Mwanamme Kuwahi Kufika Kileleni, Nini Chanzo?

tatizo a kuwahi kufika kileleni

Tatizo La Kuwahi Kufika Kileleni Ni Nini?

Kuwahi kufika kileleni (premature ejaculation – PE) au kuwahi kumaliza tendo la ndoa au kwa lugha ya mtaani kukojoa upesi ni hali ambayo inampata mwanamme ambapo hutoa shahawa kabla ya kuanza tendo la ndoa au muda mfupi tu baada ya kuanza tendo, bila yeye mwenyewe kukusudia . Kwa kawaida mtu mwenye tatizo hili hutoa mbegu zake za kiume hata baada ya maandalizi kidogo sana. Tatizo hili hujidhihirisha zaidi kwa vijana wenye umri mdogo na hupungua kadiri umri wa mtu unavyoongezeka. Karibu kila mwanamme kwa wakati fulani hupata tatizo hili, lakini baadhi ya wanaume wenye umri wa kati huwa na tatizo la kudumu. Kwa bahati nzuri tatizo hili limepatiwa ufumbuzi na tiba inapatikana.

Chanzo Cha Tatizo La Kuwahi Kufika Kileleni

Chanzo kamili cha tatizo hili bado hakijafahamika. Lakini imethibika kwamba wasiwasi au mishipa ya fahamu inahusika sana na tatizo hili. Hali hii inaweza kutokea unapompata mpenzi mpya au unapofanya tendo hili baada ya muda mrefu kupita toka ulipotoa shahawa mara ya mwisho. Hii ndiyo sababu iliyofanya baadhi ya wanaume kugundua kuwa wakinywa pombe kidogo, huwapunguzia wasiwasi na huwasaidia wachelewe kufika kileleni. Mara nyingine tatizo hili linatokana na matatizo katika mfumo wa homoni za mtu au likiwa ni matokeo ya matumizi baadhi ya madawa.

Tatizo hili la kuwahi kumaliza tendo la ndoa ambalo kitaalamu huitwa premature ejaculation ni la kawaida linaloweza kuwapata karibu asilimia 20-30 ya wanaume.

Linaweza kutokea kwa sababu za kisaikolojia au za kimaumbile, ikiwa ni pamoja na kisukari na high blood pressure au pombe au matumizi ya madawa ya kulevya.

Kuna sababu kadhaa zinazosababisha tatizo la kuwahi kufika kileleni.

Sababu Za Kisaikolojia

Mara nyingi tatizo hili huanzia na sababu za kisaikolojia, ikiwa ni pamoja na:

. masuala ya mwonekano wa mwili
. kusisimkwa au kuchachawishwa kupita kiasi
. msongo wa mawazo unaoanzia kwenye mahusiano
. wasiwasi
. hisia za kuwa mkosefu au kukosa ukamilifu
. mfadhaiko
. matarajio potofu kuhusu uwezo wa tendo la ndoa
. historia ya kushindwa kukamilisha tendo la ndoa
. matatizo ya mahusiano

Matatizo haya ya kisaikolojia yanaweza kumwathiri mtu ambaye hapo awali alikuwa na uwezo mzuri tu wa kukamisha tendo la ndoa. Sababu hizi huitwa secondary au acquired PE.

Sababu Za Kibayolojia

Zifuatazo ni sababu zitokanazo na shida katika mwili.

. kisukari
. high blood pressure
. shida katika thyroid
. matumizi yasiyo sahihi ya madawa
. unywaji wa pombe wa kupitiliza.

Ugonjwa wa multiple sclerosis unaweza kuleta matatizo ya utoaji wa mbegu, pamoja na PE.

Njia Za Kutumia Kuondokana Na Tatizo La Kuwahi Kufika Kileleni

Mtu mwenye tatizo hili hupata tahadhali kidogo sana kabla ya kufika kileleni, kwa sababu hiyo hawezi kuchukua hatua za kukawiza.

Premature ejaculation humpunguzia starehe ya tendo la ndoa mhusika na mwenzi wake pia. Kuna tiba na hatua zinazoweza kuchukuliwa ili kukawiza ufikaji kileleni au kumsaidia aweze kuwa na utambuzi wa hisia na jinsi ya kufanya udhibiti.

Supplements

Baadhi ya mdini yanaweza kusaidia tatizo la kuwahi kufika kileleni. Madini hayo ni kama:

1. Zinc

Kuna uhusiano wa madini kama ya zinc na ufanisi wa tendo la ndoa. Zinc husaidia katika ugumba wa mwanamme.

Madini ya zinc huongeza kiwango cha testosterine katika damu na hivyo kuongeza hamu ya kufanya tendo la ndoa.

