Lensi ni kiungo chenye umbile la mbinuko wa pande zake zote mbili (biconvex) kilicho nyuma ya iris -eneo lenye rangi la jicho. Katika mwili wa binadamu lensi ina wastani wa ureu wa milimita 9 na upana wa milimita 4. Kazi ya lensi ni kuupindisha mwanga ili utue juu ya eneo husika na kukusaidia uweze kuziona picha za kutoka dunia ya nje vizuri. Kwa sababu lensi inanyumbulika na kubadili umbo lake, inaweza kukusaidia kuviona vitu vya umbali tofauti.
Umri wa mtu unapokuwa mkubwa, lensi inaweza kuwa dhaifu au kuharibika. Kwa sababu lensi hubadili umbo ili kuona karibu au mbali, inaweza kuwa dhaifu na isifanye vizuri miaka ya baadaye.
Lensi ni angavu na hutengenezwa kwa kiasi kikubwa na protini. Karibu asilimia 60 ya lensi huundwa kwa protini -kiasi ambacho ni kikubwa kuliko karibu viungo vyote vya mwili.
Maumbile manne huunda lensi hii ya kristali:
. Capsule
. Epithelium
. Cortex
. Nucleus
Ikiwa imeundwa kwa collagen na protini, lensi kwa kawaida haina miunganiko dhahiri ya damu au neva. Badala yake, hutegemea aqueous humour -majimaji angavu yaliyo kati ya lensi na cornea -kupata nishati na kuondoa taka nje.
Lensi hukua kadiri umri unavyoongezeka, ikiwa na uzito wa miligramu 65 unapozaliwa, kufikia miligramu 160 ukiwa na miaka 10, hadi miligramu 250 kwenye miaka 90.
Mtoto Wa Jicho Ni Nini?
Mtoto wa jicho ni tatizo la macho ambal kitaalamu huitwa cataract. Neno cataract limetokana na neno la
kigiriki katarraktes lenye tafsiri ya maporomoko ya maji. Ilisadikiwa kuwa majimaji kutoka kwenye ubongo yalipita juu ya lensi za macho yako.
Cataract ni maeneo ya ukungu yanayojijenga juu ya lensi ya jicho lako. Cataract nyingi hutokea wakati umri unapokwa mkubwa au kuumia kunaposababisha mabadiliko kwenye tishu zinazojenga jicho. Protini na fibers ndani ya lensi huanza kuvunjikavunjika na kunatana na kuuzuia mwanga unaopita kuelekea kwenye retina.
Hali hii husababisha ukunngu wakati wa kuona (mtu kuona kama anatazama kupitia kioo kilichochafuka).
Muda ukipita hali itazidi kuwa mbaya zaidi na mwishowe utashindwa hata kufanya kazi zako za kila siku.
Wataalamu wa afya wanaamini kuwa cataract ni tatizo ambalo halikwepeki umri ukiwa mkubwa.
Cataract Zinazotokana na Umri (Age-related cataracts)
Nuclear Cataract
Nuclear cataract ni kiwingu kwenye kiini cha lensi ya jicho. Nuclear cataracts hujijenga taratibu kwa kipindi kirefu na huweza kuwa kubwa na ngumu sana na kuifanya kazi ya kuziondoa kuwa kubwa. Hii ni moja ya cataracts zinaoonekana kwa wingi zaidi. Sehemu ya katikati ya lensi hubadilika na kuwa njano na kuwa ngumu zaidi kadiri umri unavyoongezeka. Sehemu hii ya kawaida ya kuzeeka huitwa nuclear sclerosis. Kama hali itazidi kuwa mbaya zaidi nuclear cataract hutokea.
Dalili za nuclear cataract ni:
. Kupata shida kuendesha gari, kusoma mabango
. Kupata shida ya kusoma vitu vya mbali
. Uonaji wa ukungu, rangi hafifu, kutoona vizuri kwenye maeneo yasiyo na mwanga mkubwa. Unaweza kujiona kuwa unatazama kupitia kioo kichafu
. Mng’ao mkali kutoka vyanzo vya mwanga
Kubadili miwani hakuwezi kusaidia kuliondoa tatizo.
