Ugonjwa Wa Corona (COVID-19)

 

tiba ya covid 19

 

Katika historia yake binadamu amekuwa akipatwa mara kwa mara na magojwa ya mlipuko (epidemics), wakati mwingine yakibadili kabisa mwelekeo wake na hata kutishia kuwa ndiyo mwisho wa hali bora ya maisha aliyokwishajipatia.

Kuna mlipuko (Prehistoric epidemic: Circa 3000 B.C.) unaokisiwa kuwa ulitokea miaka 5,000 iliyopita na kukifagia kijiji huko China. Miili ya maiti ilijazwa ndani ya nyumba na kisha nyumba kuchomwa moto. Sehemu hii iitwayo “Hamin Mangha” iliyopo kaskazini- mashariki mwa China, ni moja ya sehemu zinazotunzwa sana kama kituo cha elimu ya mambo ya kale.

Mnamo mwaka 430 BC, muda mfupi baada ya vita ya Athens na Sparta kuanza, ugonjwa wa mlipuko ulitokea Athens na ulidumu kwa takribani miaka mitano. Inakadiriwa kuwa watu wapatao 100,000 walikufa kwa ugonjwa huu. Wanahistoria wanaseama watu ghafla waliumwa vichwa, macho kuwa mekundu na kuvimba, sehemu za ndani kama koo na ulimi kuwa na damu, na kutoa harufu mbaya ya uvundo kinywani. Inasadikika kuwa waliumwa typhoid na ebola, hali iliyochangiwa zaidi na kusongamana kwa watu sababu ya vita.

 

epidermic spanish flu
SPANISH FLU

 

Vivyo hivyo kulitokea milipuko mingine kama ya Antonine Plague (A.D. 165-180), Plague of Cyprian (A.D. 250-271), Plague of Justinian (A.D. 541-542), The Black Death (1346-1353) iliyotokea Asia hadi Ulaya na kufagia nusu ya wakazi wa Ulaya, Cocoliztli epidemic (1545-1548) iliyoua watu milioni 15 wa Mexico na Marekani ya Kati, American Plagues (16th century), Great Plague of London (1665-1666), Great Plague of Marseille (1720-1723), Russian plague (1770-1772), Philadelphia yellow fever epidemic (1793), Flu pandemic (1889-1890), American polio epidemic (1916), Spanish Flu (1918-1920), Asian Flu (1957-1958) ulioanzia China na kuua watu zaidi ya milioni moja, AIDS pandemic and epidemic (1981-present day) ugonjwa ambao bado unaendelea na tayari umeshaua watu zaidi ya milioni 35.

Kwa miaka ya hivi karibuni kumetokea H1N1 Swine Flu pandemic (2009-2010), West African Ebola epidemic (2014-2016), Zika Virus epidemic (2015-present day) , na sasa hivi tuna COVID-19.

 

epidermic ebola
EBOLA

 

SARS (Severe Acute Respiratory Syndrome)

Mwaka 2003 kirusi aitwaye SARS coronavirus (SARS-CoV) aligundulika. Kirusi huyu anayeaminika kuwa alitokea kwa wanyama, labda popo, na kwamba akahamia kwa wanyama wengine (paka), alionekana kwa binadamu kwa mara ya kwanza kwenye jimbo la Guangdong, China ya Kusini.

Kirusi alienea kwenye nchi 26 duniani na kuwapata watu wapatao 8,000.

Kirusi huyu anaenea kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Mwathirika atapata dalili za homa, kuumwa kichwa, kuharisha, baridi kali na maumivu ya misuli. Nchi nyingine zilizopata kirusi huyu ni Canada (Toronto), Hong Kong, Singapore na Vietnam (Hanoi).

 

COVID-19

 

Tarehe 20 Januari 2020, mgonjwa wa kwanza wa covid-19 aliripotiwa. Mgonjwa huyu alikuwa ni mwanamke mwenye umri wa miaka 35, raia wa China, kutoka mji wa Wuhan, jimbo la Hubei huko China. Mgonjwa huyu alipata homa, kujisikia baridi na maumivu ya misuli tarehe 18 Januari akiwa Wuhan. Alipelekwa kwenye hospitali kubwa ya taifa, na tarehe 20 Januari vipimo vilithibitisha kuwa alikuwa na virusi vya corona (2019-nCoV.)

