Maumivu Ya Kisigino – Plantar Fasciitis

 

maumivu ya kisigino

Katika mada yetu ya leo tutazungumzia tatizo la kupata maumivu kwenye sehemu ya unyayo wa mguu karibu na kisigino. Kitaalamu tatizo hili huitwa plantar fasciitis. Plantar fasciitis kwa kawaida husababisha maumivu makali ya kuchoma hasa wakati ukianza kutembea kwa mara ya kwanza asubuhi. Ukitembea kidogo maumivu hupungua, lakini yanaweza kurudi tena baada ya kipindi kirefu cha kusimama au unaposimama baada ya kuwa uliketi kwa muda. Chanzo halisi cha tatizo hili hakijafahamika. Ni tatizo linaloonekana zaidi baina wa watu wanaokimbia mbio au walio na uzito mkubwa. Tatizo hili linaweza kutibiwa kwa kutumia soli maalumu za ndani ya viatu na kufanya baadhi ya mazoezi.

 

Dalili Za Plantar Fasciitis

 

Palantar fasciitis mara nyingi husababisha maumivu makali ya kuchoma kwenye unyayo karibu na kisigino. Maumivu huwa makali zaidi unapoanza hatua chache cha mwanzo baada ya kuamka, ingawa yanaweza kusababishwa pia na vipindi virefu vya kusimama au wakati wa kusimama baada ya kuwa uliketi.

 

Sababu Za Maumivu Ya Kisigino

 

Mkanda wa tishu ngumu za nyuzinyuzi (plantar fascia) huunganisha mfupa wa kisigino na sehemu vinapoanzia vidole vya mguu. Mkanda huu huusaidia uvungu wa mguu na huwa ni shokomzoba wakati wa kutembea.

 

 

ugonjwa wa maumivu ya kisigino

 

Kuvutika na kugandamizwa kwa mkanda huu eneo unapoungana na mfupa wa kisigino huweza kusababisha nyufa ndogo. Kuvutika na kugandamizwa kwa mara kwa mara kwa mkanda huu kunaweza kuufanya uvimbe, ingawa sababu halisi bado haijabainishwa.

 

Hali Zinazochangia Tatizo La Kuumwa Kisigino

 

Pamoja na kwamba maumivu ya kisigino yanaweza kujitokeza bila sababu inayoeleweka, baadhi ya sababu zinakufanya uwe kwenye hatari kubwa zaidi. Nazo ni:

. Umri: Plantar fasciitis huwatokea zaidi watu wenye umri wa kati ya miaka 40-60.

. Aina Fulani Ya Mazoezi: Shughuli zinazoleta mgandamizo zaidi kwenye kisigino na tishu zinazoungana nacho – kama kukimbia mbio ndefu, dansi za ballet na aerobic – zinaweza kusababisha tatizo la maumivu kwenye kisigino.

 

. Umbo la mguu: Miguu isiyo na uvungu, uvungu kuwa juu au namna ya kutembea isiyo ya kawaida vinaweza kubadili mgawanyo wa uzito unapokuwa wima na kuongeza gandamizo kwenye mkanda wa tishu unaounganisha kisigino na vidole.

. Unene: Uzito wa kuzidi unasababisha mgandamizo mkubwa zaidi kwenye plantar fascia.

. Kazi Unazozifanya Ukiwa Wima: Wafanyakazi wa viwandani, walimu na wengine wanaotembea au wanaosimama juu ya maeneo magumu muda mwingi wakiwa kazini wanakuwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata plantar fasciitis.

 

Tiba Ya Maumivu Ya Kisigino

 

Watu wengi wenye tatizo hili hupona wenyewe baada ya miezi kadhaa kwa njia za kutibu wenyewe, kama za kuweka barafu sehemu yenye maumivu, kujikanda, kubadili miondoko au kukwepa shughuli zinazoleta maumivu.

Mazoezi yanayoweza kufanywa ili kujitibu na plantar fasciitis ni kama:

 

1) Towel Scrunch
2) Marble Pick-Ups
3) Arch Lifts
4) Heel Raises
5) Heel Raises on the Stairs
6) Tip Toe Walking
7) Single Leg Standing
8) Towel Stretch
9) Toe Stretch
10) Foot Roller

Upasuaji na Tiba Nyingine

 

Endapo tiba hizi ndogo hazikusaidia baada ya kutolewa kwa miezi kadhaa, daktari anaweza kushauri yafuatayo:

. Sindano: Kudunga sindano (steroids) eneo lenye maumivu kunaweza kupunguza maumivu kwa muda. Sindano nyingi hazishauriwi kwani zinaweza kudhoofisha plantar fascia. Plasma yenye uwingi wa platelets kutoka ndani ya damu yako inaweza kudungwa ili kuongeza kasi ya uponyaji.

. Extracorporeal shock wave therapy: Mionzi ya sauti inaweza kuelekezwa kwenye eneo la kisigino ili kusaidia uponyaji. Hii hutumika kwa maumivu sugu ya kisigino ambayo yalishindwa kukubali tiba nyingine.

. Ultrasonic tissue repair: Hii ni teknolojia inayotumia mionzi ya ultrasound katika kuiongoza aina ya sindano kwenye eneo lenye tatizo. Ncha ya kifaa hicho hutoa mitetemo ya haraka na kuvunja eneo lililoharibiwa na kufyonza nje ya mwili.

. Upasuaji: Watu wachache hufanyiwa upasuaji wa kutenganisha plantar fascia na mfupa wa kisigino. Ni uchaguzi unaofanywa baada ya tiba nyingine zote kushindwa na maumivu yakiwa makali sana.

Katika mada nyingine tutazungumzia  tatizo la maji ndani ya goti. Usisite kuuliza maswali uliyo nayo au kutoa maoni uliyo nayo kuhusu uandishi wa mada hii.

 

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu ndani ya saa za kazi  kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.