Umuhimu Wa Calcium Mwilini

 

 

Calcium ni madini ambayo mara nyingi yamehusishwa na afaya ya mifupa na meno, ingawa ni muhimu katika kuganda kwa damu, kusaidia misuli kukaza, kuweka vizuri mapigo ya moyo na utendaji kazi wa neva. Asilimi 99 ya calcium ya ndani ya mwili imehifadhiwa katika mifupa, asilimia moja inayosalia inapatikana katika damu, misuli na tishu nyingine.

Ili kufanya kazi zake vizuri, mwili huhakikisha kiwango cha calcium kilichomo ndani ya damu na tishu hakibadiliki. Kama kiwango cha calcium katika daku kinashuka sana, homoni ya parathyroid (PTH) itatoa ishara ili mifupa iachie calcium kuingia ndani ya damu. Homoni hiyo inaweza pia kuamsha vitamini D ili kuongeza ufyonzwaji wa calcium katika matumbo. Wakati huo huo PTH itatoa ishara ili figo ziachie calcium kidogo zaidi kwenye mkojo. Mwili ukiwa na calcium ya kutosha, homoni nyingine iitwayo calcitonin itatenda kinyume: itapunguza kiwango cha calcium katika damu kwa kuzuia utolewaji wa calcium kutoka kwenye mifupa na kuamuru figo kuachia calcium zaidi kwenye mkojo.

Mwili hupata mahitaji yake ya calcium kwa njia mbili. Moja kwa kula chakula au vitu vingine vyenye calcium, na njia nyingine ni kwa kuchukua calcium iliyomo mwilini. kama mtu hali chakula chenye calcium ya kutosha, mwili utaichukua kutoka kwenye mifupa. Calcium hii iliyoazimwa itarudishiwa baadaye. Ingawa hii haitokei kila mara, na haifanikiwi kwa kula tu calcium ziada.

Pamoja na calcium, mwili unahitaji vitamini D, vitamini ambayo unausaidia mwili kufyonza calcium. Vitamini D hupatikana katika mafuta ya samaki, bidhaa kutokana na wanyama, na mionzi ya jua.

 

Viwango Vinavyopendekezwa

 

Viwango vinavyopendekezwa -Recommended Dietary Allowance (RDA)- kwa wanawake umri kati ya miaka 19 hadi 50 ni 1,000 mg kwa siku, wanawake wa miaka 51+, ni 1,200 mg. Wanawake wenye mimba na wanaonyonyesha, RDA ni 1,000 mg. Kwa wanaume wa miaka kati ya 19 hadi 70, RDA ni 1,000 mg; kwa wanaume zaidi ya 71, RDA ni 1,200 mg.

 

Calcium Na Afya Ya Binadamu

 

Calcium husaidia afya ya mwili kwa njia nyingi. Baadhi ya kazi za calcium katika afya ya binadamu ni kama:

Afya Ya Mifupa

Karibu asilimia 99 ya calcium ya ndani ya mwili ipo ndani ya mifupa. Calcium ni ya muhimu katika kujenga, ukuaji na ukarabati wa mifupa.

Watoto wanapokua, calcium huchangia ukuaji wa mifupa yao. Wakiacha kukua, calcium husaidia kuitunza mifupa na kupunguza kasi ya kupungua kwa uzito wa mifupa, hali ambayo huambatana na kuzeeka kwa mwili.

Wanawake waliokoma hedhi wanaweza kupunguza uzito wa mifupa haraka zaidi kuliko wanaume au vijana, kwa hiyo daktari anaweza kuwashauri watumie calcium ya ziada.

Kukaza Kwa Misuli

Calcium inasaidia kudhibiti kukaza kwa misuli. Neva ikiusisimua msuli, mwili huachia calcium. Calcium huzisaidia protini za ndani ya msuli kukamilisha tendo la kukaza. Mwili ukiisukuma calcium nje ya msuli, msuli hujilegeza.

Afya Ya Moyo

Calcium inahusika katika kuganda kwa damu. Tendo la kuganda kwa damu ni gumu kulielezea na lina hatua kadhaa. Ni tendo linahusisha mabadiliko kadhaa ya kikemikali, calcium ikihusika.

Kuhusika kwa calcium katika utendaji kazi wa misuli ni pamoja na kazi za msuli wa moyo. Calcium huulegeza msuli unaozunguka mishipa ya damu. Baadhi ya tafiti zimeonyesha kwamba kuna mahusiano kati ya ulaji mkubwa wa calcium na tatizo la kuwa na msukumo mdogo wa damu (low blood pressure.)

 

Nini Kitatokea Ikiwa Calcium Ipo Chini Katika Mwili?

 

Upungufu wa calcium, kitaalamu hypocalcemia, unatokea pale kiwango cha calcium katika damu kinapopungua. Upungufu wa calcium katika damu wa muda mrefu husababisha matatizo ya meno, mtoto wa jicho, mabadiliko katika ubongo na mifupa kukosa uimara.

