Ugumba Wa Mwanamme Kutokana Na Kuwa Na Upungufu Wa Mbegu Za Kiume (Low sperm count)

 

upungufu wa mbegu za kiume uchunguzi na tiba

 

Iweje mwanamme wa umri wa kuzaa ashindwe kumpa mimba mkewe?

Inapotokea kuwa mme na mke wanahangaika kupata mtoto, wote wawili wanaweza kuwa ndiyo sababu ya tatizo. Wanaume wanachangia kwa kiwango cha theluthi moja na wanawake pia wanachangia kwa theluthi nyingine moja. Theluthi inayobakia ni matatizo yanayowahusu wote wawili. Kuna mambo mengi ya kuyachunguza, lakini tatizo kuu huwa ni katika mbegu zake mwanamme. Katika somo letu la leo tutajadili kwa kina mambo ambayo yanaweza kusababisha mbegu za mwanamme zisiwe na uwezo wa kumpa mimba mwanamke.

 

Upungufu wa Mbegu Za Kiume

 

Upungufu wa mbegu za kiume kitaalamu huitwa oligospermia. Hili ni neno linalotumika kuelezea hali ambapo idadi ya mbegu za mwanamme ni ndogo, pungufu ya mbegu milioni 15 katika mililita moja. Kama hakuna mbegu kabisa, hali hiyo huitwa azoospermia. Unapohitaji kupata mtoto, idadi ya mbegu unayotoa wakati wa tendo la ndoa ni muhimu. Idadi ya kawaida ya mbegu ni kati ya milioni 15 hadi milioni 200 kwa mililita moja.

 

mbegu za kiume

 

Ni vigumu kidogo kulielezea tatizo la upungufu wa mbegu za kiume. Kuna vipimo vingi vya kuvichukua wakati wa kufanya semen analysis. Kwanza, kama tulivyosema hapo awali, utachunguzwa uwingi wa mbegu katika ujazo wa mililita moja. Kisha daktari atataka kujua ni mililita ngapi zinatolewa. Kwa mfano, mtu mwenye mbegu milioni 40 katika mililita na anakojoa mililita moja hawezi kuwa mzuri zaidi ya yule mwenye mbegu milioni 18 kwa mililita na kutoa mililita 4 za ujazo anapokojoa. Tunapenda kuona mbegu angalau milioni 20 kwa mililita na kiasi cha mililita 2 hadi 5 za ujazo zikitolewa kwa mara moja. Ujazo wa kawaida ni mililita 2.5, ambao ni sawa na nusu kijiko cha chai.

Kipimo kingine ni kuchunguza ni asilimia ngapi ya mbegu ambazo zina uwezo wa kutembea, sperm motility, ambapo tunasema asilimia 50 ya mbegu kuwa na uwezo wa kutembea kuelekea kwenye nyumba ya uzazi ndicho kiwango cha chini kinachotakiwa.

Ukubwa na maumbo ya mbegu ni kigezo kingine kwa mbegu kuwa na uwezo wa kulirutubisha yai. Uchuguzi unafanyika kuona kuwa ni asilimia ngapi ya mbegu zenye ukubwa na maumbo yaliyokamilika – sperm morphology. Mbegu safi inatakiwa kuwa na asilimia angalau 30 ya mbegu zenye ukubwa na maumbo kamilifu.

Kiwango cha pH cha shahawa ni muhimu vile vile na kiwango kizuri ni cha kati ya pH 7.1 na 8.0. Kiwango kidogo cha pH kinamaanisha mbegu ni za utindikali zaidi na kiwango kikubwa maana yake mbegu ni alkaline. Kiwango cha pH kinaweza kuathiri afya ya mbegu zako na jinsi zitakavyosafiri.

 

upungufu wa mbegu za kiume uchunguzi

 

Mbegu zinapomwagwa huwa nzito. Mbegu hizi zinafaa kuchukua dakika kama 20 kabla ya kuwa nyepesi. Kama mbegu zako zinachukua muda mrefu zaidi au zinabaki nzito moja kwa moja, maana yake kuna tatizo.

Unapotazama uwezo wa mbegu kulirutubisha yai, lazima kuchunguza haya yote. Upungufu kidogo katika idadi ya mbegu, kwa mfano, unaweza kusaidiwa na mbegu kuwa na uwezo mkubwa sana wa kutembea au mbegu kuwa na ujazo mkubwa sana.

 

Dalili Za Upungufu Wa Mbegu Za Kiume

 

Dalili kubwa ya kuwa na upungufu wa mbegu za kiume ni kukosa uwezo wa kumpa mimba mke. Kunaweza kutokea dalili nyingine za wazi. Dalili nyingine zinaweza kuwa:

. Matatizo katika tendo la ndoa – kwa mfano, kukosa hamu ya tendo la ndoa au matatizo ya uume kusimama kwa muda mrefu ili kukamlisha tendo la ndoa.
. Maumivu, uvimbe kwenye maeneo ya korodani
. Kupungua kwa nywele za usoni au za mwilini au ishara nyingine za dosari za homoni.

