Mtoto Wa Jicho (Cataract) Ni Nini?

 

Kama una miaka zaidi ya 60 na unaona ukungu unapovitazama vitu mbele yako, unaweza kuwa na tatizo la mtoto wa jicho (cataract). Cataract ni kufunikwa kwa lensi ya jicho na tabaka la protini lililojijenga kuizunguka lensi. Mtu mwenye mtoto wa jicho huviona vitu mathali ya mtu anayetazama kupitia kioo chenye ukungu. Hali hii humfanya mtu kushindwa kusoma vizuri, kushindwa kuendesha gari (hasa usiku) au kutambua hisia kutoka sura ya rafiki yake. Cataract kwa kawaida hujijenga taratibu na haisumbui katika kuona kwenye hatua zake za mwanzo. Lakini, taratibu mtoto wa jicho ataanza kuvuruga uonaji wako. Ni tatizo linalowasumbua watu wengi wenye umri mkubwa.

Mwanzoni, mwanga mkali au kuvaa miwani ya jua kutaweza kukusaidia. Ikifika hatua ya kushindwa kufanya kazi zako vizuri, unaweza kuhitaji upasuaji. Kwa bahati nzuri, upasuaji wa mtoto wa jicho ni salama, na unamsaidia mgonjwa kurudia kwenye hali yake ya awali. Katika mada zetu zinazofuata tutajadili chanzo cha mtoto wa jicho, dalili zake, aina za mtoto wa jicho na tiba kwa ajili ya ugonjwa wa mtoto wa jicho.

Dalili Za Mtoto Wa Jicho

Dalili za mtoto wa jicho zaweza kuwa:

. Kuona ukungu au mwanga kupungua
. Kupata matatizo zaidi ya kuona usiku
. Kutopenda mwanga mkali
. Kuhitaji mwanga zaidi wakati wa kusoma na kufanya shughuli nyingine
. Kuona mwanga wa mviringo kuzunguka vyanzo vya mwanga (halos)
. Kuhitaji kubadili miwani mara kwa mara
. Kupungua kukolea kwa rangi
. Kuona vitu mara mbili kwenye jicho moja

Chanzo Cha Mtoto Wa Jicho

Cataracts nyingi hutokea kwenye umri mkubwa au kutokana na kuumia kunakobadili tishu zinazojenga lensi ya jicho lako. Cataracts zinaweza pia kutokea kwa sababu ya  upasuaji wa jicho au matatizo ya kiafya kama kisukari. Matumizi ya muda mrefu ya homoni za kutengenezwa (steroids), pia, huweza kuleta cataracts.

Jinsi Mtoto Wa Jicho Anavyotokea

Lensi, eneo ambapo cataract hujenga, ipo nyuma ya sehemu ya jicho yenye rangi (iris). Lensi hukusanya mwanga unaoingia jichoni na kutengeneza picha angavu juu ya sehemu moja iitwayo retina – ngozi nyembamba yenye usikivu wa mwanga inayofanya kazi kama filamu kwenye kamera.

jicho

Umri unapokuwa mkubwa, mnyumbuliko wa lensi hupungua, uangavu wake hupungua na lensi huwa nene. Mabadiliko yanayotokana na umri na madhara mengine ya kiafya husababisha tishu ndani ya lensi kuvunjika na kunatana, na kufunika maeneo machache ya lensi.

Cataract inavyozidi kukua, kufunikwa kwa lensi kunaongezeka na kuathiri maeneo mengine ya lensi. Cataract huutawanya na kuuzuia mwanga unaopita kwenye lensi, na kuzuia retina isipate picha bora yenye ncha kali. Kwa hiyo, utaona ukungu unapotazama.

Cataracts hutokea kwenye macho yote mawili, lakini yakiwa na tofauti. Cataract katika jicho moja huweza kuwa mbaya zaidi ya jicho jingine, na kuleta utofauti katika kuona.

Aina Za Cataract

Aina za cataracts ni pamoja na:

. Cataract za sehemu ya kati ya lensi (nuclear cataract).
. Cataract za pembezoni mwa lensi (cortical cataracts).
. Cataract za sehemu ya nyuma ya lensi (posterior subcapsular cataract).
. Cataract za kuzaliwa nazo(congenital cataracts).

Katika mada nyingine ya kipekee tutazichambua aina za cataracts.

Mambo Yanayochangia Kutokea Kwa Mtoto Wa Jicho

. Umri mkubwa
. Kisukari
. Kukaa kwenye mwanga mkali kwa muda mrefu
. Kuvuta sigara
. Unene
. High blood pressure
. Kuumia jicho
. Upasuaji wa jicho
. Matumizi ya madawa
. Unywaji wa pombe wa kupindukia.

