Endometriosis Ni Nini?

Endometriosis ni hali ambayo mara nyingi huleta uchungu ambapo tishu zinazofanana na zile zinazotanda juu ya nyumba ya mimba (uterus) huota sehemu nyingine ambazo hazistahili. Hali hii huweza kuleta maumivu ya nyonga, hedhi nzito, na hata ugumba. Mara nyingi endometriosis huathiri ovari, mirija ya uzazi (fallopian tubes) na tishu zinazozunguka nyonga. Mara chache sana endometriosis huweza kuathiri maeneo ya mbali na viungo vya nyonga. Tiba ni pamoja na dawa, upasuaji au vyote kwa pamoja.

Tishu za endometriosis zinafanana na tishu zinazotanda juu ya nyumba ya mimba ambazo huongezeka unene, hujivunja na kutoka kila wakati hedhi ikitokea. Lakini zimeota sehemu isiyostahili, na haziondoki kwenye mwili. Wakati endometriosis inahusishwa na ovari, cysts ziitwazo endometriomas huweza kutokea.

Dalili Za Endoemetriosis

Dalili kubwa ya endometriosis ni maumivu ya nyonga. Mara nyingi maumivu haya huendana na hedhi. Ingawa wengi hupata maumivu wakati wa hedhi, watu wenye endometriosis huelezea maumivu yaliyo makali zaidi ya kawaida. Maumivu huweza kuendelea na mwishowe hali ikawa mbaya sana.

Dalili za kawaida za endometirosis ni:

. Hedhi zenye maumivu: Maumivu ya nyonga na misuli ya tumbo yanayoanza kabla ya hedhi na kuendelea siku kadhaa wakati wa hedhi. Unaweza kupata maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo au tumbo. Jina jingine kwa maumivu wakati wa hedhi ni dysmenorrhea.

. Maumivu wakati wa tendo la ndoa: Maumivu wakati au baada ya tendo la ndoa ni ya kawaida kwa mtu mwenye endometirosis.

. Maumivu ya tumbo na wakati wa haja ndogo: Unaweza kupata hali hizi kabla au wakati wa hedhi.

. Damu kutoka kwa wingi: Wakati mwingine utatoa damu nyingi wakati wa hedhi au kutoa damu katikati ya mzunguko wa hedhi.

. Ugumba: Kwa baadhi ya watu, endometirosis hubainika wakati wa vipimo vya kwanza kwa ajili ya tiba ya ugumba.

. Dalili nyingine: Unweza kuona uchovu, kuharisha, kukosa choo, tumbo kujaa au kichefuchefu. Dalili huonekana zaidi kabla au wakati wa hedhi.

Hakuna uhusiano wa moja kwa moja baina ya maumivu unayopata na kiwango cha endometriosis uliyo nayo. Kuna baadhi ya watu hawapati dalili zo zote. Wanajua kuwa wana tatizo hili pale wanapokosa ujauzito au baada ya kufanyiwa upasuaji kwa tatizo jingine.

Chanzo Cha Endometriosis Ni Nini?

Chanzo halisi cha endometirosis bado hakijajulikana. Lakini baadhi ya sababu zinaweza kuwa:

. Retrograde menstruation. Hii inaweza kutokea pale damu inaporudi nyuma kupitia mirija ya uzazi na kuingia kwenye uwazi wa nyonga badala ya kutoka nje ya mwili. Damu hii ina seli za endometrium kutoka kwenye utando laini unaotanda juu ya nyumba ya mimba. Seli hizi zinaweza kunata juu ya kuta za nyonga na maeneo mengine ya viungo vya nyonga. Pale, zinaweza kuota na kuendelea kuwa nene zaidi na kutoa damu wakati wa vipindi vya hedhi.

. Transformed peritoneal cells. Wataalamu wanaamini kuwa homoni au immune factors vinaweza kusaidia kubadilisha seli zinazotanda ndani ya tumbo, ziitwazo peritoneal cells, na kuwa seli zinazofanana na zile za ndani ya nyumba ya mimba.

. Embryonic cell changes. Homoni kama ya estrogen inaweza kubadilisha embryonic celss -seli zilizo katika hatua ya mwanzo ya ukuaji- na kuwa seli zinazofanana na zile za endometrium wakati wa balehe.

. Matatizo yatokanayo na upasuaji. Seli za endometrium zinaweza kunata kwenye tishu za makovu yaliyotokana na upasuaji wa maeneno ya tumbo, kama C-section.

. Endometrial cell transport. Mishipa ya damu au maji ya ndani ya tishu yanaweza kusafirisha seli za endometrium hadi sehemu nyingine ya mwili.

. Immune system condition. Tatizo katika mfumo wa kinga unaweza kuuzuia mwili kutambua na kuzivunja tishu za endometriosis.

