Ukurutu Juu Ya Ngozi (Eczema)

 

ukurutu miguuni

 

Ukurutu (eczema) ni hali ambapo mabaka juu ya ngozi huvimba, huwasha, ngozi huchanika na kuwa ya kukwaruza. Aina nyingine za ukurutu husababisha malengelenge. Eczema ni neno linalotumika kwa kundi la magonjwa yanayoifanya ngozi kuvimba na kuwa na harara. Ni neno ambalo halielezei ugonjwa mmoja bali mtiririko wa athari juu ya ngozi unaoleta baadhi ya magonjwa. Watu wengi hutumia neno eczema kumaanisha atopic dermatitis, ambayo ni aina ya eczema inayoonekana zaidi. Neno atopic linajumisha hali zinazohusiana na mfumo wa kinga za mwili, pamoja na atopic dermatitis, asthma, na mafua yaletwayo na vumbi (hay fever). Neno dermatitis linaashiria uvimbe juu ya ngozi.

Eczema ni ugonjwa unaoonekana zaidi kwa watoto, lakini watoto wengi hupona baada ya kufikia balehe. Ingawa hadi sasa hakuna tiba, watu wanaweza kujikinga kwa kuwa waangalifu, kutumia moisturizers, na kubadili staili ya maisha.

 

Chanzo Cha Ukurutu

 

Sababu halisi za kutokea ukurutu bado hazijabainishwa, lakini mabingwa wa afya wanaamini kuwa ukurutu unatokea kwa sababu za mchanganyiko wa urithi na mazingira.

Watoto wanakuwa na hatari kubwa zaidi ya kuapata eczema kama mmoja wa wazazi wake anao au ana tatizo jingine la kinga za mwili. Kama wazazi wote wana shida zinazohusu kinga za mwili, hatari inakuwa kubwa zaidi.

Baadhi ya vipengele vinaweza kuleta dalili za eczema. Navyo ni:

 Vitu vya kuwasha: Hivi vinajumuisha sabuni, sabuni za unga/maji (detergents), shampoo, dawa za kuulia viini vya maradhi (disinfectants), juisi kutoka matunda freshi, nyama, na mboga za majani.

 Allergens: Wadudu wa kwenye vumbi, wanyama, na poleni vuinaweza kusababisha ukurutu. Huu huitwa allergic eczema.

 Microbes: Hii inahusisha bakteria kama Staphylococcus aureus, virusi, na baadhi ya fungus.

 Joto na baridi kali: Hali ya hewa ya joto au baridi kali, unyevu hewani (humidity) ukiwa mwingi au mdogo, na kutoka jasho kutokana na mazoezi vinaweza kuleta eczema.

 Chakula: Bidhaa za mifugo, mayai, mbegu na njugu, bidhaa za soya, na shayiri vinaweza kusababisha kulipuka kwa ukurutu.

 Msongo wa mawazo: Hiki si chanzo halisi cha ukurutu, lakini huzizidisha dalili zake.

 Homoni: Wanawake huona dalili zaidi za eczema wakati viwango vya homoni zao vikibadilika, kama wakati wa ujauzito na muda fulani wakati wa mzunguko wa hedhi.

 

Aina Za Ukurutu

 

Kuna aina kadhaa za eczema. Pamoja na atopic dermatitis, aina nyingine ni:

 

ukurutu mkononi

 

. Allergic contact dermatitis: Huu ni mjibizo wa ngozi unaotokea wakati ngozi ikigusana na kitu (au allergen) ambacho kinga za mwili zinakitambua kama kigeni.

. Dyshidrotic eczema: Hii inamaanisha kuwasha juu ya ngozi kwenye viganja na kwenye nyayo. Hujitambulisha kwa malengelenge.

. Neurodermatitis: Huu huleta mabaka ya magamba juu ya ngozi utosini, mikononi, kwenye viwiko, na miguuni. Hutokea kwa sababu ya mwasho kwenye eneo moja, kama vile uking’atwa na mdudu.

. Discoid eczema: Hii pia hujulikana kama nummular eczeama, aina mabayo hutengeneza mabaka ya mviringo juu ya ngozi ambayo yanaweza kuwa kama gamba, yanayobambuka, na kuwasha.

. Stasis dermatitis: Hii inamaanisha kuwashwa kwenye sehemu ya chini ya miguu. Mara nyingi huhusiana na mfumo wa mzunguko wa damu.

 

Dalili Za Eczema

 

Dalili za atopic dermatitis zinakuwa tofauti kulingana na umri wa mtu aliye na tatizo hili. Atopic dermatitis huonekana sana kwa watoto, kukiwa na mabaka makavu yenye magamba yaliyo juu ya ngozi. Mabaka haya mara nyingi huwasha sana. Kujikuna kwa mara kwa mara husababisha maambukizi juu ya ngozi.

