Lupus ni ugonjwa wa muda mrefu unaotokana na kinga za mwili kufanya kazi kupita kiasi na kushambumbilia tishu za mwili zisizo na dosari. Ugonjwa wa lupus hushambulia zaidi wanawake, na huonekana zaidi kwenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 44. Lupus ilianza kujulikana zaidi mwaka 2015 baada ya mwimbaji Selena Gomez kueleza kuwa aligundilika na ugojwa huu alipokuwa msichana na kupata tiba. Lupus ni ugojwa usioambukiza. Ugonjwa huu hauenezwi kwa ngono au kwa njia nyingine yo yoye ile. Mara chache, mama anaweza kuzaa mtoto mwenye dalili za lupus. Hii huitwa neonatal lupus.
Aina Za Lupus
Kuna aina nyingi za lupus. Katika mada yetu ya leo, tutazungumzia zaidi systemic lupus erythematosus (SLE), lakini aina nyingine ni pamoja na discoid, drug-induced, na neonatal lupus.
Systemic lupus erythematosus
SLE ndiyo aina ya lupus inayoonekana mara nyingi zaidi. Huu ni ugonjwa unaoathiri mwili mzima. Dalili zake zaweza kuwa ndogo hadi zile kali kabisa.
SLE ni ugonjwa wenye madhara zaidi kuliko aina nyingine, kama discoid lupus, kwa sababu huweza kuathiri kiungo cho chote cha mwili au mfumo wa viungo vya mwili. Unaweza kufanya shambulizi kwenye ngozi, maungio ya mifupa, mapafu, figo, damu, moyo, au vitu zaidi ya kimoja ya hivi.
SLE hufanya mashambulizi kwa vipindi. Wakati ukiachia, mtu hataona dalili. Ukiamka, mtu ataumwa na dalili zitaonekana.
Discoid lupus erythematosus
Ugonjwa wa discoid lupus erythematosus (DLE) au cutaneous lupus hutoa dalili zinazoathiri ngozi tu. Vipele vidogo (ukurutu) hutokea usoni, shingoni, na ngozi ya kichwani.
Maeneo yaliyoathirika yanaweza kuwa na ngozi ngumu yenye magamba, na makovu huweza kutokea. Ukurutu huu unaweza kudumu kwa siku kadhaa au kwa miaka kadhaa, mara nyingine unaweza kumrudia mgonjwa.
DLE haiathiri viungo vya ndani, lakini asilimia 10 ya waathirika baadaye hupata SLE.
Subacute cutaneous lupus erythematosus
Subacute cutaneous lupus erythematosus inamaanisha madonda yanayotokea juu ya ngozi ya viungo vinavyopigwa na jua. Madonda haya hayasababishi magamba.
Drug-induced lupus
Kiasi cha asilimia kama 10 ya watu wenye SLE, dalili hutokea kwa sababu ya athari ya baadhi ya dawa.
Dawa hizi ni pamoja na dawa ambazo watu wanazitumia kwa ajili ya kifafa na high blood pressure. Dawa nyingine ni pamoja na zile za thyroid, antibiotics, antifungal, na dawa za kunywa za kuzuia mimba. Dawa zilizothibika kuleta aina hii ya lupus ni Hydralazine (BP), Procainamide (moyo) na Isoniazid (TB).
Drug-induced lupus kwa kawaida huondoka yenyewe mtu akiacha kuzitumia dawa hizi.
Neonatal lupus
Watoto wengi wanaozaliwa kwa akina mama wenye lupus huwa na afya njema. Lakini, yapata asilimia moja ya akina mama wenye matatizo ya kingamwili yanayoendana na lupus huzaa mtoto mwenye neonatal lupus.
Mama huyu anaweza kuwa na SLE, Sjogren’s syndrome, au asiwe na dalili kabisa.
Sjogren’s syndrome ni hali nyingine inayotokana na matatizo ya kinga za mwili ambayo huendana na lupus. Dalilil zake kuu ni ukavu machoni na midomo kukauka.