Vitu Hatarishi Vya Endometriosis

Vipengele vinayoweza kuongeza uwezekano wa kupata endometriosis ni:

. Kutozaa mtoto
. Kuanza hedhi kwenye umri mdogo
. Kukoma hedhi mapema
. Mzunguko wa hedhi mdogo -kwa mfano, pungufu ya siku 27
. Hedhi nzito zinazoenda kwa zaidi ya siku 7
. Kuwa na viwango vya juu vya estrogen
. Kuwa na uzito mdogo kuliko kiwango.

. Ndugu mmoja kuwa na endometirosis, kama mama, shangazi au dada.

Kitu cho chote ambacho kitazuia damu kutoka nje ya mwili wakati wa hedhi kinaweza kuwa kisababishi.

Baadhi ya sehemu ambazo endometrisis huonekana mara nyingi ni:

. Sehemu ya nyuma ya nyumba ya uzazi
. Myometrium (tabaka la juu la ukuta wa nyumba ya kizazi )
. Ovari
. Peritoneum
. Mirija ya uzazi

Mara chache endometriosis huonekana kwenye maeneo ya:

. Sehemu ya haja kubwa
. Utumbo
. Kibofu cha mkojo
. Diaphragm
. Uke
. Mapafu

Endometriosis kwa wastani humpata mtu mmoja katika watu 10. Watu wanaobainika zaidi ni wale wa umri wa kati ya miaka 20 hadi zaidi kidogo ya 30.

Mambo Mabaya yanayoweza Kutokea Ukiwa Na Endometriosis

Ugumba

Tatizo kubwa kuliko yote linaloweza kutokea kwa sababu ya kuwa na endometriosis ni shida ya kupata mtoto yaani ugumba. Nusu ya watu wenye endometriosis wanapata shida ya kupata watoto.

Ili ujauzito utokee, yai lazima litolewe na ovari. Kisha yai hilo lazima lisafiri ndani ya mirija ya uzazi na kurutubishwa na mbegu za kiume. Yai liliorutubishwa linatakiwa linate kwenye kuta za nyumba ya uzazi na kuanza kukua. Endometriosis inaweza kuziba mirija na kuzuia yai lisikutane na mbegu. Lakini uharibifu wa aina nyingine unaweza pia kutokea ambao yai au mbegu zinaharibiwa.

Hata hivyo, watu wengi wenye tatizo la kiasi la endometriosis wanapata mimba inayokua hadi kuzaa. Wataalamu wa afya wanawashauri watu wenye endometriosis kuwahi kuzaa kabla ya tatizo kuwa kubwa.

Saratani

Utafiti mwingine unaonyesha kuwa endometriosis huongeza uwezekano wa kupata saratani ya ovari.

Tiba Ya Endometriosis

Tiba ya endomeetriosis ni dawa au upasuaji. Hatua ipi itachukuliwa na wauguzi wako itategemea ukubwa wa dalili unazopata na kama unategemea kuapata ujauzito au la.

Kwa kawaida, dawa hushauriwa kwanza. Kama dawa haziztasaidia, upasuaji utashauriwa.

Dawa Za Maumivu

Unaweza kupewa dawa za kuondoa maumivu ambazo unaweza kuzinunua. Dawa hizi ni pamoja na nonsteroidal anti-inflammatory drugs (NSAIDs) ibuprofen (Advil, Motrin IB, na nyinginezo) au naproxen sodium (Aleve). Dawa hizi zinaweza kupunguza maumivu wakati wa hedhi.

Wauguzi wako wanaweza kushauri hormone therapy pamoja na dawa za maumivu kama hutarajii kupata mimba.

Hormone therapy

Wakati mwingine, dawa za homoni zinaweza kupunguza au kuondoa maumivu yatokanyo na endometiriosis. Kupanda na kushuka kwa homoni kwenye mzunguko wa hedhi hufanya tishu za endometriosis kuwa nene, kupasuka na kuvuja damu. Homoni za kutengenezwa kwenya maabara zinaweza kupunguza kasi ya ukuaji wa tishu hizo na kuzuia kujijenga kwa tishu mpya.

Hormone therapy si tiba ya kudumu. Dalili zinaweza kurudi baada ya kuacha tiba.

Njia Zinazotumika Kutibu Endometriosis Ni Pamoja Na:

. Hormonal contraceptives. Vidonge vya uzazi wa mpango, sindano, vijiti na vya kuweka ukeni husaidia kudhibiti homoni zinazosisimua endometriosis. Watu wengi hupata hedhi ndogo na fupi zaidi wakitumia njia za mpango za kudhibiti homoni. Kutumia vidonge vya homoni kunaweza kuondoa au kupunguza maumivu ya wakati wa hedhi. Yamkini ya kupata nafuu huongezeka matumizi ya vidonge hivi vya uzazi wa mpango vikitumika kwa mwaka mmoja au zaidi bila kukatisha.

