Umuhimu Wa Potassium Katika Mwili

 

 

Potassium ni moja ya madini saba yanayohitajika kwa wingi (macronutrients) katika mwili. Mwili unahitaji potassium kuenndesha shughuli muhimu katika mwili.

Potassium inahusika kwa kiwango kikubwa katika ufanyaji kazi wa figo, moyo, misuli, na usafirishaji wa taarifa kupitia mfumo wa neva.

Mahitaji Ya Mwili Ya Potassium

Kiwango cha kutosha cha potassium kwa mwili ni milligramu 3,400 kwa siku kwa mwanamme wa umri mkubwa mwenye afya na milligramu 2,600 kwa mwanamke.

Jedwali la hapa chini linabainisha mahitaji kwa watu wa makundi mbalimbali.

Mahitaji ya mwili wakati wa ujauzito ni milligramu 2,900, na milligramu 2,800 wakati wa kunyonyesha.

Faida Za Potassium Katika Mwili

Potassium ni elektroliti inayohitajika kwa afya ya mwili. The American Heart Foundation (AHA) inasema kuwa chakula chenye potassium kinasaidia kuweka vizuri pressure ya mwili kwa kupunguza madhara ya sodium.

Uwepo wa sodium kwa wingi kunaweza kuongeza pressure. Ndani ya mwili mwenye afya, potassium huondoa hatari ya pressure kwa kuusaidia mwili kutoa sodium. Potassium husaidia kuweka pressure vizuri kwa kulegeza kuta za mishipa ya damu.

Blood Pressure Na Afya Ya Moyo

Kula chakula chenye potassium kwa wingi kunaweza kusaidia kuzuia au kudhibiti pressure ya damu. Na kama mtu anapata potassium kwa wingi na sodium kidogo, anapunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo na stroke.

Kukarabati Mifupa Na Misuli

Potassium inaweza kusaidia afya ya mifupa. Utafiti unashauri kuwa watu wanaopata potassium kwa wingi kupitia matunda na mboga wanaweza kuwa na mifupa iliyojaa madini.

Chakula chenye uwingi wa potassium kinaweza pia kusaidia kutunza misuli kwa watu wenye umri mkubwa na kwa watu wenye matatizo ya kiafya yanayopunguza misuli.

Afya Ya Figo

Baina ya watu wenye afya, upungufu wa potassium hupunguza uwezo wa figo wa kufyonza tena calcium. Kiwango kikubwa cha calcium katika figo huweza kusababisha kidney stones.

Hata hivyo, watu wenye figo zilizofeli hawatakiwa kupata potassium kwa wingi, kwa sababu huweza kuleta madhara.

Chakula Chenye Potassium

Potassium hupatikana ndani ya chakula cha aina nyingi kinachotokana na mimea, lakini uandaaji hupunguza viwango vya kirutubishi hiki.

Chakula cha aina nyingi kinachoandaliwa viwandani kina uwingi wa sodium, kwa mlaji mkubwa wa chakula cha aina hii anahitaji kuongeza potassium katika mlo wake.

Kiujumla, matunda mengi yaliyokaushwa na chakula cha jamii ya kunde vina uwingi wa potassium. Jedwali la hapa chini linaonyesha viwango vya potassium katika mlo mmoja.

Supplements

Kwa kawaida, chakula kilichoandaliwa vizuri kina potassium ya kutosha, na hasa kama chakula hicho kina kiwango kidogo cha sodium.

Kuna wakati ambapo daktari anaweza kukushauri upate supplements. Kuna ushahidi kuwa supplements hizo zinaweza kusaidia:

. kudhibiti pressure
. kuzuia stroke
. kuzuia mawe ndani ya figo (kidney stones)
. kuweka vizuri afya ya mifupa
. kudhibiti kiwango cha sukari katika damu.

Upungufu wa Potassium

Upungufu wa potassium (hypokalemia) katika mwili unaweza matatizo kadhaa ya kiafya, yakiwa ni pamoja na:

. pressure kuwa juu
. uwezekano wa mawe katika figo
. uoungufu wa calcium katika mifupa

Mtu mwenye afya, upungufu wa potassium ni pale anapokuwa na kiwango chini ya millimoles 3.6 kwa lita ya blood serum. Mtu mwenye magonjwa ya figo kiwango chake ni cha chini zaidi.

Mtu mwenye upungufu wa potassium hata kidogo tu anaweza kuona dalili zifuatazo:

. kufunga choo
. uchovu
. misuli dhaifu
. hali ya kutojisikia vizuri

Kiwango cha potassiumu kikisshuka chini ya millimoles 2.5 kwa lita ndani ya mwili wa mtu mwenye afya madkatari huchulia hali hii kuwa ni mabaya kiasi. Inaweza kuleta yafuatayo:

. mkojo kutengenezwa kwa wimgi
. mwili kuikataa glucose
. ganzi katika misuli
. matatizo ya upumuaji
. mabadiliko ya mapigo ya moyo, baina ya watu wenye magonjwa ya moyo
. kuchanganyikiwa, baina ya watu wenye matatizo ya figo

Upungufu mkubwa sana unaweza kuwa ni hatari kwa maisha kwa sababu unaweza kuathiri moyo:

 

Potassium Ikizidi Mwilini

 

Kwa kawaida mwlini una uwezo wa kuvumilia endapo potassium itazidi, ambayo itatolewa na figo.

Hata hivyo, kuzidi kwa potassium (hyperkalemia), kunaweza kua na madhara katika mwili kwa watu wenye matatizo ya figo pale figo zao zinaposhindwa kuitoa potassiumu ya kutosha. Hii ninaweza kuwa hatari endapo viwango vitapanda kwa haraka.

Madaktari wanachukulia kuwa potassium imezidi pale inapofikia millilole 5.1 hadi 6 kwa lita ya blood serum. Katika hali hii uangalizi huwa ni wa lazima na kiwango kikizidi kidogo tu juu ya millimole 6 kwa lita hatua za haraka zinahitajika.

Watu wewenye potassium iliyozidi wanaweza kuwa na dalili chache au wakakosa dalili kabisa. Pale dalili zinapojitokeza, zitafanana na zile za hypokalemia.

Potassium ya juu ya ghafla inaweza kuleta:

. mapigo ya moyo kwenda mbio
. kukosa pumzi
. maumivu ya kifua