Faida Za Kufanya Mapenzi Ni Zipi?

faida ya kufanya mapenzi

Baadhi ya tafiti zimeonyesha kuwa kufanya mapenzi kunaweza kuwa na faida katika kuinua ustawi na afya ya mwili ya mtu. Unaweza kuzipata faida hizi kwa kufanya mapenzi na tendo la ndoa  na mwenzi wako. Hata matendo madogo madogo, kama kushikana mikono au kukumbatiana yanaweza kuboresha utendaji kazi wa ubongo wako. Kwa kifupi, kufanya mapenzi kunaboresha namna tunavyojisikia, mahusiano, afya ya ubongo na mwili.

Asubuhi ni muda mwafaka wa kufanya tendo la ndoa kwa sababu mwili huwa tayari kwa tendo hilo. Hii ni kwa sababu viwango vya homoni za estrogen na testosterone katika mwili huwa juu kabisa. Utafiti wa 2013 ulionyesha kuwa hamu ya kufanya tendo la ndoa huongezeka kulingana na viwango vya homoni hizi katika mwili  -na viwango vinapokuwa juu zaidi ndivyo starehe ya tendo hilo inavyoongezeka. Tendo la ndoa likifanywa asubuhi linakufanya uwe karibu zaidi na mpenzi wako. Kwa nini? Tendo la ndoa hutengeneza homoni iitwayo Oxytocin ambayo pia hujulikana kama “cuddle hormone.” Oxytocin ni kemikali katika ubongo inayosimamia upendo (love) na kuwafanya wawili wawe karibu zaidi (bonding.) Homoni hii ikitolewa wakati wa tendo la ndoa, utajisikia kuwa karibu zaidi na mwenzi wako.

Katika ukurasa huu  tutajadili faida za kushiriki katika mapenzi, kufika mshindo na ukaribu wa kimapenzi.

Kusaidia Afya ya Moyo

Kama ilivyo kwa shughuli yo yote ya kimwili, tendo la ndoa ni zuri kwa moyo wako. Utafiti uliofanywa Januari 2015 ulibaini kuwa wanaume waliofanya mapenzi mara mbili au zaidi kwa wiki walikuwa kwenye hatari ndogo zaidi ya magonjwa ya moyo, hatari ndogo zaidi ya kupata kiharusi au mshituko wa moyo, ukilinganisha na wale waliofanya mapenzi mara moja kwa mwezi au pungufu ya hapo.
Kufanya tendo la ndoa kunaweza kufikiriwa kuwa ni aina moja ya mazoezi. Utafiti wa 2013 ulionyesha kuwa mwanamme anatumia wastani wa kalori 4 kwa dakika akifanya tendo la ndoa la wastani wa dakika 25, na mwanammke anatumia kalori 3. Hiki ni kiwango cha kutosha kabisa ukilinganisha na kusumbuka kwenye kinu cha kuendesha kwa miguu (treadmill).

Kupunguza Pressure

Tafiti zinasema pressure ya juu ni moja ya viashiria vha ugonjwa wa mshtuko wa moyo. Utafiti ulionyesha kuwa wanawake wa umri mkubwa waliotoshelezwa kimapenzi walikuwa wana yamkini ndogo zaidi ya kuwa na high blood pressure.

Na kulingana na American Heart Association (AHA), high blood pressure inaweza kuleta tatizo la kukosa hamu ya kufanya mapenzi na uume kushindwa kusimama au kusimama kwa muda wa kutosha kwa mwanamme.

Madawa yanayotumika kwa high blood pressure yanaweza vile vile kupunguza hamu ya kufanya mapenzi au kusababisha uume kushindwa kusimama

Kuongeza Kinga Za Mwili

Homoni inayohusika na msongo wa mawazo ni cortisol. Utafiti unaonyesha kuwa theluthi mbili ya watu hupata msongo wwa mawazo au wasiwasi angalau mara moja kwa wiki, na asilimia 15 ya watu hupata msongo wa mawazo wa siku nzima kila siku. Msongo wa mawazo wa kuzidi huathiri kinga zetu za mwili.
Wakati wa tendo la ndoa mwili hutoa kemikali ziitwazo endofins, dopamine na oxytocin, zote zikifanya kazi ya kuondoa madhara ya cortisol, ili kuuwezesha mwili wako kupumzika na kufanya kinga zako za mwili kupanda. Homoni hizi zinaweza kukusaidia kupunguza wasiwasi na hali ya kujisikia vibaya.

