Fat (Mafuta)

Fats ni aina ya lipid iitwayo triglycerides. Mwili wako unahitaji lipids, ikiwa ni pamoja na fats, ili uweze kufanya kazi vizuri. Kuta nyingi za seli zako zimeundwa kwa lipids. Na lipids husaidia kutunza au kusambaza vitu vingi ndani ya mwili. Moja ya mifano mizuri ni vitamini zinazoyeyuka katika mafuta, A, D, E na K. Mwili wako unahiji fats ili kuzitumia vitamini hizi vizuri.

Fats katika mwili wako zinaamsha hisia ya kushiba. Yaani hisia kuwa huna njaa tena na kwamba usiendelee kula.

Mwili hutunza fats ikiwa umeingiza kalori nyingi kutokana na protini, wanga au fats kuliko mahitaji ya mwili ya kuviunguza ili kupata nishati.

Kuna Aina Ngapi Za Fats

Watu hugawanya fats katika makundi mawili: saturated na unsaturated fats. Lakini fats hazigawanyiki kirahisi hivyo. Kiukweli, kuna makundi manne ya fats zinazopatikana katika chakula:

. Monounsaturated fats
. Polyunsaturated fats
. Saturated fats
. Trans fats

Monounsaturated fats

Fats hizi pia hujulikana kama monounsaturated fatty acids (MUFAs), nazo hupatikana kwa wingi kutoka:

. Maparachichi na mafuta ya parachichi
. Njugu na mafuta ya njugu
. Zeituni na mafuta ya zeituni

Wataalamu wanashauri kuwa monounsaturated fats zitengwe hadi kutozidi asilimia 20 ya jumla ya kalori za siku. Kiasi cha juu kikiwa kalori 400 katika kalori 2,000 zinazokubalika kwa siku.

Polyunsaturated fats

Fats hizi pia huitwa polyunsaturated fatty acids (PUFAs). Baadhi ya fats hizi ni za lazima, kwa maana mwili hauwezi kufanya vizuri bila fats hizi. Mwili hauwezi kuzitengeneza, kwa hiyo ni lazima kujenga tabia ya kuzipata katika chakula.

Polyunsaturated fatty acids za muhimu ni:

. Omega-3. Wanaume wanahitaji gramu 1.6 kwa siku, wanawake gramu 1.1 kwa siku.
. Omega-6. Wanaume wanahitaji gramu 17 kwa siku, wanawake gramu 12 kwa siku.

Kuna aina mbili za omega-3 fatty acids, kila moja ikipatikana kutoka vyanzo tofauti:

. Long chain. Unaweza kupata omega-3 aina hii kutoka kwenye samaki hasa heringi, samoni, samaki wa jamii ya bangala, sadini na trout, na mussels, aina ya shelfish. Hupatikana pia kwenye maziwa ya mama.

. Short chain. Omega-3 za aina hii hupatikana zaidi kwenye mimea na mboga za majani. Mfano ni mboga za majani, canola oil, flaxseed na mafuta ya faxseed, soybeans, na walnuts na mafuta ya walnuts.

Baadhi ya vyanzo vya omega-6 fatty acids ni:

. Nafaka (mahindi, ngano, mtama, mchele) na mafuta yatokanayo na nafaka
. Mayai
. Legumes kama soybeans na mafuata ya soybeans
. Ufuta na mafuta ya ufuta
. Alizeti na mafuta ya alizeti
. Wheat germ

Saturated Fatty Acids

Saturated fatty acids huwa ni kitu kigumu (solid) kwenye hali ya joto la kawaida (room temperature). Hakuna madhara katika kutumia saturated fatty acids kwa kiwango kidogo. Wataalamu wanashauri kuwa matumizi ya saturated fatty acids yasizidi asilimia 10 ya kalori zinazohitajika kwa siku.

Utafiti umeonyesha pia kuwa fatty acids zikizidi katika mwili huleta madhara. Hii ni kwa sababu huongeza uwezekano wa kupata magonjwa ya mishipa ya moyo na magonjwa ya moyo. Wataalamu wanahisi hii inatokana na jinsi fatty acids zinavyopandisha kiwango cha LDL cholesterol.

