
Pumu ya ngozi -atopic dermatitis (eczema) ni hali ambayo husababisha ngozi lkuwa kavu, miwasho na kuvimba. Ni hali ambayo huonekana zaidi baina ya watoto lakini yaweza kutokea kwenye umri wo wote. Pumu ya ngozi ni tatizo sugu na kuweza kuleta mlipuko wakati fulani. Ni tatizo linalosumbua lakini haliambukizi.
Watu wenye pumu ya ngozi wanakuwa kwenye hatari kubwa ya kupata mzio wa chakula, hay fever na asthma.
Kuiweka ngozi kwenye hali ya unyevunyevu na kuzingatia masharti mengine ya utunzaji wa ngozi vinaweza kusabidia kuondoa miwasho na kuzuia milipuko mipya. Tiba inaweza kuhusisha mafuta ya kupaka yenye dawa au cream.
Dalili Za Pumu Ya Ngozi
Dalili za pumu za ngozi zinaweza kutokea sehemu yo yote ya mwili na hutofautiana kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Dalili zinaweza kuwa pamoja na:
. Ngozi kavu, iliyochanikachanika
. Kuwasha (pruritus)
. Vijipele vidogo (ukurutu) vyenye rangi tofauti tofauti kulingana na rangi yako juu ya ngozi iliyovimba
. Maeneo madogo yaliyovimba juu ya ngozi ya kahawia au nyeusi
. Kutoa maji na kujenga gamba gumu juu a ngozi
. Ngozi kuwa nene
. Kubadilika rangi kwa ngozi kuzunguka macho na kuwa nyeusi
. Kupenda kujikuna.

Mara nyingi pumu ya ngozi huanza chini ya miaka mitano na kuendelea kwenye miaka ya balehe hadi utu uzima. Baina ya watu wachache, pumu ya ngozi huweza kulata milipuko na kisha kutulia kwa muda, hata kwa miaka kadhaa.
Chanzo Cha Pumu Ya Ngozi
Baina ya watu wengine, pumu ya ngozi inahusiana na mabadiliko katika jeni ambayo huathiri uwezo wa ngozi wa kujilinda. Kukiwa na tabaka dhaifu la ulinzi kwenye ngozi, uwezo wake wa kutunza unyevu hupungua pamoja na kinga dhidi ya bakteria, vivamizi, allergens na sababu za kimazingira -kama moshi wa tumbaku.
Baina ya watu wengine, pumu ya ngozi husababishwa na uwepo wa kuzidi kipimo wa bakteria aitwaye Staphylococcus aureus juu ya ngozi. Hali hii huondoa bakteria wazuri na kuvuruga kazi za kizuizi cha juu ya ngozi.
Utendaji dhaifu wa kizuizi cha ngozi unaweza kuamsha kinga za mwili ambazo husababisha uvimbe juu ya ngozi na dalili nyingine.
Pumu ya ngozi ni moja katika aina kadhaa za magonjwa ya ngozi. Aina nyingine ni contact dermatitis na seborrheic dermatitis (dandruff).

Kuzuia Milipuko Ya Pumu ya Ngozi
Kuzingatia utunzaji wa ngozi wa msingi kunaweza kuzuia milipuko ya pumu ya ngozi (eczema flares). Hatua zifuatazo zinaweza kuzuia madhara ya kukauka kwa ngozi baada ya kuoga:
. Ifanye ngozi yako kuwa ya unyevunyevu angalau mara mbili kwa siku. Cream, mafuata, losheni hutunza unyevu. Chagua bidhaa zinazofanya vizuri kwa ngozi yako.
Matumizi ya petroleum jelly kwa ajili ya ngozi ya mtoto wako kyanaweza kuzuia kutokea kwa pumu ya ngozi.
. Oga kila suku. Tumia maji ya uvuguvugu, na si ya moto na hakikisha hutumii zaid ya dakika kumi.
