Afya Yako Baada Ya Kukoma Hedhi

 

postmenopause

 

Kipindi cha maisha ya mwanamke baada ya kukoma hedhi huitwa postmenopause. Wakati huu, dalili nyingi za kusumbua alizopata mwanamke wakati anakaribia kukoma hedhi (perimenopause) huishia. Lakini kwa sababu ya vipengele kadhaa, kimoja kikiwa ni kiwango kidogo cha estrogen, wanawake walio katika postmenopause wanakuwa hatarini kupatwa baadhi ya matatizo ya kiafya, kama kupungua kwa uzito wa mifupa (osteoporosis) na magonjwa ya moyo.

Mwanamke anachukuliwa kuwa yupo kwenye postmenopause anapokuwa amekosa siku zake kwa kipindi kizima cha mwaka mmoja. Daktari anaweza kupima kiwango cha follicle stimulating hormone (FSH) na kujua kama unakaribia kukoma hedhi. FSH hutolewa na tezi ya pituitary (tezi iliyo chini ya ubongo). FSH hupanda ghafla na kuwa juu pale ovari zinapoacha kufanya kazi. FSH huweza kupanda na kushuka wakati wa perimenopause, kwa hiyo njia bora ya kujua kuwa upo kwenye postmenopause ni pale unapokuwa umekosa siku zako mfululizo kwa kipindi cha mwaka mzima.

 

Ni Mabadiliko Gani Utayaona Wakati Wa Postmenopause?

Ukiingia kwenye postmenopause, mwili wako unaweza kuwa umerudiwa na nguvu zake, lakini unakuwa kwenye hatari ya baadhi ya changamoto za kiafya. Matumizi ya dawa na staili za maisha vinaweza kupunguza baadhi ya chamgamoto hizo.

 

Vidokezi Vya Namna Ya Kuishi Baada Ya Kuokoma Hedhi

Kuna hatua za kuchukua ili mwanamke uliye kwenye postmepause ujisikie vizuri na kuwa mwenye afya nzuri.

. Epuka kuvuta sigara, kafeini (kiambato ndani ya kahawa na chai), pombe, chumvi nyingi, na sukari
. Kula mlo kamili (balanced diet)
. Tumia calcium kuweka imara mifupa yako
. Tumia pia vitamini D kuimarisha mifupa
. Fanya mazoezi, kila siku, angalau dakika 30
. Tumia chakula chenye mafuta kidogo (low saturated fat and cholesterol.)

 

Vidokezi Vya Kupunguza Hot Flashes

Hot flashes ni dalili inayojionyesha zaidi kwa mwanamke aliyekoma  hedhi. Mwanamke hupatwa na vipindi vya joto la ghafla, sehemu za juu za mwili likiambatana na jasho. Hapa chini ni vidokezi vya namna ya kukabiliana hali hiyo:

. Epuka kuvaa nguo nyingi na lala sehemu zenye ubaridi
. Epuka kula chakula cha moto na chenye viungo vingi
. Epuka kunywa pombe
. Punguza mawazo
. Kula chakula chenye soya

 

postmenopause symptoms

 

 

Vidokezi Vya Kupunguza Uyabisi Wa Uke

. Tumia vilainishi na vitu vya kuongeza unyevunyevukuwa (moisturizers.)
. Mwombe daktari akuongoze kuhusu vitu vinavyoongeza estrogen.

 

Vidokezi Vya Kupunguza Tatizo La Mifupa Kuwa Myepesi

. Tumia calcium na vitamini D ya kutosha
. Fanya mazoezi

 

Vidokezi Vya kuzuia magonjwa ya moyo

Yamkini ya kupata magonjwa ya moyo huongezeka umri unapokuwa mkubwa. Vidokezi vya kuulinda moyo wako ni pamoja na:

. Chukua vipimo vya cholesterol na blood pressure kila wakati
. Chukua hatua za kupunguza cholesterol na kupunguza blood pressure kama vimepanda.
. Kama una kisukari, iweke sawa sukari yako kila wakati

 

Kutoka Damu Wakati Wa Postmenopause

 

Kama umeshaingia kipindi cha kukoma hedhi, hupaswi kuona tena damu ikitoka. Kukoma hedhi maana yake, kutotokwa na damu kwa kipindi kizima cha mwaka mmoja.

Ukiona damu – hata kama ni vijitone tu – unashauriwa kumwona daktari, ili ajiridhishe kuwa si tatizo kubwa, kama la saratani.

 

Ni Nini Chanzo?