Vyanzo vikuu vya saturated fatty acids ni:

. Mafuta yatokanayo na ng’ombe na kondoo na mafuta ya nguruwe
. cocoa butter na chocolate
. Coconut milk na mafuta ya nazi
. Bidhaa za maziwa, hasa siagi, cream, maziwa na aina fulani ya jibini
. Mafuta ya mawese
. Nyama nyekundu

Trans fats

Trans fats zinafanana na saturated fats. Tofauti pekee ni katika muundo wa kikemikali. Zote ni vitu vigumu (solids) kwenye mazingira ya kawaida (room temperature), na zote hupandisha LDL cholesterol. Lakini trans fats zinateremsha pia HDL cholesterol (ambazo ni cholesterol nzuri).

Trans fats hutengenezwa kwa kutumia joto na pressure ili kuongeza molekuli za hydrogen kwenye mafuta yatokanayo na mboga za majani. Hii hubadilisha muundo wa kikemikali wa mafuta hayo na kuyafanya yawe kitu kigumu kwenye joto la kawaida na kuyawezesha kudumu muda mrefu bila kuharibika, na kuongeza ladha kwenye chakula.

Trans fats pia hutumika kama emulsifiers ambazo husaidia chakula kuungana na kuzuia baadhi ya vitu vilivyotumika kusambaratika.

Trans Fats zinatokana na:

. Vyanzo asilia na vya kutengeneza: Kuna kiasi kidogo cha trans fats katika nyama nyekundu na bidhaa za maziwa. Kiasi kidogo pia hutokea wakati mafuta (oils) yanapofikia kiwango cha juu cha joto.

. Vyanzo bandia: Trans fats zinaweza kutengenezwa kwa kuyapitisha mafuta ya majimaji yatokanayo na mimea (liquid vegetable oils) kwenye hatua kadhaa za kwenye mitambo.

Kuna madhara mengi ya kiafya ya muda mrefu  yanayoweza kutokea kwa kutumia trans fats ikiwa ni pamoja na kuongeza uwezekano wa kupata saratani na madhara mengine.

Fats ni kitu chenye mchango mkubwa katika afya ya binadamu. Miili yetu hutegemea mafuta ili kupata nishati, kwa ajili ya ukuaji wa ubongo, kwa ajili ya utendaji kazi wa neva, kwa ajili ya kujikinga na baridi, kwa ajili ya kulinda na kujenga seli, na kwa ajili ya kutunza afya ya nywele na ngozi. Dietary fat ni muhimu vile vile katika kufyonza vitamini fulani na kwa ajili ya kutengeneza homoni.

Fat ni kitu cho chote kinachotokana na mimea au wanyama ambacho si fukivu (nonvolatile), kisichoyeyuka katika maji, na ambacho ni oily au greasy kikiguswa. Fats kwa kawida huwa ni kitu kigumu (solid) kwenye hali ya joto la kawaida, kama 25C (77F), lakini huanza kuyeyuka joto likizidi hapa. Kikemikali, fats zinafanana na animal na vegetable oils, ambazo zina glycerides, ambazo ni esters zinazotokana na reaction ya molekuli tatu za fatty acids na molekuli moja ya glycerol.

Pamoja na oils, fats ni moja ya makundi makuu matatu ya chakula, makundi mengine yakiwa protini na kabohaidreti. Karibu seli zote huwa na makundi haya matatu. Fat mara nyingine huitwa hifadhi asilia ya nishati kwa sababu uzito kwa uzito, fat huwa na nishati karibu zaidi ya mara mbili ya ile iliyomo katika kabohaidreti au protini. Huenda ni kwa sababu ya kuwa ni hifadhi kubwa ya nishati, fat huonekana katika viungo vya uzazi vya mimea, kama punje za poleni na mbegu. Ni fat ambayo binadamu huvuna kutoka kwenye mimea ili waitumie kama chakula au katika viwanda. Kiwango cha fat katika mimea ambayo haizaliani ni kidogo hivi kwamba si rahisi kuvunwa.

Zaidi ya asilimia 90 ya fat inayovunwa katika dunia hutokana na spishi kama 20 ya mimea na wanyama. Fat iliyo nyingi katika hii ikivunwa hutumika kama chakula cha binadamu. Kwa hiyo, teknolojia ya fat ipo zaidi katika kuchuja na kutengeneza fats kuwa kwenye maumbo yanayokubalika na watu wa desturi mbalimbali.

