Chunjua Za Sehemu Za Siri – Genital Warts – Tiba Yake Ni Nini?

 

Genital warts – chunjua zinazoota seheme za siri – husababishwa na human papillomavirus. Kuna aina tofauti zaidi ya 100 za human papillomavirus (HPV) lakini ni aina kama 40 tu ya hizi ndizo zinazoweza kusababisha chunjua za sehemu za siri. Katika mada yetu ya leo tutaona dalili za genital warts na tiba za chunjua hizi za sehemu za siri.

Chunjua za sehemu za siri husababishwa zaidi na aina mbili za virusi (HPV-6 na HPV-11), na aina hizi mbili huhesabiwa kama virusi wasio na madhara makubwa kwa maana kuwa ni mara chache sana wanaweza kusababisha kansa. Aina moja ya kirusi huyu, HPV-16, anahesabiwa kama ni wa hatari na ndiye chanzo cha asilimia 50 ya kansa zote za shingo ya kizazi kwa wanawake. Aina nyingine za virusi wa hatari “high risk” ni HPV wa aina za 18, 31, 33, 35, 39, 45, 51, 52, 56, 58, 59 na 68. Saratani zote, asilimia 100, za shingo ya kizazi husababishwa na HPV.

Wadudu hawa wanaenea kwa haraka sana kwa hupenya kupitia juu ya ngozi au kupitia sehemu laini zenye unyevu za siri wakati wa tendo la ndoa. Seli za mwili zikishashambuliwa, hupita kipindi cha miezi au miaka kadhaa bila kuonyesha dalili za kuwa kuna maambukizo.

Kwa kawaida, theluthi mbili za watu waliofanya mapenzi na mtu mwenye chunjua za sehemu za siri huota chunjua hizi.

Dalili Za Chunjua Za Sehemu Za Siri Ni Nini?

Pamoja na kuwa genital warts hazina maumivu, zinaweza kuwa kero kwa sababu ya sehemu zilizopo, ukubwa wake na miwasho. Ukubwa wa chunjua huwa kama milimeta moja mapana yake hadi sentimeta moja ya mraba endapo chunjua nyingi zitaungana. Chunjua huweza kuota sehemu zaidi ya moja.

. Kwa wanaume, genital warts huweza kutokea kwenye mrija wa mkojo, uume, au kwenye eneo la mkundu. Zinaweza kuwa kama vijinyama laini vilivyovimba visivyo na mkwaruzo (juu ya uume) au kama vijidole vinavyoning’inia (kwenye eneo la mkundu). Nyingine zinaweza kuwa na umbo la koliflawa, au zenye kukwaruza na zenye rangi nyeusi. Wakati mwingine hujificha kwenye unywele au zikawa ndani ya govi la mtu ambaye hajatahiriwa.

 

 

 

 

. Kwa wanawake, chunjua huwa na sura hiyo hiyo ila mara nyingi huwa kwenye sehemu zenye unyevu za mashavu ya ndani (labia minora) au kuzunguka tundu la uke.

 

 

Tiba Ya Chunjua Za Sehemu Za Siri Ni Nini?

Hakuna tiba ambayo ni ya uhakika kabisa kwa chunjua za sehemu za siri. Kuna tiba nyingi zinazotumika, lakini hakuna yenye uhakika wa asilimia 100 katika kuondoa chunjua za sehemu za siri na kuzizuia zisirudie tana. Genital warts huweza kuondoka zenyewe kutoka asilima 10 hadi 20 ya watu walioathirika katika kipindi cha miezi 3 hadi 4.

. Cryotherapy: Njia hii hugandisha chunjua kwa kutumia naitrojeni ya maji (liquid nitrogen). Ni njia bora sana kwa sababu imetoa matokea mengi mazuri ikiwa na side effects chache sana.

. Laser treatment: Njia hii hutumika kwa chunjua za sehemu za siri zilizoenea au zinazojirudirudia. Mionzi ya laser huharibu kabisa uvimbe  uliotokana na HPV. Dosari ni bei yake kubwa, muda mrefu wa tiba, na kuacha makovu.

. Elecrodesiccation: Njia hii hutumia peni ya umeme kuua chunjua.

 

 

 

 

Ni Zipi Dawa za Genital Warts?

Kuna dawa kadhaa zinazotumika kutibu chunjua za sehemu za siri na unaweza kuzitumia kama mbadala wa tiba nyingine.

. Podophyllum resin ni dawa inayotolewa na mtaalamu wa tiba
. Podofilox (Condylox) ni dawa unayoweza kuitumia nyumbani na ina uwezo mkubwa wa kutibu kuliko podophyllum resin. Dawa hii pia hutumika kwa kinga.
. Trichloroacetic acid au bichloroacetic acid haina uhakika sana na chunjua huweza kurudi, inaweza kusababisha maumivu na kujisikia kama unaungua.
. 5-Fluorouracil (Efudex) hutumika kama cream, huchukua muda mrefu kutibu, na ina madhara mengine mengi ya kiafya.
. Interferon alpha -n3 (Alferon N) ni sindano inayotumika kwa chunjua ambazo hazisikii dawa nyingine, lakini ina madhara mengine mengi.
. Imiquimod (Aldara) hutumika kama cream na maumivu wakati ukipaka hutokea.

Katika ukurasa mwingine tumezielezea chunjua za aina nyingine zikiwemo common warts, flat warts, filiform warts na periungual warts.

Usisite kuuliza maswali uliyo nayo au kutoa ushauri wako kuhusu mada yetu ya leo.

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu ndani ya saa za kazi kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu