Kwikwi Ni Nini?

 

Kwikwi hutokea pale upumuaji wako unapositishwa kwa kipindi kifupi. Kwikwi inaweza kutokea bila sababu yo yote. Kwa kawaida kwikwi si kitu cha kusumbua sana, lakini kwikwi ikiendelea kwa muda mrefu ni ishara ya tatizo la kiafya. Watu wengi hupata kwikwi mara kwa mara, na kwikwi hiyo huondoka yenyewe bila tiba yo yote baada ya dakika chache. Mara chache, kwikwi za muda mrefu au chronic hiccups, ambazo zinadumu kwa mwezi mmoja au zaidi zinaweza kutokea. Kama kwikwi ikiendelea kwa zaidi ya saa 48, unahitaji msaada wa daktari. Hii inaweza kuwa kuwa ni ishara ya tatizo kubwa la kiafya. Kwikwi huwasumbua zaidi wanaume kuliko wanawake.

Kwikwi iliyomsumbua mtu kwa muda mrefu zaidi ilichukua miaka 60.

Kwa Nini Tunapata Kwikwi?

Kwikwi inapotokea, diaphragm (misuli inayotenganisha kifua na tumbo na ambayo ina mchango mkubwa katika upumuaji) pasipo kukusudiwa hujikunyata ghafla wakati huo huo larynx (zoloto- sehemu ya mwanzo ya koromeo inayohusika na utoaji sauti) ikijibana, na kusababisha kufunga kabisa kwa koo (glottis.) Hii husababisha hewa kuingia ghafla kwenye mapafu, na kutokea kwa sauti iliyozoeleka ya “hic”.

 

GloTtis ni sehemu ya kati ya larynx, eneo ambalo linahusika na sauti (vocal cords.)

Kwikwi moja tu inaweza kutokea au zikaja mfululizo. Zikija huwa zina mpangilio maalumu, maana yake muda kati ya kwikwi mbili huwa ni ule ule. Kwikwi zinazodumu zaidi ya saa 48 mara nyingi hubainika baina ya wanaume. Kwikwi huweza kutokea kwa kichanga kilicho bado tumboni (fetus). Kitaalamu kwikwi huitwa singultus.

Kuna vitu vinavyochangia kutokea kwa kwikwi, ambavyo ni pamoja na:

. Kula kwa haraka na kumeza hewa pamoja na chakulakwikwi hutokeaje
. Kula chakula kingi cha mafuta au chenye viungo vingi, au kunywa vinywaji vyenye kaboni au pombe
. Ugonjwa wo wote ambao utashambulia neva zinazohusika na utendaji kazi wa diaphragm (kama magonjwa ya ini, pneumonia, au magonjwa mengine ya mapafu.)
. Kiharusi au uvimbe kwenye ubongo
. Mvuke usio salama kwa afya unaweza kusababisha kwikwi
. Mabadiliko ya ghafla ya hali ya hewa
. Hofu au msisimko.

Baadhi ya dawa zinaweza pia kusababisha kwikwi, nazo ni kama:

. dawa za acid reflux
. Benzodiazepines
. Levodra, nicotine, na ondansetron.

Namna Ya Kuondokana Na Kwikwi Ukiwa Nyumbani

Kuna namna nyingi na kuondokana na kwikwi ukiwa nyunbani kwako. Unaweza kujaribu yafuatayo:

Njia ambazo zitatunza kaboni dayoksaidi, ambayo inasadikika kusimamisha kujikaza kwa diaphragm na kuondoa kwikwi:

. Vuta pumzi na usiitoe kwa muda

Mbinu ambazo zitazisisimua nasopharynx na vagus nerve ambayo inatoka kwenye ubongo hadi tumboni, na kupunguza kwikwi:

. Kunywa glasi moja ya maji kwa haraka
. Mpate mtu wa kukutisha
. Vuta hewa ndani taratibu kuyajaza mapafu yako. Ukiwa unatoa hewa, toa ulimi wako nje. Tumia vidole vyako kuuvuta ulimi mbele. Rudia hadi mara tatu kama kwikwi haiachi.
. tafuna limau
. Gogomoa kwa kutumia maji
. Weka sukari, nusu ya kijiko cha chai, chini ya ulimi.
. Wakati unameza, zibane pua zako kwa vidole
. Kunywa mvinyo kidogo
. Ukiwa umeketi, inyanyue miguu yako kuelekea kifuani kadiri utakavyoweza
. Inamie mbele ili ukimenye kifua chako taratibu
. Fikicha macho yako.

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini, au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu ndani ya muda wa kazi kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.