Mazingira mengi yanaweza kuwa sababu ya damu wakati wa postmenopause:

. Polyps: Hivi ni vivimbe vya tishu vinavyoota ndani ya nyumba ya uzazi au mkondo wa shingo ya uzazi, au kwenye cervix. Kwa kawaida si saratani, lakini vinaweza kusababisha vitone vya damu, kutoka damu nzito, au damu baada ya tendo la ndoa.

 

polyps

 

. Endometrial atrophy (thinning of the uterine lining): Endometrium ni tishu inayotanda juu ya nyumba ya uzazi (uterus). Hupokea ishara za homoni kama estrogen na progesterone. Viwango vidogo vya homoni wakati wa postmenopause huweza kuifanya isinyae na kuwa nyembaba sana. Hii inaweza kusababisha kutoka damu.

. Endometrial hyperplasia (thickening of the uterine lining): Baada ya kukoma hedhi, unaweza kuwa na estrogen nyingi zaidi na progesterone kidogo sana. Hali hiyo inaweza kupelekea endometrium kuwa nene zaidi na kutoa damu. Wakati mwingine seli ndani ya endometrium zinaweza kugeuka na kuwa si za kawaida. Hii inaweza kuleta saratani.

. Vaginal atrophy (thinning of vaginal tissue): Estrogen husaida katika afya ya uke. Baada ya kukoma hedhi, upungufu wa estrogen unaweza kusababisha
kuta za uke kusinyaa, kuwa kavu, na kuvimba. Hali hii mara nyingi husababisha kutoka damu baada ya tendo la ndoa.

. Cancer: Kutoka damu ni dalili inayoashiria zaidi uwepo wa saratani ya endometrium au uterus. Inaweza pia kuwa ishara ya saratani ya uke au saratani ya shingo ya kizazi.

. Sexually transmitted diseases: Baadhi ya magonjwa, kama ya chlamydia na gonorrhea, yanaweza kusababisha kutoka matone ya damu na damu baada ya tendo la ndoa.

. Madawa: Kutoka damu mara nyingi ni madhara yanayotokana na matumizi ya madawa, kama dawa za hormone therapy, tamoxifen, na dawa za kuifanya damu kuwa nyepesi.

 

Tiba Yake Ni Nini?

 

Tiba itategemea chanzo cha kutokwa damu.

. Estrogen therapy: Homoni hii hutolewa ili kutibu kusinyaa kwa uke au utando wa juu ya nyumba ya uzazi (vaginal and endometrial atrophy.) Daktari anaweza kushauri matumizi ya:

. Vidonge vya kunywewa
. Cream ya ukeni: Kifaa maalumu kitatumika kuingiza cream hii mwilini
. Vaginal ring: Namna ya pete ambayo daktari ataiweka kwenye uke. Pete hii hutoa estrogen kwa miezi 3.
. Vaginal tablet: Utakiweka ukeni kutumia kifaa maalumu. Utatakiwa kuweka kila siku, au mara chache katika wiki.

. Progestin therapy: Hii ni namna ya progesterone iliyotengenezwa kwenye maabara inayotumika kutibu endometrial hyperplasia. Dakatri anaweza kukuandikia vidonge au sindano, cream ya ukeni , au kifaa cha kuweka kwenye nyumba ya uzazi.

. Hysteroscopy: Njia hii huweza kuondoa polyps. Madaktari huitumia kuondoa sehemu zilizovimba za utando wa nyumba ya uzazi kutokana na endometrial hyperplasia. Ataingiza hysteroscope kupitia uke na kupitisha vifaa vidogo vya upasuaji kupitia kijibomba.

 

 

 

 

. D&C (dilation and curettage): Katika upasuaji wa aina hii, madaktari huipanua cervix. Kisha hutumia kifaa chembamba kuondoa polyps au sehemu zilizotuna za uterus zilizosababishwa na endometrial hyperplasia.

. Hysterectomy: Upasuaji huu huondoa sehemu au tumbo lote la uzazi. Hii ni tiba kwa saratani ya endometrium au cervix. Wakati mwingine, daktari ataamua kuondoa ovari zako, mirija ya uzazi, au sehemu za karibu (lymph nodes).

. Radiation, chemotherapy, and hormone therapy: Unaweza kupewa tiba zaidi ya kansa baada ya upasuaji. Daktari ataamua cha kufanya kutokana na aina ya kansa uliyo nayo na ipo katika hatua gani.

. Madawa: Daktari anaweza kukuandikia dawa kama za antibiotics kwa magonjwa ya ngono. Dawa hizi zinaweza pia kutibu maambukizi kwenye cervix au tumbo la uzazi.

 

Katika mada nyingine tutazungumzia maana ya kukoma hedhi. Usisite kuuliza maswali uliyo nayo, ni furaha kwetu kuona kuwa tumekujibu vizuri.

 

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

 

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.