Namna Ya Kutibu Cataracts

Njia pekee ya kutibu cataracts ni upasuaji, lakini si lazima ufanyiwe upasuaji mara baada ya tatizo kuanza. Endapo utagundua tatizo katika hatua zake za mwanzo, unaweza kupata msaada kwa kubadilishiwa miwani yako na ukaona vizuri zaidi kwa muda.

Kama utapata shida kusoma, unaweza kujaribu kutumia mwanga mkali zaidi au ukatumia magnifying glasses.

Hali ikiwa mbaya hadi kushindwa kuendesha gari vizuri, unaweza sasa kumwona daktari ukafanya utaratibu wa kufanyiwa upasuaji.

Upasuaji wa jicho ni ni wa kawaida na hauumizi. Daktari anaweka ganzi kwenye eneo la jicho na upasuaji utaendelea ukiwa na fahamu zako. Upasuaji huu huchukua kama dakika 15 hadi 20 na si lazima ulazwe baada ya upasuaji. Kama una mtoto wa jicho kwenye macho yote mawili, daktari atasubiri upone jicho la kwanza kabla ya kufanya upasuaji wa jicho la pili.

Small-incision surgery. Mara nyingine madaktari huuita upasuaji huu phacoemulsification. Daktari hukata sehemu ndogo kwenye cornea ya jicho lako na kuweka kifaa kidogo kinachotoa mionzi ya ultrasound ambayo itaivunjavunja lensi yako iliyozibwa. Kisha, atatoa vipande nje ya jicho na kuweka lensi yako bandia.

mtoto wa jicho upasuaji

Large-incision surgery. Upasuaji huu hufanywa mara chache, hasa pale daktari atakapoona kuwa cataract ni kubwa sana na inaleta usumbufu mkubwa katika kuona. Upasuaji huu huitwa pia extracapsular cataract extraction. Daktari huitoa lensi iliyozibwa, na kukuwekea lensi bandia. Lensi hii bandia iitwayo intraocular lens, huwekwa sehemu ile ile ya lensi yako ya zamani. Unaweza kuhitaji muda mrefu zaidi kupona baada ya upasuaji huu ukilinganisha na upasuaji wa small-incision.

Katika mada yetu nyingine ya kipekee, tutachambua aina mbalimbali za upasuaji wa mtoto wa jicho tukielezea faida na mapungufu ya kila aina ya upasuaji.

Nina Mtoto Wa Jicho. Hospitali Gani Ni Bora?

Naitwa Laurian, ni mkazi wa Dar Es Salaam, Tanzania.

Mimi nilikuwa mhanga wa tatizo la mtoto wa jicho. Hadi kufikia Mei 2024, nilikuwa nimefikia hatua ya kutoona kabisa. Niliongozwa kwa kushikwa mkono ili kufanya lo lote nililokuwa nimetarajia. Nilianza kufanya utafiti ili kujua ni sehemu gani ilikuwa bora ili niweze kupata tiba. Niliambiwa sehemu nyingi.

Kuna hospitali za wamisionari nyingi zinazofanya upasuaji wa mtoto wa jicho -kusini , mikoa ya kati na ya kaskazini, kote kuna hospitali za wamisionari zinazofanya upasuaji huo.

Kuna hospitali za serikali nyingi zinazofanya upasuaji wa mtoto wa jicho.

Nchini Kenya, kuna hospitali kubwa na mahsusi  kwa magonjwa ya macho mjini Nairobi.

Baada ya kukusanya taarifa nyingi,niliamua kwenda International Eye Hospital iliyopo mjini  Dar Es Salaam. Nilipangiwa tarehe 22 Agosti 2024 kufanyiwa upasuaji wa jicho moja la kulia. Maandalizi yalianza saa 7.00 mchana na nikaingia chumba cha upasuaji baada ya maandalizi kukamilika. Upasuaji halisi ulichukua dakika kama ishirini tu. Saa 8.00 nilitoka ndani ya chumba cha upasuaji nikiwa naona vizuri nikiwa nyuma ya nesi aliyeniambia nimfuate. Kuanzia mwanzo hadi mwisho wa upasuaji sikusikia maumivu ya namna yo yote. Nilipumzishwa kwa dakika kadhaa na kuruhusiwa kurudi nyumbani siku hiyo hiyo.

Nilipewa dawa za matone za kutumia kwa mwezi mmoja na baada ya kuzimaliza nilikwenda kwa vipimo na kuambiwa kuwa jicho langu lilikuwa limepona kikamilifu na linaona kwa asilimia 70. Nina umri wa miaka 68, hivyo uonaji huo kwangu ni mkubwa sana.

Hizi ni baadhi ya sifa ninazoweza kuzielezea kuhusu International Eye Hospital.