Matumizi Ya Fats

Binadamu ametumia fat asilia kwa ajili ya chakula na shughuli nyingine toka zamani sana. Wamisri, kwa mfano, walitumia mafuta ya mzeituni kama mafuta ya kulainisha waliposukuma vifaa vizito vya ujenzi. Pia walitengeneza axle greases kutokana na fat na ndimu, wakichanganya na vitu vingine, miaka yapata 1400BCE. Homer anataja oil kama kitu cha kusaidia katika ufumaji, na Pliny anazungumzia hard na soft soaps. Mishumaa na taa za oil au tallow zimetumika kwa maelfu ya miaka.

Matumizi ya kibiashara ya fats yameongezeka kutokana na kukua kwa uelewa wa tabia za kikemikali za fats. C.W. Scheele, mkemia wa Sweden, aligundua mwaka 1779 kuwa glycerol iliweza kupatikana kutokana na mafuta ya mzeituni kwa kuipasha moto pamoja na lithage (lead monoxide), lakini ilikuwa hadi 1815 ndipo mkemia wa Ufaransa Michel-Eugene Chevreul (1786-1889) alipobainisha tabia za kikemikali za fats na oils. Miaka michache baadaye liquid acids ziliweza kutenganishwa kutoka kwenye solid acids. Margarine iligunduliwa na mkemia wa Ufaransa Hippolyte Mege-Mouries, ambaye katika mwaka 1869 alipata zawadi iliyotolewa na Napoleon III kwa kupata mbadala sahihi wa siagi. Hydrogenation hii ya sasa ina historia kutoka tafiti za mwishoni kwa karne ya 19 zilizoanzisha vegetable-oil-shortening industry na matumizi kadhaa ya viwandani.

Baada ya vita ya kuu ya kwanza ya dunia, organic chemistry ilijiongezea elimu kubwa kwanza ya fatty-acid compositions na kisha glyceride compositions.

Kazi Za Fats Katika Mimea Na Wanyama

Kuwemo kwa fat katika tishu za mimea na wanyama kote ulimwenguni kunaashiria umuhimu wa fat katika maumbile ya mimea na wanyama zaidi ya kazi ya kutoa nishati kwenye seli. Katika wanyama kazi iliyo bayana ya fat ni kuwa hifadhi ya chakula ili kutoa nishati (kupitia enzymatic oxidation-yaani kuungana na oksijeni kunakosaidiwa na enzymes). Kuhifadhiwa kwa fat katika mbegu za mimea kunaweza kuelezewa kwa msingi wa hifadhi ya chakula kwa ajili ya embryo. Si rahisi, hata hivyo, kueleza kwa nini kuna kiasi kikubwa cha fat katika matunda kama ya mzeituni, avocado, na miti ya jamii ya michikichi; kwani kiasi kikubwa cha fat hizi hupotea au huharibika kabla ya mbegu kuota. Fats hufanya kazi nyingine za thamani katika mimea na wanyama. Hifadhi za fat za chini ya ngozi huwakinga wanyama waishio kwenye maji ya baridi au hali ya hewa ya baridi dhidi ya baridi-kwa mfano, nyangumi, dubu na sili wa bahari wenye pembe.

Wanyama wengi wanahitaji angalau fat moja yenye essential fatty acids (linoleic, arachidonic, na kiasi kidogo linolenic) ili kuzuia dalili za kwenye maumbile za ukosefu wa essential-fatty-acid zinazojionyesha kama vidonda juu ya ngozi, magamba kwenye ngozi, nywele kushindwa kukua vizuri, na ukuaji mdogo. Essential fatty acids hizi ni lazima zipatikane katika chakula kwa sababu haziwezi kutengenezwa na mwili.

Prostaglandins zilizogunduliwa na Mshindi wa Nobel U.S. von Euler wa Sweden, ni vitu vinavyofanana na homoni vinavyotokana na arachidonic acid. Fatty acids hizi zinazofanya kazi kibayolojia, ambazo zinapatikana kwa kiasi kidogo kwenye tishu za wanyama, zinahusika katika kujikamua kwa misuli laini, shughuli za enzymes katika lipid metabolism, utendaji kazi wa central nervous system, udhibiti wa mapigo ya moyo na blood pressure, utendaji wa steroid hormones, ukusanyaji wa fat katika adipose tissue, na shughuli nyingine zilizo muhimu.

