Jee, Kisukari Kinasababisha Ganzi, Viungo Kuwaka Moto Na Kukatwa Vidole Au Mguu? Ujue Ugonjwa Wa Diabetic Neuropathy

 

 

ugonjwa wa diabetic neuropathy

 

 

Bila shaka umeshamwona mtu aliyekatwa vidole au mguu/viungo vya mguu kwa sababu ya kisukari. Katika mada yetu ya leo tutalijadili tatizo linalotokana na kisukari ambalo husababisha watu kukatwa viungo na matatizo mengine mengi kama viungo kufa ganzi au kuwaka moto. Tatizo hili kiutaalamu huitwa diabetic neuropathy. Diabetic neuropathy ni namna ya uharibifu wa neva unaotokana na mtu kuwa na kisukari. Uwepo wa sukari (glucose) kwa wingi ndani ya damu unaweza kuharibu neva za sehemu mbalimbali za mwili wako. Lakini mara nyingi diabetic neuropathy huharibu neva za kwenye nyayo na miguu.

 

diabetic peripheral neuropathy nerve damage

 

 

Kutokana na neva ambazo zimeharibiwa, dalili za diabetic neuropathy zinaweza kuwa ni maumivu na kufa ganzi kwenye miguu na nyayo, matatizo ya mfumo wa mmeng’enyo wa chakula, mkondo wa mkojo (urinary tract,) mishipa ya damu na moyo. Watu wengine hupata dalili ndogo lakini kwa wengine huweza kuwaletea maumivu makali au kuwafanya washindwe kufanya kazi.

Diabetic neuropathy ni tatizo la kawaida linalojitokeza baada ya mtu kuwa na kisukari. Unaweza kuzuia diabetic neuropathy au kupunguza makali yake kwa kudhibiti kiwango chako cha sukari na kufuata mtindo wa kimaisha unaoilinda afya yako.

Chanzo Cha Diabetic Neuropathy

 

Chanzo kamili hutofautiana kulingana na aina ya neuropathy. Watafiti wanafikiria kuwa baada ya muda, sukari ambayo haikudhibitiwa huharibu neva na kuziondolea uwezo wake wa kutuma taarifa (signals), na kuleta diabetic neuropathy. Sukari nyingi katika damu vile vile hudhoofisha kuta za mishipa midogo ya damu (capillaries) inayoleta oksijeni na virutubishi kwenye neva.

 

diabetic peripheral neuropathy

 

Muunganiko wa sababu huweza kuleta uharibifu wa neva, zikiwemo:

. Kuvimba kwa neva kunakotokana na kushambuliwa na kinga za mwili. Kinga za mwili kwa bahati mbaya hushindwa kuzitambua neva (huzifikiria ni vitu kutoka nje vyenye madhara) na kuzishambulia

. Sababu za kiurithi ambazo hazihusiani na kisukari zinaweza kuwasababishia baadhi ya watu kupata uharibifu wa neva

. Matumizi ya tumbaku na pombe huharibu neva na mishipa ya damu na kuongeza uwezekano wa kushambuliwa na wadudu.

 

Diabetic neuropathy inaweza kugawanywa katika makundi yafuatayo:

Sensory neuropathy: Aina hii ya diabetic neuropathy hutokea pale neva (sensory neves) zinapoharibiwa kwa sababu ya kuwa na kiwango kikubwa cha glucose ndani ya damu kwa muda mrefu. Sensory neuropathy huanzia kwenye sehemu ambali za viungo vya mwili kama nyayo au viganja na huweza kuendelea hadi kuathiri miguu na mikono. Dalili zitatokea kwenye eneo la mwili ambako neva zimeathiriwa zikiwa ni pamoja na ganzi, kuoungua uwezo wa kusikia maumivu au joto kali, vitu kuchomachoma, kuwaka moto, maumivu makali hasa usiku.