Wakati umri mkubwa ndiyo sababu kubwa ya kupata nuclear cataract, yafuatayo yanaweza pia kuchangia kwa kiwango kikubwa:
. Uvutaji wa sigara
. Mionzi ya UV
. matumizi ya madawa (steroids)
. Kisukari
Cortical Cataracts
Cortical cataracts hujijenga kwa kasi kubwa zaidi kuliko ile ya nuclear cataracts, huwa ni laini zaidi na hivyo si kazi kubwa sana kuziondoa. Inafikiriwa kuwa cataracts hizi hutokea kwa sababu ya kuongezeka kwa kiwango cha maji katika lensi. Aina hii huwapata zaidi wanawake, watu weusi na wale wa Carribean.
Ukungu kwenye cortical cataract huanzia pembezoni mwa lensi. Hii ni aina nyingine inayoonekana kwa wingi. Mwanzoni cortical cataract itaonekana kama spoku nyeupe za gurudumu. Baadaye zinasambaa zaidi kuelekea katikati ya lensi na kuzuia zaidi mwanga kufikia retina. Hali hi hufanya dalili za cataract kuwa kali zaidi.
Dalili kubwa zaidi ni mng’ao makali, ambao hufanya vyanzo vya mwanga mkali (kama taa za mbela za gari) kusumbua zaidi. Cortical cataracts huweza kuathiri uonaji wa karibu, uonaji wa mbali, uwezowa kutambua umbali wa kitu kilicho mbele yako, uwezo wa kutoa tofauti ya vitu vyenye mng’ao na wakati mwingine kuona vitu mara mbili.
Watu walio kwenye hatari kubwa ya kupata cortical cataract ni pamoja na wenye kisukari, wenye pressure ya juu, wenye tatizo kubwa la kuona karibu na wanaovuta sigara.
Posterior subcapsular cataracts
Posterior subcapsular cataracts (PSC) ni ukungu kwenye tabaka la nyuma la lensi yako. Cataracts hizi
hazionekani mara nyingi kama nuclear au cortical cataracts, lakini huonekana zaidi baina ya watu wa umri
mdogo. PSCs hukua kwa haraka zaidi kuliko aina nyingine za cataracts zinazoendana na umri. Hii huweza
kuharibu uonaji wako kwa haraka zaidi.
Watu wenye PSCs huweza kuona mng’ao na kupata shida ya kuvitazama vitu vyenye mwanga mkubwa. Inaweza pia kusababisha kupata shida ya kuviona vitu vya karibu au vya mbali, lakini shida ya vitu vya karibu hujitokeza zaidi.
Aina Nyingine Za Cataracts
Cataracts haziendani na umri tu. Kuna aina nyingine ambazo ni pamoja na:
. Anterior subcapsular cataracts. Anterior subcapsular cataracts hutokea upande wa mbele wa lensi. Cataracts hizi nyingi hutokea baada ya kuumia kwa jicho. Nyingine hutokea endapo ugonjwa au tiba ya ugonjwa mwingine umesababisha uvimbe kwenye jicho.
Wakati mwingine madaktari wanashindwa kuelezea sababu za cataracts hizi.
. Traumatic cataracts. Traumatic catarcts hutokea mtu anapoliumiza jicho lake. Ajali zinawezsa kuwa za kitu butu ambacho kitapiga kwa kishindo kwenye eneo la jicho au kitu cha kupenya ambacho mara nyingine kitaingia jichoni.
Zinaweza kumpata mtu aliyenaswa na umeme, aliyeunguzwa na kemikali au aliyekuwa kwenye mazingira ya mionzi mikali.
Cataracts hizi hujijenga saa chache au dakika chache tu baada ya kuunia kwa jicho. Nyingine huchukua miezi au miaka.
Traumatic cataracts nyingi zina umbo la waridi au nyota.
. Snowflake cataracts. Watu wenye kisukari wanakuwa kwenye hatari mara tano zaidi ya kupata cataracts, pamoja na snowflake cataracts. Mara nyingine huitwa “diabetic cataracts” ingawa kisukari kinaonyesha kusababisha zaidi cortical, posterior subcapsular na aina nyingine za cataracts.
Snowflake cataracts hujenga eneo la ukungu katikati ya lensi na mifano ya mikono ikielekea kwenye kingo. Hujenga mfano wa umbo la snowflake.
