Kiungulia Ni Nini?

 

kiungulia ni kitu gani

 

Kiungulia ni tatizo linalowapata watu wengi. Kiungulia ni hali ya kukukosesha raha ya kusikia kuwaka moto kwenye eneo la kifua na kuenea hadi shingoni na kwenye koo. Ukiwa na kiungulia unaweza kusikia ladha ya uchachu nyuma ya koo. Kiungulia kinaweza kudumu kwa muda mfupi au kikaenda kwa saa kadhaa. Kiungulia huwa kikali zaidi baada ya kula au ukilala mara baada ya kula.

Ukiwa na kiungulia cha mara kwa mara au kikali, unaweza kuwa na matatizo ya kiafya ya chronic acid reflux, au gastroesophageal reflux disease (GERD) au pengine ujauzito. Kiungulia kinaweza kutibika nyumbani kwa dawa za kununua.

 

Dalili Za Kiungulia

 

Unapokuwa na kiungulia unaweza kuziona dalili zifuatazo:

. Kuwaka moto sehemu za kifua hali inayodumu kwa  dakika au saa kadhaa
. Maumivu ya kifua ukiinama au kulala
. Kuwaka moto kooni
. Ladha ya uchachu, ya chumvi, asidi nyuma ya koo
. Shida katika kumeza.

Kiungulia Husababishwa Na Nini?

 

Ili kujua kwa nini kiungulia kinatokea, ni muhimu kujua jinsi umio (esophagus) na tumbo vinavyofanya kazi. Unapokula, chakula huteremka kupitia kijibomba kirefu kinachounganisha mdomo na tumbo. Kijibomba hiki huitwa esophagus. Chini ya esophagus kuna vali (valve), inayoitwa esophageal sphincter. Vali hii hufunguka ilichanzo cha kiungulia kuachia chakula kipite na kisha hufunga kuzuia chakula kilichopo ndani ya tumbo kisirudi. Ndani ya tumbo kuna mchanganyiko wa tindikali kali ambayo huanza kazi ya kukimeng’enya chakula. Tumbo limetengenezwa kuuhimili mchanganyiko huu. Lakini, umio (esophagus) hauwezi kuuhimili mchanganyiko huu bila kupata madhara.

Wakati mwingine, vali inayotenganisha tumbo na umio haifungi vizuri na kuruhusu mchanganyiko wa tumboni kupanda juu kwenye umio. Hii huitwa reflux. Unapokuwa na reflux, utasikia hisia ya kuwaka moto na hali hiyo ndiyo inayoitwa kiungulia.

Kuna baadhi ya hali zinazoweza kukuletea kiungulia na ukahisi kuwaka moto, nazo ni:

. Ujauzito.
. Hiatal hernia (wakati tumbo linatuna kuingia kifuani).
. Gastroesophageal reflux disease (GERD).
. Baadhi ya madawa, na hasa anti-inflammatory drugs na aspirin.

Kiungulia kinaweza kusababishwa pia na tabia za kiulaji -ikiwa ni pamoja na chakula ukilacho, ukubwa wa milo yako na ukaribu wa kula kabla ya kulala -pamoja na tabia nyingine za kimaisha.

Vitu Gani Ukila Vitachochea Kiungulia?

 

Kiungulia huweza kusababishwa na vitu vingi kadhaa ambavyo ni sehemu ya maisha yako ya kila siku. Kwa walio wengi, kiungulia husababishwa na tabia za ulaji na kuishi. Vitu sababishi vya kiungulia ni pamoja na kula chakula kingi, kula chakula muda mfupi kabla ya kulala au pengine kuwa na msongo wa mawazo.

Aina fulani za chakula na vinywaji huweza kusababisha kiungulia kwa baadhi ya watu. Chakula na vinywaji vinavyoweza kuleta kiungulia ni pamoja na:

. Vitunguu
. Matunda ya jamii ya michungwa
. Chakula chenye mafuta mengi
. Bidhaa za nyaya
. Pombe
. Juisi zinazotokana na matunda ya jamii ya michungwa
. Vinywaji vyenye kafeini
. Vinywaji vyenye kaboni.

Hali nyingine zinawezoweza kusababisha kiungulia ni:

. Unene
. Uvutaji wa sigara
. Kuwa na msongo mkali wa mawazo
. Kuvaa nguo zinazobana na mikanda.