Motor neuropathy: Aina hii ya diabetic neuropathy hutokea pale uharibifu unapotokea kwenye neva (motor nerves) ambazo hudhibiti utendaji wa misuli. Sehemu ambazo huathiriwa zaidi na tatizo hili ni nyayo, viganja,miguu na mikono. Motor neuropathy huathiri uwezo wa kusimamia miondoko, na hasa kutembea, tatizo ambalo baadaye linaweza kuharibu umbo la unyayo (Charcot foot). Dalili za motor neuropathy ni pamoja na udhaifu wa misuli, kushindwa kuvimudu viungo, misuli kucheza na misuli kufa ganzi.

Autonomic neuropathy: Autonomic neuropathy hutokea wakati neva zinazosaidia shughuli zinazojiendesha zenyewe (involuntary functions), kama kumeng’enya chakula, kutoa jasho, zinapoharibika. Dalili zake hutegemea kiungo kinachohusika na ni pamoja na kufunga choo, kuharisha, kichefuchefu, shida kukojoa, jasho jingi, mapigo ya juu ya moyo, uume kushindwa kusimama n.k.

Moyo Na Autonomic Neuropathy

Kama neva zinazodhibiti mapigo ya moyo zitaathiriwa utaambiwa una tatizo la Cardiac Autonomic Neuropathy (CAN.) Neva hizi zikiharibika, mapigo ya moyo yanaweza kubaki juu hata wakati umepumzika na hali ambayo inaweza kusababisha low blood pressure, kama wakati wa kusimama (postural hypotension). Tatizo jingine ni uwezekano wa kupata heart attack bila maumivu (silent myocardial infarction.)

Tumbo Na Autonomic Neuropathy

Kama neuropathy itaiathiri neva ya vagus (neva inayosukuma chakula ndani ya tumbo), ambazy husaidia kudhibiti utendaji wa tumbo, hali iitwayo gastroparesis hutokea. Gastroparesis huathiri utolewaji wa mabaki tumboni na kufanya chakula kikae ndani ya tumbo kwa muda mrefu. neva hii isipofanya kazi vizuri, chakula hugeuka kuwa kigumu, kuziba njia na kusababisha maambukizi.

Dawa za gasroparesis ni pamoja na:

. Metoclopramide
. Erythromycin
. Antiemetics.

 

Autonomic neuropathy na uume kushindwa kusimama

(Erectile Dsysfunction)Tatizo hili ni la kawaida kwa wanaume wenye kisukati, inakadiriwa kuwa asilimia 35-75 ya wanaume wenye kisukari hupata tatizo moja au jingine linalohusiana na utendaji wa uume. Chanzo chake kidogo ni kigumu kufahamika, lakini kinahusiana na mabadiliko yanayotokea mwilini kwa muda mrefu na kuathiri neva, misuli na mishipa ya damu. Kusudi uume usimame, wanaume wanatakiwa kuwa na afya ya mishipa ya damu, neva, homoni za kiume na hamu ya tendo la ndoa. Hata kama mwanamme ana hamu ya kufanya tendo la ndoa na homoni zake zipo sawa, tatizo bado litatokea.

Hoja nyingine zinazochangia tatizo hili ni:

. unene
. uvutaji wa sigara
. kutofanya mazoezi ya mwili

Matatizo ya kisaikolojia huchangia wa kiwango kikubwa. Wasiwasi, kujisikia kuwa na hatia, mfadhaiko, kutojiamini (low self-esteem) na wasiwasi wa kushindwa tendo, huchangia kati ya asilimia 10-20.

Kwa wanawake, autonomic neuropathy husababisha mwanamke apate shida ya kuwa tayari kwa tendo la ndoa na kufika kileleni na huweza kusababisha uyabisi wa uke.

 

Autonomic neuropathy na  kibofu cha mkojo

Endapo neva zinazohusika na utendaji kazi wa kibofu cha mkojo zitaharibiwa na autonomic neuropathy, matatizo yatatokea ambayo ni pamoja na:

. Kushindwa kutoa mkojo wote nje
. Maambukizi ya bakteria ndani ya kibofu
. Mkojo kutoka bila ridhaa (incontinence).

