Cytolytic Vaginosis Ni Nini? Mwanamke Kutoka Uchafu Mweupe Ukeni Ni Tatizo Gani?

 

uchafu ukeni

 

Kutoka uchafu ukeni ni moja ya matatizo yanayowasumbua sana wanawake. Uchafu huu unaweza kutoka kwa sababu nyingi, sababu zinazoonekana zaidi zikiwa ni yeast, trichomoniasis na bacterial vaginosis. Katika mada yetu ya leo tutalijadili moja la matatizo haya ambalo linasababisha mwanamke kutokwa uchafu mweupe unaoambatana na miwasho sehemu za siri ambalo kiutaalamu huitwa cytolytic vaginosis..

Kimaumbile uke wa mwanamke ulio katika hali yake nzuri una aina nyingi sana za bakteria na idadi ndogo ya fungus wanaoishi ndani yake. Katika viumbe hawa wadogo wapo ambao ni rafiki na wengine ni wabaya kwa afya ya mwanamke. Bakteria rafiki hufanya kazi ya kuwadhibiti wale wabaya. Bakteria mmoja anayejulikana sana ni lactobacillus acidophilus ambaye anafanya kazi ya kuwaweka viumbe wengine pamoja na fungus kwenye idadi inayotakikana.

 

Cytolytic Vaginosis Husababishwa Na Nini?

 

Mwanasayansi Doderlein ndiye aliyegundua kuwa kiumbe ambaye anapatikana kwa wingi zaidi katika uke wa mwanamke wa umri wa kuzaa ni bakteria aitwaye lactobacillus acidophilus. Aligundua kuwa uwepo wa bakteria huyu pamoja na oestrogen ni muhimu katika kuuweka uke wa mwanamke kwenye kiwango kinachotakiwa cha pH 4.0-4.5. Lactobacilli hutengeneza tindikali (lactic acid) kutokana na glucose na kuuweka uke katika hali ya utindikali. Baada ya balehe, kwa kuwezeshwa na uwepo wa oestrogen, glycogen hutunzwa kwenye seli za ngozi laini inayotanda kuuzunguka uke, ambayo huvunjwavunjwa na seli za epithelial za uke na kuwa glucose. Lactobacilli huigeuza glucose hii kuwa lactic acid.

Baadhi ya aina za lactobacilli hutengeneza hydrogen peroxide (H2O2) ambayo ni antiseptiki (inaua baadhi ya viumbe wadogo waharibifu). Hydrogen peroxide inaweza kuzuia ukuaji wa baadhi ya wadudu wadogo kama E. coli, aina za Candida albicans, Gardnerella vaginalis na aina za Mobilincus. Inafikiriwa kuwa hydrogen peroxide inayotengenezwa na lactobacilli inaweza pia kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI (VVU). Utafiti mwingine unaonyesha kuwa lactobacilli huzuia kukua kwa candida kwa kuzuia yeast kunata kwenye seli za ngozi laini ya inayofunika uke.

Idadi ndogo ya lactobacilli (bacilli 5 kwa seli 10 za squamous) katika ute unaotoka ukeni imeonekana kuwa inasaidia kuulinda uke dhidi ya candida. Wakati mwingine bakteria hawa wa lactobacilli huongezeka sana katika mwili wa mwanamke huyu wa umri wa kuzaa. Hali hii husababisha bakteria hawa (wakati mwingine wakisaidiana na bakteria wa aina nyingine) kuharibu ngozi inayotanda uke kwa kuziua seli za ngozi hiyo wakati wakimeng’enya glycogen iliyotunzwa katika seli hizo. Cytolysis maana yake kufa kwa seli kutokana na kuharibiwa kwa ngozi laini (cell membrane) inayotanda juu ya seli hiyo. Cytolysis hutokea pale seli inaposhambuliwa na virusi, bakteria au kinga za mwili kuua seli zilizoshambuliwa na wadudu. Seli hizi zilizokufa hutoka nje ya uke na ndizo zinazosababisha uchafu mweupe, hali ambayo huitwa cytolytic vaginosis.

Tatizo hili la kutoa uchafu ukeni mara nyingine husababishwa na tiba ya fungus au bakteria pale uchunguzi unapofanywa na kwa makosa kutoa tiba za antifungal au antibiotics.

Wanawake wenye kisukari wanaweza kuwa na kiwango kikubwa cha glycogen (glucose kwenye maeneo ya uke) ambayo huwalisha lactobacilli na kuwafanya wazaliane kupita kiasi. Dalili huonekana zaidi wakati wa luteal (kipindi kinachoanza baada ya kutoa yai hadi siku ya kwanza ya hedhi), wakati ambapo kiwango cha oestrogen ndani ya mwili hupanda, na kusababisha kutolewa zaidi kwa glycogen na kuwalisha lactobacilli.

 

Dalili Za Cytolitic Vaginosis

 

uchafu wa ukeni

 

Dalili za cytolytic vaginosis zinafanana sana na zile za yeast hivyo uchunguzi wa kina unahitajika. Kwa ujumla dalili huwa zifuatazo:

. Uchafu mweupe, mwepesi au mzito
. Miwasho ndani ya uke au nje (pruritus vulvae)
. Maumivu hasa wakati wa kukojoa (dysuria)
. Maumivu wakati wa tendo la ndoa (dyspareunia)
. Uchafu kuogezeka zaidi kila mwanamke aingiapo kipindi cha luteal (baada ya kutoa yai)
. Kuwa na hasira

 

Tiba Ya Tatizo La Kutoa Uchafu Ukeni 

 

Bakteria hawa wa lactobacilli wanaweza kupunguzwa idadi kwa kupandisha pH ya uke kwa kutumia sodium bicarbonate (baking soda). Tiba inapaswa iwe imeweza kuurudisha uwiano wa bakteria hawa katika wiki tatu. Kama katika kipindi hicho, hali itakuwa mbaya zaidi au itabaki vile vile, acha matumizi ya baking soda na fanya uchunguzi upya.

 

uchafu ukeni

 

Mchanganyiko Wa Baking Soda Kwa Tiba Ya Cytolitic Vaginosis:

. Kijiko 1-2 cha baking soda
. Vikombe 4 vya maji

Jisafishe mara mbili kwa wiki, pumzika wiki moja, vivyo hivyo kwa wiki tatu.

Yafuatayo yanaweza kusaidia kuongeza pH ya uke na hivyo kupunguza mwongezeko wa lactobacilli:

– Kupunguza au kuacha kutumia sukari
– Kuacha kutumia sabuni au maji ya baridi
– Kuacha kutumia antibiotics au dawa za fungus
– Kupumzika kufanya tendo la ndoa
– Kuacha kutumia spray za ukeni
– Vaa chupi za pamba na nguo zisizobana
– Usivae chupi usiku                                                                                                                                         – Kupunguza kiwango cha sukari katika mlo

Katika mada nyingine tutayajadili matatizo mengine yanayosababisha mwanamke kutoa uchafu ukeni ya candida albicans, trichomoniasis  na bacterial vaginosis. Usisite kuuliza maswali au kutoa maoni yako kuhusu mada yetu ya leo. Tutafurahi sana kukujibu.

 

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

 

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.