Utengenezaji Na Uvunjwaji Wa Fat Katika Viumbehai

Utengenezaji wa fat katika mbegu na matunda hutokea katika hatua ya mwisho wakati wa kuiva au kukomaa. Sukari na starch huchukua nafasi kubwa katika matunda, mbegu, na maji ya kwenye mti au jani kabla ya kufikia hatua ya kukomaa au kuiva. Vitu hivi hubadilishwa na enzymes wakati wa hatua za kukomaa na kuwa fatty acids na glycerol, ambavyo baadaye hutengeneza glycerides. Uchunguzi kwa kutumia teknolojia ya radioactive-tracer ulithibitisha utengenezaji wa fat kutokana na kabohaidreti katika mimea na wanyama.

Utumiaji wa hifadhi za fat katika embryo za mimea haujaeleweka vizuri, lakini inafahamika kuwa katika embryo zinazoota glycerides huvunjwa na kuwa glycerol na fatty acids (glycerides are hydrolyzed—that is, decomposed to glycerol and fatty acids)- kupitia lipolytic (fat-splitting) enzymes. Glycerol na fatty acids hizi vinaweza kuwa oxidized na kuleta metabolic products za muda mfupi ambazo zinaweza kuwa oxidezed tena na kuleta carbon dioxide na maji au kubadilishwa na kuwa kabohaidreti ambayo inaweza kuendelea kwenye hatua nyingine za carbohydrate metabolism.

Katika mifumo ya mmeng’enyo wa chakula ya wanyama, fat ya ndani ya chakula huchanganyika na mchanganyiko wa kusaidia mmeng’enyo unaotolewa na tumbo wenye lipase, enzyme inayofanya hydrolysis ya kiasi kidogo cha glycerides. Glycerol, kiasi kidogo cha glycerol esters, fatty acids, na kiasi cha glycerides kisha hufyonzwa na utumbo na angalau kiasi fulani kuungana na kutengeneza glycerides na phospholipids. Fat katika umbo la matone madogo sana, husafirishwa na damu hadi sehemu itakayotumika au kuhifadhiwa.

Fat inayotumika au kuhifadhiwa ndani ya tishu za wanyama hutokana an vyanzo viwili-enzymatic synthesis au mlo.

Muundo Wa Kikemikali Wa Fats

Pamoja na kuwa katika fats asilia glycerides (glyceride ni ester ambayo huundwa na glycerol na fatty acids) huwa ndiyo nyingi zaidi, kuna lipids nyingine kwa viwango vidogo. Mafuta yatokanayo na mahindi (Corn oil), kwa mfano, yanaweza kuwa na glycerides pamoja na phospholipids, glycolpids, phosphoinositides (phospholipids zenye inositol), isomers nyingi za sitosterol na stigmasterol (plant steroids), tocopherols (vitamini E) kadhaa, vitamini A, waxes, unasaturated hydrocarbons kama squalene, na kiasi kikubwa cha michanganyiko ya carotenoids na chlorophyll na vitu vingine.

Fatty acids hufikia asilimia 94 hadi 96 ya uzito wote wa fats na oils mbalimbali. Kwa sababu ya kuwa na uzito mkubwa zaidi katika molekuli za glycerides na kwa kuwa huwa ndiyo sehemu ya molekuli yenye uhai zaidi kikemikali, fatty acids huwa ndizo zinazotoa sifa za kimaumbile na kikemikali za glycerides. Fats zinatofautiana sana, nyingine zina kiasi kidogo cha fatty acids, wakati upanda wa pili, kwa mfano, zaidi ya fatty acids tofauti 100 zimetambuliwa katika butterfat, ingawa nyingi zimeonekana kwa kiasi kidogo sana. Oils na fats nyingi huundwa na fatty acids yapata kama dazani hivi. Tunapotazama miundo ya glycerides yafaa kujua tofauti kati ya saturated acids (asidi zenye single bonds baina ya atomu za kaboni, kama palmitic au stearic), zenye melting temperatures za juu sana, na unsaturated acids (asidi zenye pea moja au zaidi ya atomu za kaboni zilizoungwa kwa double bonds, kama oleic au linoleic), zenye low melting na zilizo hai zaidi kikemikali.