 

Autonomic neuropathy na tezi za jasho

Neuropathy inaweza kuziathiri tezi za jasho na kuathiri utokaji wetu wa jasho. Jasho husaidia kuweka vizuri joto la mwili na huweza kusaidia pia kuitunza ngozi.

Kama tezi za jasho zitaathiriwa na uharibifi wa neva utokaji jasho utaathirika na kusababisha ukavu au mipasuko ya wa ngozi kwenye nyayo.

 

Peripheral Neuropathy

Hii ni aina ya diabetic neuropathy inayoonekana zaidi. Huanza kwa kuathiri nyayo na miguu, kisha mikono na viganja. Dalili zake huonekana zaidi usiku, nazo zinaweza kuwa:

 

diabetic peripheral neuropathy in legs

 

 

. Ganzi na kupungua kwa usikivu wa maumivu au mabadiliko ya joto
. Kuhisi misisimko au viungo kuwaka moto
. Maumivu makali au kukakamaa misuli
. Kuzidi kwa usikivu wa kugusa – kwa wengine hata uzito wa shuka huwaumiza
. Udhaifu wa misuli
. Kupoteza ushiriakiano wa viungo
. Matatizo makubwa ya miguu, vidonda, maumivu ya maungio ya mifupa na mifupa.

 

diabetic neuropathy gangrene

 

 

Radiculoplexus Neuropathy (diabetic amyotrophy)

Radiculoplexus neuropathy inaathiri neva za kwenye mapaja, nyonga, matako au miguu. Huonekana zaidi baina ya waathirika wa kisukari cha Type 2 na watu wenye umri mkubwa. Aina hii ya neuropathy huitwa pia amyotrophy, femoral neuropathy au proximal neuropathy.

 

diabetic amyotrophy

 

Dalili huonekana zaidi upande mmoja wa mwili, ingawa huweza kusambaa na upande wa pili. Unaweza kuwa na:

. Maumivu makali kwenye paja na nyonga au tako yanayodumu siku nzima au zaidi
. Baadaye udhaifu na kusinyaa kwa misuli ya paja
. Ugumu kunyanyuka baada ya kuketi
. Kuvimba tumbo
. Kukonda

Mononeuropathy

Mononeuropathy au focal neuropathy ni kuharibika kwa neva fulani iliyo usoni, katikati ya mwili (torso) au mguuni. Mononeuropathy mara nyingi humpata mtu ghafla na huweza kuambatana na maumivu makali sana. Lakini , mara nyingi haileti madhara ya kudumu.

Dalili mara nyingi huondoka bila tiba yo yote baada ya wiki au miezi kadhaa. Dalili hutofautiana kulingana na neva iliyoharibiwa. Unaweza kupata maumivu sehemu za:

. Unyayo au katikati ya goti na ankle
. Sehemu ya chini ya mgongo au nyonga
. Sehemu ya mbele ya paja
. Kifua au tumbo

Mononeuropathy huweza vile vile kusababisha matatizo ya neva kwenye macho na uso, na kuleta:

. Matatizo katika kuona vitu vizuri
. Kuona vitu viwiliviwili
. Kuwashwa nyuma ya jicho moja
. Kupooza upande mmoja wa uso (Bell’s palsy)

Wakati mwingine mononeuropathy hutokea pale kitu kinapogandamiza juu ya neva. Carpel tunnel syndrome ni aina moja ya nephropathy itokanayo na mgandamizo kwa watu wenye kisukari. Inaweza kusababisha ganzi au msisimko mkononi au kwenye vidole, isipokuwa kidole cha mwisho. Mkono unaweza kuwa dhaifu, na kuangusha vitu.

Matatizo Yatokanayo Na Diabetic Neuropathy

Kuna madhara makubwa yanayoweza kutokana na diabetic neuropathy, ikiwa ni pamoja na:

. Kupoteza dole gumba, nyayo au mguu.

