
Bila shaka umewahi kumwona mtu au wewe mwenyewe una uvimbe juu ya ngozi kwenye eneo la mwili. Mara nyingi uvimbe huu huonekana maeneo ya mgongoni, mabegani, shingoni, kifuani, mikononi, miguuni au hata kwenye paji la uso. Kitaalamu uvimbe huu huitwa lipoma. Mada yetu ya leo ni kutazama uvimbe huu unasababishwa na nini, madhara yake na namna ya kuweza kuuondoa.
Lipoma Ni Nini?
Lipoma ni kijinundu cha mafuta chenye umbo la mviringo au umbo la yai kinachoota chini tu ya ngozi. Lipoma hucheza kirahisi ikiguswa na ina ulaini kama wa mpira. Lipoma nyingi hazileti maumivu na huwa hazina madhara ya kiafya hivyo mara nyingi hazihitaji tiba. Lipoma huweza kutokea sehemu yo yote ya mwili lakini hasa mgongoni, kifuani, mikononi, mabegani na shingoni.
Lipoma ni uvimbe wa tishu laini usio na madhara (benign soft tissue tumors.) Huota na kukua taratibu na si uvimbe wa saratani. Lipoma nyingi hazihitaji tiba. Kama lipoma inakusumbua unaweza kuwaona wataalamu ili waiondoe.
Lipoma ni uvimbe uliozoeleka kwa wengi. Kila mtu mmoja katika 1000 ana lipoma. Lipoma huonekana zaidi kwenye umri wa miaka 40 hadi 60, ingawa huweza kutokea kwenye umri wo wote. Mtoto anaweza kuzaliwa na lipoma. Wanawake hupata lipoma zaidi ya wanaume.
Dalili Za Lipoma
Lipoma mara nyingi hazina maumivu ila zinaweza kuleta usumbufu kama zitasukuma neva au kuota karibu na maungio ya mifupa. Watu wengi wenye lipoma hawaoni dalili zo zote. Kwa kawaida lipoma zina:
. Zingirwa (encapsulated): Haziwezi kuenea kwenye tishu za pembeni
. Hazina maumivu: Ingawa baadhi huleta maumivu kulingana na sehemu zilipo, ukubwa na kama kuna mishipa ya damu
. Umbo la mviringo au umbo la yai: Vijinundu hivi vya mafuta vina maumbo yenye mlingano
. Hutembea: Vijinundu hivi huwa chini tu ya ngozi na husogea ukivigusa
. Chini ya nchi mbili za kipenyo: Aghalabu, lipoma zinaweza kuzidi kipenyo cha nchi 6.
Lipoma huota Wapi?
Lipoma huweza kuota sehemu yo yote ya mwili. Mara chache sana lipoma huota juu ya msuli, viungo vya ndani au kwenye ubongo. Watu wengi wenye lipoma huwa na uvimbe mmoja, ingawa lipoma zaidi ya moja huweza kuota pia. Lipoma nyingi huota chini tu ya ngozi maeneo ya:
. Mikono au miguu
. Mgongo
. Shingo
. Mabega
. Kifua
. Paji la uso

Lipoma Husababishwa Na Nini?
Madaktari bado hawajajua ni nini kinachosababisha kuota kwa lipoma. Lipoma hurithishwa. Una yamkini kubwa sana ya kuota lipoma endapo una ndugu mmoja katika familia mwenye lipoma.
Kuna baadhi ya mazingira yanayochangia kuota lipoma zaidi ya moja katika mwili. Mazingira yanayochangia kuota kwa lipoma ni pamoja na:
. Dercum’s disease: Hali hii inayotokea mara chache husababisha kuota kwa lipoma zenye maumivu, mara nyingi kweye mikono, miguu naa kiwiliwili. Hali hii pia huitwa adiposis dolorosa or Ander’s syndrome.
. Gardner syndrome: Hali isiyo ya kawaida iitwayo familiar adenomatous polyposis (FAP), Gardner syndrome husababisha lipoma na magojwa mengine mengi.
. Hereditary multiple lipomatosis: Pia huitwa familiar multiple lipomatosis, dosari hii ya kiafya ni ya kurithi.
. Madelung’s disease: Hali hii hutokea mara nyingi kwa wanaume wanaokunywa pombe kwa wingi. Hali ambayo pia huitwa multiple symmetric lipomatosis, Madelung’s disease husababisha lipoma kuota maeneo ya shingo na mabega.
Aina Za Lipoma
Lipoma zote huundwa kwa mafuta. Baadhi ya lipoma huwa na mishipa ya damu au tishu nyingine. Kuna aina kadhaa za lipoma ambazo ni:
. Angiolipoma: Aina hii ina mafuta na mishipa ya damu. Angiolipomas mara nyingi huleta maumivu.
. Conventional: Aina inayoonekana kwa wingi zaidi, conventional lipoma huundwa kwa seli nyeupe za mafuta. Seli nyeupe za mafuta hutunza nishati.
. Fibrolipoma: Mafuta na tishu za nyuzinyuzi hujenga aina hii ya lipoma
. Hibernoma: Aina hii ya lipoma hujengwa na mafuta ya kahawia (brown fat). Lipoma nyingi huwa na mafuta meupe. Seli za mafuta za kahawia hutengeneza joto na kusaidia mwili kuweka joto lake.
. Myelolipoma: Lipoma aina hii zina mafuta pamoja na tishu za kuzalisha seli za damu.
. Spindle cell: Seli za mafuta katika lipoma za aina hii zina marefu zaidi ya mapana.
. Pleomorphic: Lipoma hizi huwa seli za mafuta za maumbo na ukubwa tofauti.

Tiba Ya Lipoma
Lipoma nyingi hazihitaji tiba. Kama lipoma inakuletea usumbufu, madaktari wanaweza kuiondoa kupitia upasuaji. Taratibu za kuondoa lipoma ni salama na zinafanya kazi, na unaweza kurudi nyumbani siku hiyo hiyo ya upasuaji.
Kama mbadala wa njia hii ya upasuaji, madaktari ewnaweza kushauri liposuction ili kuondoa lipoma yako. madkatari wanatumia sindano ndefu, nyembamba ili kuziondoa tishu za mafuta kutoka kwenye uvimbe.
Katika mada nyingine tutajadili tatizo la mtoto wa jicho -cataract. Tunaomba mchango wako wa mawazo kuhusu mada yetu ya leo.
Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu NDANI YA MUDA WA KAZI kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.
Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.