Dopamine ni moja ya homoni za kuufanya mwili ujiskie vizuri hutolewa na mwili wakati wa tendo la ndoa na wakati wa kuwa karibu na mwenza. Ni neurotransmitter katika ubongo wetu ni ni kitu muhimu katika kuuweka sawa mfumo wa kinga za mwili. Tafiti zimeonyesha kuwa kuongeza dopamine katika mwili kunaboresha kinga za mwili.

Usingizi ni moja ya vigezo vikubwa vya afya ya kinga za mwili. Tusipopata usingizi wa kutosha kinga za mwili hudhoofu. Homoni zitolewazo wakati wa tendo la ndoa zinaweza kusaidia kuapata usingizi na hivyo kuboresha kinga za mwili.

Tafiti zimeonyesha kuwa homoni ya oxytocin inayoyolewa wakati wa tendo la ndoa ina fanya kazi kama anti-inflammatory na hivyo kuboresha kinga za mwili.

Kupunguza Uwezekano Wa Saratani Ya Tezi Dume

Utafiti wa Desemba 2016 ulibaini kuwa wanaume waliokojoa shahawa zaidi ya mara 21 kwa mwezi wakilinganishwa na wale waliokojoa shahawa mara 4 hadi 7 kwa mwezi, walikuwa wamepunguza yamkini ya kupata saratani ya tezi dume kwa asilimia 20. Pamoja na kwamba utafiti zaidi unahitajika, inaonekana kuwa kukojoa shahawa mara nyingi kunaweza kupunguza uwezekano wa saratani ya tezi dume.

Kuondoa Msongo Wa Mawazo Na Wasiwasi

Tendo la ndoa ni njia ya asili ya kupunguza msongo wa mawazo. Utafiti wa 2019 ulichunguza namna ukaribu wa kimapenzi unavyoweza kuwa na matokeo kwenye viwango vya cortisol katika mwili. Cortisol ni steroid hormone inayozunguka katika mwili kufuatia msongo wa mawazo.

faida za tendo la ndoa

Matokeo yalionyesha kuwa kuwa na ukaribu wa kimapenzi, wa tendo la ndoa au vinginevyo, kulisaidia kuweka viwango vya cortisol ndani ya mwili kufikia vile ambavyo ni vya kawaida.

Tendo la ndoa husababisha utolewaji ndani ya mwili wa oxytocin, endorphins, na homoni nyingine za kukufanya ujisike vizuri, ambazo zinaweza kuwa na mchango katika kupunguza msongo wa mawazo.

Kuboresha Usingizi

Kulingana na National Sleep Foundation, mshindo hutoa homoni ya prolactin, ambayo inaweza kukusaidia kupata usingizi na kujisikia burudani. Kwa hiyo usishangae ukiona wewe na mwenzi wako mnapata usingizi punde baada ya kufanya tendo la ndoa la kuridhisha -na kuamka ukijisikia umeburudika.

Ngozi Kung’aa Na Kuonekana Mtu Wa Umri Mdogo

Neno “morning after ” glow ni hekaya? Si neno la kutunga, ukweli ni kwamba unakuwa na mwonekano mzuri zaidi kimwili baada ya kufanya tendo la ndoa. Na tendo la ndoa linakufanya uonekane wa umri mdogo. Mng’ao wa ngozi yako unatokana na mchanganyiko wa homoni na kuondoa msongo wa mawazo, homini za kujisikia vizuri (better mood hormones) ambazo ni pamoja na oxytocins,  beta endorphins na antiinflammatory molecules;  na mwongezeko wa damu kwenye ngozi yako kunakoendana na kusisimuliwa kimapenzi.

BBC newa waliripoti kuwa kuna utafiti wa zamani  ulioonyesha kuwa kufanya tendo la ndoa angalau mara tatu kwa wiki kuliwafanya watu waonekane wenye umri mdogo zaidi kuliko wale ambao walijihusisha na mapenzi mara chache zaidi. Kufika mshindo wakti wa tendo la ndoa kuna faida nyingi sana kwa ngozi ya binadamu.

Kuongeza Hamu Ya Tendo La Ndoa

Kufanya tendo la ndoa kunaleta uboreshaji wa ufanyaji wa tendo hilo na hivyo kuongeza hamu ya kufanya tendo la ndoa.

 

Kwa wanawake, kufanya tendo la ndoa kunaongeza ulainishaji wa uke, mzunguko wa damu, na mnyumbuliko wa uke, vyote hivi vikisaidia kulifanya tendo la ndoa kuwa zuri zaidi na hivyo kumfanya mwanamke apende zaidi kulifanya tendo hilo.

