Mwanamke Kukosa Hedhi (Amenorrhea), Nini Chanzo Cha Tatizo?

Katika mada yetu ya leo tutalijadili tatizo la kukusa hedhi ambalo kitaalamu huitwa amenorrhea.
Kuna aina mbili za tatizo la kukosa hedhi ambazo ni primary na secondary amenorrhea. Primary amenorrhea ni wakati ambapo mtu hajawahi kupata hedhi hata mara moja hadi anapofikia umri wa miaka 15. Secondary amenorrhea inatokea wakati mtu anakosa hedhi kwa kipindi cha miezi mitatu mfululizo. Katika ukurasa huu tutajadili sababu za kukosa hedhi na kuna ni nini unaweza kufanya endapo unatokewa na hali hii.

Sababu ya kawaida ya kukosa hedhi ni ujauzito. Sababu nyingine ya kukosa hedhi ni dosari katika viungo vinavyojenga mfumo wa uzazi au tezi zinazosaidia kudhibiti viwango vya homoni katika mwili. Tiba ya chanzo cha tatizo mara nyingi huondoa tatizo hili la mwanamke kukosa hedhi.

Amenorrhea hugawanywa katika aina mbili ambazo ni  Primary amenorrhea na Secondary Amenorrhea

. Primary amenorrhea ni kukosekana kwa hedhi na mabadiliko ya kijinsia (kama kuota maziwa na kuota mavuzi) kwa msichana wa miaka 14 au kukosekana kwa hedhi kukiwa na mabadiliko ya kijinsia kwa msichana wa miaka 16.

Sababu Za Primary Amenorrhea

Primary amenorrhea inaweza kutokea kwa sababu kuu mbili:

. Chromosomal or genetic abnormalities. Dosari kwenye kromosomu(nyuzinyuzi katika kiini cha seli zenye jeni na jeni (sehemu ya DNA inayorithisha tabia au umbile fulani.) Tatizo hili linaweza kusababisha ovari zisimame kufanya kazi vizuri. Turner syndrome, hali ambayo inayotokana na liwango kidogo au kukosekana kabisa kwa X chromosome na androgen insensitivity syndrome, ambazo dalili zake ni kuwa na kiwango cha juu cha testosterone, ni mifano miwili ya dosari za kijenetiki ambayo inaweza kusababisha kuchelewa au kuvuruga hedhi.

. Problems with the hypothalamus or pituitary gland. Matatizo ya tezi za hypothalamus au pituitary katika ubongo yanaweza kusababisha kuvurugika kwa uwiano wa homoni na kuzuia uanzaji wa hedhi. Hali kama za tabia mbaya ya kula, mazoezi ya kupita kipimo, na msongo mkali wa mawazo au mchanganyiko wa vitu hivi, zinaweza kuvuruga utendaji wa kawaida wa tezi ya hypothalamus au pituitary, na kuchelewesha uanzaji wa hedhi.

Aghalabu, matatizo ya kimaumbile -kama ukosefu wa viungo vya uzazi au kuziba kwa njia za uzazi-kunaweza kusababisha primary amenorrhea. Kukosekana kwa sehemu kadhaa za ndani ya mkondo wa uzazi kunaweza kusababisha kuvurugika kwa homoni na kunaweza kuchanganyikana na matatizo ya tezi za hypothalamus na pituitary na kusimamisha hedhi. Kuziba kwa njia za uzazi kunaweza pia kutoka kwa damu, ikaonekana kuwa kuwa msichana ana tatizo la kukosa hedhi, hata kama mzunguko wake wa hedhi upo sawa.

Secondary amenorrhea ni kukosekana kwa hedhi kwa mwanamke ambaye awali alikuwa anapata hedhi lakini baadaye akasimama kwa miezi 3 au zaidi bila ya kuwa na ujauzito, bila ya kuwa na maziwa ya kunyonyesha, bila kuzuia mzunguko wa wa hedhi kwa vidonge, au kukoma hedhi.

Sababu Za Seecondary Amenorrhea

Kuna sababu kadhaa zinazoweza kuleta hali hii ikiwa ni pamoja na:

. Sababu za asili.

. Ujauzito ni sababu ya kawaida sana ya asili ya secondary amenorrhea
. Sababu nyingine ni kama kunyonyesha na kukoma hedhi.

. Dawa Na Tiba.

Baadhi ya vidonge vya uzazi wa mpango, sindano za kuzuia mimba, na hormonal intrauterine devices (IUDs) vinaweza kusababisha seecondary amenorrhea. Inaweza kupita miezi kadhaa baada ya kusimama kutumia njia hizi za uzazi wa mpango kabla ya mzunguko wa hedhi hedhi kurudi na kuwa wa kawaida.

