Kwa Nini Kipindi cha Luteal Phase Katika Mzunguko Wa Hedhi Ni Cha Muhimu Sana?

 

Kipindi cha Luteal (luteal phase) ni muda baada ya yai kuachiwa (au muda kati ya yai kuachiwa na ovari na kuanza hedhi) mpya. Jina luteal phase linatokana na corpus luteum, ambayo ni mabaki ya follicle (kifuko cha yai) ambayo ilikuwa inahifadhi yai lililoangushwa. Corpus luteum hutoa homoni ya progesterone, ambayo inahitajika na mwili ili kuandaa endometrium (ngozi laini iliyotanda juu na kuzunguka nyumba ya uzazi – uterus). Progesterone huigeuza endometrium kuwa ni kitanda kizuri laini ambacho juu yake yai lililopevushwa linaweza kunata na mtoto akakua. Progesterone huindaa endometrium kwenye kila mzunguko wa hedhi baada ya yai kuachiwa, yai liwe limerutubishwa au la. Kama yai halikurutubishwa, corpus luteum huacha kutoa progesterone baada ya siku 12 hadi 16.

Kipindi hiki kwa mwanamke mmoja kwa kawaida huwa hakibadiliki kwa zaidi ya siku moja au mbili. Kwa hiyo kama luteal phase yako huchukua kwa kawaida siku 12, mara chache inaweza kuchukua siku 11 au 13, lakini haiwezi ikafika siku 15 au 16. Rafiki yako anaweza kuwa na kawaida ya siku 15. Ambaye ataweza kuchukua siku 14 au 16, lakini si siku 12.

Hedhi huanza pale corpus luteum inapoacha kutoa progesterone. Unaweza kuilinganisha progesterone  na muziki kwenye sherehe. Muziki ukisimama, wageni waalikwa huanza kuondoka. Vivyo hivyo, corpus luteum ikaacha kutoa progesterone, utando wa endometrium hutoka nje kupitia uke, na unakuwa umeanza  hedhi.

Luteal Phase Na Kutunga Mimba

Urefu na ubora wa kipindi hiki unahusiana sana na uwezo wako wa kupata mtoto. Kama urefu wa luteal phase ni chini ya siku 10, unaweza kupata shida sana kuitunza mimba yako. Hii inatokana na kwamba kama corpus luteum inaacha kutoa progesterone kwenye siku ya 9, ule utando laini juu ya endometrium uliotengenezwa, utabanduka na hedhi kuanza kabla ya yai lililopevushwa kuwa limesafiri ndani ya mirija ya uzazi lilikorutubishwa na kufika kwenye nyumba ya uzazi, ambako ukuaji wa mtoto hufanyika. Yai lililopevushwa halisafiri ndani ya mirija ya uzazi kuelekea kwenye uterus kutafuta mbegu za kiume, bali yai hukaa ndani ya mirija ya uzazi baada ya upevushwaji. Kama yai litakutana na mbegu za kiume, yai lililopevushwa sasa litaanza safari kuelekea kwenye nyumba ya uzazi. Sasa kama hakuna sehemu ya yai hili kunata juu ya endometrium, hakuna mimba inayoweza kutokea.

Tofauti kati ya kupevushwa yai (fertilization) na kutunga mimba (implantation) ni kuwa: Upevushwaji ni pale yai linapokutana na mbegu na kuwa zygote. Yai hili haliwezi kuwa mtoto hadi linate juu ya endometrium na kukua pale. Ujauzito unaanzia na kutunga mimba, yaani zygote inapopata pahali pa kunata juu ya endometrium.

Vivyo hivyo, kama kuna kiwango kidogo cha progesterone kinachotolewa wakati wa kipindi chako cha luteal, unaweza kupata wakati mgumu kuitunza mimba. Pamoja na kuwa urefu wa kipindi chako ni wa kutosha, kama kiwango cha progesterone kinachotolewa ni kidogo, kitanda juu ya endometrium kinakuwa hakijafikia ukamilifu, na yai litakosa msingi mzuri unaohitajika ili kuanza ukuaji. Hii ni sababu moja ya mimba kutoka (miscarriage).

Si kila mwezi yai litakutana na mbegu za kiume na kuleta ujauzito. Hata kama yai halikutani na mbegu za kiume, litasafiri kuelekea kwenye uterus ambako baadaye litapasuka na viwango vya estrogen na progesterone vitashuka.

Kama una tatizo la premenstrual syndrome (PMS) au tatizo kubwa zaidi la premenstrual dysphoric disorder (PMDD), katika kipindi cha kama wiki moja kabla ya hedhi, utaanza kujisikia kuwa na wasiwasi, na mwenye sonona. Hii inasadikika kuwa inachangiwa na kushuka kwa viwango vya estrogen na progesterone.

Katika mada yetu nyingine tutauzungumzia mzunguko wa hedhi wa mwanamke. Usisite kutuuliza maswali uliyo nayo wala kutoa maoni yako kuhusu uandishi wa mada yetu hii ya leo.

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.