Kumsaidia Mwanamke Kudhibiti Kibofu Cha Mkojo

Misuli ya pelvic floor iliyo imara ni muhimu ili kuweza kuzuia mkojo kutoka wenyewe (incontinence), tatizo ambalo huwasumbua asilimia 30 ya wanawake kipindi fulani katika maisha yao.

Tendo la ndoa lililofanywa vizuri ni kama zoezi kwa misuli yako ya kwenye uvungu wa mifupanyonga. Unapofika mshindo, unasababisha misuli kujikaza, na hivyo kuiimarisha.

Ni Kama Umefanya Mazoezi

Tendo la ndoa linaweza kuwa ni zoezi la mwili la ukali wa wastani, sawa la jogging au kuogelea taratibu. Mapigo ya moyo wakati wa tendo la ndoa huwa ya wastani kuanzia 90-130 kwa dakika (beats per minute) na huweza kufika hadi 170 (bpm).

Namba hizo zinaweza kuwa tofauti kulingana na mkao wa tendo la ndoa, hali ya afya,  na vilainishi vilivyotumika. Kwa hiyo, tendo la ndoa lina mchango kwenye afya ya maungo ya mwili na linaweza kuhesabiwa kama aina moja ya mazoezi ya mwili.

Kujithamini Na Kujiamini

Unahitaji kiasi fulani cha kujiamini (self-confidence) ili kufanya tendo la ndoa, lakini baadaye tendo hilo linakulipa. Kulingana na utafiti wa Chuo Kikuu cha Texas, kufanya tendo la ndoa mara kwa mara kunaongeza hali ya kujiamini na kujithamini (self-esteem) na kuwa na mtazamo  chanya wa nafsi yako.

Kupunguza Maumivu

Kwa kumwangalia tu mpenzi wako -au picha ya mpenzi wako -kunaweza kusaidia kupunguza maumivu. Katika utafiti mmoja uliofanyika Stanford University huko California, wataalamu wa nusukaputi waliwaonyesha washiriki picha za wapenzi wao warembo au picha picha za watu wasiowafahamu wenye mvuto wa kimapenzi (warembo.)  Waligundua kuwa kuangalia picha za watu wenye mvuto wa kimapenzi kulipuguza kwa kiasi kikubwa maumivu.

Tafiti nyingine zilionyesha kuwa wanawake wanaweza kuondokana na maumivu ya wakati wa hedhi wakifika  mshindo kwa kufanya tendo la ndoa.

Tendo la ndoa likifanywa asubuhi linaufanya mwili utoe endorfins, kemikali zenye uwezo wa kimaajabu wa kuondoa maumivu katika mwili wako na kukufanya ujisikie vizuri. Hii ndiyo sababu unajisikia vizuri baada ya kufika mshindo kwenye tendo la ndoa.

Kuongeza Ukaribu Na Kuwafanya Wawili Wafungamane

Utafiti umeonyesha kuwa tendo la ndoa huongeza mapenzi, kuaminiwa, na ukaribu katika mahusiano. Watu wanaweza kutambua na kuonyesha hisia zao.

faida za mapenzi

Kufika mshindo kunatoa oxytocin, homoni ambayo husaidia kuwaweka watu kuwa karibu (kuwa kitu kimoja). Utajisikia kuwa karibu zaidi na mwenzi wako kama utakuwa umekutana naye mara nyingi.

Kusaidia Kutunza Ufahamu

Utafiti uluionyesha kuwa kushiriki mapenzi baina ya watu wa umri mkubwa kulisababisha matokea mazuri zaidi katika mitihani ya utambuzi.

Utafiti wa Januari 2016 uliochapishwa katika jouranal of Age and Aging ulionyesha kuwa watu wa kati ya miaka 50-89 walioshiriki kufanya mapenzi walifanya vizuri kwenye mitihani ya kumbukumbu =na katika stadi kama za kutoa maamuzi, uwezo wa kubadilika kifikra, na kujitawala.
Waandishi walikuja na nadharia kwamba hii inaweza kuwa ilitokana na utolewaji wa dopamine wakati wa tendo la ndoa homoni iliyoonyesha kuboresha uwezo wa kufikiri.

Katika mada yetu nyingine tutatazama sababu za kuchelewa  kufika kileleni. Usisite kutoa maoni yako kuhusu uandishi wa mada hii.

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini, au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu ndani ya muda wa kazi kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.