Baadhi ya dawa, zikiwa ni pamoja na baadhi ya antidepressants na dawa za pressure, zinaweza kuongeza kiwango cha homoni inayozuia mayai kukua na mzunguko wa hedhi.

. Chemotherapy na tiba za mionzi kwa ajili ya hematologic cancer (ikiwa ni pamoja na damu, bone marrow, na lymph nodes) na saratani ya matiti au saratani ya viungo vya uzazi zinaweza kuziharibu seli zinazotengeneza homoni ya estrogen na mayai kwenye ovari, na kusababisha kukosa hedhi. Ukosefu wa hedhi wa namna hii unaweza kuwa wa kipindi kifupi, na hasa kwa wanawake wa umri mdogo.

Wakati mwingine tabaka la kovu linaweza kujijenga juu ya ngozi inayotanda juu ya mji wa mimba, na kuzuia kujibandua kwa kawaida kwa ngozi ya juu ya mji wa mimba kwenye mzunguko wa hedhi. Makovu haya hutokea baada ya dilation and curettage (D&C), ambapo tishu za nyumba ya mimba hutolewa kwa ajili ya vipimo au kutibu hedhi nzito au kuondoa ngozi ya juu ya nyumba ya mimba baada yamimba kutoa, baada ya cesarean section, au kutibu fibroids.

Hypothalamic amenorrhea.

Hali hii hutokea wakati hypothalamustezi katika ubongo inayosimamia shughuli za mwili, unapunguza kasi au kusitisha utolewaji wa gonadotropin-releasing hormone (GnRH), homoni inayoanzisha mzunguko wa hedhi. Sifa za wanawake wenye tatizo la gonadotropic amenorrhea ni pamoja na wale:

. Wenye uzito mdogo wa mwili
. Wenye asilimia ndogo ya mafuta
. Wanaopata kalori ndogo au mafuta katika chakula
. Wenye msongo wa mawazo
. Wanaofanya mazoezi mazito ya mwili na kuchoma kalori nyingi zaidi kuliko wanayoingiza mwilini kupitia chakula
. Wenye upungufu wa leptin, homoni inayojengwa na protini inayosimamia hamu ya kula na umeng’enyaji wa chakula
. Baadhi ya magonjwa wa mwili.

Ili mwanamke awe na mzunguko wa hedhi mzuri, hypothalamus, tezi ya pituitary, ovari, na uterus vyote vinatakiwa vifanye kazi ipaswavyo. Hypothalamus huiamuru tezi ya pituitary kutoa homoni za follicle-stimulating (FSH) na luteinizing (LH). FSH na LH husababisha ovari kutoa homoni za estrogen na progesterone. Estrogen na progesterone zinahusika katika mzunguko wa mabadiliko katika endometrium (utando unaofunika uterus), pamoja na hedhi. Pamoja na hayo yote, mkondo wa uke lazima uwe wazi ili kuruhusu damu ya hedhi.

Gynecological conditions

Matatizo ya uzazi na hasa yale yanayoweza kuleta au yanayotokana na hormone imbalance, yanaweza kuonyesha secondary amenorrhea kama dalili.

. Polycystic ovary syndrome (PCOS) hutokea endapo mwanamke anatengeneza homoni ya androgen kwa kiasi kikubwa zaidi kuliko kawaida. Kiasi kikubwa cha androgen kinaweza kusababisha vifuko vilivyojaa majimaji (cyst) kukua kwenye ovari, na kuzuia utolewaji wa mayai (ovulation). Wanawake wengi wengi wenye PCOS au wanakosa hedhi au wanapata hedhi zisizotabirika, hali iitwayo oligomenorrhea.

. Fragile X-associated primary ovarian insufficiency (FXPOI) ni neno linalotumika kuelezea hali ambapo ovari za mwanamke zinasimama kufanya kazi kabla ya muda wa kawaida wa kukoma hedhi, muda mchache baada y miaka 40. FXPOI hutokea kwa sababu ya mabadiliko fulani ya jeni kwenye X chromosome. FXPOI hubainika mara nyingi baina ya wanawake wanaotafuta tiba ya amenorrhea.