. Gonadotropin-releasing hormone (Gn-RH) agonists and antagonists. Dawa hizi husimamisha mzunguko wa hedhi na kushusha homoni za estrogen. Hii hufanya tishu za endometriosis kusinyaa. Dawa hizi hutengeneza kukoma hedhi bandia. Kutumia kiasi kidogo cha estrogen au progestin pamoja na Gn-RH na antagonists kunaweza kupunguza matatizo yanayoendana na hedhi. matatizo hayo ni pamoja na hot flashes, kukauka kwa uke na kupoteza kwa mifupa. Hedhi na uwezo wa kupata mimba hurudi baada ya kuacha kutumia dawa.

. Progestin therapy. Progestin ni homoni ya kimaabara yenye mchango mkubwa kwenye mzunguko wa hedhi na ujauzito. Tiba za progestin kadhaa zina uwezo wa kusimamisha hedhi na kukua kwa tishu za endometriosis, na kupunguza maumivu. Tiba za progestin ni pamoja na kifaa kidogo kinachowekwa ndani ya nyumba ya mimba kinachotoa levonorgestrel (Mirena, Skyla, n.k.), kijiti kinachowekwa chini ya ngozi ya mkono (Nexplanon), sindano za mpango (Depo-Provera) au vidonge vya uzazi wa mpango vya progestin pekee (Camila,Slynd).

. Aromatase inhibitors. Hili ni kundi la dawa zinazopunguza estrogen katika mwili. Madaktari wanaweza kukushauri kutumia aromatase inhibitor pamoja na progestin au machanganyiko wa vidonge ili kutibu endometriosis.

Conservative surgery

Huu ni upasuaji wa kuondoa tishu za endometriosis. Upasuaji huu unalenga kubakisha nyumba ya uzazi na ovari. Kama una endometriosis na unataka kupata ujauzito, upasuaji huu unaweza kusaidia kufikia malengo yako. Ni uapsuaji unaoweza kukusaidia pia endapo unapata maumivu makali, lakini endometriosis na maumivu yanaweza kurudi tena baada ya muda.

Daktari anaweza kuifanya operesheni hii kwa kukata sehemu ndogondogo, upasuaji ambao pia huitwa laparoscopic surgery. Mara chache sana upasuaji wa kukata eneo kubwa huhitajika ili kuondoa vipande vinene vya tishu za makovu. Lakini hata hali ikiwa mbaya sana, watu wengi wanaweza kutibiwa kwa njia ya laparoscopic.

Wakati laparoscopic surgery ikiendelea, daktari hutumia kifaa kidogo cha kuangalia kiitwacho laparoscope kupitia kijitundu kidogo karibu na kitovu. Vifaa vya upasuaji vinaingizwa ili kuondoa tishu za endometriosis kupitia kijitundu kingine. Baada ya upasuaji , madaktari wanaweza kushauri kutumia dawa za homoni ili kupunguza maumivu.

Fertility treatment

Endometriosis inaweza kusababisha mwanamke asipate mimba. Endapo una shida katika kupata mimba dakrtari anaweza kushauri fertility treatment. Unaweza kupelekwa kwa daktari mahsusi wa uzazi aitwaye reproductive endocrinologist. Tiba ya uzazi inaweza kuwa ni dawa inayosaidia ovari kutengeneza mayai mengi zaidi. Inaweza kuwa pia kuwa ni taratibu kadha za kuchanganya mbegu za kiume na mayai nje ya kizazi, kitaalamu in vitro fertilization. Tiba sahihi kwako italingana na hali uliyo nayo.

Hysterectomy Inayoambatana Na Kuondoa Ovari

Hysterectomy ni upasuaji wa kuondoa nyumba ya mimba. Kuondoa nyumba ya mimba na ovari ilifikiriwa hapo awali kuwa ndiyo tiba pekee ya endometriosis. Lakini sasa hivi hiyo inafikiriwa kuwa ndilo suluhisho la kuondoa maumivu baada ya tiba nyingine zote kushindwa. Wataalamu wengine wanashauri upasuaji ambao utalenga kwenye umakini zaidi katika upasuaji wa kuondoa tishu zote za endometriosis.

Upasuaji wa kuondoa ovari, unaoitwa oophorectomy, husababisha kukoma hedhi mapema. Ukosefu wa homoni zinazotengenezwa na ovari unaweza kusaidia kupunguza maumivu. Lakini kwa wengine, endometriosis inayobakia baada ya upasuaji huendelea kutoa dalili. Kukoma hedhi mapema huongeza yamkini ya kupata magonjwa ya mishipa ya damu na moyo, matatizo kadhaa ya kimetaboliki na kifo cha mapema.

Kwa watu ambao hawana haja ya kupata ujauzito, hysterectomy mara nyingine hutumika kutibu dalili zinazoambatana na endometriosis. Hizi ni pamoja na hedhi nzito na hedhi zenye maumivu. Hata pale ovari zinapoachwa, hysterectomy inaweza kuwa na madhara ya muda mrefu kwa afya yako. Hii ni kweli hasa pale unapofanyiwa upasuaji ukiwa na umri wa chini ya miaka 35.

Katika mada yetu nyingine tutazungumzia tatizo la uvimba katika kizazi (fibroids). Uwe huru kutoa maoni yako kuhusu uandishi wa mada zetu.