Posterior Capsular Opacification au secondary cataract ni kuota ukungu kwenye kapsuli ya lensi yako
kunakoweza kutokea kukiwa ni matokeo ambayo hayakutarajiwa ya upasuaji wa mtoto wa jicho. Kwa lugha nyepesi tunaweza kusema kuwa secondary cataract ni mtoto wa jicho wa pili anayetokea muda fulani baada ya operesheni ya kutoa cataract. Mtoto wa jicho wa pili ni tatizo ambalo linawakuta baadhi na si wote waliofanyiwa upasuaji. Kwa bahati nzuri tatizo hili linaeleweka na tiba ya uhakika inapatikana. Mada hii ya leo ni kujadili matatizo baada ya upasuaji wa mtoto wa jicho na namna ya kuyakabili.
Wakati wa upasuaji wa mtoto wa jicho, daktari wa macho (ophthalmologist) huiondoa lensi yako ya asili na kukuwekea lensi ya kutengenezwa -intraocular lens (IOL). Lensi hii mpya ni angavu na hurudishia uonaji wako.
Watu wengu hufurahia matokeo ya upasuaji wa mtoto wa jicho. Lakini, kitu kimoja ambacho hakikutarajiwa ambacho hutokea mara nyingi ni kujijenga kwa secondary cataract, hali ambayo kwa lugha nyepesi unaweza kuita mtoto wa jicho wa pili.
Unaweza kuwaza kuwa hii maana yake mtoto wa jicho aliyetolewa karudi. Hilo haliwezeikani. Ukungu ambao wataalamu huuita cataract hujenga kwenye lensi ya kristali uliyozaliwa nayo tu. Cataracts haziweza kujenga juu ya lensi za kutengenezwa (IOLs). Badala yake, posterior cataract opacification maana yake tabaka za ukungu juu ya kapsuli ya lensi yako.
Kapsuli ya lensi yako ni utando laini mwembamba unaoizunguka lensi na kutoa umbo la lensi. Upasuaji wa mtoto wa jicho huondoa lensi na si kapsuli. Unaweza kuifikiria kapsuli kama chumba fulani kinachopata mpangaji mpya. Lensi yako asili ikiondolewa, IOL inaingia. Kapsuli hubakia pale pale ndani ya jicho. Kapsuli huundwa kwa seli na vitu vingine vya asili, na ni angavu. Kama ilivyo kwa lensi ya asili, kapsuli huweza kujenga mabaka ya ukungu baada ya muda.
Mabaka haya ya ukungu, au secondary cataracts, yanaweza kutokea kama sehemu ya uponaji baada ya upasuaji. Hii ikitokea, tabibu wako anaweza kuondoa mtoto huyu wa jicho wa pili kwa kutumia mionzi ya laser, kazi isiyochukua muda mrefu.
Secondary cataract huweza kutokea miezi au miaka kadhaa baada ya upasuaji wa mtoto wa jicho. Tatizo hili huweza kuathiri kati ya asilimia 20 hadi 50 ya watu waliofanyiwa upasuaji wa mtoto wa jicho katika kipindi cha miaka miwili hadi mitano.
Dalili Za Posterior Capsular Opacification
Dalili za tatizo ni pamoja na:
. Ukungu wakati wa kuona. Utaona kama vile kupitia kioo kilichofunikwa na theluji
. Ming’ao au miduara ya mwanga kuzunguka vyanzo vya mwanga
. Macho kuogopa mwanga
. Shida wakati wa kusoma
Dalili hizi zinafanana na zile za mtoto wa jicho kabla ya upasuaji.
Nini Husababisha Mtoto Wa Jicho wa Pili?
Wakati wa upasuaji wa kuondoa lensi yako ya asili, kunaweza kukabakia seli za epithelial za lensi yako ya
asili. Seli hizi zinaweza kusafiri na kujikusanya juu ya kapsuli ya lensi yako. Kusafiri huku kwa seli hizi
ni sehemu ya mtiririko wa kawaida wa mwili wa uponaji. Kadiri seli hizi zinavyojikusanya, zinaweza
kusababisha kapsuli yako ambayo kwa kawaida huwa angavu, kugeuka na kuwa na ukungu. Kama utafikiria kuwa kapsuli ni chumba kinachotunza lensi, basi secondary cataract ni kujijenga kwa uchafu juu ya dirisha la chumba chako. Uchafu huu utakufanya ushindwe kuona nje kupitia dirisha lako kama ilivyokuwa kawaida. Kwa hiyo utaanza kuona dalili zile zile ulizoziona kabla ya upasuaji.