Mara nyingi, eczema huwa si kali. Dalili za kawaida za atopic dermatitis ni pamoja na:

. ngozi kavu, yenye magamba
. ngozi kuwa nyekundu
. kuwasha
. vidonda vya wazi, vyenye magamba

Baadhi ya dalili za eczema huwa tofauri kwa watu wenye ngozi nyeusi. Watu wengi wenye eczema huipata wakiwa chini ya miaka 5, lakini asilimia 60 kati ya watoto hao huwa wamepona wanapofikia umri wa balehe.

 

Dalili Za Eczema Kwa Vichanga

Dalili zifuatazo za atopic eczema ni za kawaida kwa watoto walio chini ya miaka 2:

. vijipele juu ya ngozi ya kichwa na mashavu
. vijipele vinavyojaa hewa kabla ya kuanza kutoa majimaji
. vijipele vyenye miwasho mikali sana, vinavyoweza kukosesha usingizi.

 

Dalili Za Eczema Kwa Watoto

Dalili za kawaida za atopic eczema kwa watoto wa miaka 2 na zaidi ni :

. ukurutu nyuma ya mikunjo ya viwiko na magoti
. ukurutu unaotokea shingoni, kwenye vifundo vya mikono, vifundo vya miguu (ankles), na mikunjo katikati ya matako na miguu
. ukurutu wenye uvimbe
. ngozi kuwa nene (lichenification), hali ambayo inaweza kusababisha miwasho ya kudumu

 

Dalili Za Eczema Kwa Watu Wazima

 

 

ukurutu kwenye kiwiko

 

 

Dalili zifuatazo ni za kawaida baina ya watu wazima:

. ukurutu wenye magamba zaidi ya ule unaowatokea watoto
. ukurutu unaotokea zaidi kwenye mikunjo ya viwiko au magoti au shingoni
. ukurutu unasambaa karibu mwili mzima
. ngozi iliyo kavu sana kwenye maeneo yaliyoathiriwa
. ukurutu unaowasha wa kudumu
. maambukizi juu ya ngozi

Watu wazima waliowahi kuugua atopic dermatitis utotoni lakini sasa hawana dalili wanaweza bado wakawa na ngozi kavu au inayowasha mara kwa mara, eczema ya mikononi, na matatizo ya macho.

Mwonekano wa ngozi ya mtu mwenye atopic dermatitis utategemea ni kwa kiwango gani mtu huyu anajikuna na kama ngozi ina maambukizi au la. Kujikuna na kujisugua kunaweza kuongeza miwasho na uvimbe.

 

Tiba ya Ukurutu

 

Hadi sasa hivi hakuna dawa ya eczema. Tiba hulenga kuponya maeneo yaliyoathiriwa na kuzuia kuenea kwa dalili.

Daktari atatoa tiba kulingana na umri wa mwathirika, dalili zilizopo, na hali iliyopo.

Kwa baadi ya watu, eczema hutooweka yenyewe baada ya muda. Lakini, kwa wengine ni hali inayodumu maisha yote.

 

 

ukurutu mgongoni

 

 

Baadhi ya mambo yanayoweza kufanyika ni:

Uangalizi Wa Nyumbani

Kuna tahadhari kadhaa ambazo mtu mwenye eczema anaweza kuzichukua ili kusaidia afya ya ngozi yake na kuondoa dalili.

Kwa mfano, mtu anweza kuyafanya yafuatayo:

. kuoga maji ya uvuguvugu
. kutumia moisturizer dakika 3 baada ya kuoga kuuzuia unyewvu
. kutmia moisturizer kila siku
. kuvaa nguo za pamba
. kukwepa nguo zinazokwaruza na nguo zinazobana
. kutumia humidifier vipindi vya hewa kavu au vya baridi
. kutumia sabuni nyepesi au kutotumia sabuni wakati wa kujisafisha
. kuchukua tahadhali dhidi ya mlipuko wa eczema wakati wa baridi (winter)
. kujikausha kwa hewa au kwa kujipapasa kwa taulo, badala ya kusugua ngozi baada ya kuoga
. Epuka mabadiliko ya ghfla ya joto la hewa na shughuli za kutoa jasho
. Soma vitu visababishi vya eczema kwa mwili wako
. Hakikisha kucha zako ni fupi ili usijikune na kuchana ngozi

Unaweza pa kujaribu matumizi ya vitu vya asili vya kuzuia eczema, ikiwa ni pamoja na aloe vera, mafuta ya nazi na apple cider vinegar.

 

Katika mada yetu nyingine, tutazungumzia chanzo, aina na jinsi ya kutibu chunusi. Usisite kuuliza maswali uliyo nayo kuhusu uandishi wa mada hii yetu ya leo.

 

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

 

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.