Sickle Cell Ni Ugonjwa Gani?

 

Sickle cell disease (SCD) ni kundi la maradhi ya kurithi ya chembechembe nyekundu za damu. Chembechembe nyekundu za damu zenye afya huwa za mviringo, na hutembea ndani ya mishipa midogo ya damu kusambaza oksijeni kwenye sehemu zote za mwili. Ndani ya mwili wa mtu mwenye ugonjwa wa sickle cell, chembechembe nyekundu za damu hugeuka kuwa ngumu na zinazonatanata na huwa na umbo la C, umbo linalofanana na kifaa cha shambani cha kukatia majani kiitwacho mundu  “sickle”.  Seli hizi hufa mapema, hali ambayo husababisha mtu awe na upungufu wa damu kila wakati. Na, wakati seli hizi zikisafiri ndani ya mishipa midogo ya damu, hukwama na kuuziba mtiririko wa damu. Hali hii huweza kuleta maumivu makali na matatizo mengine makubwa kama maambukizo, acute chest syndrome na stroke.

sickle cell chanzo chake

Aina Za Sickle Cell Disease

Aina za ugonjwa wa sickle cell ambazo huonekana kwa wingi ni zifuatazo:

HbSS

Watu wenye aina hii ya SCD wanarithi jeni “S” mbili (jeni: sehemu ya DNA inayorithisha tabia au umbile fulani), moja toka kwa kila mzazi. Hii mara nyingi huitwa sickle cell anemia (anemia selimundu) na ndiyo aina ya ugonjwa huu inayosumbua zaidi.

HbSC

Watu wenye aina hii ya SCD wanarithi jeni “S” moja ya sickle cell toka kwa mzazi mmoja na hemoglobin isiyo ya kawaida iitwayo “C”. Hemoglobini ni protini inayowezesha chembechembe nyekundu za damu kusafirisha oksijeni kuelekea sehemu nyingine za mwili. Kwa kawaida hili si tatizo kubwa sana la SCD.

HbS beta thalassemia

Watu wenye aina hii ya SCD wanarithi jeni moja ya sickle cell “S” kutoka kwa mzazi mmoja na jeni moja ya beta thalassemia, aina nyingine ya anemia, kutoka kwa mzazi wapili. Kuna aina mbili za beta thalassemia: “O” na “+”. Wale wenye HbS beta O -thalassemia huwa na hali mbaya zaidi ya SCD. Watu wenye HbS + -beta thalassemia huonyesha nafuu kidogo ya SCD.

Kuna aina nyingine za CSD ambazo huonekana mara chache:

HbSD, HbSE, na HbSO

Watu wenye aiana hizi za SCD hurithi jeni moja ya sickle cell “S” na hemoglobin isiyo ya kawaida (“D”, “E”, au “O”). Ukali wa aina hizi hutofautiana.

Sickle Cell Trait (SCT)

HbAS

Watu wenye sickle cell trait hurithi jeni moja ya sickle cell “S” kutoka kwa mzazi mmoja na jeni “A” moja ya kawaida kutoka kwa mzazi mwingine. Hali hii huitwa sickle cell trait. Watu hawa hawaonyeshi dalili zo zote za ugonjwa na huishi maisha ya kawaida, lakini huweza kuwarithisha ugonjwa watoto wao.

Sickle cell anemia

Sickle cell anemia ni moja ya kundi la matatizo ambayo kwa pamoja huitwa sickle cell disease. Sickle cell anemia ni tatizo la chembechembe nyekundu za damu la kurithi ambapo kunakuwa na upungufu wa chembechembe hizo za damu kwa ajili ya kusafirisha oksijeni kuzunguka mwili mzima.

Kwa kawaidi, seli nyekundu za damu zenye uwezo wa kunyumbuka na kupindika husafiri kiurahisi ndani ya mishipa ya damu. Mgonjwa wa sickle cell anemia huwa na seli nyekundu zenye umbo la mwezi mchanga. Seli hizi ngumu , zinazonata huweza kuziba mishipa midogo ya damu, hali ambaayo huweza kusababisha damu kwenda polepole au kuziba mtiririko wa damu na oksijeni kuelekea sehemu nyingine za mwili.

Hakuna dawa kamili kwa wagonjwa wengi wa sickle cell anemia. Lakini tiba hutolewa ili kupunguza maumivu na kuzuia madhara yanayoweza kutokea kwa sababu ya ugonjwa huu.

Dalili Za Sickle Cell Anemia

Dalili za sickle cell anemia huanza kuonekana mtoto akiwa na umri wa miezi mitano. Dalili huwa tofauti kwa watu tofauti na hubadilika na wakati. Dalili zinaweza kuwa ni pamoja na:

. Anemia. Seli za mgonjwa wa sickle cell huvunjika haraka na kufa, na kumwacha mgonjwa akiwa na seli nyekundu chache. Kwa kawaida seli nyekundu huishi kwa siku 120 kabla ya kuhitaji kubadilishwa. Lakini seli za mgonjwa wa sickle cell huishi kwa siku 10 hadi 20, na kuacha pengo la seli nyekundu (anemia).

Bila ya kuwa na kiwango kizuri cha seli nyekundu, mwili haupati oksijeni ya kutosha hali ambayo husababisha uchovu wa mwili.

