Nini Chanzo Cha Kutoona Vizuri Usiku (Night Blindness)?

 

kutoona usiku chanzo

 

Night blindness ni aina moja ya matatizo ya kutoona vizuri ambayo pia huitwa nyctalopia. Watu wenye tatizo hili hupata shida kuona usku au kwenye mazingira yenye mwanga hafifu. Haimaanishi kutoona kabisa usiku, bali kuona kwa shida au kushindwa kuendesha gari usiku.

Mwanga ukiwa hafifu, jicho linatakiwa kuwa na wepesi wa kubadilika na kuendana na mazingira. Night blindness hukufanya ushindwe kuona vizuri mwanga ukipungua. Unaweza kushindwa kuziona alama za barabarani wakati ukuendesha. Unaweza pia kuchukua muda mrefu kuendana na mazingira wakati ukitoka eneo lenye mwanga mkali na kuindia eneo la giza. Night blindness huweza pia kukufanya ushindwe kuziona nyota usiku, au vitu ndani ya chumba cha giza.

Unapata kutambua sura za watu mwanga ukiwa hafifu? Au, unapata shida kutoka chumba kimoja na kuingia kingine kukiwa na giza? Kama majibu ni ndiyo, basi unaweza kuwa na tatizo hili.

Aina nyingine za night blindness hutibika wakati kuna aina ambazo hazina tiba. Ukikijua chanzo cha tatizo lako, unaweza kuja hatua za kuchukua ili kuboresha uonaji wako.

 

Nini Husababisha Usione Usiku?

 

Sababu kubwa ya kushindwa kuona usiku ni upungufu wa vitamini A, ambayo huhusika na afya ya seli za rod (rod cells) na retina. Kuna sababu nyingine pia zinazoweza kuchangia. Hapa chini tunazijadili sababu za kushindwa kuona vizuri gizani:

. Retinitis pigmentosa: Ni ugonjwa wa kurithi ambao huharibu uwezo wa kuona. Kuodhoofika kwa taratibu kwa seli za rod photoreceptor ndani ya retina husababisha hali hii. Huanza taratibu kwa kushindwa kuona maeneo ya pembeni na sehemu za mwanga mdogo.

. Retinal detachment: Tatizo hutokea pale retina ya mgonjwa huachana na tabaka la chini yake. Hali hii hufanya namna ya pazia jeusi mbele ya sehemu unayoiona. Mwisho wake uwezo wa jicho kuona kwenye maeneo ye mwanga mdogo au gizani hupungua.

. Oguchi disease: Ni ugonjwa unaopunguza uwezo wa jicho kuendana na mabadiliko ya mazingira unapoingia sehemu za giza.

 . Myopia: Huu ni ugonjwa unaokufanya uone vizuri vitu vya karibu yako. Ugonjwa huu hukufanya kutoviona vitu vizuri ukiwa gizani, na hasa usiku.

. Cataract: Ingawa huu ni ugonjwa wa kipekee, mtoto wa jicho huchangia sana katika kutoona vizuri usiku. Mwathirika mara nyingi huviona vitu kwenye ukungu, rangi zilizopauka na kutoona katika giza.

. Vitamin A deficiency: Vitamini A ina nafasi kubwa katika kuubadili mwanga na kuwa signali za umeme ndani ya seli za rod. Utafiti imethibitisha kuwa upungufu wa vitamini A huathiri uwezo wa kuona usiku moja kwa moja. Mama mjamzito mwenye upungufu wa vitamini A anaweza kuzaa mtoto mwenye tataizo la kuona usiku toka utotoni.

. Medications: Sumu kwenye retina zinazotokana na madawa kama phenothiazenes zinaweza kuathiri uwezo wa kuona rangi za bluu-njano, tatizo linalojionyesha zaidi kwenye mwanga mdogo.

. Refractive surgery: Baadhi ya upasuaji kama radial keratotomy, photorefractive keratectomy na LASIK unaweza kuathiri uwezo wa kuona na kupambanua rangi kwa kipindi fulani.

 

Dalili Za Night Blindness

 

Kuna dalili za night blindness ambazo ukiziona inakubidi kuchukua tahadhari mapema. Baadhi ya dalili hizo ni:

. Kutumia nguvu ili kuweza kuona vizuri sehemu za giza
. Kujiona huna uwezo wa kuona mbali wakati ukivichungulia vitu vya mbali
. Kuona kama kuna ukungu mbele yako
. macho makavu, mekundu yanayowasha
. Kutopata raha usiku ukiingia.

 

Aina Za Night Blindness

 

. X1A: Hujionyesha kwa conjuctiva xerosis – ukavu kwenye ngozi angavu, nyembamba yenye majimaji, inayotanda juu ya jicho na ngozi ya ndani ya kope. Dalili kuu ni rangi, kukosa uangavu, kujikusanya kwa uchafu na baadaye kuvimba kwa conjuctiva.

. X1B: Dalili zake ni kutokea kwa doa la kijivu, linalotanda juu ya conjuctiva.

. X2: Eneo la juu la cornea huwa na sura ya chembechemba ndogo, hali inayoifanya cornea kuwa na ukungu wa kudumu.

. X3A: Vidonda huweza kutokea juu ya cornea, ambavyo vinaweza kupunguza unene wa cornea.

. X3B: Keratomalacia huweza kuonekana, ambayo husababisha cornea kuwa laini kupita kiasi na taratibu kuanza kuliharibu jicho.

 

Ufanyeje Kuzuia Tatizo La Kutoona Vizuri Usiku?

 

Huwezi kulizuia tatizo la kutoona usiku linalotokana na mapungufu ya kurithi, kama Usher syndrome. Lakini, unaweza kufuatilia kiwango cha sukari ndani ya damu yako na kula mlo uliokamilika ili kuondokana na tatizo la kutoona vizuri uasiku.

Unashauriwa kula chakula chenye uwingi wa antioxidants, vitamini na madini, ambavyo vinaweza kuzuia mtoto wa jicho (cataract). Vile vile, chagua chakula chenye viwango vikubwa vya vitamini A ili kuondoa uwezekano wa kupata tatizo la kutoona vizuri usiku.

Baadhi ya vyakula ambavyo ni vyanzo bora vya vitamini A ni pamoja na:

vitamin A

. cantaloupes
. viazi vitamu
. karoti
. maboga
. butternut squash
. maembe

Pia vitamini A hupatikana ndani ya:

. spinach
. collard greens
. maziwa
. mayai.

 

 

DAWA YA KUTOONA VIZURI USIKU

 

 

Katika ukurasa mwingine, tutauzungumzia ugonjwa  wa mtoto wa jicho (catract). Usisite kuuliza maswali uliyo nayo kuhusu mada yetu ya leo. Tutafurahi kuona kuwa tumekujibu vizuri na kwa wakati.

 

Kwa mawasiliano na maelezo zaidi tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu kwenye nambari zifuatazo: +255 655 858027 au +255 756 181651.

 

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wetu wa Facebook wa LINDA AFYA YAKO kupata mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya mwanadamu na tiba mbalimbali. Usikose kuweka LIKE endapo utafurahishwa na mada hizo.