Maji (hyponatraemia)

Kunywa maji kupita kiasi kunaweza kuuharibu mwili na kuleta hali iitwayo hyponatraemia au sumu ya maji, ingawa ni hali ambayo huweza kutokea mara chache sana.

Hyponatraemia hutokea wakati sodium katika damu, ambayo hutakiwa kwa ajili ya kujikunja kwa misuli na kupeleka taarifa za neva, inaposhuka kufikia kiwango ambacho ni hatarishi.

Kama kiasi kikubwa sana cha maji safi kitanywewa kwa muda mfupi sana, figo hazitaweza kutoa kiasi cha maji ya kutosha kupitia mkojo na damu huwa imezimuliwa (diluted).

Hyponatraemia huweza kuleta:

. maumivu ya kichwa
. kutoona vizuri
. kubanwa kwa misuli (na baadaye mtukutiko wa maungo)
. kuvimba ubongo
. coma na pengine kifo.

Ili kuepuka kufikia hali hii ya sumu ya maji lita nyingi zitakuwa zimenywewa kwa muda mfupi sana.

Katika mada yetu nyingine, tutalizungumzia umuhimu wa madini katika mwili. Usisite kutoa maoni yako kuhusu mada yetu ya leo.

Pata ushauri zaidi kwa kututumia ujumbe kupitia ukurasa huu hapa chini kwa kujaza fomu, au kututumia barua pepe kupitia promota927@gmail.com au tupigie simu ndani ya saa za kazi kwa namba zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.