2. Magnesium

Magnesium ni madini mengine muhimu kwa afya ya uzalishaji wa mbegu za kiume. Utafiti mmoja ulionyesha kuwa viwango vidogo vya magnesium katika mwili vilichangia tatizo la kuwahi kufika kileleni.

Kwa hiyo, kupata madini ya magnesium ya kutosha katika chakula kutasaidia tatizo la PE.

3. Madini Mengine

Utafiti wa 2019 ulionyesha kuwa kuna madini mengine ambayo ni muhimu katika afya ya mbegu za kiume.

Madini hayo ni:

. calcium
. copper
. manganese
. selenium

BIdhaa Zinazosaidia

 

Kwa kawaida tatizo la kuwahi kufika kileleni mapema ni tatizo ambalo huondoka lenyewe kadiri umri unavyokuwa unasogea mbele. Kama tatizo sio kubwa sana, kwa mfano, kama unamudu kuendelea na tendo la ndoa kwa dakika tano na ungependa kufikisha dakika kumi, wewe sio mtu wa kumwona daktari bali mtu ambaye unaweza kufanya mazoezi fulani ya kuongeza muda wako. Vitu rahisi vya kufanya ni kutokuwa na papara, kutulia na kondoa mawazo yako kutoka kwenye tendo na kuyapeleka mbali kwenye jambo jingine tofauti kabisa unapokaribia kufika kileleni. Unaweza kufanya utafiti na mpenzi wako mkapata mtindo (sexual position) ambao utakusaidia usifike kileleni mapema. Kama hali yako ni mbaya zaidi, unaweza kutumia njia zifuatazo:

1. Anesthetic creams na sprays

GOLDEN KNIGHT SPRAY Tshs 50,000

Kupata msaada wa muda mfupi,wamaume wengi wanatumia creams na sprays ambazo zina anesthetic kama vile lidocaine. Hizi husiadia kutia ganzi kwenye uume. Husaidia kwa kuchelewesha hisia kwenye uume, na hivyo kuongeza muda wa kufika kileleni.

Kwa kawaida, mwanamme anatakiwa apake cream au kupulizia spray kwenye uume dakika 20-30 kabla ya tendo na kisha kuuosha uume dakika 5-10 kabla. Mwanamme anaweza kugundua pia kuvaa condom kunaweza kuongeza ufanisi.

Kuvaa condom wakati wa tendo la ndoa kunaweza kuwa na matokeo kama ya cream na sprays kwa kufifisha kwa muda hisia za kwenye uume. Wakati mwingine, uvaaji wa condom huongeza muda wa kufika kileleni na hasa zikitumiwa pamoja na cream au sprays.

Baadhi ya kampuni hutengeneza condom nene zaidi au kupulizia vitu vya kutia ganzi kwa ndani ili kupunguza usikivu wa hisia na hivyo kuongeza muda wa kufika kileleni.

Mbinu Nyingine

Mwanamme unatakiwa ujaribu mbinu mbalimbali wakati na kabla ya tendo ili kupata msaada wa kuondoa tatizo la kuwahi kufika kileleni. Mbinu hizo ni pamoja na:

Baadhi ya mazoezi yaitwayo pelvic floor exercises yanaweza kusaidia kuiimarisha misuli inayohusika na utoaji mbegu. Kwa kujenga uwezo wa kugundua na kuiimarisha misuli hii, unaweza kuongeza udhibiti wa umwagaji mbegu.

Utafiti wa 2014 uligundua kuwa programu ya wiki 12 ya mazoezi hayo yaliwasaidia wanaume wenye tatizo la kuwahi kufika kileleni kudhibiti tendohiari la kumwaga mbegu na kuongeza muda wa kufika kileleni.

Pelvic floor muscles ni misuli ile ile tunayoitumia katika kukatisha mkojo. Ili kuigundua mwanamme anatakiwa akojoe na kisha akatishe mkojo katikati.
Ikaze misuli inayohusika na kukatisha mkojo, shikilia kwa nguvu zote unazoweza kwa sekunde 5. Utaona misuli yako kama inapanda.

Ilegeze misuli yako kisha pumzika kwa sekunde 5. Rudia tendo hili mara 10 kama raundi moja. Fanya raundi 2 au 3 kwa siku.

2. Mazoezi

Wale ambao wanasumbuka na udhibiti wa tendo lao la ndoa na kuwahi kufika kileleni wanaweza kuwa ni wale wenye uzoefu mdogo wa kufanya mapenzi. Vijana wa balehe huwa wanajifunza kuhusu mwitiko wa kimapenzi wa miili yao na hisia zao kutokana na tabia zao za mwanzo za kupiga punyeto.

