Chakula Cha Kuotesha Nywele

 

 

Watu wengi hupenda nywele imara na zenye afya na hasa watu wenye umri mkubwa. Kwa wastani, nywele huota nusu inchi kwa mwezi, na kama inchi 6 kwa mwaka. Kasi ya kuota nywele hutegemea vipengele kadhaa kama, umri, afya, urithi na chakula. Pamoja na kwamba huwezi  kubadilisha vipengele vya umri na afya, chakula ni kitu unachoweza kukidhibiti. Kula chakula kinachokosa virutubishi sahihi kunasababisha ukosefu wa nywele. Kwa hiyo, ulaji wa chakula chenye virutubishi sahihi kutasaidia kuota kwa nywele zenye afya.

Katika mada yetu ya leo, tutazungumzia aina mbalimbali za chakula ambacho unaweza kula ili uweze kuwa na nywele zinazokua na zenye afya.

 

Mayai

 

Mayai ni chanzo kizuri cha protini na biotin, viambato viwili ambavyo vinaweza kusaidia kuota kwa nywele. Kula protini ya kutosha ni muhimu kwa uotaji wa nywele kwa sababu vitundu vya nywele (hair follicles)  hujengwa kwa kiasi kikubwa na protini. Kukosekana kwa protini katika chakula kumethibitishwa kuwa kunachangia kutoota kwa nywele.

Biotin ni muhimu katika utengenezaji wa aina ya protini ya nywele iitwayo keratin. Utafiti umeonyesha kuwa ulaji wa biotin kwa wingi unasaidia katika uotaji wa nywele baina ya watu wenye ukosefu wa biotin. Lakini si rahisi ukapungukiwa biotin kama unapata chakula cha kawaida. Kuna ushahidi mdogo sana kuonyesha kuwa watu wenye afya nzuri wananufaika kwa kula biotin zaidi.

Mayai pia ni chanzo kizuri cha zinc, selenium na virutubishi vingine muhimu kwa uotaji wa nywele. Hii huyafanya mayai kuwa chakula bora cha kutumia ili kuwa na afya nzuri ya nywele.

 

Matunda (Berries)

 

Berries zimesheheni vitu na vitamini zenye manufaa ambavyo vinaweza kusaidia ukuaji wa nywele. Ni pamoja na vitamini C ambayo ni antioxidant yenye nguvu. Antioxidants zinalinda vitundu vya nywele dhidi ya molekuli haribifu zinazoitwa radikali huru (free radicals.)

 

Molekuli hizi hupatikana ndani ya mwili na kwenye mazingira. Mwili vilevile hutumia vitamini C katika uzalishaji wa collagen, aina ya protini inayoimarisha nywele na kuzifanya zisikatike ovyo.

 

Vitamini C pia huusaidia mwili kufyonza madini ya chuma kutoka kwenye chakula chetu. Viwango vidogo vya madini ya chuma katika mwili vinaweza kusababisha ukosefu wa damu ambao unahusishwa na kupoteza nywele.

 

Spinachi

 

Spinachi ni mboaga ya kijani yenye uwingi wa virutubishi vyenye manufaa kama folate, chuma, na vitamini A na C, hivi vyote vikiwa muhimu katika kusaidida ukuaji wa nywele.

Vitamini A husaidia tezi za ngozi kutengeneza sebum. Sebum ni kitu chenye mafuta kinachosaidia kuweka unyevu kwenye ngozi ya kichwa na kufanya nywele kuwa na afya. Spinachi vile vile ni chanzo kikubwa sana cha chuma inayotokana na mimea, na ambayo ni muhimu sana katika ukuaji wa nywele. Chuma huzisaidia chembechembe nyekundu za damu kusafirisha oksijeni kuzunguka mwili mzima ili kuendesha shughuli za kimetabiliki na, ukuaji na ukarabati wa nywele.

Ukosefu wa madini ya chuma unahusishwa na kupunyuka kwa nyewle.

 

Samaki (Fatty Fish)

 

Samaki wenye mafuta kama samoni, heringi na mackerel wana virutubishi ambavyo vinaweza kusaidia ukuaji wa nywele. Hawa ni chanzo kizuri cha omega-3 fatty acids, ambazo zimehusishwa na ukuaji wa nywele.

