Amoeba Ni Ugonjwa Gani?

 

 

ugonjwa wa amiba

 

Amiba ni maambukizo ya kwenye utumbo mkubwa yanayosababishwa na vimelea wa seli moja (one-celled parasites) wajulikanao kama amoebas. Ugonjwa huu huitwa amoebiasis au amebic/amoebic dysentery. Kimelea mhusika ni Entamoeba histolytica au anaweza kuwa kimelea mwingine, kwa mfano, E. dispar. Kwa sababu vimelea hawa wanaishi ndani ya utumbo mpana, wanasafiri ndani ya kinyesi cha watu walioambukizwa, na kuchafua vyanzo vya maji kwenye maeneo ambako udhibiti wa maji taka ni dhaifu. Vimelea hawa wanaweza kuchafua matunda na mboga yanayolimwa na kinyesi kutumika kama mbolea. Wanaweza pia kusafirishwa na mikono ya watu wasiosafisha mikono yao mara kwa mara au wasiojisafisha kwa usahihi au hata kupitia ngono ya mdomo au ya kunyume na maumbile. Mada yetu ya leo itazungumzia namna amiba anavyoenezwa, dalili za amiba na tiba inayoweza kutumika kwa mgonjwa wa amoeba.

 

Chanzo Cha Amiba

 

mzungukoo wa amoebiasis

 

Amiba wakiingia mdomoni, husafiri kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na kutulia ndani ya utumbo mpana. Kuna koo za vimelea hawa (Entamoeba dispar) wanaoishi hapa bila kuleta madhara. E. histolytica anaweza pia kuishi hapa bila madhara. Mtu akila chakula au kunywa maji yenye kimelea aliye kwenye hatua fulani (cystic stage), vimelea hawa watashambulia kuta za utumbo, na kasababisha amoebic dysentery, ugonjwa unaoleta vidonda, unaosababisha damu kuvuja, kusababisha ute (mucus) na kuharisha. Kimelea aliye kwenye hatua hii (cystic form), hubadilika na kuwa trophozoites (invasive form) ndani ya ilium au colon na kuanza mashambulizi. Trophozoites hawa wanaweza kuingia kwenye mtiririko wa damu na kusafiri hadi kwenye maini, au mara chache, hadi kwenye ubongo, ambako watajenga vifuko vya maambukizo (abscesses).

E. histolytica ni uzao wa kimelea huyu anayesababisha dalili kwenye asilimia kumi ya watu wenye maambukizo. Karibu asilimia kumi ya watu duniani wana maambukizo ya amoebas, na hasa watu wanaishi Mexico, India, Central America, Afrika na maeneo ya tropiki ya Asia. Inakadiriwa kuwa amebiasis husababisha vifo vya watu 50,000-100,000 duniani kila mwaka.

 

Dalili Za Amebiasis Ni Zipi?

 

Ingawa ni asilimia 10 -20 tu ya watu wenye maambukizi ndiyo itakayokuwa na wagonjwa, watu hawa wanaweza kuziona dalili zifuatazo:

. Dalili za awali (kama wiki 1-4 hivi) ni pamoja na choo laini na kusokota kwa tumbo kwa mbali

. Ugonjwa ukiendelea, choo cha mara kwa mara, na majimaji/damu ndani ya choo vikiambatana na maumivu makali ya tumbo

. Trophozoites wakifika kwenye kuta za utumbo na kupenyeza, dalili za maambukizo kwenye maini kama maumivu kwenye ini na homa huashiria kujijenga kwa usaha kwenye ini (hepatic amebiasis)

. Viungo vingine (moyo, mapafu, ubongo [meningoencephalitis], kwa mfano) vinaweza kutoa dalili zinazoambatana na kiungo chenyewe na kuleta maumivu makali au kifo.

. Maumivu ya tumbo

. Tenesmus (maumivu yanayokuja na kupotea eneo la haja kubwa yakiambatana na hali ya kutaka kujisaidia haja kubwa bila kinyesi kutoka)

. Kujamba ovyo

. Kukosa hamu ya kula

. Kukonda

. Uchovu wa mwili

. Upungufu wa damu

. Mara chache vidonda kwenye ngozi (cutaneous amebiasis).

 

Tiba Ya Amiba

 

Amiba hutibiwa na dawa za nitroimidazole, ambazo zinaua amiba ndani ya damu, kwenye kuta za utumbo na kwenye usaha ulio kwenye maini. Dawa hizi ni pamoja na metronidazole (Flagyl) na tinidazole (Tindamax, Fasigyn). Metronidazole kwa kawaida hutolewa kwa siku 10, ikiwa ni ya kunywa au sindano.

 

Katika ukurasa mwingine tutauona ugonjwa wa homa ya matumbo ambamo tutaona jinsi bakteria waitwao salmonella typhi wanavyoshambulia na kuathiri mfumo wa mmeng’enyo wa chakula wa binadamu.

Usisite kutona maono uliyo nayo kuhusu mada yetu ya leo au kuuliza maswali uliyo nayo. Tutafanya kila juhudi kuona kwamba tumekujibu ipasavyo.

 

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

 

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.