Umuhimu Wa Iodine Katika Mwili

 

 

Iodine ni madini yanayotakiwa yapatikane kutoka kwenye chakula ili kuhakikisha tezi ya thyroid inafanya kazi vizuri.

Homoni za thyroid ni za muhimu sana katika utendaji kazi wa mwili, ikiwa ni pamoja na shughuli za kimetaboliki, afya ya mifupa, kinga za mwili, na katika ukuaji wa mfumo wa central nervous system (CNS).

Iodine husaidia kuibadilisha thyroid stimulating hormone (TSH) kuwa triiodothyronine (T3) na thyroxine (T4). Ubadilishwaji huu ni wa muhimu ili thyroid ifanye kazi vizuri.

Uwiano usio mzuri wa iodine unaweza kusababisha kufanya kazi kwa ziada (overactive) au ufanyaji kazi wa chini (underactive) wa thyroid.

Karibu asilimia 70 hadi 80 ya iodine inapatikana ndani ya tezi ya thyroid kwenye shingo. Kiasi kinachosalia hupatikana ndani ya damu, misuli, na ovari, na sehemu nyingine za mwili.

Upungufu wa iodine huonekana mara chache kwa sababu chumvi huwekwa iodine. Lakini, inakadiriwa kuwa karibu watu bilioni 2 wapo kwenye hatari ya kuwa na upungufu wa iodine, na karibu watu milioni 300 duniani wana shida ya utendaji kazi wa tezi za thyroid.

 

Ukweli Kuhusu Iodine

 

Hapa chini hoja za msingi kuhusu iodine

. iodine ni ya muhimu kwa utendaji kazi wa thyroid.
. iodine kupita kiasi au upungufu wa iodine hulata dalili za hyperthyroidism au hypothyroidism.
. Vyanzo vizuri vya iodone ni chumvi (seaweed and iodized salt).
. Upungufu wa iodne ni nadra katika nchi za magharibi, na iodine ya ziada itumiwe kwa ushauri wa daktari.

 

Kiasi Cha Iodine Kinachopendekezwa Na Vyanzo Vya Iodine

 

Kiasi cha iodne kinachopendekezwa kwa mtu wa miaka kuanzia 14 ni microgramu 150, kwa wote, wnawake na wanaume. Wakati wa ujauzito kiasi kinapanda hadi microgramu 220, na kufikia microgramu 290 wakati wa kunyoyesha.

Chakula ndicho chanzo bora cha iodine.

Kiasi cha iodine katika chakula kinategemea eneo mimea hiyo ilikopatikana. Kiwango cha iodnie katika udongo kilipooteshwa chakula, au sehemu mifugo ilikolishwa kina uhusiano na kiwango cha iodine katika chakula. Bidhaa kutoka baharini ni chanzo kizuri cha iodine.

Kiwango cha iodine katika chakula kitategemea chakula hicho kimepatikana wapi. Katika matunda na mboga za majani, kinaweza kuanzia microgramu 10 hadi gramu moja kwa kilo ya bidhaa iliyokaushwa.

Kwa sababu ya tofauti hizi, kiwango cha iodine katika chakula ni cha kukadiria

Hapa chini ni vyanzo vizuri vya iodine:

. Seaweed: gramu moja ya seaweed nzima ina microgramu 16 hadi 2,984 za iodine
. Iodized salt: robo ya kijiko, au gramu 1.5 ina microgramu 71, au asilimia 47 ya mahitaji ya mwili ya siku
. Baked cod: kipande cha aunzi 3 kina microgramu 99 au asilimia 65 ya mahitaji ya siku
. Reduced-fat milk: kikombe kimoja kina microgramu 56, au asilimia 37 ya mahitaji ya siku ya mwili
. White, enriched bread: Slice mbili zina microgramu 45, au asilimia 30 ya mahitaji ya siku ya mwili
. Yai: yao moja kubwa lina microgramu 24, au asilimia 16 ya mahitaji ya siku
. Cheddar cheese: Aunzi moja ina microgramu 12, au asilimia 8 ya mahitaji ya mwili ya siku.

 

Upungufu Wa Iodine Katika Mwili

 

Upungufu wa iodnie kwa mama mjamzito au katika miaka ya mwanzo ya utotoni unaweza kusababisha matatizo ya ukuaji wa mwili.

Mwili kupata iodine kwa kiwango kidogo kunaweza kusababisha utolewaji mkubwa zaidi wa thyroid stimulating hormone (TSH). TSH ikiongezeka, tezi ya thyroid itachukua kiwango kikubwa zaidi cha iodine kutoka kwenye damu, ili kuweka sawa mahitaji ya iodine. Hali hii inaweza kutokea kama kiwango cha iodine kitashuka chini ya microgramu 100 kwa siku.

Ikiwa kiwango kitashuka hadi chini ya microgramu 10 hadi 20 kwa siku, tezi ya thyroid haipati iodine ya kutosha, na hypothyroidism hutokea, na kutoa dalili  za goita, ambao ni uvimbe unaoonekana kwenye eneo la shingo.

Mama mjamzito akiwa na upungufu huu, kiumbe wake wa tumboni ataathirika katika ukuaji wa akili, wa kimaumbile na wa neva.

Baina ya watoto wadogo, upungufu wa iodine husababisha kuwa na ufahamu mdogo. Kama tiba haitatolewa, ulemavu wa akili unaweza kutokea.

Pamoja na goita, hypothyroidism yaweza kuleta dalili zifuatazo:

. uchovu, mfadhaiko, na usahaulifu
. udhaifu wa nywele na kupunyuka nywele
. ukavu wa ngozi
. unene
. kushindwa kuhimili baridi
. kukosa choo

Goita kubwa yaweza kuleta matatizo ya kumeza au kupumua.

 

Athari Za Iodine

 

Kiwango cha juu kinachoshauriwa cha iodine inayoingia mwilini kwa siku ni microgramu 1,100 kwa watu wazima na microgramu 300 kwa watoto wa hadi miaka 8.

Iodine ina matokeo yasiyotabirika kwenye tezi ya thyroid. Iodine kwa wingi mno au upungufu wa iodine vyote vinaweza kusababisha goita na matatizo mengine ya tezi ya thyroid. Kwa sababu hiyo, yafaa kupata ushauri wa daktari kabla ya kutumia supplements za iodine.

Iodine kupita kiasi inaweza kuleta dalili kama zile za upungufu wa iodine, ikiwa ni pamoja na goita na matatizo mengine ya thyroid.

Iodine kupita kiasi inaweza kusababisha thyroiditis na thyroid papillary cancer.

Katika viwango vikubwa, iodine inaweza kuleta:

. kuungua kwa midomo, koo, na tumbo
. homa
. maumivu ya tumbo, kichefuchefu, kutapika, na kuharisha
. mapigo ya moyo dhaifu
. coma.

Katika mada yetu nyingine tutazungumzia umuhimu wa zinc katika mwili. Usisite kutoa maoni yako kuhusu uandishi wa mada hii au kuuliza maswali uliyo nayo:

Pata ushauri zaidi kwa kututumia ujumbe kupitia ukurasa huu hapa chini kwa kujaza fomu, au kututumia barua pepe kupitia promota927@gmail.com au tupigie simu ndani ya  saa za kazi kwa namba zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

 

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.