Chembe Ya Moyo (Angina) Ni Tatizo Gani?

 

Chembe ya moyo ni hali ya kusikia kubanwa, kwamba kuna uzito, au maumivu kwenye kifua. Watu wengine wenye chembe ya moyo husema kuwa wanasikia kama vifua vyao vinaminywa au kama kuna kitu kizito kimewekwa kwenye kifua. Tatizo hili kitaalamu huitwa angina au angina pectoris. Pamoja na kwamba ni tatizo linalowapata watu wengi, bado ni vigumu kutofautisha angina na maumivu ya aina nyingine, kama kutojisikia vizuri kutokana na chakula kutoyeyushwa vizuri tumboni (indigestion.) Angina ni aina ya maumivu ya kifuani yanayotokana na kupungua kwa mtiririko wa damu kwenye eneo la misuli ya moyo. Chembe ya moyo si tatizo la kutishia sana maisha, lakini inaweza kuwa na dalili za heart attack , na ni kiashiria cha ugonjwa wa moyo (coronary heart disease -CHD.) Kwa kawaida, angina hutokea kutokana na moja au ateri zaidi ya moja za kupeleka damu kwenye moyo zikiwa nyembamba au zikiziba.

Dalili Za Chembe Ya Moyo

Dalili za chembe ya moyo ni pamoja na maumivu ya kifuani, ambayo yanaweza kuelezewa kama kubana, kuwaka au kujaa kwa kifua. Unaweza kuona maumivu kwenye mikono, shingo, taya, mabega au mgongoni. Dalili nyingine za chembe yachembe ya moyo moyo ni:

. Kizunguzungu
. Uchovu
. Kichefuchefu
. Kukosa pumzi
. Kutoka jasho

Dalili hizi zinatakiwa zichunguzwe na daktari ili kuweza kubaini kama una stable angina au unstable angina, ambayo inaweza kuwa ni kiashiria cha heart attack.

Stable Angina

Stable angina hutokea wakati moyo ukifanya kazi zaidi ya kawaida -kama wakati wa mazoezi. Hali hii huchukua kama dakika tano. Ni tatizo linalojirudiarudia, na linaweza kumpata mtu kwa miezi kadhaa au miaka. Kupumzika au kutumia dawa huondoa tatizo. Kwa mfano, maumivu wakati unapanda mlima au kwenye hali ya baridi.

Unstable Angina (inahitaji uangalizi)

Unstable angina hutokea hata wakati wa kupumzika na huwa tofauti na maumivu yale uliyoyazoea. Unstable angina huja bila kutarajia, maumivu huwa makali zaidi na huchukua muda mrefu zaidi, dakikia 30 au zaidi. Unstable angina inaweza isiondoke kwa kupumzika au kutumia dawa. Unstable angina inaweza kuwa ni kiashiria cha heart attack.

Kuna aina nyingine ya angina, iitwayo variant angina au Prinzmental’s angina. Hii huonekana mara chache sana. Angina hii husababishwa na kukaza kwa ghafla kwa ateri za moyo ambako kwa muda mfupi hupunguza mtiririko wa damu kuelekea kwenye moyo.

Variant Angina

Variant angina mara nyingi hutokea ukiwa unapumzika na huja kwa nguvu sana. Angina hii huondoka kwa matumizi ya dawa.

Angina Kwa Wanawake

Dalili za angina kwa wanawake zinaweza kuwa tofauti na zile zinazowatokea wanaume. Tofauti hizi huweza kusababisha wanawake kupata tiba. Kwa mfano, maumivu ya kifuani ni dalili ya kawaida kwa wanawake wenye angina, lakini inaweza isiwe dalili pekee au inayojionyesha zaidi. Wanawake wanaweza kuwa na dalili nyingine kama:

. Kichefuchefu
. Kubanwa pumzi
. Maumivu ya tumbo
. Usumbufu shingoni, kwenye taya au mgongoni
. Maumivu ya kuchoma badala ya kubanwa kifua.

Chanzo Cha Chembe Ya Moyo

Chembe ya moyo hutokana na kupungua kwa mtiririko wa damu kwenye misuli ya moyo. Damu huisafirisha oksijeni, ambayo huhitajika na moyo ili uwe na afya. Misuli ya moyo ikikosa oksijeni kwa kiwango cha kutosha, hali iitwayo ischemia hutokea.