 

 

Utafiti uliofanywa kati ya wanawake 120 ulionyesha kuwa matumizi ya virutubishi vyenye omega-3  na omega-6 fatty acids pamoja na antioxidants yalisaidia kupunguza kupunyuka kwa nyewle na kuongeza unene wa nywele.

 

Samaki wenye mafuta ni chanzo kizuri pia cha protini, selenium, vitamini D3 na vitamini za D, virutubishi vinavyosaidia uimara na afya ya nywele.

 

Viazi Vitamu

 

Viazi vitamu ni chanzo kikubwa cha beta-carotene. Mwili hubadili beta-carotene kuwa vitamini A, ambayo inahusishwa na afya ya nywele.

Utafiti umebaini kuwa vitamini A husaidia utengenezwaji wa sebum, ambayo husaidia kutunza afya ya nywele.

 

Zaidi ya hayo, vitamini A huweza kuongeza kasi ya ukuaji wa nywele na kufanya nywele ziwe nene, wakati huo huo  ikisaidia kuzuia vijitundu vya nywele kurudi ndani.

 

Avocado

 

Maparachichi ni matamu, yana virutubishi vingi na ni chanzo bora cha mafuta yenye afya. Ni chanzo bora cha vitamini E, ambayo inaweza kusaidia ukuaji wa nywele. Kama vitamini C, vitamini E ni antioxidant ambayo inafanya kazi ya kupunguza madhara ya radikali huru.

 

Katika utafiti mmoja, watu waliokuwa wamepoteza nywele waliongeza nywele zao kwa asilimia 34.5 baada ya kutumia kirutubishi cha vitamini E kwa muda wa miezi 8 .

 

Vitamini E pia hulinda maeneo ya ngozi, kama ngozi ya kichwa, dhidi ya radikali huru. Ngozi ya kichwa iliyoharibiwa inaweza kuotesha nywele dhaifu na kuwa na vijitundu vichache.

Maparachichi ni chanzo bora cha mafuta muhimu kwa mwili. Mafuta haya hayawezi kutengenezwa na miili yetu, lakini ni ya lazima katika kujenga seli zetu. Ukosefu wa mafuta muhimu katika mwili kumehusishwa na kupunyuka kwa  nywele.

 

Njugu

 

Njugu zina ladha, hupatikana kwa wingi na zina virutubishi vinavyoweza kusaidia nywele kukua. Njugu vile vile zina vitamini za B, zinc na mafuta muhimu kwa mwili. Ukosefu wa moja katika hivi umehusishwa na kukosa nywele zenye afya.

Njugu vile vile zimebainika kuwa na faida nyingine nyingi za kiafya licha ya afya ya nywele, pamoja na kupunguza uvimbe na magonjwa ya moyo.

Hii hufanya njugu kuwa kitu bora cha kuongeza kwenye mlo wako.

 

Mbegu

 

Mbegu hutoa kiasi kikubwa cha virutubishi vyenye kalori ndogo. Idadi kubwa ya virutubishi hivi vinaweza kusaidia ukuaji wa nywele. Hivi ni pamoja na vitamini E, zinc na selenium.

Gramu 28 za alizeti zinatoa karibu asilimia 50 ya mahitaji ya mwili ya vitamini E kwa siku, pamoja na vitamini za B muhimu kwa afya ya nywele.

Flaxseeds na chia seeds zina mafuta ya omega-3.

 

Pamoja na hayo yote, flaxseeds hutoa aina ya omega-3 ambayo haitumiki kirahisi na mwili kama ile inayotokana na samaki. Hata hiyo, ni nyongeza nzuri kwa mlo.

Ili kupata mchanganyiko mzuri wa virutubishi, yafaa kula mbegu mchanganyiko.

 

Pilipili (Sweet Peppers)

 

Pilipili ni chanzo bora cha vitamini C, ambayo yaweza kusaidia ukuaji wa nywele.

Pilipili inaweza kuwa na vitamini C mara 5.5 ya chungwa.

 

Vitamini C husaidia katika utengenezaji wa collagen, ambayo inasaidia kuimarisha nywele. Ni antioxidant yenye nguvu, ambayo inaweza kuzuia madhara ya radikali huru dhidi ya nywele. Radikali huru zimebainika kuchangia katika kukosa nywele na nywele kuwa na mvi.