. Vipindi Vya Maumivu.  Vipindi vya maumivu vya kujirudia (pain crises), ndiyo dalili kuu ya sickle cell anemia. Maumivu hutokea wakati seli nyekundu za damu zenye umbo la sickle zinapoziba mtirirko wa damu kwenye mishipa midogo ndani ya kifua, tumbo na joints. Maumivu huweza kutokea vile vile ndani ya mifupa.

Maumivu huwa ya uzito tofauti na huweza kudumu kwa saa chache hadi siku chache. Watu wengine hupata vipindi vya maumivu vichache katika mwaka. Wengine huwa na maumivu mara nuyingi zaidi. Maumuvu ya kupindukia huhitaji uangalizi hospitalini.

Vijana wengine wa umri wa balehe na watu wazima wenye sickle cell anemia hupata maumivu sugu, ambayo yanaweza kutokana na kuharibika kwa mifupa na joints, ulcers, na sababu nyingine.

.  Rangi Kubadilika na Kuwa Njano. Rangi ya ngozi, macho na midomo hubadilika na kuwa njano (jaundice) kwa sababu sickle cells haziishi muda mrefu kama seli za damu za kawaida. Seli hizi hufa haraka zaidi ya uwezo wa ini wa kuzitoa nje ya mwili. Rangi ya njano hutokana na billurubin ambayo hutolewa wakati seli nyekundu za damu zinapokufa.

. Acute Chest Syndrome. Hii ni hali iinayotokea wakati sickle cells zinaponatana pamoja na kuzuia oksijeni isifike kwenye vishipa vidogo vya damu ndani ya mapafu. Ni hali inayoweza kusababisha kifo. Mara nyingi hutokea ghafla wakati mwili umeshambuliwa na vijidudu, homa, au upungufu wa maji (dehydration). Huonekana kama pneumonia na inaweza kuambatana na homa, maumivu au kikohozi cha hali ya juu.

. Kuvimba mikono na miguu. Kuvimba kunatokana na seli zenye umbo la sickle kuziba damu isifike kwenye mikono na miguu.

. Maambukizo ya kila wakati. Sickle cells zinaweza kuliharibu bandama, na kukuacha kwenye hali ya kuweza kupata mambukizo ya haraka. Madaktari huwapa watoto wadogo wenye sickle cell anemia sindano au antibiotics kuzuia maambukizo hatari kwa maisha yao, kama pneumonia.

. Kuchelewa kukua na balehe. Chembechembe nyekundu za damu huupa mwili oksijeni na virutubishi muhimu kwa ukuaji. Upungufu wa seli hizo huweza kusababisha ukuaji wa taratibu kwa watoto wadogo na kuchelewesha balehe kwa vijana.

. Matatizo ya kuona. Vijishipa vidogo vya damu ndani ya macho vinaweza kuzibwa na sickle cells. Hali hii inaweza kuharibu retina – sehemu ya jicho inayoratibu uonaji – na kusababisha matatizo ya kuona.

Chanzo Cha Sickle Cell

Ugonjwa wa sickle cell anemia ni wa kurithi toka unapozaliwa. Mtoto huupata ugonjwa huu anaporithi  jeni mbili za sickle  cell -moja kutoka kwa kila mzazi.

Tiba Ya Sickle Cell

Tiba ya sickle cell hulenga kupunguza vipindi vya maumivu, kuzipunguza dalili na kuzuia madhara yatokanayo na ugonjwa huu. Tiba inaweza kuwa ni dawa na kuongezewa damu. Kwa baadhi ya watoto na vijana, tiba ya stem cell transplant inaweza kuuponya ugonjwa.

Watoto wenye sickle cell anemia wanaweza kupewa penicillin wakiwa na umri kama wa miezi 2 hadi miaka 5 kuzuia maambukizi ambayo yanaweza kuwahatarishia maisha yao, kama pneumonia..

Watu wazima wenye sickle cell anemia wanaweza kulazimika kutumia penicillin maisha yao yote , kama walikwisha pata pneumonia au kufanyiwa upasuaji wa kuondoa bandama.

Bone Marrow na Stem Cell Transplant

Bone marrow au stem cell transplant ndiyo njia pekee ya uponyaji kwa mgonjwa wa SCD. Bone marrow, kwa kiswahili uboho, ni tishu laini ya mafuta iliyo katikati ya mifupa ambako chembechembe za damu zinatengenezwa. Bone marrow au stem cell transplant ni utaratibu wa kuchukua seli za kutengeneza damu zenye afya kutoka kwa mtu – donor – na kuziweka kwa mtu ambaye uboho wake haufanyi kazi vizuri.

Bone marrow na stem cell transplant ni taratibu za kubahatisha, na zinaweza kuleta matokeo mabaya, ikiwa ni pamoja na kifo. Ili utaratibu huu ufanikiwe, uboho wa watu hawa wawili inatakiwe ulingane. Kwa kawaida, mtoaji mzuri ni kaka au dada. Bone marrow na stem cell transplant hufanywa kwa watoto wadogo.

Katika mada yetu nyingine, tutauzungumzia ugonjwa wa kuhara. Usisite kutoa maoni yako kuhusiana na mada hii yetu ya leo.

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu ndani ya muda wa kazi kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.