Tarehe 30 Januari 2020, kamati ya dharula ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ilitangaza kuwa ugonjwa wa corona ni janga la kimataifa.

Kirusi wa corona aligundulika siku nyingi. Kwa kawaida husababisha mafua, lakini hapa karibuni amebadilika na kuwa aina ya kirusi ambaye anaweza kuambukiza kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Mkurugenzi wa WHO, Dr Tedros Adhanom Ghebreyesus katika kikao alichokiongoza, alitoa jina la 2019 Novel Coronavirus (2019-nCoV) kwa kirusi huyu mpya. Hadi tarehe 10 Februari 2020, kirusi huyu alikuwa amewalaza watu 40,548 na kuua wengine 910 duniani.

 

Dalili Za COVID-19

Dalili za ugonjwa huu ni pamoja na:

. Kupungua kwa seli nyeupe za damu
. Uharibifu wa mfumo wa mzuguko wa damu
. Kuharisha
. Homa
. Uchovu
. Kukohoa na kupiga chafya
. Kutokwa kamasi
. Pumzi kubana
. Matatizo ya kupumua
. Kukauka koo
. Pneumonia
. Matatizo katika mapafu
. Figo kushindwa kufanya kazi
. Figo kufeli.

 

Chanzo Cha Ugonjwa Wa COVID-19

 

orona chanzo chake

 

Virusi wa corona wakiingia ndani ya mapafu huzaliana kwa haraka, hushambulia na kuziharibu seli za mapafu. Hali hii husababisha pneumonia. Vifuko vya hewa (alveoli) ambavyo kwa kawaida huwa vikavu, hujaa majimaji au usaha, na kufanya upumuaji kuwa wa shida. Majimaji haya huzuia oksijeni isiingie kiurahaisi mwilini kupitia damu.

 

corona kushindwa kupumua

 

Kwa sababu hiyo, viungo muhimu kama ini na figo husimama kufanya kazi baada ya kukosa oksijeni. Ripoti za WHO zinaonyesha kuwa wagonjwa wengi hufariki baada ya viungo zaidi ya kimoja kushindwa kufanya kazi.

Watu waliovuta sigara kwa muda mrefu na wazee wenye matatizo ya mapafu ni kundi ambalo huathirika zaidi na COVID-19.

 

Tiba Ya COVID-19

 

Hadi sasa, bado majaribio ya madawa yanaendelea kufanywa, hakuna sindano iliyokwishwa thibitishwa kutibu COVID-19 na vifaa vya kumtunza mgonjwa wa corona bado ni adimu.

Ili kujikinga na ugonjwa huu yafaa kuzingatia yafuatayo:

. Kuepuka kugusana na watu wenye dalili za matatizo ya afya ya mapafu
. Kuosha mikono mara kwa mara, hasa baada ya kugusana na watu wanaoumwa au kuwa kwenye mazingira yao.
. Epuka kugusa wanyama bila kujikinga
. Watu wenye dalili wahakikishe wanavaa barakoa (wakae mbali, wazibe midomo wanapokohoa au kupiga chafya kwa nguo na kuosha mikono)

Unashauriwa kuuweka mwili wako katika hali nzuri ya kiafya kwa kuhakikisha unayafanya yafuatayo:

1) Imarisha afya ya kinga zako za mwili na afya ya mapafu yako.

 

 

2) Hakikisha mwili wako unapata vitamini kwa kiwango  cha kutosha, na hasa vitamini C.

 

 

vitamini

 

3) Hakikisha unaupa mwili wako mafuta ya Omega 3. EPA na DHA kutoka mafuta hayo husaidia kupunguza utolewaji wa majimaji ndani ya vifuko vidogo vya hewa (alveoli) vilivyomo ndani ya mapafu, endapo kutatokea maambukizi ya virusi.

 

omega 3

Usisite kutoa maoni yako kuhusu mada yetu hii ya leo au kuuliza maswali uliyo nayo. Katika mada nyingine tutauzungumzia ugonjwa wa UKIMWI.

 

Pata ushauri zaidi kwa kututumia ujumbe kupitia ukurasa huu hapa chini kwa kujaza fomu, au kututumia barua pepe kupitia promota927@gmail.com au tupigie simu kwa namba zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

 

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.