Chakula Cha Kukwepa Ukiwa Na Gout

 

 

 

Gout ni ugonjwa unaosababisha maumivu makali ya maungio ya mifuapa (joints). Gout  hushambulia joint moja au zaidi, lakini mara nyingi hutokea miguuni. Mashambulizi hutokea wakati uric acid inapoganda na kujijenga kwenye joints. Uric acid, ambayo ni antioxidant inayolinda utando wa ndani wa mishipa ya damu, huzalishwa mwilini wakati chakula cha kundi la purines kikivunjwavunjwa. Kupata au kutopata gout kunategemea zaidi urithi.  Mabadiliko katika namna ya kuishi yanaweza kuzuia maumivu. Kuwa mwangalifu na vitu unavyokula na kuacha kula chakula chenye purines kwa wingi kunaweza kukuondolea dalili za gout.

Nyama Zinazoleta Gout

Nyama za viungo zinatakiwa kuachwa kabisa kama una ugonjwa wa gout kwa sababu zina viwango vikubwa vya purines. Nyama hizo za viungo ni kama: maini, kongosho za ndama au kondoo, figo, ubongo, na utumbo unaoliwa. Nyama nyingine zote zinatakiwa kuliwa kwa kiasi, kiasi kisichozidi wakia (ounce) 4, sasawa na ukinunua robo kilo na ukaigawanya mara mbili.

Nyama zifuatazo zinatakiwa kuliwa kidogo:

. nyama ya nguruwe
. nyama ya kuku
. nyama ya bata
. nyama ya bata bukini
. nyama ya sungura
. nyama ya kondoo
. nyama ya ndama
. nyama ya paa

Chakula kinachotokana na wanyama kama mchuzi, supu ya kuku, vile vile vina purines kwa wingi.

Samaki Na Chakula Cha Bahari Wanaoleta Gout

 

Samaki na chakula cha baharini ni vyanzo vya purines vinavyoeleweka. Samaki wabaya kabisa kwa kuleta gout ni kama samaki wa scallops, sadini (sardines), heringi (herring), aina ya dagaa wa maji chumvi (anchovies) na samaki wa aina ya bangala (mackerel).

Samaki wengine wenye purines kwa kiwango cha kiasi ni:

. jodari (tuna)
. kambare mamba au kamongo wa maji baridi (carp)
. chewa (codfish)
. halibati (halibut)
. sangara (perch)
. samoni (salmon)
. snapper
. trout

Chakula cha baharini kama chaza, kambamti (kambakoche), kaa, na uduvi nacho kinatakiwa kuliwa kidogo kwa sababu kina purines kwa wingi.

Pombe

Bia (beer) ina purines, na hamila inayotumika kwa pombe ndiyo haswa yenye purines kwa wingi. Utafiti umeonyesha kuwa kunywa pombe ukiwa una maumivu ya gout, huongeza ukali wa maumivu hayo.

Pamoja na kwamba pombe za aina nyingine zinaweza kuwa na purines kidogo, zinaweza kuongeza kasi ya uzalishaji wa purines mwilini. Hali hiyo inaweza kuongeza kiwango cha purines ndani ya mwili. Matumizi makubwa ya pombe yanaweza kuongeza yamkini ya kushambuliwa na gout.

Katika mada nyingine tutauzungumzia ugonjwa wa rheumatoid arthritis. Usisite kutoa mchango wako wa mawazo au kuuliza maswali kuhusu mada hii.

 

Pata ushauri zaidi kwa kututumia ujumbe kupitia ukurasa huu hapa chini kwa kujaza fomu, au kututumia barua pepe kupitia promota927@gmail.com au tupigie simu ndani ya muda wa kazi  kwa namba zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

 

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.