Sababu Za Mwanamme Kuwa Na Upungufu Wa Mbegu

Tendo la kutengeneza mbegu za mwanamme lina vipengele vingi sana na linahitaji afya nzuri ya korodani na tezi za pituitary na hypothalamus – tezi katika ubongo zinazotengeneza homoni na zinazoruhusu utolewaji wa mbegu. Mbegu zilizotengenezwa ndani ya korodani husafirishwa kupitia mirija myororo hadi zitakapochanganywa na shahawa na kutolewa nje kupitia uume. Tatizo lo lote katika mlolongo huu linaweza kuathiri utolewaji wa mbegu bora.

Kunaweza kujitokeza matatizo katika maumbile ya mbegu au utembeaji wa mbegu. Kwa kawaida ni vigumu kulijua tatizo hili la kuwa na upungufu wa mbegu za kiume.

 

Sababu Za Kiafya

Kuwa na upungufu wa mbegu za kiume kunaweza kusababishwa na baadhi ya matatizo ya kiafya au tiba. Baadhi ni :

. Varicocele. Varicocele ni kuvimba kwa veni zilizomo ndani ya mfuko wa ngozi unaoshikilia korodani. Hii ni moja ya sababu kubwa ya ugumba kwa mwanamme.

 

upungufu wa mbegu za kiume varicocele

 

Varicoceles husababisha mapungufu katika ubora wa mbegu.

. Maambukizi. Baadhi ya maambukizi yanaweza kuathiri uzalishaji wa mbegu au afya ya mbegu au kusababisha makovu yatakayozuia mtiririko wa mbegu. Hii ni pamoja na maambukizi kwenye epididymis (epididymitis) au korodani (orchitis) na baadhi ya magonjwa ya kuambukiza kama gonorrhoea au UKIMWI.

. Matatizo Katika Umwagaji Mbegu. Mbegu zaweza kuingia kwenye kibofu cha mkojo (retrograde ejaculation) wakati mwanamme anapofika kileleni badala ya kutoka kupitia uume. Baadhi ya sababu zinaweza kulisababisha hili au kushindwa kutoa shahawa, zikiwa ni pamoja na kisukari, kuumia uti wa mgongo, upasuaji wa kibofu cha mkojo, tezi dume au urethra.

Kuna madawa mengine yanayoweza kuleta matatizo ya umwagaji mbegu, kama dawa za blood pressure zinazojulikana kama alpha blockers.

. Kingamwili (Antibodies) kushambulia mbegu. Kingamwili (anti-sperm antibodies) – seli za mfumo wa kinga za mwili ambazo kwa bahati mbaya hutambua mbegu kama vivamizi katika mwili na hujaribu kuziharibu.

. Uvimbe. Kansa na uvimbe wa aina nyingine usio na madhara vinaweza kuuathiri mfumo wa uzazi wa mwanamme moja kwa moja, kupitia tezi zinazotoa homoni zinazohusiana na uzazi, kama tezi ya pituitary. Upasuaji, mionzi au tiba ya chemotherapy zinazotolewa kutibu uvimbe vinaweza kuathiri uwezo wa mwanamme wa kuzalisha. 

. Korodani ambazo hazijashuka. Wakati kiumbe akiwa anakua tumboni korodani moja au zote zinaweza kushindwa kuteremka hadi kwenye mfuko wa pumbu kutoka tumboni. Watu wenye hali hii wanakuwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kuwa wagumba.

. Hormone imbalances. Tezi ya pituitary, hypothalamus na korodani huzalisha homoni muhimu katika utengenezaji wa mbegu mwilini. Mabadiliko katika homoni hizi, na mabadiliko katika mifumo ya tezi za thyroid na adrenal, huathiri uzalishaji wa mbegu.

. Matatizo katika mirija ya kusafirisha mbegu.  Mirija ya aina nyingi inahusika katika usafirishaji wa mbegu. Mirija hii inaweza kuziba kwa sababu nyingi, ikiwa ni pamoja na kuumia kwa bahati mbaya katika upasuaji, maambukizi au kuota kwa vitu kama cystic fibrosis.

Kuziba kunaweza kutokea kwenye hatua yo yote, ikiwa ni pamoja na ndani ya korodani,kwenye mirija inayotoka kwenye korodani, ndani ya epididymis, ndani ya vas diferens, au ndani ya urethra.

. Dosari za chromosome. Dosari za kiurithi kama Klinefelter’s syndrome – ambapo mwanamme anazaliwa akiwa na chromosomes mbili za X na moja ya Y badala ya moja ya X na moja ya Y – zinasababisha ukuaji wa viungo vya uzazi vya kiume usio wa kawaida. Matatizo mengine ya kiurithi yanayohusiana na ugumba ni cystic fibrosis, Kallmann’s syndrome na Kartagener’s syndrome.