 

Tiba Kwa Ajili Ya Kiungulia

 

Mara nyingi kiungulia huweza kutibiwa nyumbani kwa kununua dawa au kwa kubadili staili ya kuishi. Kuwa na kiungulia mara chache ni kitu cha kawaida na mara nyingi hakuleti madhara makubwa. Lakini endapo unapata kuingulia mara kwa mara na kikali, unahitaji msaada wa tiba kwani inaweza kuwa ni dalili ya tatizo sugu kama la GERD. GERD huweza kusababisha matatizo makubwa zaidi kama esophagitis (hali inayoweza kuharibu tishu za umio), Barret’s esophagus au hata kansa. Wakati mwingine daktari anaweza kuhitaji kuchukua kipimo cha endoscopy kujua chanzo cha tatizo. Endoscopy ni uchunguzi wa mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kwa kutumia kifaa kinachopindika kinachotoa mwanga.

 

dawa za kiungulia

 

Dawa unazoweza kununua ukiwa nyumbani ni pamoja na antacids na acid blockers. Antacids hupunguza kiwango cha tindikali ndani ya tumbo, na kwa hiyo kuondoa kiungulia. Dawa hizi zinaweza pia kutumika kupunguza mchafuko wa tumbo, kuvimbiwa na maumivu mengine ya tumbo. Acid blockers hupunguza utengenezwaji wa tindikali ndani ya tumbo.

Unawezaje Kukizuia Kiungulia?

 

Unaweza kukizuia kuingulia au kukiondoa kwa kufanya mabadiliko katika namna yako ya ulaji na staili yako ya maisha. Hii ni pamoja na:

. Kuacha kuingia kitandani ukiwa na tumbo lililojaa. Yafaa kula chakula angalau saa 3 au 4 kabla ya kwenda kulala. Hii itatoa muda wa tumbo lako kuwa tupu na kuondoa uwezekano wa kukipata kiungulia usiku.

. Acha kula kupita kiasi. Kupunguza ukubwa wa mlo wako kunaweza kupunguza uwezekano wa kupata kiungulia. Unaweza pia kujaribu kula milo midogo mara nne au tano kwa siku badala ya milo mitatu mikubwa.

. Kula taratibu kunaweza kuzuia kiungulia. Weka kijiko chini ukianza kutafuna ili ujizuie kula kwa haraka.

. Kuvaa Nguo Zinazopwaya. Mikanda na nguo za kubana zinaweza wakati mwingine kuchochea kiungulia. Kwa kubadilisha uvaaji wako unaweza kukizuia kiungulia.

. Kwepa aina fulani za chakula. Kwa watu wengi kuna baadhi ya chakula kinachowasababishia kiungulia. Kukwepa chakula cha aina hizo kunaweza kusaidia. Jaribu kuweka kumbukumbu ya chakula ili kuweza kukikwepa siku za baadaye. Tabibu anaweza pia kukushauri kuacha pombe.

. Jiweke kwenye uzito unaofaa. Kupunguza unene mara nyingi huondoa kiungulia.

. Usivute sigara. Nicotine inaweza kuidhoofisha esophageal sphincter ya chini. Kuacha kuvuta sigara kunashauriwa kwa afya njema, na kuiimarisha vali hiyo.

. Kulalia upande wa ushoto. Kulala kwa upande wa kushoto kunaweza kuuboresha mmeng’enyo wa chakula na uondoaji wa tindikali kwenye tumbo na umio haraka zaidi.

. Kunyanyua sehemu ya juu ya kitanda chako. Kunyanyua sehemu ya juu ya kitanda kutafanya kichwa na kifua kuwa juu zaidi ya miguu. Weka matofali ya nchi sita au vitabu chini ya mihimili ya juu ya kitanda chako. Usitumie mito. Mito inaweza kuleta msukumo mkubwa zaidi juu ya tumbo na kukuongezea kiungulia.

. Weka plani ya mazoezi yako ya mwili. Subiri angalau saa mbili baada ya kula ndipo ufanye mazoezi. Mazoezi ya kabla yanaweza kuamsha kiungulia. Yafaa kunywa maji mengi kabla na wakati ukiendelea na mazoezi. Maji husaidia umeng’enywaji wa chakula na kuzuia ukosefu wa maji mwilini.

Katika ukurasa wetu mwingine tatalijadili tatizo la vidonda vya tumbo. Usisite kutoa maoni yako au kutuuliza maswali kuhusiana na mada yetu hii ya leo.

 

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

 

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.