 

Zaidi ya hayo, pilipili ni chanzo bora cha vitamini A. Vitamini A husaidia ukuaji wa haraka wa nywele na uzalishwaji wa sebum, ambayo hutunza afya ya nywele.

 

Chaza

 

Chanza ni moja ya vyanzo vizuri vya zinc.

Zinc ni madini yanayosaidia ukuaji wa nywele na katika mzunguko wa ukarabati wa nywele. Ukosefu wa zinc katika mlo huchangaia kwenye tatizo la telogen effluvium, kupunyuka kwa nywele kunakotokea mara nyingi (hali inayorekebishika) kutokana na ukosefu wa virutubishi katika chakula.

 

Utafiti umeonyeasha kuwa kutumia zinc ya ziada kunaweza kurudisha hali ya kupunyuka nywele kulikotokana na upungufu wa zinc.

 

Matumizi ya zinc ya kupita kiasi kunaweza kusababisha kupunyuka kwa nywele. Hii ndiyo sababu inayofanya zinc kutoka kwenye chakula kama chaza kuwa bora zaidi kuliko zinc ya ziada (supplements), chakula hutoa zinc kwa kiasi kidogo lakini kwa dozi zilizo salama.

 

Uduvi

 

Uduvi ni samaki wa magamba wanaosifika kuwa na virutubishi vingi na kwa hiyo kuwa na uwezo wa kusaidia ukuaji wa nywele.

 

Kwa mfano, uduvi ni chanzo bora cha protini, vitamini za B, zinc, chuma na vitamini D. Gramu 100 za uduvi zinakidhi asilimia 38 ya mahitaji ya mwili ya vitamini D ya siku.

 

Kuna tafiti zilizohusisha vitamini D3 na ukosefu wa nywele.

Pamoja na kuwa na mafuta kidogo, uduvi unatoa kiasi kidogo cha omega-3. Chakula chenye omega-3 kimehusishwa na afya ya nywele.

 

Maharagwe

 

Maharagwe ni chanzo kikubwa cha protini inayotokana na mimea, ambayo ni muhimu katika ukuaji wa nywele. Kama ilivyo kwa chaza, maharagwe yana zinc, ambayo husaidia ukuaji na mzunguko wa ukarabati wa nywele.

Gramu 100 za maharagwe meusi yanatoa hadi asilimia 7 ya mahitaji ya siku ya mwili ya zinc.

Maharagwe yana virutubishi vingine muhimu kwa afya ya nywele, pamoja na chuma, biotin na folate.

 

Soya

 

Utafiti umeonyesha kuwa kuna vitu ndani ya soya vyenye uwezo wa kusaidia ukuaji wa nywele. Moja ya vitu hivi ni spermidine, ambayo hupatikana kwa wingi katika soya.

Kwa mfano, utafiti baina ya watu 100 wenye afya ulionyesha kuwa virutubishi vyenye spermidine vilirefusha kipindi cha ukuaji wa nywele kiitwacho anagen phase. Kadiri kijitundu cha nywele (hair follicle) kinavyokaa zaidi katika kipindi cha ukuaji cha anagen, ndivyo nywele zitakavyokuwa ndefu zaidi.

Lakini utafiti huu wa spermidine na ukuaji wa nywele ni wa siku za karibuni sana, na utafiti zaidi unahitajika kabla ya kufikia ushauri wa matumizi ya spermidine.

 

Nyama

 

Nyama ni chakula kikuu katika milo ya watu wengi na ina uwingi wa virutubishi vinavyoweza kusaidia katika ukuaji wa nywele.

Protini katika nyama inasaidia ukuaji wa nywele na katika ukarabati na uimarishaji wa vijitundu vya nywele.

Nyama nyekundu ina uwingi wa aina ya chuma kinachoweza kufyonzwa kirahisi. Madini haya husaidia chembechembe nyekundu za damu kusafirsha oksijeni kwenye seli zote za mwili, pamoja na vijitundu vya nywele.

Kukosekana kwa protini na chuma kumehusishwa na ukosefu wa nywele.

 

Katika mada nyingine kama hii, tutazungumzia chakula cha kupunguza kasi ya kuzeeka kwa mwili. Usisite kutoa maoni yako au kuuliza maswali uliyo nayo.

 

Kwa mawasiliano nasi tuma tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu kwenye nambari zifuatazo: +255 655 858027 au +255 756 181651.

 

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.