Monoglycerides na diglycerides ni partial esters za glycerol na zina fatty-acid radicals moja au mbili. Ni nadra sana kupatoikana kiasili, mara nyingi ni mazao ya partial hydrolysis ya triglycerides. Zinaweza kutengenezwa kirahisi na hutumika katika utengenezaji wa coatings na resin

Tabia Za Kimaumbile Na Kikemikali

Fats (na oils) zinaweza kugawanywa kama animal na vegetable fat kulingana na sehemu ilikopatikana. Vile vile fats zinaweza kugawanywa kwa viwango vya unsaturation kwa kutumia kipimo cha uwezo wao wa kufyonza iodine kwenye double bonds. Kipimo hiki cha unsaturation mwisho wa siku ndicho kinachotumika kuchagua matumizi ya fat.

Liquid fat (yaani, vegetable na marine oils) ndizo zenye kipimo kikubwa cha unsaturation, wakati solid fats (vegetable na animal fats) zina kipimo kikubwa cha saturation. Solid vegetable fats zenye melting points kati ya 20C na 35C hupatikana mara nyingi katika kiini cha mbegu ya ngano (kernels) na mbegu za matunda yapatikanayo kwenye nchi za tropiki. Zina viwango vidogo vya iodine na zina glycerides zenye asilimia kubwa za saturated acids kama lauric, myristic, na palmitic. Fats kutoka kwenye matunda mengi ya miti ya jamii ya michikichi, hasa nazi na babassu oils, huwa na kiasi kikubwa cha lauric acid iliyochanganywa. Fats nyingi za wanayama ni solid kwenye joto la kawaida.

Fats haziyeyuki katika maji na, isipokuwa kwa castor oil, haziyeyukikatika alcohol ya baridi na kuyeyuka kwa kiasi kidogo kwenye alcohol ya moto. Huyeyuka katika ether, carbon disulfide, chloroform, carbon tetrachloride, petroleum benzin, na benzene. Fats hazina melting points wala solidifying points zinazoeleweka kwa sababu huwa ni michanganyiko ya aina nyingi mno ya glycerides, kila moja ikiwa na melting point tofauti.

Fats zinakuwa hydrolyzed kirahisi sana. Tabia hii hutumika katika kutengeneza sabuni na katika kuandaa fatty acids katika viwanda. Fats zinaweza kuwa hydrolyzed kwa kutumia maji pekee kukiwa na msukumo mkubwa (under high pressure) au kwa maji kwenye mazingira ya msukumo mdogo kukiwepo caustic alkali, alkaline-earth metal hydoxides, au basic metallic oxides zikiwa catalysts. Free fatty acids na glycerol hutengenezwa.

Lipid

Lipid ni moja katika kundi kubwa la organic compounds linalojumuisha fats, oils, homoni, baadhi ya membranes, vinavyowekwa katika kundi moja kwa sababu haviingiliani na maji. Aina moja ya lipids, triglycerides, hutunzwa kama fat ndani ya adipose cells, ambapo hufanya kazi ya hifadhi ya nishati katika viumbe na kusaidia kutunza joto. Baadhi ya lipids kama steroid hormones hufanya kazi ya kutuma taarifa za kikemikali kati ya seli, tishu, na viungo, na nyingine husambaza taarifa ndani ya seli moja. Utando (membrane) wa seli na maumbile madogo ndani ya seli ni mwembamba sana unaojengwa na matabaka mawili ya molekuli za phospholipid. Utando hufanya kazi ya kutenganisha seli kutoka kwenye mazingira na kukusanya pamoja maumbile madogo yaliyomo ndani ya seli yenye kazi maalumu. Kazi hii ya ukusanyaji huu ni ya muhimu mno hivi kwamba utando wa seli, na lipids zinazojenga utando huo, lazima viwe vitu muhimu kwa mwanzo wa maisha.