Wanapozaliwa, watoto wenye neonatal lupus wanaweza kuwa na ukurutu kwenye ngozi, matatizo ya ini, na damu kuwa chini. Asilimia 10 kati yao huwa na upungufu wa damu.
Madonda hupona baada ya wiki chache. Lakini, watoto wengine huwa na congenital heart block, ambapo moyo hushindwa kusukuma damu kwa misukumo inayolingana. Mtoto huyu anaweza kuhitaji pacemaker, hali ambayo ni hatari kwa maisha yake.
Chanzo Cha Lupus
Lupus ni tatizo la kinga za mwili (autoimmune condition), lakini chanzo chake hakijawa bayana.
Mfumo wa kinga za mwili huulinda mwili kwa kupambana na vivamizi (antigens), kama bakteria, virusi, na germs. Unafanya kazi hiyo kwa kutengeneza protini ziitwazo kingamwili (antibodies). Seli za chembechembe nyeupe za damu, B lymphocytes, hutengeneza kingamwili hizo.
Mtu anapokuwa na kinga za mwili zilizo kama zile za mtu mwenye lupus, mfumo wake hauwezi kutofautisha kati ya vitu visivyotakiwa na mwili (antigens), na tishu zenye afya. Mapato yake, kinga za mwili hutuma kingamwili kushambulia tishu zanye afya na vivamizi vyote kwa pamoja. Hii husababisha uvimbe, maumivu, na uharibifu wa tishu.
Aina ya kingamwili inayotengenezwa mara nyingi zaidi na miili ya watu wenye lupus ni ya aina ya antinuclear antibody (ANA). ANA hudhuriana na baadhi ya sehemu za kiini cha seli (cell’s nucleus), ambacho ni kitovu cha seli. Kingamwili hizi huzunguka pamoja na damu, lakini baadhi ya seli za mwili huwa na kuta zinazopenyeka na huziruhusu kingamwili kupenya. Kingamwili hizi sasa huweza kuharibu DNA ndani ya kiini cha seli hizi. Hii ndiyo sababu lupus hushambulia baadhi ya viungo na si vyote.
Kwa Nini Mfumo Wa Kinga Za Mwili Hufanya Makosa?
Sababu kadhaa za kijenetiki pengine ndizo zinazosababisha kutokea kwa SLE. Kuna jeni (genes) ndani ya mwili zinazosaidia utendaji wa mfumo wa kinga za mwili. Kwa watu wenye SLE, mabadiliko katika jeni hizi husababisha mfumo wa kinga za mwili kushindwa kufanya kazi ipaswavyo. Nadharia moja inahusu kufa kwa seli, nayo inasema kuwa kwa sababu ya sababu za kujenetiki, mwili unashindwa kutoa nje seli ambazo zimekufa. Seli hizi zilizokufa zinaweza kutoa vitu ambavyo vitasababisha mfumo wa kinga za mwili kutofanya kazi vizuri.
Dalili Za Lupus
Dalili za lupus huonekana wakati ugonjwa ukifumuka. Kuna vipindi vya kati ambapo mtu huona kama ugonjwa umetulia na dalili hupotea au kuonekana kidogo sana.
Lupus ina dalili nyingi sana, zikiwemo:
. uchovu
. kukosa hamu ya kula na kukonda
. maumivu na uvimbe miguuni au kuzunguka macho
. kuvimba tezi
. ukurutu kwenye ngozi, kwa sababu ya damu kuvuja chini ya ngozi
. madonda mdomoni
. kutopenda jua
. homa
. kichwa kuuma
. maumivu kifuani ukivuta hewa kwa nguvu
. kupunyuka nywele
. maumivu kwenye maungio ya mifupa.
Tiba Ya Lupus.
Kwa sasa hivi hakuna dawa ya lupus, lakini mtu unaweza kubadili staili ya maisha na kupata matibabu ya kuondoa dalili zilizokwishajitokeza.
Katika mada yetu nyingine tutalizungumzia tatizo la mzio (allergy). Usisite kuuliza swali ulilo nalo au kutoa maoni yako kuhusu uandishi wa mada hii.
Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu ndani ya saa za kazi kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.
Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.