Kuharibika kwa neva kunaweza kukufanya ushindwe kuzisikia nyayo zako. Mikwaruzo au kujikata kwenye nyayo kunaweza kulifanya eneo hilo kupata maambukizi na taratibu jeraha likageuka kuwa kidonda kikubwa. Hata mikwaruzo midogo isiyopona baadaye huwa madonda. Hali ikiwa mbaya zaidi, maambukizi husambaa hadi kwenye mifupa, na vidonda kusababisha kufa kwa tishu (gangrene). Kukatwa kwa dole gumba, unyayo au sehemu ya chini ya mguu huwa sasa ni lazima.

 

diabetic neuropathy madhara

 

. Uharibifu wa maungio ya mifupa. Uharibifu wa neva unaweza kusababisha maungio ya mifupa kupotea ubora wake, na kuleta hali iitwayo Charcot joint. Hii kwa kawaida hutokea kwenye maungio ya mifupa madogo ya kwenye mguu. Dalili ni kukosa hisia na kuvimba kwa sehemu hizo za maungio, wakati mwingine kuharibika kwa umbo la joint.

. Mambukizi ya njia ya mkojo na kutokwa mkojo ovyo. Neva zinazosimamia utendaji wa kibofu cha mkojo zikifa, unaweza ukashindwa kuutoa mkojo wote kutoka kwenye kibofu. Bakteria huweza kujijenga ndani ya kibofu cha mkojo na figo, na kusababisha maambukizi ya njia ya mkojo. Uharibifu wa neva unaweza pia kuathiri uwezo wako wa kutambua kuwa unahitaji kukojoa au kudhibiti misuli inayoruhusu mkojo utoke, na kusababisha kuvuja kwa mkojo (incontinence).

. Kutotambua uwingi wa sukari.

. Kushuka kwa pressure kwa ghafla. Kuharibika kwa neva zinazosimamia mtiririko wa damu kunaweza kuathiri uwezo wa mwili wa kurekebisha pressure. Hii inaweza kusababisha kushuka kwa ghafla kwa pressure unaposimama baada ya kuwa uliketi (orthostatic hypotension), na kukufanya usikie kizunguzungu na ukazimia.

. Matatizo ya mmeng’enyo wa chakula.

. Kushindwa kumudu tendo la ndoa. Autonomic neuropathy mara nyingi huharibu neva zinazoathiri viungo vya uzazi. Wanaume wanaweza kupata tatizo la uume kushindwa kusimama. Wanawake wanaweza kupata tatizo la uke kuwa mkavu au kutosikia hamu ya kufanya mapenzi.

. Kutotoka au kutoka jasho jingi. Uharibifu wa neva unavuruga utendaji kazi wa tezi za jasho na kuufanya mwili wako kushindwa kudhibiti kiwango chake cha joto ipaswavyo. Baadhi ya watu wenye autonomic neuropathy wanatoa jasho kwa wingi sana, na hasa usiku au wakati wakila chakula. Jasho kidogo au kutotoka jasho (anhidrosis) kunaweza kuhatarisha maisha.

 

Tiba Ya Diabetic Neuropathy

 

Hakuna dawa inayojulikana kuponya diabetic neuropathy. Tiba inayotolewa inalenga:

. Kupunguza kasi ya ugonjwa
. Kuondoa maumivu
. Kudhibiti matatizo yatokanayo na ugonjwa na kurudisha utendaji wa viungo.

 

 

 

Glucoblock Capsule
DAWA YA KUDHIBITI KIWANGO CHA SUKARI
CHAI YA KUDHIBITI KIWANGO CHA SUKARI

 

 

Katika mada nyingine tumejadili;  Jee, Kisukari huleta Upofu? Ujue Ugonjwa Wa Diabetic Retinopathy, Ni zipi dalili za kisukari, tiba ya kisukari, chakula na mazoezi kwa mgonjwa wa kisukari  .

Usisite kuuliza maswali uliyo nayo kuhusu somo letu la leo. Kwa ushauri zaidi tupigie kupitia namba 0655 858027 na 0756 181651.