Watu walio wengi wanaweza kuwa na uzoefu ulio mdogo sana wa kupiga punyeto au shughuli za kimapenzi, labda kutokana na imani zao za kidini au kimila au kuwa na aibu.

Kutafuta starehe kwa kupiga punyeto kunawasaidia watu kutambua hisia za miili yao zinazowafanya kufika kileleni. Kufanya mazoezi ya mara kwa mara ya kupiga punyeto yanamsaidia mtu kujua ishara za mshindo na kutafuta njia za kuzuia msisimko kabla ya mshindo..

Vile vile, watu wengine wanashauri kupiga punyeto saa moja au mbili kabla ya kufanya mapenzi. Hii inasaidia kupata faida ya mwili ya refractory period, ambao ni muda ambao haiwezekani kufika au kufika mshindo kwa shida. Urefu wa refractory period huwa tofauti kutoka mtu mmoja hadi mtu mwingine.

Refractory period ni kipindi kinachopita baada ya kufika mshindo ambapo mtu hasikii kufanya tendo la ndoa. Kinaweza kuwa urefu tofauti, kati ya dakika chache hadi zaidi ya siku moja.

Wakati ukiwa ndani ya kipindi hiki, mtu unapoteza hamu ya kufanya mapenzi, au unashindwa kufanya tendo la ndoa. Uume unaweza kushindwa kusimama, unaweza kushindwa kumwaga mbegu, au kifika mshindo.

Kumwaga mbegu (ejaculation) ni tendo la kutoa manii kutoka kwenye uume. Mshindo (orgasm) ni hali ya kisikia raha sana ambayo inaambatana na kufikia kilele cha tendo la ndoa. Baina ya wanaume wengi, mshindo na kumwaga mbegu vinaenda sambamba lakini hivi ni vitu viwili tofauti na ambavyo vinaweza kutokea kila kimoja kwa wakati tofauti.

Madaktari wanafafanua kuwa resolution stage ni hatua katika tendo la ndoa ambapo mtu anajisikia kuridhika, mara nyingi baada ya mshindo au, kwa wanaume, baada ya kumwaga mbegu.

Refractory period hutokea baada ya resolution stage.

Wakati wa kipindi hiki cha refractory, uume wa mwanamme hauwezi kusimama. Aina hii huitwa physiological refractory period, maana yake maumbile ya mwanamme hayaweza kufanya mapenzi tena.

Tofauti na wanaume, wanawake wengi wanaweza kufika mshindo mara kadhaa mfululizo, maana yake kikawaida hawana physiological refractory priod. Isitoshe, maumbile ya mwanamke yanaweza kubaki yakiwa na ute baada ya tendo la ndoa hata kama hajasisimka, na kuhusu kuendelea na tendo la ndoa.

Hata hivyo, watu wote waume kwa wake wanaweza kufikia psychological refractory period.

Aina hii hutokea [ale mtu asipotaka kufanya tena tendo la ndoa. Wanajiskia wametosheka na hawapenda kuguswa tena kimapenzi. Wengine hujisikia wamechoka wakiwa katika kipindi hiki.

Utafiti wa akili ya mtu, unashauri kuwa matamanio ya kimapenzi hufuata hatua zile zile za vitu vingine vya kujistarehesha. Huanza na hamu kali, hufikia kuridhika na huisha kwa kupungua kwa hamu.

Utafiti umeshindwa kujua ni nini kinasababisha refractory period na kwa nini huwa tofauti kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Lakini, si wamaume wote wana refractory period.

Wakati wanawake wengi hupoteza hamu ya mapenzi baada ya mshindo, kimaumbile bado wanaweza kuendelea kufanya tendo la ndoa.

Uwezo wa kufanya mapenzi hubadilika na umri. Watu watahitaji muda mrefu zaidi kuamka kimaumbile na kiakili kadiri umri unaavyokuwa mkubwa. Maana yake, refractory period huwa ndefu zaidi umri ukiwa mkubwa zaidi.

Reractory period ya mtu akiwa kijana huamua mabadiliko atakayoyaona umri ukisogea. Kijana mwenye refractory period ndefu ataona ikiwa ndefu zaidi umri ukisogea.

3. The squeeze technique

Squeeze technique husaidia kuudhibiti mshindo. Inaweza pia kusaidia kutambua hisia zinazoashiria kufika mshindo na kujifunza namna ya kufanya udhibiti.