Thyroid problems

Thyroid ni tezi ndogo iliyo na umbo la kipepeo iliyoko chini kidogo ya kikoromeo. Thyroid hutengeneza homoni zinazosimami ujenzi na uvunjaji wa kemikali mwilini na zina nafasi kubwa katika balehe na hedhi. Tezi inaypfanya kazi kupitiliza (hyperthyroidism) au kufanya kwa kiwango cha chini (hypothyroidism) inaweza kusababisha mvurugano wa mzunguko wa hedhi, pamoja na kukosa hedhi.

Pituitary tumors

Tezi ya pituitary katika ubongo husimamia utolewaji wa homoni zinazoathiri utendaji wa viungo vingi vya mwili, ikiw ano pamoja na umeng’enyaji wa chakula na mfumo wa uzazi. Uvimbe juu ya pituitary mara nyingi zsi hatarishi (benign) lakini unaweza kuvuruga utolewaji wa homoni za kusimamia hedhi katika mwili.

Ili mwanamke awe na mzunguko wa hedhi mzuri, hypothalamus, tezi ya pituitary, ovari, na uterus vyote vinatakiwa vifanye kazi ipaswavyo. Hypothalamus huiamuru tezi ya pituitary kutoa homoni za follicle-stimulating (FSH) na luteinizing (LH). FSH na LH husababisha ovari kutoa homoni za estrogen na progesterone. Estrogen na progesterone zinahusika katika mzunguko wa mabadiliko katika endometrium (utando unaofunika uterus), pamoja na hedhi. Pamoja na hayo yote, mkondo wa uke lazima uwe wazi ili kuruhusu damu ya hedhi.

Nini Kinasababisha Kukosa Hedhi?

Amenorrhea inaweza kutokea kwa sababu nyingi. Baadhi zikiwa ni za kawaida katika maisha ya mwanamke, wakati nyingine zikisababishwa na matumizi ya madawa au zikiwa ni ishara ya tatizo la kiafya. Tatizo la kukosa hedhi linaweza kusababishwa na dosari yo yote kwenye hypothalamus, pituitary, ovari, mkondo wa uke au za kiutendaji kimwili.

Sababu za kawaida

. Ujauzito
. Kunyonyesha
. Kukoma hedhi

Dawa za Kuzuia Mimba

Wanawake wengine wakitumia vidonge vya kuzuia mimba hukosa hedhi. Hata baada ya kuacha matumizi ya vidonge hivyo, huwachukua muda miili yao kurudi kwenye hali za kawaida na kuanza kuona hedhi zao. Njia za sindano au kupandikiza zaweza pia kuleta tatizo la kukosa hedhi.

Mitindo Ya Maisha

Baadhi ya mitindo ya maisha huweza kuchangia mwanamke kukosa hedhi. Kwa mfano:

. Kuwa na uzito mdogo sana. Kuwa na uzito mdogo kupita kiasi – asilimia 10 chini ya uzito wa kawaida – husimamisha shughuli nyingi za homoni ndani ya mwili, hivyo kusimamisha uzalishaji wa mayai.

. Mazoezi zaidi ya kawaida. Wanawake wanaoshiriki shughuli zinazodai mazoezi ya juu, hujikuta wakipoteza hedhi zao. Baadhi ya sababu zinachangia kwa wanariadha, ikiwa ni pamoja na uzito mdogo, kuwa na mafuta kidogo ndani ya mwili, msongo wa mawazo na matumizi makubwa ya nishati ya mwili.

. Msongo wa mawazo. Msongo wa mawazo huweza kubadilisha kwa muda utendaji kazi wa hypothalamus – sehemu ya ubongo inayosimamia homoni zinazoratibu hedhi. Uzalishaji wa mayai na hedhi, hivyo vyaweza kusimama. Hedhi za kawaida hurudi baada ya msomgo wa mawazo kupungua.

Kukosa Uwiano Wa Homoni

Matatizo kadhaa katika viungo vya mwili huweza kuvuruga mpangilio wa homoni katika mwili, ikiwa ni pamoja na:

Sababu Zinazotokana Na Hypothalamus
. Uvimbe karibu na tezi ya pituitary (Craniopharyngioma)
. Kallman syndrome (upungufu wa gonadotropins, homoni zenye uwezo wa kusimamia ukuaji na ufanyaji kazi wa viungo vya uzazi )
. Upungufu wa lishe
. Uzito mdogo au kuchelewa kukua

Sababu Za Tezi Ya Pituitary
. Uwingi wa homoni ya prolactin, homoni inayosimamia utoaji wa maziwa wakati mama ananyonyesha, katika damu. Hali hii kitaalamu huitwa prolactilemia na husababishwa na uvimbe (prolactinoma) katika tezi ya pituitary.