. Tumia bidhaa isiyo ya sabuni. Tumia cleanser isiyo na isiyo na rangi, alcohol na vitu vya kunukia. Kwa watoto wadogo, kwa kawaida unahitaji maji ya vuguvugu tu ili wawe safi – hakuna sabuni inayohitajika. Sabumni huweza kuleta matatizo kwenye ngozi ya mtoto mdogo. Kwa watu wa rika zote, sabani za kunukia na za antibacterial huweza kuondoa kiwango kikbwa mno cha mafuta ya asili na kuikausha ngozi. Usisugue ngozi yako ya kutumia kitambaa au kitu kingine kigumu.
Jifute kwa kijipapasapapasa. baada ya kuoga, jipapasepapase taratibu kwa kutumia taulo laini. Tumia moisturizer wakati ngozi ikiwa bado haijakauka (ndani ya dakika tatu).
Vitu vinavyoamsha pumu ya ngozi huwa ni tofauti kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Jaribu kufanya uatafiti na kujua ni nini huamsha tatizo kwako.kwa ujumla, epuka vitu vinavyosababisha miwasho kwa kujikuna maa nyingi huamsha mlipuko wa pumu ya ngozi.
Vitu ambavyo huamsha pumu ya ngozi kwa kawaida ni:
. Kitambaa cha sufu kinachokwaruza
. Ngozi kavu
. Mambukizo juu ya ngozi
. Joto na jasho
. Msongo wa mawazo
. Vifaa vya kusafishia
. Vijidudu katika vumbi na manyoya ya wanyama wafugwao
. Udongo wa mboji
. Poleni
. Moshi wa tumbaku
. Upepo wa baridi na mkavu
. Manukato.
Watoto wadogo wanaweza kupata milipuo inayotokana na kula baadhi ya chakula, kama mayai na maziwa ya ng’ombe.
Tiba Ya Pumu Ya Ngozi
Tiba ya pumu ya ngozi inaweza kuanza na kuweka ngozi yako kwenye hali ya unyevu mara zote na tahadhari nyigine kwa ngozi. Kma hiv havisaidii, daktari anaweza kushauri kutumia cream za dawa ambazo zinasaidia kuondoa miwasho na kurekebisha ngozi.
Pumu ya ngozi inaweza kuwa endelevu. Unaweza kutakiwa kujaribu tiba mbalimbali kwa miezi au miaka kadhaa hadi kuwea kuidhibiti. na hata kama tiba itafanikiwa, dalili zinaweza kujirudia (kutokea mlipuko).
Dawa
. Bidhaa za dawa za kutumia juu ya ngozi. Kuna aina nyingi za dawa za kusaidia kuondoa miwasho na kuikarabati ngozi. Dawa zipo za nguvu tofauti na kama cream, gels na mafuta. Mara nyingi utatakiwa kutumia mara mbili kwa siku kabala ya kapaka moisturizer. Kutumia corticosteroids zaidi ya kiwango kuna madhara kwa ngozi, kama kupunguza nene wa ngozi yako.
Cream au mafuta yenye calcineurin inhibitor zinaweza kuwa chaguo zuri kwa wale wenye umri wa zaidi ya miaka miwili. Kwa mfano, tacrolimus (Protopic) na pimecrolimus (Elidel). Kuwa mwangalifu na jua kali unapotumia dawa hizi.
. Madawa ya kupambana na maambukizo. Daktari anaweza kukupa antibiotics kutibu maambukizo.
. Vidonge vya kudhibiti uvimbe. Kwa pumu ya ngozi iliyofika mbali kidogo, daktari anaweza kukushauri vidonge vya kudhibiti dalili. Anaweza kukuchagulia cyclosporine, methotrexate, prednisone, mycophenolate na azathioprine. Dawa hizi hufanya kazi lakini hazifai kwa matumizi ya muda mrefu.
. Tiba nyingine kwa pumu ya ngozi kali. Sindao za monoclonal antibodies, dupilumab (Dupixent) na tralokinumab (Adbry) zinaweza kuwa ndilo chaguo kwa tatizo lililofika mbali kidogo au kali na ambalo halisikii tiba nyingine. Dupilumab kwa umri unaozidi miaka 6 na tralokinumab ni kwa ajili ya watu wazima.