Chanzo kikubwa cha kupungua kwa mtiririko wa damu kwenye misuli ya moyo ni ugonjwa wa ateri ya coronary -coronary artery disease (CAD).

Ateri za coronary za moyo zinaweza kupungua kipenyo kwa sababu ya matabaka ya mafuta yaitwayo plaques. Hali hii huitwa atherosclerosis.

Wakati wa mahitaji madogo ya oksijeni -kwa mfano, wakati unapumzika -misuli ya moyo wako inaweza kuendelea kufanya kazi vizuri bila ya kukuletea dalili za tatizo la chambe ya moyo. Lakini ukiongeza mahitaji ya oksijeni, kama unapofanya mazoezi ya mwili, angina itatokea.

. Stable angina. Stable angina kwa kawaida husababishwa na mwili kufanya kazi. Unapopanda ngazi, ukifanya mazoezi au kutembea, mwili wako unahitaji damu zaidi, lakini mishipa ya ateri iliyosinyaa hupunguza mtiririko wa damu. Zaidi ya mwili kufanya kazi, vitu vingine kama msongo wa mawazo, hali ya hewa ya ubaridi, milo mizito na kuvuta sigara vinaweza kuzifanya ateri zisinyae na kusababisha angina.

Unstable angina. Kama matabaka ya mafuta (plaques) yatavunjikia ndani ya mshipa wa damu au damu ikiganda na kutengeneza vijibonge ndani ya mishipa, vinaweza kwa haraka kuziba au kupunguza mtiririko wa damu kwenye mshipa ulio na kipenyo kidogo na kupunguza kwa kiasi kikubwa damu inayofika kwenye misuli ya moyo. Unstable angina inaweza vile vile kusababishwa na vibonge vya damu vinavyoziba kabisa au kuziba kwa kiasi fulani mishipa ya damu ya moyo.

Unstable angina huendelea kuwa mbaya na haipungui kwa kujipumzisha au kutumia dawa. Mtiririko wa damu usipoongezeka, moyo wako utakosa oksijeni na heart attack inaweza kutokea. Unstable angina ni hatari na huhitaji tiba ya dharura.

chembe ya moyo coronary artery

. Prinzmetal’s angina. Aina hii ya angina inatokana na mkazo wa ghafla kwenye ateri ya coronary, ambao kwa kipindi kifupi huibana ateri. Kubana huku hupunguza mtiririko wa damu kwenye moyo, na kusababisha maumivu makali ya kifua. Aina hii ya angina kwa kawaida hutokea wakati umepumzika, na hasa usiku. Maumivu hutokea mfululizo kisha kuacha kwa muda. Msongo wa mawazo, uvutaji wa sigara, madawa yanayosababisha mishipa ya damu kubana (kama dawa za kipandauso) na matumizi ya cocaine yanaweza kusababisha Prinzmetal’s angina.

Tiba Ya Chembe Ya Moyo

Kuna tiba nyingi kwa tatizo la chembe ya moyo, ikiwa ni pamoja na kubadili staili ya namna ya kuishi, dawa, angioplasty na stenting, au upasuaji. Malengo ya tiba hizi ni kupunguza kujirudiarudia na ukali wa dalili zake na kupunguza yamkini ya kupata heart attack au kifo.

Lakini, kama unapatwa na unstable angina au maumivu ya angina yaliyo tofauti na yale uliyoyazoea, kama kupata maumivu wakati umepumzika, unahitaji tiba ya haraka kwenye hospitali.

Dawa

Kama kubadili staili yako ya maisha hakuleti mabadiliko kwenye tatizo lako la chembe ya moyo, utatakiwa upate dawa. Dawa zinazotumika ni pamoja na:

. Nitrates. Nitrates hutumika mara nyingi kutibu angina. Nitrates hulegeza na kupanua mishipa ya damu, na kuruhusu damu nyingi zaidi kufika kwenye misuli ya moyo. Unaweza kutumia nitrate kabla ya kufanya tendo ambalo huamsha angina (kama mazoezi) au kuitumia muda wote. Nitarate iliyozoeleka zaidi katika kutibu angina ni vidonge vya nitroglycerin, ambavyo unaviweka chini ya ulimi.