. Dosari zinazoanzia kwenye uvimbe wa aina nyingine wa kwenye pituitary (kama, cushing syndrome, acromegaly, au thyroid-stimulating hormone)
. Kufa kwa seli za pituitary baada ya mwanamke kujifungua

. Seli za pituitary kufa baada ya kushambuliwa na kinga za mwili (autoimmune hypophysitis)

. Uvimbe ndani ya tezi ya pituitary

. Ugonjwa ambao hushambulia pituitary (sarcoidosis)

Sababu Zinazotokana Na Ovari

. Kutozalishwa kwa mayai (anovulation)

. Kuwa na uwingi wa homoni za kiume ndani ya damu (hyperandrogenemia)

. Kuvurugika kwa homoni (Polycystic ovary syndrome)

amenorrhea polycystic ovarian syndrome

. Kufeli kwa ovari mapema

. Ugonjwa wa kurithi unaodumaza ovari,  kuzuia hedhi (Turner syndrome)

. Seli za ovari kushambuliwa na kinga za mwili (Autoimmune oophoritis)

. Mionzi au tiba za chemotherapy

. Ugonjwa wa kurithi unaojaza galactose ndani ya damu (Galactosemia)

. Dosari za kimaumbile katika mkondo wa njia ya uzazi

Sababu za Kiutendaji

. Kuwa na uzito mdogo kwa sababu ya kuogopa kula (anorexia)/kula kupita kiasi (bulimia)

amenorrhea uzito mdogo

 

. Magonjwa sugu kama TB

.Kunenepa au kukonda kupita kiasi

. Utapiamlo

. Mfadhaiko au matatizo mengine ya kiakili

. Msongo wa mawazo wa kupitiliza

 

Matatizo Ya Kimaumbile

Matatizo katika viungo vya uzazi yanaweza kusababisha amenorrhea. Mifano ni kama:

Makovu kwenye tumbo la uzazi. Tatizo lilitwalo Asherman’s syndrome – kujenga kwa makovu juu ya ngozi ya juu ya uterus – huweza kutokea baada ya oparesheni ya uzazi, au baada ya tiba ya fibroids. Makovu kwenye uterus huzuia ujenzi wa kawaida na kujibandua kwa ngozi hiyo ya juu.

amenorrhea ovary

 

 

 

 

 

 

 

Kukosa Viungo Vya Uzazi. Wakati mwingine matatizo yanaanzia kwenye ukuaji wa mtoto tumboni yanayosababisha msichana azaliwe bila baadhi ya viungo vya uzazi, kama uterus, cervix au uke. Kwa sababu viungo vyake havikukua vizuri, haweza kupata hedhi.

Dosari Za Kimaumbile Za Uke. Kitu kitakachoziba njia ya uke kinaweza kusababisha kuonekana kwa hedhi ya wazi. Kunaweza kukatokea utando au ukuta katika uke ambao utazuia utokaji wa damu kutoka kwenye uterus na cervix.

Dalili Za Amenorrhea

Amenorrhea ni dalili kuwa kuna tatizo lililochificha na si ugonjwa ka yenyewe. Dalili nyingine huwez kutokea kulingana na chanzo cha tatizo hilo la kukosa hedhi.

. Kutoka maziwa kwa mwanamke ambaye hana ujauzito, hali ambayo kitaalamu huitwa Galactorrhea, maumivu ya kichwa, kutokuona vizuri kingo za vitu vinaweza kuwa dalili za uvimbe ndani ya fuvu la kichwa.

. Kuongezeka kwa uotaji wa nywele kwa mtindo wa kiume (hirsutism), sauti nzito, chunusi kunaweza kusababishwa na kuzidi kwa androgen (homoni inayochangaia ujenzi wa tabia za kiume).

. Uyabisi wa uke, vipindi vya mwili kuwa na joto, kutoa jasho usiku, kukosa usingizi mzuri vinaweza kuashiria dasari katika ovari au kufeli kwa ovari.

. kuongeza kwa mwili au kukonda.
. Kuwa na wasiwasi kunaweza kujitokeza kwa mwanamke mwenye matatizo ya kiakili

Katika kurasa nyingine tutazungumzia matatizo ya maumivu kabla ya hedhi, maumivu wakati wa hedhi na matatizo ya kukoma hedhi. Jisikie huru kuuliza maswali uliyo nayo au kutoa ushauri wako kuhusu uandishi wa mada yetu hii ya leo. Tutafurahi sana kukujibu.

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini, au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu ndani ya muda wa kazi kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.