Nyama Za Pua (Nasal Polyps)

Nyama za pua ni vitu visivyo na maumivu vilivyoota ndani ya pua au sehemu za uwazi ndani ya mifupa ya uso au kitaalamu sinuses. Nya,a za pua si saratani. Nasal polyps zikiwa ndogo zinaweza zisilete dalili zo zote, Nyama hizi za pua zikiwa kubwa zinaweza kuziba pua. Zinaweza kuleta matatizo katika kupumua, kushindwa kugundua harufu na maambukizi ya vijidudu. Nyama zapua zinaweza kumpata mtu yr yote, lakini huonekana zaidi baina ya watoto na watu wa umri wa kati. Madawa huweza kufanya nyama za pua kunywea au kuondoka. Lakini wakati mwingine upasuaji hulazimika kufanyika. Hata baada ya tiba hizi, nyama za oua mara nyingi hurudi tena.