  1.  Hospitali ina vipimo vingi, kipimo kwa kila tatizo la macho, na vyote ni vya kisasa kabisa
  2.  Upasuaji unaotumika ni wa kisasa sana. Teknolojia ya Phaco ndiyo inayotumika. Dawa za matone hutumika kuweka ganzi na si sindano. Phacoemulsification ni utoaji wa mtoto wa jicho bila kulichana jicho na kisha kulishona nyuzi kama inavyofanywa kwenye hospitali nyingine. Ni tundu dogo sana linalotobolewa kwa mashine za mionzi (laser) hivyo uponaji ni wa siku chache sana.Teknolojia hii inakuwezesha kuanza kuona dakika hiyo hiyo unapowekewa lensi bandia (IOL).
  3. Hospitali ina timu ya madaktari wenye uzoefu mkubwa ikiongozwa na madaktari bingwa kutoka Uturuki. Madaktari hawa wa kutoka Uturuki wana sifa za juu za kitaaluma. Wote wana viwango vya juu kitaaluma (PhD) na ni washiriki wa taasisi kubwa za tiba za macho za kimataifa.
  4. Hospitali ina manesi wa kutosha wenye viwango vya juu kitaaluma.
  5. Hospitali inapokea malipo ya fedha taslimu na bima.

Jee, Cataracts Huweza Kurudi Tena Baada Ya Upasuaji?

Asilimia 20 hadi 40 ya watu waliofanyiwa upasuaji wa mtoto wa jicho wanaweza kupata tatizo la posterior capsular opacification au wengine huita secondary cataract. Mtu mwenye tatizo hili huona dalili zile zile za mtoto wa jicho. Bahati nzuri, tatizo hili huondolewa kirahisi sana. Katika ukurasa mwingine tutalijadili tatizo hili kwa kina. Tembelea ukurasa wetu wa posterior capsular opacification kujisomea kuhusu tatizo hili.

Namna Ya Kuondoa Mtoto wa Jicho Bila Upasuaji

Unataka kuondoa mtoto wa jicho bila upasuaji? Inaonekana kama ni kitu kisichowezekana, lakini waweza kuondoa mtoto wa jicho bila kisu.

Kuna tovuti moja – healing the eye and Wellness Center – iliyoandika kuhusu namna unavyoweza kuondoa mtoto wa jicho bila upasuaji. Hapa chini, ndivyo walivyoshauri:

1. Tumia Zaidi Virutubishi

Kuitunza afya ya jicho lako, tumia zaidi glutathione na antioxidants kwenye chakula chako cha kila siku. Tumia mboga za majani kwa wingi kama spinach, broccoli, Brussels sprouts, na asparagus. Unaweza pia kula matunda yenye uwingi wa glutathione kama mabalungi (grapefruit), strawberries, na avocado. Kama hupendi kuyala yakiwa mazima, unaweza kuyachanganya na kuyanywa kama juice.

 

Vile vile kula chakula chenye uwingi wa lutein na zeaxanthin kuboresha uonaji wako na afya ya jicho kwa ujumla. Chakula chenye uwingi wa lutein na zeaxanthin ni pamoja na mahindi, collard greens, mayai na turnip greens. Chakula hiki kina carotenoids, ambayo pia hupatikana ndani ya lensi ya jicho, na kinaweza pia kuzuia matatizo ya macular degeneration na kujijenga kwa cataract.

Madaktari wanashauri kuacha sukari (white sugar) high-fructose corn syrup ambayo husaidia kukua kwa mtoto wa jicho. Yafaa pia kuacha juice za matunda (fruit juice concentrates).

2. Kunywa Maji Mengi

Unywaji wa maji mengi ni muhimu ili kuweka sawa afya ya jicho na katika kuondoa dalili za magonjwa ya macho, pamoja na mtoto wa jicho. Mwili huhitaji maji kwa wingi ili kutoa sumu (detoxification) nje ya mwili.

Madaktari hushauri kunywa angalau lita mbili za maji kwa siku. Inashauriwa kuacha kutumia maji ya bomba au maji yanayouzwa ndani ya chupa za plastiki kwani yaweza kuwa na phthalates au benzene, ambazo ni sumu kali sana kwa mwili. Yafaa kutumia kifaa cha reverse osmosis kilichofungwa nyumbani kwako.

3. Punguza Msongo Wa Mawazo

Utafiti bado unaendelea kuhusu uhusiano wa msongo wa mawazo na matatizo mbalimbali ya macho kama macular degeneration, glaucoma, na cataracts. Hadi sasa imebainika kuwa msongo wa mawazo huathiri afya macho kama unavyoathiri afya yako kwa jumla.

Mazoezi ya mwili, meditation na sala ni baadhi ya vitu unavyoweza kuvifanya kupunguza msongo wa mawazo.

DAWA ZA MTOTO WA JICHO

Katika mada nyingine, tutauzungumzia ugonjwa  wa glaucoma. Usisite kuuliza maswali uliyo nayo kuhusu mada yetu ya leo. Tutafurahi sana kukujibu.

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu NDANI YA MUDA WA KAZI kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.