Chanzo Cha Chunjua (Warts) Ni Nini? Jee, Ni Nini Tiba Ya Chunjua?

 

 

 

 

Kuna tatizo linalosumbua watu wengi la kuota vitu juu ya ngozi zao. Vitu hivi huota mikononi, miguuni na hata sehemu za siri. Vitu hivi vimeitwa chunjua au wengine wameviita masundosundo. Lakini hasa, chunjua ni nini au masundosundo ni nini? Mada yetu ya leo ina dhamira ya kutoa jibu kwa swali hilo na kuelezea aina za chunjua, dalili za chunjua na kudokezea juu ya tiba za chunjua.

Chunjua au wengine wanavyoyaita masundosundo ni uvimbe juu ya ngozi unaosababishwa na kirusi aitwaye human papillomavirus (HPV). Kuna aina tofauti zaidi ya 150 za HPV. Aina nyingine ya kirusi huyu hushambulia sehemu za siri na sehemu za mdomo na kujenga uvimbe mkubwa , ambao mara nyingine huendelea na kuwa saratani. Aina nyingine hushambulia ngozi na kujenga uvimbe ambao hauhusishwi na saratani. Pamoja na kuwa chunjua huambukiza, si ajabu kuona kuwa mtu mmoja tu ndani ya familia ndiye aliyeathirika. Vile vile chunjua hushambulia sehemu moja tu ya mwili (kama vile mikono au miguu), ingawa huweza kuenea hadi sehemu nyingine za mwili. Aina ya chunjua inayotokea huendana na aina ya kirusi wa chunjua na kiungo kilichoshambuliwa. Kwa mfano, kirusi wa aina moja huweza kusababisha chunjua za aina ya ‘common warts’ kwenye mikono na vile vile akasababisha chunjua za aina ya plantar.

 

 

HPV wamethibitika kuwa ni chanzo katika kukua kwa kansa za viungo vya uzazi kama kansa ya shingo ya kizazi na kansa za mkundu. HPV vile vile wamehusishwa na ukuaji wa kansa za kichwa na shingo zinazoanzia kwenye findo (tonsils).

HPV wengine wasio na madhara makubwa sana huleta uvimbe sehemu za siri, genital warts. Wengine hushambulia ngozi na kuleta chunjua sehemu mbalimbali za mwili. Wapo HPV wengine wanaosababisha uvimbe kwenye viungo vya sauti (vocal cords).

Aina za chunjua zinazoonekana kwa wingi ni common warts, flat warts, plantar warts, periungual warts, filiform warts na genital warts.

 

Chunjua Za Aina Ya Common Warts

 

Common warts ni chunjua ndogo zinazojengwa na uvimbe wa chambechembe ndogo chunjua common warts za ngozi ambazo mara nyingi hutokea kwenye vidole au mikono. Chunjua hizi ambazo hukwaruza ziguswapo, mara nyingine huja kama vijidoa vyeusi, ambavyo ni mishipa midogo ya damu yenye damu iliyovia.

Common warts husababishwa na kirusi anayeenezwa kwa kugusana. Inaweza ikachukua miezi 2 hadi 6 chunjua kuanza kujijenga baada ya kugusa kitu chenye kirusi huyu. Chunjua hizi hazina madhara makubwa na baadaye hupotea zenyewe. Watu walio wengi huamua kuziondoa kwa sababu tu huona kama ni bughudha kwao.

Dalili Za Common Warts

Common warts kwa kawaida hutokea kwenye vidole au mikono na huwa:

– Kama uvimbe mdogo uliojengwa kwa chembechembe ndogo za nyama
– Zenye rangi ya nyama, nyeupe, pinki au hudhurungi
– Zenye mikwaruzo zikiguswa
– Zenye alama nyeusi zilizojitawanya, ambazo ni mishipa midogo ya damu.

 

Chanzo Cha Chunjua Za Common Warts

Common warts husababishwa na human papillomavirus (HPV). Kirusi huyu anapatikana kwa wingi sana na kuna aina tofauti zaidi ya 150 za kirusi huyu, lakini ni aina chache sana zinazoweza kuleta chunjua kwenye mikono. Aina nyingine za HPV hupatikana kwa kushiriki ngono. Aina nyingi zaidi hupatikana kwa kugusana ngozi au kuchangia vitu , kama taulo au vifaa vya kujioshea. Kirusi huingia mwilini kupitia michubuko kwenye ngozi. Kukata kucha kwa meno kwaweza kusababisha kusambaa kwa kirusi huyu kwenye ncha za vidole au kuzunguka kucha.

 

Chunjua Za Aina Ya Flat Warts

 

Flat warts ni uvimbe juu ya ngozi ulio laini, bapa, wenye rangi ya ngozi au kahawia ya

warts flat wartsnjano wenye ukubwa wa ncha ya sindano. Mara nyingi hupatikana usoni, maeneo ya nyuma ya mikono au miguu na huwa kwenye kikundi cha chunjua 20 hadi 200 kwa pamoja. Chunjua hizi huwapata zaidi watoto wadogo na vijana. Flat warts husababishwa na kirusi ambaye anaambukiza, lakini asiye na madhara wala maumivu.

