Free Radicals Ni Nini, na Oxidative Stress Maana Yake Ni Nini?

 

free radicals ni nini

Oksijeni ni elementi ya lazima ili maisha yaendelee. Seli za mwili hutumia oksijeni ili kutengeneza nishati na katika kufanya hivyo, hutokea vitu viitwavyo reactive oxygen species (ROS) na reactive nitrogen species (RNS) kama mapato ya ziada (by-products). Vitu hivi huitwa free radicals.  Free radicaks zinahusishwa kwa namna nyingi na matatizo ya afya ya binadamu, ikiwa ni pamoja na kuzeeka haraka. Mada yetu ya leo itaelezea maana ya free radicals na kwa nini ni kitu hatari kwa afya zetu.

Free radicals ni molekuli zenye oksijeni ambazo zina tabia kubwa ya kuathiri vitu vingine (highly reactive) na zisizo na utulivu (unstable). Free radicals hutokea wakati molekuli au atomu zinapopata au kupoteza elektroni. Hali hiyo husababisha kutokea kwa elektroni iliyo peke yake (isiyo na mwenzi) ambayo inaweza kuziathiri (react with) molekuli nyingine.

Elektroni hizi ambazo hazina wenzi hazipendi kuwa pekee, kwa hiyo hutafuta elektroni ndani ya mwili ili ziweze kuungana na kufanya pea. Katika kufanya hivyo, uharibifu unaohusishwa na free radicals ndipo unapotokea.

Kuna aina nyingi za free radicals, ingawa katika mwili wa binadamu, free radicals za oksijeni (reactive oxygen species) ndizo zinazofahamika zaidi. Mifano ni pamoja na oksijeni moja (wakati oksijeni ikigawanywa kwenye atomu moja moja zenye elektroni ambazo haziko kwenye pea), hydrogen peroxide, superoxides, na hydroxyl anions.

Antioxidants Ni Nini?

Antioxidant ni molekuli ambayo inaweza kutoa elektroni kwa free radical na kuifanya free radical hiyo isiwe na madhara. Mwili huwa una uwezo wa kuzipoza free radicals katika shughuli zake za kimetaboliki lakini kwa kiasi kikubwa hutegemea msaada wa antioxidants.

Hapa chini ni baadhi ya tabia zinazohusu free radicals:

. Free radicals ni mapato ya ziada yanayoweza kuondolewa kabisa.
. Free radicals zinaweza kutengenezwa ndani ya mwili katika utendaji wake wa kazi za kimetaboliki au kutoka nje kama kutokana na X-ray, kuvuta sigara, vichafuzi vya hewa, na kemikali za viwandani.
. Free radicals zikizidi husababisha oxidative stress ambayo huweza kuleta uharibifu.
. Antioxidants huuweka sawa uwiano wa free radicals nazo hupatikana kutoka kwenye lishe.
. Historia ya kiurithi na mazingira ndivyo vinavyosimamia athari anayoweza kuipata mtu.
. Free radicals ni sehemu ya shughuli za kawaida za kibayolojia katika mwili, haswa unapofanya mazoezi ya mwili na kumeng’enya chakula ili kupata nishati.
. Mwili ukizeeka unapunguza uwezo wake wa kushindana na free radicals na kasi ya kuzeeka inaongezeka kwa sababu ya kujazana kwa free radicals.
. Kuzeeka na magonjwa sugu vinavyotokana na free radicals huanzia kwenye mitochondria, chembechembe ndogo za ndani ya seli zinazobadilisha virutubishi kuwa nishati.

Oxidative Stress Ni Nini?

Mara free radicals zikishatengenezwa, iwe kutokana na kuwa karibu na carcinogen au shughuli za kawaida za kimetaboliki za mwili, huwa zipo huru kuleta uharibifu. Uwepo wa free radicals kwa wingi ndani ya mwili husababisha oxidative stress. Mlolongo wa matukio huwa ni mrefu, na wenye tabia ya kujirudiarudia. Free radical moja ikiiba elektroni moja kutoka kwenye molekuli, molekuli ile inakosa elektroni (na hugeuka free radical), na hivyo hivyo. Free radicals huharibu si DNA (nucleic acids) peke yake, bali na protini, lipids, cell membranes, na vitu vingine zaidi katika mwili. Uharibu wa protini na vitu vingine katika mwili huweza kusababisha magonjwa moja kwa moja.

Unaweza kuwa umekwishasikia kuwa inflammation ndiyo chanzo cha magonjwa mengi. Ni kweli, na oxidative sress ndiyo inayochochea inflammation, na ndiyo inayosemwa kuwa ndiyo chanzo cha magonjwa kama ya:

. inflammatory diseases, pamoja na arthritis

. kansa

. magonjwa ya moyo na mishipa ya moyo

. high blood pressure

. diabetes

. neurodegenerative diseases, kama Parkinson’s na Alzheimer’s

. Kuzeeka

Free Radicals Zina Faida?

Ndiyo. Wakati mwingine mwili unaweza kutumia free radicals kwa manufaa. Hii ni pamoja na kuua viini vya magonjwa kama virusi na bakteria, na kusimamia ukuaji wa seli za mwili.

Mfumo wa kinga za mwili, kwa mfano, hutumia sifa ya free radicals za kuua seli, ili kuua viini vya magonjwa. Isitoshe, free radicals huhusika kwenye shughuli nyingine muhimu katika mwili -pamoja na ukuaji na kufa kwa seli, usikiaji wa msongo wa mawazo, na shughuli za kimetaboliki.

Ni Antioxidants Zipi Zinazosaidia dhidi ya Free Radicals?

Kama tulivyokwishakuona, free radicals huwa ni mbaya kwa mwili wakati zikizidi kiwango. Lakini, miili yetu ina kinga dhidi ya free radicals. Ulinzi wa mwili dhidi ya free radicals ni kwa kutumia antioxidants na detoxifying enzymes. Antioxidants huzilinda sehemu za nje na za ndani za seli kwa kuzuia free radicals zisiibe elektroni. Detoxifying agents hulinda sehemu za ndani za seli zisidhurike kutokana na free radicals. Baadhi ya antioxidants na enzymes zinazosaidia ulinzi dhidi ya free radicals ni:

. Vitamin C
. Flavonoids
. Beta carotene
. Lipoic acid
. Vitamin E
. Dependent enzymes za copper/zinc na manganese
. Selenium
. Uric acid
. Bilirubin

Katika ukurasa mwingine tutazungumzia ugonjwa wa UKIMWI. Usisite kutoa maoni yako au kuuliza maswali uliyo nayo kuhusu mada hii ya leo. Tutakuwa na furaha kukujibu.

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu ndani ya saa za kazi kwenda nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.