Kutoka Maziwa Bila Kuwa Na Mimba (Galactorrhea)

 

 

kutoka maziwa bila ya kuwa na mimba

 

 

Ni kawaida kwa mwanamke mzazi kutokwa maziwa na maziwa, na wakati mwingine maziwa yanaweza kutoka wakati wa ujauzito. Lakini yawezekana majimaji yenye rangi ya maziwa yakatoka kwenye chuchu moja au zote za mwanamke -hata kwa baadhi ya wanaume -wakati mwanamke hana ujauzito au hanyonyeshi. Tatizo hili kitaalamu huitwa galactorrhea na linaweza kutokea kwa sababu nyingi. Inasemekana tatizo hili huwatokea asilimia 20 hadi 25 ya wanawake. Makala yetu ya leo inaelezea sababu za mwanamke kutoka maziwa bila ya kuwa na mimba, na ni wakati gani wa kumwona daktari.

Homoni iitwayo prolactin ndiyo inayosababisha maziwa kutoka wakati wa ujauzito au wakati wa kunyonyesha baada ya kuzaa. Watu wenye tatizo la kutoka maziwa bila ya kuwa na mimba wanaweza kuwa wanatengeneza prolaction kwa wingi mno katika miili yao. Kiwango cha prolactin katika mwili huweza kupanda kutokana na:

. matumizi ya madawa
. magonjwa kwenye matiti
. uvimbe
. kutomasatomasa sana maziwa

Baadhi ya madawa husababisha kutoka maziwa. Dawa hizo ni pamoja na:

. antipsychotic
. dawa za kutibu mfadhaiko (antidepressant)
. uzazi wa mpango
. dawa za kuingulia
. baadhi ya dawa za maumivu
. dawa za blood pressure
. dawa zenye homoni

Matatizo ya kimwili huweza pia kuchangia kwenye tatizo la kutoka maziwa bila ya kuwa na mimba, nayo ni pamoja na:

. matatizo ya thyroid
. matatizo ya figo na ini
. msongo wa mawazo ulio sugu
. uvimbe au magonjwa kwenye hypothalamus
. kuumia ua uharibifu kwenye tishu za ubongo
. viwango vikubwa vya estrogen (kwa vichanga)
. upungufu wa testosterone kwa wanaume

Matumizi ya madawa

Matumizi ya mara kwa mara ya madawa, kama opiates, marijuana, na cocaine, yanaweza kuchangia kwenye kutoka kwa maziwa bila mimba.

Kutomasatomasa Maziwa

Kwa baadhi ya watu, kutomasatomasa maziwa kwa mara kwa mara kunaweza kusababisha kutoka kwa maziwa. Hii inaweza kuwa ni kuyatomasatomasa maziwa wakati wa tendo la ndoa, kuchekiwa kwa mara kwa mara kwa matiti, au kutokana na nguo kusugua mara kwa mara kwenye chuchu.

Mara chache, watu wanaweza kutoka maziwa kutokana na mwitiko wa kihisia kutokana na mtoto wa jirani. Utafiti mmoja ulibaini kuwa mwanamke alitoka maziwa alipopapaswa alipokuwa karibu na kichanga cha jirani. Maziwa yaliacha kutoka alipokuwa mbali na kichanga. Katika hali hii, madaktari waliamini kuwa kutoka kwake kwa maziwa kulihusiana na hisia zilizoanzia kwa kile kichanga.

Wakati mwingine, madaktari wanashindwa kubaini chanzo halisi cha tatizo hili. Katika hali hii, ugonjwa huu huitwa idiopathic galactorrhea. Watu wenye idiopathic galactorrhea wanaweza kuwa na matiti yenye usikivu mkubwa mno wa prolactin, maana yake ni kwamba hata viwango vidogo vya kawaida vya prolactin husababisha maziwa kutoka.

Dalili Za Maziwa Kutoka Bila Mimba

 

Dalili za tatizo hili la kutoka maziwa bila mimba zinaweza kuwa tofauti kulingana na chanzo cha tatizo, lakini mara nyingi huwa ni:

 

kutoka maziwa bila ujauzito

. Kutoka maziwa muda wote au mara chache kutoka kwenye chuchu moja au zote
. Kuvuja kwa maziwa, yenyewe au kwa kukamua kwa mkono
. Hedhi ambazo hazitabiriki
. Kuumwa kichwa au matatizo ya kuona.

Wanaume wenye tatizo hili wanaweza pia kuona yafuatayo:

. kuvimba matiti kwenye eneo linalozunguka chuchu
. maumivu ya mbali kwenye eneo la titi
. kupata shida ya uume kusimama
. kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa.

 

Tiba Ya Maziwa Kutoka Wakati Huna Mimba

 

Baada ya daktari kujua chanzo cha tatizo atakushauri tiba. Kuna vitu unavyoweza kuvifanya mwenyewe, kama kuacha kuvaa nguo zinazobana na kupunguza kutomasatomasa matiti wakati wa tendo la ndoa.

Tiba ambazo zinaweza kushauriwa na daktari ni kama kubadili dawa unazotumia (kama kutumia aina nyingine ya dawa ya kupunguza mfadhaiko) au kuongeza dawa za kudhibiti homoni.

Kuacha matumizi ya dawa za kulevya, kuacha matumizi ya marijuana, na opiates, husaidia kuliondoa tatizo hili. Lakini inaweza kupita miezi michache kabla ya tatizo kuondoka kabisa.

Kama chanzo ni uvimbe au tatizo katika tezi ya pituitary, unaweza kuhitaji upasuaji.

Dawa zinaweza kutumika kupunguza kiwango cha prolactin. Bromocriptine ni dawa inayoweza kutolewa ili kupunguza kiwango cha homoni ya prolactin katika damu, dawa ambayo pia inaweza kuondoa dalili za kutoka maziwa.

Taarifa nzuri ni kwamba tatizo la kutoka maziwa linaweza kuondoka lenyewe au baada ya kupata dawa ya chanzo chake. Lakini kama majimaji yanayotoka hayana rangi ya maziwa na yanaonekana kuwa kama maji kabisa, au yana damu, au ya njano, sasa tatizo linaweza kuwa kubwa. Hizi zinaweza kuwa ni dalili za saratani ya matiti. Unatakiwa kumwona daktari mara moja.

Katika mada nyingine tutalizungumzia tatizo la saratani ya matiti. Usisite kutoa maoni yako kuhusu mada yetu ya leo au kuuliza maswali uliyo nayo.

 

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

 

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.