Flat warts huingia kupitia majeraha ya kwenye ngozi. Wanaume hupata chunjua hizi baada ya kunyoa ndevu, wakati wanawake huwa na chunjua hizi miguuni.

Kama ilivyo kwa chunjua za aina nyingine, husababishwa na human papillomavirus (HPV). Flat warts husababishwa na HPV wa koo za 3, 10, 28 na 49. HPV hawa hawana madhara, tofauti na wengine, kama genital warts, wanaosababisha saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake. Flat warts wanaweza kuenezwa kwa kugusana na ngozi yenye chunjua au kutumia taulo au chombo ambacho kimetumika na mwathirika. Unaweza pia kueneza chunjua hizi kutoka sehemu moja ya mwili wako hadi nyingine.

Flat warts kwa kawaida huondoka zenyewe bila kuhitaji tiba. Unaweza kupata tiba ili kupona haraka zaidi. Daktari anaweza kukuandikia cream, lakini cream hizi huchubua ngozi ili kuondoa chunjua. Cream hizi ni kama:

. retinoic acid 0.05 percent cream
. Imiquimod 5 percent cream (Aldara, Zyclara)
. Topical 5-fluorouracil (Carac, Efudex, Fluoroplex, Tolak), 1 percent or 5 percent cream

Daktari anaweza pia kukuandikia 5 percent benzoyl-peroxide (Del Aqua, NeoBenz Micro, au Clearskin, EFFACLAR).

 

Chunjua Za Aina Ya Plantar Warts

 

Plantar warts ni vijiuvimbe vidogo vinavyotokea kwenye kisigino au sehemu ambazo zinabeba uzito za kwenye mguu. Mgandamizo kwenye maeneo hayo kunaweza kusababisha plantar warts kuota kuelekea ndani, chini ya tabaka nene la ngozi (callus).

Plantar warts husababishwa na HPV. Kirusi huyu huingia mwilini kupitia sehemu ndogo ulizojikata, au sehemu nyingine dhaifu za maeneo ya chini ya mguu.

Plantar warts nyingine hazihatarishi afya na hujiondokea zenyewe baada ya muda bila tiba yo yote.

 

Chanzo Cha Plantar Warts

Plantar warts zinasababishwa na HPV anapoingia kwenye tabaka la juu la ngozi ya kwenye unyayo kupitia vijijeraha vidogo au maeneo mengine yaliyo dhaifu yaliyo maeneo ya chini ya mguu.

HPV hupatikana kwa wingi, na kuna aina tofauti zaidi ya 100 ya kirusi huyu. Lakini ni aina chache tu ambazo zinaweza kuleta chunjua kwenye mguu. Aina nyingine warts plantar chunjuazinaweza kuleta chunjua kwenye maeneo mengine ya ngozi au kwenye utando telezi.

Kila mtu ana kinga zake za mwili zenye uwezo tofauti wa kupambana na HPV. Si kila mtu atakayegusana na kirusi huyu atapata chunjua. Hata watu wa familia moja watahimili kirusi huyu kwa viwango tofauti.

HPV wanaoeneza plantar warts hawaambukizi kirahisi. Kwa hiyo chunjua hizi haziambukizi kwa kugusana. Lakini wanapenda kuishi kwenye mazingira ya vuguvugu, yenye unyevu. Kwa hiyo unawea kumpata kirusi huyu kwa kutembea peku kwenye mabwawa ya kuogelea. Kirusi akipenya sehemu moja, anaweza kuenea hadi maeneo mengine na kusababisha chunjua.

 

Chunjua Za Aina Ya Periungual Warts

 

Chunjua za aina hii hujijenga kuzunguka kucha za vidoleni au kwenye dole gumba. Zikikua huweza kukukosesha raha au kuleta maumivu na huweza kuathiri ukuaji wa kucha. Watoto na vijana wa umri wa balehe wana nafasi kubwa zaidi ya kupata periungual warts na hasa kama wana tabia ya kung’ata kucha zao.

 

warts periungual chunjua mkono

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Periungual warts huwa ndogo sana mwanzoni, ukubwa wa ncha ya sindano, zikiwa laini na za kung’aa. Katika wiki au miezi michache, huweza kufikia ukubwa wa njegere zikiwa na umbo la kaliflawa.

Periungual warts huweza kuwa na rangi ya kahawia, kujivu, au nyeusi. Baadaye hujijenga na kuwa nyingi kwa pamoja. Zikiwa kubwa huweza kuleta maumivu.

Periungual warts huletwa na baadhi ya koo za human papillomavirus (HPV). Kirusi warts periungual chunjuahuyu huambukiza kupitia kugusana na mtu mwenye ugonjwa huu au kupitia mataulo au vimwanasesere. Kirusi huyu hupitia sehemu zenye majeraha, na hii ndiyo sababu watu wanaopenda kutafuna kucha zao huwa kwenye hatari zaidi. Watu wenye upungufu wa kinga za mwili au wenye magonjwa ya ngozi nao huathirika kirahisi zaidi.