. Celiac disease. Tatizo katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula linalosababishwa na usikivu wa mwili kwa gluten, ugonjwa uitwao celiac disease unaweza ukasababisha ugumba kwa mwanamme. Ugumba unaweza kuondoka baada ya kula chakula kisicho na gluten.

. Baadhi Ya Tiba. Tiba ya Testosterone replacement therapy, matumizi ya dawa za kansa (chemotherapy), baadhi ya dawa za fungus na antibiotics, baadhi ya tiba za vidonda vya tumbo, vinaweza kuathiri utengenezaji wa mbegu na kusababisha ugumba.

 

Sababu Za Kimazingira

Uzalishwaji wa mbegu na ubora wake unaweza kuathiriwa kwa kukaa muda mrefu kwenye mazingira fulani, yakiwa ni pamoja na:

. Kemikali za viwandani. Kuwa karibu kwa muda mrefu na benzene, toluene, xylene, herbicides, pesticides, organic solvents, rangi na madini ya lead kunaweza kuchangia matatizo ya kuwa mbegu chache.

. Metali nzito. Kuwa karibu na lead na madini mengine mazito kunaweza kusababisha ugumba.

. Mionzi au X-rays. Kuwa karibu na mionzi kunaweza kupunguza uzalishaji wa mbegu. Inaweza kuchukua muda mrefu kabla uzalishaji haujarudi na kuwa sawa. Mionzi mikali inaweza kusababisha upungufu wa mbegu wa milele

.Joto kali kwenye korodani. Joto kali linaharibu uzalishaji wa mbegu na ubora wake. Kuoga maji ya moto, mathalani, kunaweza kupunguza uzalishaji kwa muda fulani. Kukaa kitako kwa muda mrefu, kuvaa nguo za kubana, kufanya kazi kwenye laptop au kompyuta kwa muda mrefu vinaweza kuongeza joto kwenye korodani ma kupunguza uzalishaji wa mbegu.

 

Sababu Za Mtindo Wa Maisha

Sababu nyingine za upungufu wa mbegu ni:

. Matumizi ya dawa. Matumizi ya anabolic steroids kwa ajili ya kuipa nguvu misuli yanaweza kusababisha korodani kusinyaa, na kupunguza uzalishaji wa mbegu. Matumizi ya cocaine na marijuana yanaweza kupunguza idadi na ubora wa mbegu.

. Matumizi ya pombe.  Kunywa pombe knaweza kupunguza homoni ya testosterone na kupunguza uzalishaji wa mbegu.

. Kazi. Baadhi ya kazi zinahusishwa na ugumba, zikiwemo uchomeleaji wa vyuma (welding), au zinazomtaka mtu kukaa kwa muda mrefu, kama kuendesha magari makubwa.

 

kukaa kwa muda mrefu huharibu uzalishaji wa mbegu

 

. Uvutaji wa sigara. Watu wanaovuta sigara wanaweza kuwa na mbegu pungufu ukilinganisha na wale ambao hawavuti.

. Msongo wa mawazo. Msongo wa mawazo wa muda mrefu, na msongo kuhusu uwezo wa kuzalisha, unaaweza kuathiri uzalishwaji wa mbegu.

. Unene. Unene unaweza kuathiri uwezo wa kuzalisha mbegu kwa namna nyingi.

 

Tiba Ya Tatizo La Kuwa Na Mbegu Chache

 

Baadhi ya tiba zinazoweza kutolewa ni :

. Upasuaji. Kwa mfano, varicocele inaweaza kurekebishwa kupitia upasuaji au hata kuziba kwa vas deferens.

. Kuponya maambukizi. Matumizi ya antibiotics yanaweza kuangamiza wadudu kwenye njia ya uzazi.

. Kuondoa matatizo katika tendo la ndoa. Dawa au ushauri vinaweza kutumika kuondoa matatizo ya ugumba unaotokana na uume kushindwa kusimama au kuwahi kufika kileleni.

. Tiba ya homoni. Daktari anaweza kushauri tiba ya homoni akiona ugumba unasababishwa na viwango vya juu au chini vya baadhi ya homoni.

. Virutubishi. Hapa chini ni baadhi ya virutubishi ambavyo vimeonekana kusaidia kuondoa tatizo la upungufu wa mbegu kwa mwanamme kwa kiwango kikubwa sana.

vigpowe and zinc
                                                   Bei Kwa Dawa Zote Mbili  140,000.00

 

Katika mada nyingine zinazofanana na hii tutaona matatizo ya uume kushindwa kusimama imara kwa ajili ya tendo la ndoa, tutajadili vilevile tatizo la kuwahi kufika kileleni na sababu za mwanamme kushindwa kufanya tendo la ndoa kutokana na wasiwasi. Tunaomba mchango wako wa maoni  kuhusu mada yetu ya leo na itakuwa faraja kubwa kwetu kuweza kukujibu maswali utakayoyauliza.

 

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

 

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.