Maji ni kitu kinachowezesha kuwepo kwa maisha-hivi kwamba karibu vitu vyote vinavyojenga molekuli ya seli hai, bila kujali kuwa ni vya mimea, wanyama au viumbe wadogo wasioonekana kwa macho, huyeyuka katika maji. Molekuli kama za protini, nucleic acids, na kabohaidreti hupenda maji na huitwa hydrophilic (“water-loving”). Lipids, kwa upande mwingine, hazipendi maji hydrophobic (“water-fearing”). Baadhi ya lipids ni amphipathic-sehemu moja ya maumbo yao ni hydrophilic na sehemu nyingine, na kwa kawaida hii ni sehemu kubwa zaidi, ni hydrophobic. Amphipathic lipids zina tabia ya kipekee ndani ya maji: hutengeneza mara moja mikusanyiko ya molekuli zilizojipanga kwa mpango, hydrophilic zikiwa nje, zikigusana na maji, hydrophobic zikiwa ndani, zikiwa zimekingwa kutokana na maji. Tabia hii ndiyo ufunguo wa kuzifanya kuwa ndivyo viungo muhimu vya utando wa seli na viumbe wengine wadogo. Lipids hugawanywa katika makundi makuu machache: fatty acids, derivatives za fatty acids, cholesterol na derivatives zake, na lipoproteins. Lipids hufanya kazi nyingi kama molekuli za kuhifadhi nishati, kupitisha taarifa za kikemikali, na kama viungo katika maumbile ya seli.

Fatty Acids

Fatty acids ni mara chache sana kuonekana kama molekuli huru katika mazingira lakini huonekana zikiwa zimeungana na molekuli za lipids nyingi kama za fats na phospholipids (viungo vikuu vya utando wa seli).

Neno saturated lina maana idadi kubwa kabisa inayowezekana ya atomu za hydrogen zimeungana na kila kaboni katika molekuli.

Unsaturated fatty acids zina carbon-carbon double bonds moja au zaidi. Neno unsaturated linamaanisha idadi ya atomu za hydrogen zilizoungwa kwenye kila kaboni katika molekuli hazijafikia kiwango chake cha juu kabisa kinachowezekana. Idadi ya double bonds huaininishwa kwenye jina-monounsaturated kwa ajili ya molekuli zenye double bond moja au polyunsaturated kwa ajili ya molekuli zenye double bonds mbili au zaidi. Oleic acid ni mfano wa monounsaturated fatty acid.

Fatty acids zenye carbon-carbon double bond zaidi ya moja (polyunsaturated fatty acids) hupatikana kwa kiasi kidogo sana. Jedwali hapo chini linaonyesha polyunsaturated fatty acids za kawaida, linoleic na arachidonic ‘, pamoja na nyingine chache hupatikana kwa kiasi kidogo. Arachidonic acid ina umuhimu kwa sababu ndiyo ndiyo familia ya molekuli inayotangulia, ziitwazo eicosanoids, inayojumuisha prostaglandins, thromoxanes, na leukotrienes. Wanyama hawawezi kutengeneza fatty acids muhimu mbili, linoleic acid (omega-6 fatty acid) na alpha-linoleic acid (omega-3 fatty acid), ambazo hutangulia (precursors) katika utengenezaji wa eicosanoids kwa hiyo ni lazima zipatikane kutoka kwenye chakula kinachotokana na mimea.

Trans polyunsaturated acids, pamoja na kwamba hazitengenezwi na wanyama, hutengenezwa na viumbe wadogo wasioonekana kwa macho ndani ya matumbo ya ruminant animals kama ng’ombe na mbuzi, hutengenezwa vile vile viwandani kwa partial hydrogenation ya fats na oils katika utengenezaji wa margarine. Kuna ushahidi kuwa kula trans fats kuna madhara kwenye shughuli za kimetaboliki za mwili.

Fatty acid derivatives

Triglycerides

Muundo

Triglycerides (jina la kikemikali Triacylglycerol), njia kuu ya kutunza fatty acids katika mifumo ya kibayolojia, ni kundi la mchangaaanyiko wa vitu ambavyo vina glycerol ambayo ina fatty acid zilizounganishwa kwenye kila kila moja ya makundi matatu ya OH kwa kutumia ester bond. Mfano mzuri wa triglyceride ni tristearin.

Triglycerides ni hydrophobic substances ambazo huyeyuka katika baadhi tu ya organic slovents.