Mwanamme au mwenzi wake atausisimua uume hadi ufike karibu ya kumwaga mbegu. Kisha mpini wa uume utaminywa kwa nguvu hadi hali ya uume ukianza kunywea kidogo na kufifisha uwezekano wa kufika mshindo. Uume unatakiwa uendelee kuminywa kwa takribani sekunde 30.

Akifuata utaratibu huu mwanamme anaweza akajifunza kutambua mhemuko unaoashiria kufika mshindo. Kuitambua mihemko hii kunaweza kusaidia katika kudhibiti umwagaji wa mbegu.

4. The stop-start method

Mbinu ya star-stop ni njia nyingine ya kimaumbile ya kufanya mazoezi ya kufanya tendo la ndoa.

Njia hii inahusisha mwanamme au mwenzi wake kuusisimua uume hadi mshindo unapokaribia kufikiwa. Wanatakiwa kusimamisha usisimuaji na kuuruhusu mshindo upotee kabisa.

Baada ya raha ile kupotea kabisa, mwanamme au mwenzi anausisimua uume tena na kusimama kabla tu ya kufika mshindo. Rudia mzunguko huu mara kadhaa ili kuboresha uwezo wa kutambua ishara zinazoashiria kumwaga mbegu.

Mbinu hii inaweza pia kutumika kwa kufanya tendo la ndoa na mwanamke hadi unapokaribia mshindo na kusimama hadi dalili za mshindo zikipotea kabisa.  Wawili hawa warudie tena kufanya tendo landoa hadi hali ya kufikia mshindo inapokaribia.  Mzunguko huu unaweza kurudiwa mara kadhaa.

Mbinu hii inaweza kumsaidia mwanamme kutambua mihemko inayotokea kabla ya kufika mshindo. Ugunduzi huo utarahisisha utambuzi au udhibiti wa umwagaji mbegu.

Kuhitimisha

Kufanya mazoezi yanayosaidia kuondoa tatizo la kuwahi kufika kileleni. Hapa chini ni orodha ya baadhi ya mazoezi unayoweza kufanya;

  • Kuvuta Na Kutoa Pumzi (Deep Breathing)
  • Kuanza Na Kukatisha (The Stop-and-Start Method)
  • Kuminya (The Squeeze Method)
  • Mazoezi Ya Kegel (Kegel Exercises)
  • Mazoezi Ya Tantra (Tantric Techniques)

Mazoezi ya Kegel tumeyapa umuhimu wa kipekee kutokana na ubora wake katika kuondoa tatizo la kukojoa upesi na tumeandika ukurasa wa pekee kwa mazoezi hayo. Katika ukurasa huo (Mazoezi Ya Kegel – Kegel Exercises) tumeweka video moja ya kuonyesha jinsi ya kufanya mazoezi hayo.

Kutumia kondomu maalumu (Condoms With Benzocaine). Kondomu hizi hukusaidia uendelee na tendo la ndoa na kuongeza muda wako wa kufika kileleni kwa kiwango cha hadi dakika tano. Kondomu hizi huwekwa benzocaine ambayo hutia ganzi kwa kiwango kidogo sehemu ya kichwa ya uume ili kupunguza usikivu wa nyege (sexual sensation) na kumfanya mwanamme aweze kutawala muda wake wa kufika kileleni.

Kutumia dawa zilizotengenezwa mahsusi kwa tatizo hili (Antidepressant medicines). Dawa ambazo zimekuwa zikitumika ni pamoja na Vig Power, Clomipramine (Anafranil) na Dapoxetine (Priligy). Tramadol (Ultram), dawa ambazo hutumika kuondoa maumivu, hutumika pia kuondoa tatizo hili.

Kuna creams, gels na sprays ambazo zimetengenezwa kupambana na tatizo la kukojoa haraka. Hizi hufanya kazi kwa kupunguza usikivu wa nyege kwenye dhakari. Mfano wa dawa hizi ni lidocaine au lidocaine-prilocaine ambayo hupakwa kwenye uume kabla ya kuanza kujamiiana.

Katika mada nyingine tutalizungumzia tatizo ambalo linasumbua watu wengi sana katika jamii yetu, nalo ni tatizo la jogoo kushindwa kuwika (Erectile dysfunction) au kwa lugha ya mitaani tatizo la uume kushindwa kusimama.

Kama una tatizo kama hili na ungependa kupata maelezo zaidi au msaada wa dawa, usisite kuwasilana nasi kwa njia yo yote unayoona inakufaa kati ya hizi hapa:

Kwa maelezo zaidi na ya kina, tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu hapa chini kwa kujaza fomu, au tutumie barua pepe kupitia promota927@gmail.com au tupigie simu ndani ya saa za kazi   kwa namba zifuatazo: +255 655 858027 au +255 756 181651.