Busha ni mkusanyiko wa maji usio na maumivu kuzunguka korodani moja au zote unaosababisha uvimbe kwenye mfuko wa korodani au kinena. Uvimbe huu unaweza kuwa unakosesha raha, lakini mara nyingi hauna maumivu wala kuleta matatizo. Mabusha huonekana sana kwa watoto na mara nyingi huwa yameondoka yenyewe bila tiba mtoto anapokuwa amefikia umri wa mwaka mmoja. Wavulana wakubwa na watu wazima wanaweza kupata mabusha kwa sababu ya uvimbeuchungu au kuumia.
Neno hydrocele linatokana na maneno ya kigiriki “hydor” lenye maana ya maji na kele linalomaanisha uvimbe. Neno hili lilitumika kwa mara ya kwanza katika miaka ya mwisho ya 1500.
Mabusha huathiri yapata asilimia moja ya watu wazima. Asilimia 80 ya vichanga huwa na processus vaginalis (mwanya usio wa kawaida unatenganisha kurodani na peritoneal cavity) ya wazi, lakini wengi katika hawa hufunga wanapofikia miaka 1.6.
Mabusha yanazidi kuonekana kwa wingi zaidi kutokana na kuongezeka kwa kunusurika kwa watoto wanaozaliwa kabla ya muda na kuongezeka kwa matumizi ya peritoneal cavity for ventriculoperitoneal (VP) shunts, dialysis na kidney transplants.
Mabusha mengi ni ya kuzaliwa nayo na huonekana kwa watoto kwenye umri wa mwaka mmoja hadi miwili. Chronic au secondary hydocele kwa kawaida huwaathiri wanaume wenye umri wa miaka zaidi ya 40. Na noncommunicating hydroceles ndiyo mabusha yanayoonekana zaidi ya mengine.
Aina za Mabusha
Mabusha hugawanywa katika aina mbili, nazo ni:
. Primary hydrocele
. Secondary hydrocele
Primary hydrocele huwekwa tena katika aina nne tofauti, ambazo ni:
. Congenital hydrocele
. Infantile hydrocele
. Encysted hydrocele
. Vaginal hydrocele (primary vaginal hydrocele)
Secondary hydrocele
Secondary hydrocele mara nyingi hutokea kwa sababu ya ugonjwa fulani, kama maambukizo ya wadudu (filariasis, epididymal TB, syphilis), kuumia, post-herniorrhaphy hydrocele, au saratani. Mabusha ya aina hii mara nyingi ni madogo, isipokuwa yale yanayosababishwa na filariasis, ambayo yanaweza kuwa makubwa.
Namna nyingine ya kuyatambua mabusha ni kuyagawanya katika makundi mawili ambayo ni communicating hydrocele na noncommunicating hydrocele:
Communicating hydrocele
Communicating hydrocele ina mawasiliano na majimaji yaliyomo katika uwazi wa tumbo. Uwazi wa tumbo ni eneo ndani ya tumbo linalohifadhi mfuko wa tumbo, utumbo mdogo na utumbo mpana, maini, figo na viungo vingine. Communicating hydrocele hutokea wakati wa ukuaji wa kiumbe kichanga tumboni.
Wakati wa ukuaji, utando laini mwembamba hujengwa katikati ya baadhi ya tishu za tumbo la kichanga (inguinal canal) na korodani. Utando huu mwembamba ni processus vaginalis. Kwa kawaida, korodani hushuka kutoka kwenye utumbo hadi katika mfuko wa korodani (scrotum). Kishu tishu huzalishwa na kuliziba tundu. Endapo tundu halikuzibwa, majimaji kutoka kwenye uwazi wa tumbo huweza kutiririka hadi ndani ya mfuko wa korodani na kusababisha busha au hernia.
Wewe au mtoto wako akiwa na communicating hydrocele, mfuko wa korodani utaonekana kuwa mkubwa au kuvimba, na unaweza kubadilika ukubwa mara kadhaa katika siku moja.
Noncommunicating hydrocele
Kwenye noncommunicating hydrocele, processus vaginalis huziba. Lakini bado kuna majimaji ya ziada ya tumboni kuzunguka korodani ndani ya mfuko wa korodani. Noncommunicating hydrocele huweza kutokea wakati wa kuzaliwa au miaka mingi baadaye bila sababu inayoeleweka.
Wewe au mtoto wako akiwa na noncommunicating hydocele, busha hubakia la ukubwa ule ule au hukua taratibu sana.
Chanzo Cha Busha
Watoto wenye mabusha huzaliwa nayo. Mabusha kwa kawaida ni sehemu ya ukuaji wa kichanga cha tumboni, wakati majimaji ya kwenye tumbo huweza kutiririka kuelekea kwenye mfuko wa korodani endapo processus vaginalis haijaziba. Na wakati mwingine, hata kama processus vaginalis imeziba, majimaji ya tumboni yanaweza kubakia ndani ya mfuko wa korodani. Mwili wa mtoto wako huyafyonza majimaji haya katika miaka yake miwili ya kwanza.
Baina ya watoto wakubwa na watu wazima, busha hutokana na kuumia au maambukizo ya vijidudu kwenye mfuko wa korodani.
Tiba Ya Busha
Mabusha mengi hupotea yenyewe bila tiba. Lakini kama busha haliondoki lenyewe, daktari anaweza kushauri upasuaji (hydrocelectomy). Wakati wa upasuaji, daktari ataliondoa busha. Kama una communicating hydrocele, daktari ataziba tundu kati ya processus vaginalis na mfuko wa korodani.
Katika mada yetu nyingine tutazungumzia tatizo la nyama za pua. Usisite kutoa maoni yako kuhusu uandishi wa mada hii ya leo. Tutafurahi kusikia toka kwako.
Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu ndani ya saa za kazi kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.
Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.