Waxes

Kundi al apili la lipds asilia ni la waxes. Waxes hutengemezwa kwa minyororo mirefu ya fatty acids iliyounganishwa kwa kutumia ester oxygen kwenye mnyororo mrefu wa alcohol. waxes haziyeyuki katika maji na ni ngumu (solids). Tabia yao ya kuwa hydrophobic zenye nguvu huzifanya kusaidia kuzuia maji kwenye majani ya baadhi ya mimea, manyoya kaya za kucha za wanyama.

Cholesterol and its derivatives

Cholesterol inaweza kuwa ni molekuli ndogo ya kibayolojia inayofanyaiwa utafiti zaidi kwa sababu ya uhusiano wake mkubwa na binadamu. Uhusiano wa kiwango kikubwa cha cholesterol katika damu na magonjwa ya heart attack na stroke ni kitu kikubwa katika tiba.

Cholesterol ni kundi kubwa la lipids liitwalo isoprenoids ambalo linapatikana kiasili katika sehemu nyingi za ulimwengu. Kundi hili kubwa lina molekuli za kibayolojia nyingi kama steroid hormones, sterols (cholesterol, ergosterol na sitosterol), bile acids, lipid-soluble vitamins (A, D, E na K), phytol (a lipid component of the photosynthetic pigment chlorophyll), insect juvenile hormones, plant hormones (gibberellins) na polyisoprene (the major component of natural rubber).

Steroid hormones

Streroid hormones huchukua sehemu ndogo sana ya cholesterol yote iliyomo katika kiungo, lakini zina umuhimu mkubwa sana wa kibayoojia. Kuna makundi makubwa matano, yote yakitokana nacholeaterol: progestins (zinazofanya kazi wakati wa ujauzito), glucocorticoids (zinazosaidia utengenezaji wa glucose na kupunguza uvimbe), mineralocorticoids (kudhibiti kiwango cha madini ya chuma), estrogens (kusimamia tabia za jinsia ya kike ), na androgens (kusimamia tabia za jinsia ya kiume).

Viwango vikubwa vya cjholesterol katika damu vimefahamika kuwa ni sababu kubwa ya magonjwa ya moyo. Hii ndiyo sababu kubwa ya kuwa na tafiti nyingi kuhusu mtiririko wa cholesterol katika damu na utunzwaji wake katika mwili. Kiwango kilichopo cha cholesterol katika mwili ni matokeo ya uwiano wa ulaji wa cholesterol na utengenezwaji katika seli kwa upande wa mmoja na, utolewaji wake kutoka mwilini (hasa kama matokeo ya kimetaboliki, bile acids) kwa upande mwingine.

Mwili wa kawaida wa mtu una yapata gramu 100 za cholesterol, ingawa kiasi hiki kinaweza kuwa tofauti kutoka mtu mmoja hadi mwingine mwenye afya. Karibu gramu 60 za kiasi hiki huzunguka katika viungo. Kwa sababu cholesterol haiyeyuki katika maji, inachukuliwa ndani ya mfumo wa mtiririko wa damu na chembechembe ndogo za usafirishaji zilizomo katika damu ziitwazo lipoproteins. Chembechembe hizi ndogo huundwa na lipids na protini ambazo zinaweza kuwa na cholesterol na bado zikayeyuka katika damu.

Cholesterol hufyonzwa na seli zinazotanda juu ya utumbo na kuingizwa kwenye mzunguko wa mfumo wa limfu. Limfu kisha huingia kwenye damu na lipoproteins huelekea kwenye maini. Cholesterol iwe iliyotokana na chakula au kutengenezwa na maini, husafirishwa (kama VLDL na LDL) kuelekea kwenye tishu na viungo vya mwili.

Cholesterol hupotea kutoka kwenye seli za tishu zinazozunguka kwa kugeuka na kuwa aina nyigine ya lipoprotein (HDL) inayozunguka ndani ya ya damu na kurudishwa kwenye maini, ambako inavunjwavunjwa na kuwa nyongo (bile acids ) na chumvi.

Lipoproteins

Lipoproteins ni michanganyiko ya lipids na protini ambayo huruhusu lipids inayotokana na chakula au kutengenezwa na viungo vya mwili kusafirishwa ndani ya mwili wote kupitia mfumo wa mtiririko wa damu.
Kama ukolezi (concentration) wa lipoprotein moja au nyingine unakuwa wa juu mno, sehemu ya mchanganyiko huo hushindwa kuyeyuka na huganda juu ya kuta za ateri na kapilari. Kujijenga huku huitwa atherosclerosis na mwisho huziba ateri na kusababisha heart attack au stroke.