Nini Kinachangia Kutokea kwa Secondary Cataract?
Mtu ye yote ambaye amefanyiwa upasuaji wa mtoto wa jicho anaweza kupata secondary cataract. Hata hivyo, uwezekano huo utakuwa mkubwa zaidi endapo utakuwa na yafuatayo:
. Matatizo ya macho yatokanayo na kisukari
. Glaucoma
. Retinitis pigmentosa
. Tatizo la kuona karibu la kiwango kikubwa
. Uveitis- tatizo ambapo kinga za mwili zainashambulia tishu zenye afya za macho
Unakuwa kwenye hatari kubwa ikiwa ulipata matokeo yasiyotarajiwa baada ya upasuaji kama kuvimba kwa macho.
Tiba ya Secondary Cataracts
Madaktari wa macho huondoa tatizo la secondary cataract kwa kutumia YAG laser capsulotomy (posterior
capsulotomy). Upasuaji huu huchukua yapata dakika tano tu. YAG ni jina la aina ya laser anayoitumia na ni
kifupi cha “yttrium aluminum garnet,” mali ghafi iliyotumika kuitengeneza laser hiyo.)
Wakati wa upasuaji, daktari hutia ganzi jicho lako kwa matone. Kisha anatumia laser kutoboa tundu dogo kwenye kapsuli ya lensi yenye ukungu. Tundu hilo huruhusu mwanga upite kwenye lensi uliyowekewa, na kukurudishia uonaji wako.
Inachukua kama siku moja uonaji wako kurudia kwenye hali yake baada ya tiba ya YAG. Unaweza kuona floaters kwa wiki kadhaa kabla hazijapotea. Floaters ni mabaki yatokanayo na tiba ya laser (debris removed during laser treatment).
YAG laser capsulotomy ni tiba ambayo inauwezo mdogo sana wa kuleta madhara. Endapo kutatokea matokeo yasiyotarajiwa, yanaweza kuwa ni:
Retinal detachment. Hii ni hali ambapo retina inaondoka sehemu ya nyuma ya jicho. Kwa hiyo, retina
haifanyi kazi yake tena na uonaji wako ni wa ukungu. Katika hali hiyo, upasuaji utahitajika ili kuirudisha retina kwenye eneo lake. Dalili za retina iliyoondoka eneo lake ni:
. Kuona nyota au miale ya mwanga
. Kuongezeka kwa floaters katika jicho. Ni jambo la kawaida kuona floaters baada ya posterior capsulotomy, lakini hazitakiwi kuongezeka baada ya siku ya kwanza.
. Vivuli unapotazama pembeni (peripheral vision)
. Pazia la kijivu linaloziba eneo fulani unalolitazama
Watu wenye tatizo la kuona karibu wanakuwa kwenye hatari zaidi.
Kuongezeka kwa pressure ndani ya jicho. Macho yamejaa majimaji ya aina mbalimbali, kukiwa na vitreous humor na aqueous humor. Jicho lemnye afya, hutunza uwiano mzuri wa majimaji haya. Kuongezeka kidogo kwa pressure ndani ya jicho ni kitu cha kawaida. Pressure ya juu, kitaalamu ocular hypertension, inaweza kusababisha glaucoma. Glaucoma ni ugonjwa ambapo ocular hypertension imeharibu optic nerve. Optic nerve hupaleka taarifa kwenye ubongo, na ikiharibiwa, unaweza kupoteza uwezo wa kuona. Watu wenye glaucoma wanakuwa kwenye hatari zaidi.
IOL dislocation. Maana yake lensi bandia uliyowekewa inaweza kuhama.
Katika mada yetu nyingine, tutauzungumzia ugonjwa wa pressure ndani ya macho au kitaalamu glaucoma. Usisite kutoa maoni yako kuhusu mada yetu hii ya leo au kuuliza maswali uliyo nayo.
Pata ushauri zaidi kwa kututumia ujumbe kupitia ukurasa huu hapa chini kwa kujaza fomu, au kututumia barua pepe kupitia promota927@gmail.com au tupigie simu ndani ya saa za kazi kwa namba zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.
Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.