Caaracts hizi huwapata zaidi vijana ambao hawajaweza kudhiti au hawajajipima sukari katika miili yao. Wakati mwingine, madaktari hutmia kama ishara ya mwanzo ya kugundua tatizo la kisukari kwa mgonjwa.
. Christmas tree cataracts. Christmas tree cataracts haziweki ukungu wa kijivu-nyeupe kama ilicyo kwa aina nyingine. Badala yake hutokea vijidoa vingi ambavyo vitaonekana kama jicho linaakisi taa za mti wa krismasi.
Jina la kitaalamu ni polychromatic cataracts. Polychromatic linatokana na neno la kale la kigiriki
likimaanisha “rangi nyingi.”
Cataracts za aina hii huonekana mara chache. Kwa kawaida huonekana zaidi baina ya watu wenye ugonjwa wa misuli uitwao myotonic dystrophy.
Cataracts Za Watoto
Watoto wanaweza pia kupata caratacts, ingawa mara chache. Cataracts huweza kuwatokea muda wo wote hata kabla hawajazaliwa. kuna aina nyingi za cataracts za watoto. Kwa jumla huiwa pediatric cataracts. Baadhi ya cataracts hizo ni:
. Congenital
. Posterior polar. . . . . Cerulian cataracts.
Congenital cataracts. Congenital cataracts ni catarats ambazo mtoto anazaliwa nazo. Mtoto mmoja baina ya watoto 2,400 wanaochunguzwa, huonekana kuwa na cataracts hizi.
Kwa haraka hara tunaweza kusema theluthi moja ya cataracts hizi husababishwa na magonjwa mengine. theluthi nyingine inatokana na kutithi jeni kutoka kwa wazazi, na theluthi inayosalia inatokana na sababu ambazo hazieleweki.
Mtoto mmoja katika kila watoto 250 ambao wanazaliwa anakuwa na namna fulani ya ukungu kwenye lensi. Mara nyingi hali hii haiwaletei matatizo. Mara nyingine hali hii haijulikani hadi mtaalamu wa macho
anapowachunguza kwa sababu nyingine.
Posterior polar cataracts. Posterior polar cataracts (PPC) ni aina moja ya congenital cataracts. Aina hii huonekana mara chache sana.
PPC ni eneo la ukungu sehemu ya katikati ya nyuma ya lensi. Wakati mwingine huonekana kama jicho la fahali au kama michirizi ya kitunguu.
Karibu mara zote PPC huathiri macho yote mawili. Tatizo linaweza kuchunguzwa muda wo wote, lakini mara nyingine hakuna dalili hadi mtu anafikia miaka 30 hadi 50.
Cerulian catracts. Cerulian cataract ni tatizo la macho ambapo hutokea vijidoa vya bluu-nyeupe juu ya lensi. Hii ndiyo sababu watu huuita ugonjwa huu “blue dot cataract.”
Watoto wengi hawaonyeshi dalili hadi wanapofikia miezi 18 hadi 24. Upasuaji ndiyo tiba pekee lakini watu wengi husubiri hadi wafikie kuwa watu wazima ndipo wafanye upasuaji
Secondary Cataracts
Upasuaji wa mtoto wa jicho husaidia mamilioni ya watu kila mwaka, lakini unaweza kusababisha matokeo ambayo hayakutarajiwa yaitwayo posterior capsule opacification (PCO). Mara nyingine watu huita “secondary cataract”.
Hii ni hali ambapo ukungu huota nyuma ya lensi bandia uliyowekewa kwenye eneo la kapsuli. karibu nusu ya watu waliofanyiwa upasuaji wa mtoto wa jicho hupata hali katika kipindi cha mika mitano. Huyu si mtoto wa jicho, lakini hutoa dalili zil zile za mtoto wa jicho.
Kwa bahati nzuri, tatizo hili linaweza kuondolewa kirahisi kwa tiba iitwayo YAG laser capsulotomy. Watu walio wengi hufanyiwa tiba hii mara moja tu.
Kwa maelezo ya kina kuhusu secondary cataract, pitia ukurasa wetu mwingine.
Katika mada yetu nyingine, tutauzungumzia ugonjwa wa pressure ndani ya macho au kitaalamu glaucoma. Usisite kutoa maoni yako kuhusu mada yetu hii ya leo au kuuliza maswali uliyo nayo.