Umuhimu Wa Virutubishi Katika Mwili

 

uchafuzi wa mazingira

Maendeleo ya sayansi, teknolojia na viwanda yamechangia kwa kiwango kikubwa kubadilisha namna tunavyoishi na kupata chakula chetu cha kila siku. Maendeleo hayo kwa upande mmoja yametufanya kuwa wastaarabu zaidi lakini kuna athari kubwa zaidi za kiafya kwa upande wa pili. Matokeo makubwa ya maendeleo hayo ni kwamba sasa miili yetu haipati chakula chenye virutubishi vya kutosha  na tunaingiza vitu vingi ndani ya miili yetu ambavyo havitakikani na mwili . Leo tutaona baadhi ya vitu ambavyo hatuwezi kuvikwepa na ambavyo kila siku vinaathiri afya zetu:

Uchafuzi Wa Hewa

Binadamu wa sasa tunaishi kwenye mazingira ambayo hewa yake inachafuliwa kwa namna nyingi. Uwepo wa magari mengi kwenye barabara zetu yanayotoa moshi unatufanya tuvute hewa hiyo chafu.

uchafuzi wa hewa

Uwingi wa viwanda huchangia katika kutufanya tuvute hewa ambayo si salama kwa afya zetu. Hewa iliyochafuliwa huchangia katika kutenengeza radikali huru (free radicals) katika miili yetu.

Uchafuzi wa hewa maana yake uachwaji wa vichafuzi kwenda hewani ambavyo baadaye vinahatarisha afya ya binadamu na sayari ya dunia kwa ujumla.

Uchafuzi wa hewa mara nyingi hutokana na matumizi na uzalishaji wa nishati. Uunguzwaji wa mafuta hutoa gesi na kemikali zinazochafua hewa. Vichafuzi vinavyotokana na uunguzaji wa mafuta ni vya aina mbili:

– Mchanganyiko wa ukungu na moshi (smog) ambao hutokea pale mabaki ya uunguzwaji wa mafuta yanapoathiriwa na mwanga wa jua.

– Masizi ambayo hujengwa na vipande vidogo sana vya vitu vigumu vya kemikali, vya udongo, moshi, vumbi ambavyo husambaa hewani.

Vichafuzi hivi huzalishwa na magari, viwanda, mitambo ya kuzalisha umeme, injini – au vitu vingine vinavyochoma mafuta. Vipande vidogo kabisa katika hewa ni masizi – ambayo yakiwa kama gesi au vitu vidogo vigumu – yana uwezo wa kupenya kwenye mapafu na mfumo wa damu na kuleta madhara makubwa kwenye mapafu, kusababisha mshtuko wa moyo na kusababisha vifo vya haraka.

Smog huathiri macho na kuleta uharibifu kwenye mapafu – na hasa kwa watu wanaofanya kazi za nje, watoto na wazee. Smog ni hatari zaidi kwa watu wenye asthma kwani huweza kuwasababishia kubanwa na asthma.

Vichafuzi vinaweza kukatisha maisha ya binadamu au kuathiri vibaya afya yake. Vichafuzi vinavyotambulika zaidi ni zebaki, risasi, dioxins na benzene ambayo hupatikana ndani ya petroli. Benzene ambayo inatambulika pia kuwa inasababisha saratani, huathiri macho, ngozi na mapafu na uchafuzi wa muda mrefu huleta matatizo ndani ya mfumo wa mzunguko wa damu. Dioxins (sumu iliyopo katika dawa za kuulia mimea) hupatikana zaidi ndani ya chakula ingawa kwa kiwango kidogo hupatikana hewani na athari kubwa kwa maini, kinga za mwili, mfumo wa neva na viungo vya uzazi. Risasi huharibu akili na figo za watoto na kuathiri uwezo wao wa kujifunza. Zebaki huathiri mfumo wa neva.

Polycyclic aromatic hydrocarbons (PAHs) ni sumu zinazotokana na moshi wa magari na moto wa misituni. PAHs zinahusishwa na matatizo ya macho na mapafu,ain damu na mi na hata kansa.

 

kuchafua hewa

 

Uwepo wa radikali huru kwa wingi katika miili yetu umehusishwa na magonjwa ya moyo na saratani. Radikali huru pia zimebainika kuchangia katika kudhoofisha kinga za mwili, na kumfanya binadamu  kuzeeka haraka.

Uchafuzi Wa Maji

Vyanzo vya maji vinachafuliwa na mabaki ya kemikali kutoka kwenye viwanda na watu katika shughuli zao za kawaida za maisha.

uchafuzi wa maji
Hata katika uzalishaji wa kawaida wa maji ya kunywa na kupikia, kemikali (chlorine) hutumika katika jitihada za kuyafanya maji hayo kuwa salama. Binadamu tutumiapo maji haya, tunaingiza kemikali zisizotakiwa katika miili yetu.