Kuna makundi makuu manne ya lipoproteins, kila moja likiwa na protini ya aina yake na mchanganyiko wake wa lipid.

Kuna chylomicrons, very-low density lipoproteins (VLDL), low-density lipoproteins (LDL), na high-density lipoproteins (HDL). Kitu cha kipekee katika kila kundi ni viwango vyao vya lipid na protini. Kwa sababu viwango hivyo huonyesha uzito wa kila lipoprotein (molekuli za lipid zikiwa nyepesi kuliko zile za protini), uzito hutumika kugawa makundi ya lipoproteins.

Jedwali hapa chini ni muhtasari wa tabia za makundi ya lipoproteins.

Vijenzi vikuu vya sehemu ya lipid ni triglycerides, cholesterol, cholesteryl esters, na phospholipids. Kiini kisichoruhusu maji hujenhgwa na triglycerides na cholesteryl esters. Jedwali hapa chini linaonyesha kwa undani viungo tisa muhimu, viitwavyo apoproteins. Ukiondoa LDL ambayo ina apoprotein ya aina moja tu, makundi mengine yote yana mchanganyiko wa apoproteins.

Chylomicrons

Chylomicrons ndizo lipoproteins kubwa kuliko zote, zikiwa na kipenyo cha kati ya 75-600 nm. Hizo ndizo zenye uwiano mdogo kabisa wa protini kwa lipid (ikiwa ni asilimia 90 ya lipid) na kwa hiyo yenye uzito mdogo kabisa. Chylomicrons hutengenezwa na seli za ufyonzaji zinazotanda juu ya utumbo na humwagwa ndani ya mfumo wa limfu ambao huungana na mfumo wa mtiririko wa damu kwenye subclavian vein. Triglyceride, cholesteryl ester, na free cholesterol zilizomo katika chembechembe hizi hutokana na umeng’enywaji fat iliyomo katika chakula. Sehemu za mwisho za kupelekwa katika viungo vya pembeni ni misuli ya moyo, misuli ya mifupa, tishu za adipose, tishu za wanyama wanaonyonyesha.

Very low-density lipoproteins (VLDL)

VLDL ni kundi la lipoprotein linalotengenezwa na maini ambalo linafanana na chylomicrons zinazotolewa na utumbo. Kazi yake pia ni kutoa triglycerides, cholesteryl esters, na cholesterol kwenye tishu za pembeni. VLDL hupungukiwa kwa kiasi kikubwa triglyceride yake katika tishu hizi na kkuzalisha lipoprotein ya uzito wa kati (intermediate-density lipoprotein (IDL)) kama mabaki, ambayo hurudishwa kwenye maini.

Low-density lipoproteins (LDL)

Low-density lipoproteins hutokana na VLDL na IDL ndani ya plasma na huwa na kiwango kikubwa cha cholesterol na cholesteryl esters. Kazi yake kubwa ni kupeleka aina hizo za cholesterol kwenye tishu za pembeni. Karibu theluthi mbili ya cholesterol na cholesteryl esters zilizo ndani ya plasma huhusiana na LDL.

High-density lipoproteins (HDL)

Lipoproteins za kundi hili ndizo ndogo kuliko zote, zikiwa na kipenyo cha kama 10.8 nm na zenye uwiano wa protini kwa lipid wa juu zaidi. Uzito wake ndiyo unaotoa jina lake. HDL hufanya kazi kubwa ya kuondoa cholesterol ya ziada kutoka katika seli na kuirudisha kwenye maini, ambako itavunwavunjwa na kuwa nyongo na chumvi ambavyo baadaye vitatolewa nje kupitia utumbo. LDL na HDL kwa pamoja zinahusika katika kudhibiti kiasi cha cholesterol katika mwili. Kwa sababu ya uhusiano mkubwa kati ya cholesterol katika damu na atherosclerosis, viwango vikubwa vya HDL vinamaanisha uwezekano mdogo wa kupata magonjwa katika vinadamu.