Dalili Za Upungufu Wa Calcium

Matatizo ya Misuli

Mtu mwenye upungufu wa calcium anaweza kuona:

. kuumwa kwa misuli, kabanwa misuli (cramps), misuli kucheza
. Maumivu kwenye mapaja na mikono wakti wa kutembea
. Ganzi na vitu kuchezacheza kwenye mikono, miguu, nyayo na kuzunguka midomo

Dalili hizi zinaweza kuja na kutoweka

. Mtukutiko wa maungo (kwa kifafa, dege),

. Mapigo ya moyo kwenda kasi au taratibu (arrhythmia)

. Kifo

Uchovu Mkubwa

Viwango vidogo vya calcium husababisha uchovu mkubwa, unaotokana na kukosa nishati. Tatizo la kukosa usingizi pia linaweza kutokea. Uchovu unaotokana na upungufu wa calcium unaweza kuambatana na kichwa kuwa chepesi, kizunguzungu au kichwa kizito -vinavyoweza kusababisha kukosa umakini, usahaulifu na kuchanganyikiwa.

Matatizo Ya Ngozi na Kucha

Upungufu wa calcium wa muda mrefu unaweza kusababisha:

. ngozi kavu
. kucha kavu, zinazovunjikavunjika
. nywele kavu
. alopecia, tatizo la nywele kupunyuka vifunguvifungu
. eczema, uvimbe wa ngozi unaoweza kusababisha miwasho au madoa ya ngozi kavu
. Psoriasis

Mifupa kupoteza uimara

Upungufu wa calcium wa muda mrefu husababisha kupotea kwa ujazo wa madini (osteopenia) hali ambayo itasababisha mifupa kupungua unene na kuweza kuvunjika kirahisi, maumivu na matatizo ya mkao wa mwili (body posture.)

Maumivu Makali Kabla Ya Hedhi (Severe PMS)

Kiwango kidogo cha calcium katika mwili kimehusishwa na maumivu makali ya kabla ya hedhi. Utafiti umeonyesha kuwa upungufu wa vitamin D na calcium katika kipindi cha pili cha mzunguko wa hedhi unachangia dalili za PMS.

Matizo Ya Meno

Mwili ukipungukiwa calcium, huchukua calcium kutoka mwilini ikiwa ni pamoja na kutoka kwenye meno. Hii huweza kusababisha matatizo kwenye meno, yakiwa ni pamoja na:

. meno kuoza
. meno kuvunjika
. matatizo ya fizi
. udhaifu wa mizizi ya meno

Upungufu wa calcium kwa mtoto mdogo huathiri ukuaji wake wa meno.

Mfadhaiko

Ushahidi mwingine unasema upungufu wa calcium unaweza kuhusishwa na mabadiliko ya hisia za mwili, pamoja na mfadhaiko.

 

Chakula Chenye Calcium Kwa Wingi

 

Watu wanaweza kupata calcium kutokana na chakula na vinywaji vya aina nyingi:

. mtindi
. maziwa
. sardine na salmon
. jibini
. tofu
. mboga za kijani, kama broccoli, turnip, kale n.k.
. nafaka katika mlo wa asubuhi
. juisi
. mbegu kama almonds, ufuta na chia
. jamii ya kunde.

 

Supplements Za Calcium

 

Daktari anaweza kushauri matumizi ya supplements kwa watu wenye upungufu wa calcium. Supplements nyingi za calcium zina vitamini D. Vitamini D husaidia mwili kufyonza calcium. Magnesium pia ina nafasi katika kuimarisha mifupa, hivyo supplements za calcium zinaweza kuwa na magnesium.

 

Aina Za Supplements

 

Kuna aina nyingi za supplements. Daktari atakushauri ni aina gani uitumie. Hii itatokana na matakwa ya mgonjwa , hali yake ya kiafya , na iwapo kuna dawa nyingine anatumia.

Calcium kama elementi ni ile halisi (isiyochanganywa na cho chote,) lakini calcium kiasilia huchanganyika na vitu vingine.

Supplements zinakuwa na viwango tofauti vya calcium yenye mchanganyiko na ile halisi.

Kwa mfano:

Calcium carbonate: Hii huwa na asilimia 40 ya calcium halisi. Ain hii hupatikana kirahisi na ina bei ndogo. Mtu anatakiwa kuitumia pamoja na chakula, kwani asidi ya tumbo husaidia kuifyonza.

Calcium lactate: Hii huwa na asilimia 23 ya calcium halisi.

Calcium gluconate: Hii ina asilimia 9 ya calcium halisi.

Calcium citrate: Hii ina asilimia 21 ya calcium halisi. Mtu anaweza kuitumia bila chakula. Hii ni bora kwa watu wenye matatizo ya matumbo, achlorhydia na matatizo mengine ya ufyonzwaji wa chakula.

 

Madhara Ya Calcium Kupita Kiasi

 

Viwango vikubwa mno vya calcium ndani ya mwili vyaweza kusababisha:

. matatizo ya figo
. calcium kunata kwenye tishu laini na mishipa ya damu
. mawe katika figo
. kufunga choo

 

Katika mada nyingine tutazungumzia umuhimu wa vitamini katika mwili. Usisite kutoa maoni yako au kuuliza maswali uliyo nayo.

 

Pata ushauri zaidi kwa kututumia ujumbe kupitia ukurasa huu hapa chini, kwa kujaza fomu, au kututumia barua pepe kupitia promota927@gmail.com au tupigie simu ndani ya  saa za kazi kwa namba zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

 

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.