 

Chunjua Za Aina Ya Filiform Warts

 

Chunjua za aina hii zina mwonekano wa tofauti kabisa na nyingine. Filiform warts ni chunjua filiform wartsmichomozo mirefu myembamba yenye urefu wa kati ya milimeta 1 hadi 2 juu ya ngozi. Zinaweza kuwa na rangi ya njano, kahawia au rangi ya ngozi, na haijijengi kwa vikundi. Kwa vile hupenda kutokea kwenye kope au mdomoni, chunjua hizi huitwa pia facial warts. Chunjua hizi huweza kutokea pia kwenye shingo, kwenye vidole na miguuni. Zinaweza kusambaa kwa haraka sana kwenye sehemu nyingine za mwili.

Filiform warts husababishwa na human papillomavirus (HPV), ambaye huambukiza. Anaweza kuambukizwa kwa kugusana ngozi, na hasa kama kuna jeraha kwenye ngozi. Pamoja na kuwa haziwezi kusababisha saratani, huwa ni bughudha.

 

Dalili Za Chunjua Za Filiform Warts

Kwa kawaida chujua za filiform hazina maumivu na hazina dalili zo zote. Chunjua hizi hutambulika kwa macho. Dalili zinaweza kuonekana kama chunjua zitaota sehemu za ngozi zenye mikunjo. Na dalili zaweza kuwa:

. Kuwasha
. Kutoka damu
. Maumivu

Chanzo Cha Chunjua Za Filiform

Filiform warts husababishwa na HPV. Kuna aina tofauti zaidi ya 100 za HPV. HPV wa ukoo 1,2,4,27 na 27 ndiyo wanaojulikana kusababisha chunjua za filiform.

 

Tiba Ya Filiform Warts

warts filiform chunjuaTiba nyingi zinalenga kuondoa chunjua, lakini hazimwondoi kirusi. Hakuna dawa ya HPV kwa sasa hivi, isipokuwa sindano ambazo zinalenga baadhi ya koo za HPV. Hadi sasa hakuna sindano kwa ajili ya filiform warts.

Kwa walio wengi, filiform warts huondoka zenyewe baada ya muda kwa msaada wa kinga zao za mwili.

 

 

Genital Warts – Chunjua Za Sehemu Za siri

 

Genital warts ni moja ya magonjwa yanayoenezwa sana kwa ngono. Karibu watu wote wanaofanya mapenzi wamepata kuambukizwa na angalau aina moja ya human papillomavirus (HPV), kirusi anayeeneza genital warts, katika maisha yao. Wanawake kwa namna fulani wanakuwa kweye hatari kubwa zaidi ya kupata chunjua za sehemu za siri.

chunjua ukeni

Genital warts hushambulia maeneo yenye unyevu ya sehemu za siri. Chunjua hizi huweza kuonekana kama vijiumbile vidogo vya nyama au vikawa na umbo kama la koliflawa. Mara nyingi genital warts ni ndogo mno kuonekanan kwa macho.

Kama ilivyo kwa chunjua za aina nyingine, genital warts husababishwa na human papillomavirus (HPV). Koo nyingine za HPV husababisha genital warts, wakati nyingine huleta saratani. Sindano zinaweza kusaidia kujikinga na baadhi ya koo za genital HPV.

Chanzo Cha Genital Warts

Genital warts au chunjua za sehemu za siri husababishwa na human papillomavirus. Kuna koo tofauti zaidi ya 40 zinazoshambulia sehemu za siri. Genital warts huenezwa kwa kufanya tendo la ndoa. Mara nyingi kinga zako za mwili huua virusi hawa na hupati athari zo zote.

 

Madhara Yatokanayo Na Genital Warts

. Saratani.  Kansa ya shingo ya kizazi imehusishwa sana na genital HPV. Kuna baadhi ya koo za HPV ambazo zinahusishwa na kansa za vulva, mkundu, mboo, na midomo na koo.

Maambikizi ya HPV hayaleti kansa wakati wote, lakini wanawake wanashauriwa kila wakati kuchukua kipimo cha pap, na hasa wale ambao wameshambuliwa na HPV wawezao kuleta kansa.

. Matatizo wakati wa ujauzito

Genital warts huweza kuleta matatizo wakati wa ujauzito. Chunjua hizi huweza kukua na kuwa kubwa kiasi cha kuziba mkojo usitoke vizuri. Chunjua hizi za kwenye kuta za uke huweza kupunguza mnyumbuko wa tishu za uke wakati wa kuzaa. Chunjua kubwa za nje ya uke au ndani ya uke zinaweza kutoa damu zikipanuliwa wakati wa kuzaa.

Yaweza tokea mara chache sana kwamba kichanga cha mama mwenye chunjua za ukeni kikawa na chunjua kwenye koo lake ambapo upasuaji utahitajika kuhakikisha njia zake za hewa hazijazibwa.

Katika mada yetu nyingine, tutajadili tatizo la chunjua za sehemu za siri (genital warts) ambapo tutaona chanjo chake na jinsi ya kuzitibu.

Usisite kuuliza swali ulilonalo au kutoa maoni yako kuhusu mada yetu hii ya leo. Kwa mawasiliano, tumia namba 0655 858027 au 0756 181651.

 

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.