Kuvimba Miguu Wakati Wa Ujauzito

Kuvimba miguu ni hali ambayo huwatokea wanawake wengi wakati wa ujauzito. Kuvimba hutokea hasa kwenye miguu, vifundo vya miguu na nyayo. Mara chache kuvimba huku kunaweza kuenea hadi kwenye vidole. Tatizo la kuvimba kwa miguu huathiri karibu asilimia 80 ya wanawake wajawazito. Kuvimba kwa miguu huonekana zaidi kipindi cha tatu za ujauzito na huondoka baada ya kujifungua.

Wakati wa ujauzito, nyumba ya mimba (uterus) hutanuka, hali ambayo huongeza msukumo kwenye mishipa mikuu ya damu ya maeneo ya tumbo na kupunguza kasi ya mzunguko wa damu. Hii huweza kupunguza mtiririko wa damu kuelekea kwenye moyo na kusababisha damu kujazana kweye miguu.

Isitoshe, wakati wa ujazito, mabadiliko ya homoni huongeza uhifadhi wa baadhi ya madini. Moja ya madini haya ni sodium, ambayo huongeza kasi ya utunzwaji wa maji, hivyo kusababisha kujazana kwa maji kwenye viungo vya chini ya mwili. Sababu hizi kwa pamoja zinaweza kusababisha miguu na nyayo kuvimba, hali iitwayo edema.

Kama tulivyokwisha kusema, kuvimba miguu, vifundo vya muguu na nyayo wakti wa ujauzito ni kitu cha kawaidabaina ya wanawake wemnye ujauzito. Hii ni hali ya kukosesha raha lakini haina maumivu. Kuna hatua kadhaa unazoweza kuzichukua ili kulipunguza tatizo hili. Hatua hizo ni pamoja na:

  1. Punguza matumizi ya madini ya sodium: Chumvi ya ziada katika mwili husababisha mwili kutunza maji ya ziada. kwa hiyo, yafaa kupunguza matumizi ya chumvi. Madaktari huwashauri wanawake wwenye mimba kuacha kutumia chakula cha kusindikwa kwenye makopo kwa sababu ya uwingi wa chumvi na kutoongeza chumvi ya ziada kwenye chakula cho chote kile.
  2. Ongeza ulaji wa potassium: Madini ya potassium huhakikisha mwili unakuwa na uwiano mzuri wa maji. Kupungua kwa madini haya kunaweza kuongeza tatizo la kuvimba miguu. Ongeza madini ya potassium katika mlo wako kwa kula chakula kama:

. Ngozi ya viazi mviringo na viazi vitamu
. Ndizi na juisi ya matunda, kama ya prunes, pomegranate, machungwa, karoti, na passion fruit. . Spinachi, beets, maharage, na lentils.
. Maziwa ya mgando
. Samoni.

  1. Punguza matumizi ya kafeini: Kutumia kafeini mara chache hakuna madhara, lakini kutmia kafeini kwa wingi mno kunaweza kumdhuru mtoto. Jaribu kutumia green tea kabla mbadala wake.
  2. Ufunguo ni kupata maji mengi: Kupata maji mengi katika kunaweza kupunguza kuvimba kwenye vifundo vya miguu, nyayo na vidole. Hapa ndiyo maelezo. Mwili ukiwa na upungufu wa maji, hutunza maji ili kujiweka sawa. Lakini mwili ukipata angalau glasi kumi za maji, figo huanza kufanya kazi yake vizuri zaidi.
  3. Pumzika na nyanyua miguu: Kupumzika mara kwa mara ili kuupumzisha mwili wenye mimba ni muhimu. Namna moja ni kukaa na kunyanyua miguu juu kadiri unavyoweza. Hii inasaidia kurudisha maji ya ziada yaliyojikusanya.
  1. Chagua nguo zinazoachia: Nguo zinazobana huzuia damu kufika vizuri kwenye vifundo vya miguu, nyayo, na vidole, hivyo basi kuliongeza tatizo la kuvimba miguu. Vile kuacha kuvaa pete zinazobana na bangili kutasaidia mtirirko mzuri wa damu kuelekea kwenye viganja.
  2. Epuka hali ya joto: Yafaa kukaa ndani wakati wa joto kali na kuacha kufanya mazoezi mazito ili kukwepa kuongeza tatizo. Pia unaweza kutumia vitu baridi kupooza miguu au kutumia feni.
  1. Tumia Compression stockings za kufika kiunoni. Mwanamke mwenye ujauzito anaweza kupata compression stockings za aina kadhaa sokoni. Lakini zile za kufika kiunoni zafaa zaidi. Stockings hizi zinafanya kazi kwa kuiminya taratibu miguu na nyayo, na kusaidia majimaji kuzunguka vizuri. Epuka stockings za kuishia kwenye magoti kwani zinaweza kubana kupita kiasi na kufanya hali kuwa mbaya zaidi.
  2. Anza kutembea: Madaktari wengi hushauri kuwa kutembea ni zoezi salama wakati wa ujauzito. Kutembea kwa dakika kumi kila siku kunaweza kusaidia kupunguza kuvimba kwa miguu.
  1. Massage zinaweza kusaidia: Kufanyiwa massage na mtaalamu wa massage au mwenza kunaweza kusaidia.
  2. Kuoga kwenye bwawa la kuogelea: Kusimama au kuogelea kwenye bwawa lenye maji ya kufika kwenye shingo kunaweza kusaidia kupunguza tatizo la kuvimba kwa vifundo vya miguu au nyayo.
  3. Kulalia ubavu wa kushoto: Madaktari wanashauri kulalia ubavu wa kushoto ili damu itiririke vizuri zaidi na kupunguza kuvimba kwa miguu. Mwanamke mwenye mimba akilalia ubavu wa kushoto, msukumo wa nyumba ya mimba kwenye inferior vena cava -mshipa mkubwa wa damu unaorudisha damu kwenye moyo- hupungua.

Katika mada yetu nyingine, tutauzungumzia ugonjwa wa kuhara. Usisite kutoa maoni yako kuhusiana na mada hii yetu ya leo.