Uchafuzi wa maji hutokea pale kemikali au viumbe wadogo wanapochafua mito, maziwa, bahari, tabaka la maji lililopo chini ya ardhi (aquifer) linalotoa maji ya visima na hivyo kupunguza ubora wa maji au kuyafanya kuwa sumu kwa binadamu na mazingira.

Maji huchafuliwa kirahisi sana kwa sababu maji huweza kuyeyusha vitu vingi zaidi kuliko kimiminika cho chote kilicho juu ya ardhi. Vitu vyenye sumu kutoka mashambani, mijini na viwandani huyeyuka ndani ya maji na kuyachafua.

Uchafuzi wa maji huleta maafa. Mwaka 2015, watu wapatao milioni 1.8 walikufa. Maji pia huleta maradhi. Kila mwaka watu wapatao bilioni moja hupata maradhi. Na watu wa kipato cha chini huathirika zaidi kwa sababu wao ndiyo wanaoishi karibu na viwanda vinavyosababisha uchafuzi wa maji.

Vijidudu wa magonjwa waishio ndani ya maji, kama bakteria na virusi kutoka vinyesi vya binadamu na wanyama, ni chanzo kikubwa cha magonjwa yatokanayo na maji machafu. Wadudu hawa huleta magonjwa kama ya cholera, giardia na typhoid.

Uwepo wa kemikali za risasi, arsenic na zebaki, madawa ya kuulia wadudu mashambani pamoja mbolea za kemikali za nitrates katika maji huongeza pia janga la uchafuzi wa maji.

Uchafuzi huu huleta madhara ya kiafya kama kansa, matatizo ya homoni na akili. Zebaki kwa mfano, ina madhara makubwa kwa watoto na akina mama wanaolea. Zebaki huathiri ukuaji wa mfumo wa akili wa vichanga vikiwa tumboni na baada ya kuzaliwa.

Sumu Katika Chakula

Ili kupata mazao kwa kiasi kikubwa kutoka kwenye mashamba yetu, mbolea za kemikali za aina mbalimbali hutumika ili kuotesha na kuikuza mimea. Aina mbali mbali za dawa za kuulia wadudu na kutibu magonjwa ya mimea pia hutumika kwenye mashamba yetu.

uchafuzi wa mimea kwa dawa

Vitu hivi baadaye vyote huingia ndani ya mwili wa binadamu na kusababisha madhara kwenye afya zetu. Uchafuzi wa chakula chetu huongezeka pale nafaka na mimea vinapohifadhiwa na wakati wa maandalizi kabla havijaliwa, hii ni pamoja na utengenezaji wa maumbo au kuboresha rangi ya chakula.

Mionzi

Teknolojia ya sasa imekuja na vifaa vingi sana vinavyotumia mionzi. Binadamu wa sasa hatuwezi kukwepa kutumia simu za viganjani, televisheni, microwave ovens na kupata tiba kwa kutumia mionzi. Tatizo jingine ni kuishi karibu na nyaya za kusambazia umeme na mitambo inayotoa mionzo mikali.

uchafuzi kwa mionzi ya umeme

Matatizo mengi ya kiafya yanahusishwa na uchafuzi wa mazingira kwa mionzi ya umeme. Mionzi ya umeme huathiri DNA, hupunguza ujazo wa mbegu za kiume (low sperm count) na kusababisha ugumba kwa wanaume. Mionzi ya umeme husababisha saratani za aina mbalimbali, hupunguza uwezo wa kutuliza mawazo kwenye kitu kimoja – Attention Deficit Disorder (ADD), huleta hali ya kupenda upweke – Autism,  husababisha mfadhaiko, husababisha kukosa usingizi, maumivu ya mgongo, ugonjwa wa Parkinson’s na mengineyo.

Hivi vitu vyote na vingine vingi hupunguza ubora wa chakula tunachokula na kutufanya tule chakula ambacho hakina virutubishi vya kutosha kwa mahitaji ya miili yetu, kutufanya tule vitu ambavyo havihitajiki ndani ya miili yetu na kutusababishia magonjwa mbalimbali yakiwemo ya kansa, magonjwa ya moyo na kisukari.

Kutokana na maelezo hayo hapo juu, utaona kuwa matumizi ya virutubishi vya kiada hayakwepeki ili kuondoa vitu ambavyo havitakikani ndani ya miili yetu, kutoa nyongeza ya vitu ambavyo miili yetu inakosa na kuisadia miili yetu katika utendaji wake wa kazi.

Katika mada nyingine tutazungumzia chakula cha kuzuia tusizeeke haraka. Usisite kutoa maoni yako kuhusu mada yetu ya leo. Itakuwa faraji kwetu kukujibu.

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu ndani ya saa za kazi kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.