. Aspirin. Aspirin huzuia damu kuganda, na kuisadia damu kupita kwa urahisi kwenye ateri za moyo zilizosinyaa. Kuzuia kuganda kwa damu huzuia pia uwezekano wa kupata heart attack. Lakini usianze kutumia aspirin kila siku bila ushauri wa daktari.

. Clot-preventing drugs. Baadhi ya dawa kama clopidogrel (Plavix), prasugrel (Effient) na ticagrelor (Brilinta) zinaweza kusaidia kuzuia kuganda kwa damu kwa kuzuia platelets zisinatane. Moja ya dawa hizi inaweza kushauriwa kama huwezi kutumia aspirin.

. Beta blockers. Beta blockers hufanya kazi kwa kuzuia madhara ya epinephrine, au kwa jina jingine adrenaline. Kwa hiyo, moyo utadunda taratibu zaidi na kwa nguvu ndogo zaidi, hivyo kupunguza blood pressure. Beta blockers pia huifanya mishipa ilegee na kufunguka ili kusaidia mtiririko wa damu, na hivyo kuzuia au kupunguza angina.

. Statins. Statins ni dawa zinazotumika kupunguza kiwango cha cholesterol katika damu. Zinafanya kazi kwa kuvizuia vitu vinavyohitajika na mwili kutengeneza cholesterol. Zinaweza pia kuusadia mwili wako kufyonza cholesterol iliyojazana ndani ya plaques kwenye kuta za ateri, na kuzuia kuziba kwa mishipa yako ya damu.

. Calcium channel blockers. Calcium channel blockers, ambazo pia huitwa calcium antagonists, hulegeza na kupanua mishipa ya damu kwa kuboresha seli za misuli kwenye kuta za ateri. Hii huongeza mtiririko wa damu kwenye moyo, na kupunguza angina.

. Dawa za kuteremsha blood pressure (Blood pressure-lowering medications.) Kama pressure yako iko juu, kama una kisukari, dalili za heart failure au magonjwa sugu ya figo, daktari atakushauri dawa ya kupunguza pressure. Kuna makundi mawili ya dawa za pressure: angiotensin-converting enzyme (ACE) inhibitors au angiotensin II receptor blockers (ARBs).

. Ranolazine (Ranexa). Ranexa inaweza kutumika peke yake au pamoja na dawa nyingine za angina, kama calcium channel blockers, beta blockers au nitroglycerin.

Upasuaji

Kubadili staili ya maisha na dawa hutumika kwa kawaida kuitibu stable angina. Tiba nyingine kama za angioplasty, stenting na coronary artery bypass surgery huweza kutumika kutibu angina.

. Angioplasty na stenting. Wakati wa angioplasty -ambayo pia huitwa percutaneous coronary intervention (PCI) -kijiputo kidogo huingizwa ndani ya ateri iliyosinyaa. Kijiputo hiki hujazwa upepo ili kupanua ateri, kisha wire mesh coil (stent) ndogo huingizwa ili kuacha njia ya ateri wazi.

. Coronary artery bypass surgery. Upasuaji huu unapofanyika, veni au ateri kutoka eneo jingine la mwili wako inatumika kuikwepa ateri ya moyo iliyoziba au iliyosinyaa. Bypass surgery huongeza mtiririko wa damu kwenye moyo na kupunguza au kuondoa angina. Ni tiba inayotumika kwa stable na unstable angina ambayo haikusikia tiba nyingine.

. External counterpulsation (ECP). Aina hii ya tiba inatumia blood presure cuffs zinazowekwa kwenye misuli ya nyuma ya miguu kati ya goti na ankle, mapaja na nyonga ili kuongeza mtiririko wa damu kuelekea kwenye moyo.

Katika mada nyingine, tutalizungumzia tatizo jingine linahusiana na hili la  mshituko wa moyo – heart attack.

Usisite kuulizwa swali ulilo nalo au kutoa maoni yako binafsi kuhusu mada hii yetu ya leo. Tutafurahi sana kusikia kutoka kwako.

DAWA ZA CHEMBE YA MOYO

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wetu wa Facebook wa LINDA AFYA YAKO kupata mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya mwanadamu na tiba mbalimbali. Usikose kuweka LIKE endapo utafurahishwa na mada hizo.

Kwa mawasiliano na maelezo zaidi tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu kwenye nambari zifuatazo: +255 655 858027 au +255 756 181651.